Kiswahili P1 Questions and Answers - Butula Sub-County Post Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

Maagizo

 1. Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
 2. Kisha chagua insha moja nyingine kutoka kw ahizo tatu zilizobakia.
 3. Kila insha isipungue maneno 400
 4. Kila insha ina alama 20
 5. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

 

SWALI

1

2

3

4

JUMLA

         


MASWALI

LAZIMA

 1. Wewe kama rais umekerwa na kukithiri kwa ufisadi katika wizara mbalimbali. Andikia memo mawaziri wako ukiwaeleza madhara ya ufisadi na hatua utakazochukua ikiwa hawatakomesha ufisadi katika wizara zao. (alama 20)
 2. Visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi huongezeka katika muhula wa pili na wa tatu. Fafanua vyanzo na madhara ya hali hii. (alama 20)
 3. Andika kisa kinachoafiki methali:….Ukicheza ujanani, utalipa uzeeni. (alama 20)
 4. Andika insha itakayokamilika kwa maneno yafuatayo:
  …waliwasili saa tatu baadaye. Uharibifu wa mali na maisha ulikuwa umeshatendeka. Kufika kwao hakukusaidia kwa lolote. (alama 20)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SWALI LA 1.
Hii ni insha ya arifa/barua memo. Insha hii izingatie ya fuatayo:

 1. Iwe na mada/ anwani ya neno Arifa/ Memo juu ya karatasi.
 2. Chini ya anwani iandikwe idara/ sekta ambamo arifa inatokea. Mfano: IKULU YA RAIS.
 3. Ifuatwe na Tarehe ya kuandikwa.
 4. Nambari ya rejea ijitokeze chini ya tarehe. Mfano RAS /12/2021K
 5. Idhihirishe arifa inatoka kwa nani.Mfano: KUTOKA KWA:AFISI YA RAIS
 6. Idhihirishe arifa inaelekea kwa nani. Mfano: KUELEKEA KWA: MAWAZIRI WOTE
 7. Hitimisho iwe na sahihi, jina na cheo cha mwandishi.

Baadhi ya hoja za kujibia swali.
Madhara ya ufisadi

 1. Kudorora kwa uchumi.
 2. Utengano miongoni mwa viongozi.
 3. Utepetevu wa maendeleo.
 4. Ukosefu wa ajira kwa sababu ya mapendeleo katika ajira.
 5. Kukwama kwa baadhi ya miradi kutokana na kufujwa kwa fedha.
 6. Hupanua pengo kati ya matajiri na maskini.
 7. Umaskini hukithiri.
 8. Wafisadi kufutwa kazi/kupoteza ajira.
 9. Hushusha hadhi ya mtu husika na taifa kwa jumla.
 10. Huzuia wawekezaji kuwekeza katika miradi ya maendeleo.
 11. Hutamausha wananchi.
 12. Huzua uhasama baina ya viongozi na wanaoongozwa.
 13. Huchochea hisia za kikabila.
 14. Huweza kusababisha migomo katika sekta mbalimbali.
 15. Huipataifagharamayakulipadeninyingizakigeni.
 16. Walipa ushuru huumia zaidi kwa kuwekewa mzigo wa kulipa fedha zilizofujwa na wafisadi.
 17. Vifo kutokana na bidhaa ghushi na magari mabovu barabarani.

Tathmini majibu mengineyo.
Hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wafisadi.

 1. Kuachishwa kazi.
 2. Kushtakiwa kortini.
 3. Kushushwa madaraka.
 4. Kuamrishwa kurejesha mali waliyofuja.

Swali la 2.
Sababu za utovu wa nidhamu kuongezeka muhula wa pili na watatu.

 1. Kutamauka kwa watahiniwa kwa kukosa maandalizi kabambe ya kukabiliana na mtihani wa kitaifa.
 2. Dhana potovu kwa watahiniwa kuwa walimu wamedinda kuwasaidia kudanganya katika mtihani wa kitaifa.
 3. Wanafunzi kumiliki rununu shuleni kwa siri huchangia kupotoshana kwao kwa mitandao.
 4. Uhaba wa chakula na vifaa vingine muhimu shuleni hasa muhula wa tatu shule zinapokosa fedha.
 5. legevu wa wazazi kwa kutowarudi wanao jambo linalochangia wanafunzi kuwadharau walimu.
 6. Kuondelewa kwa adhabu ya kiboko huwafanya baadhi ya wanafunzi watundu kutenda watakavyo.
 7. Ulegevu wa jamii inayopakana na shule. Baadhi yao huwauzia wanafunzi vileo`/mihadharati.
 8. Sheria finyu kwa baadhi ya shule.
 9. Ulegevu wa walimu. Kutowachukulia hatua wanafunzi watundu.
 10. Idadi ndogo ya walimu shuleni.
 11. Utandaradhi. Filamu na burudani za kupotosha shuleni.
 12. Shinikizo la marika. Kutaka kuwa sawa na wengine waliokwisha kutenda uovu Fulani kama vile kuchoma mabweni.
 13. Tuhuma za kupikiwa chakula chapwa na kibichi kutokana na ulegevu wa wapishi.
  (Tathmini hoja nyinginezo za watahiniwa. Madhara ya utovu wa nidhamu lazima yawepo. Hoja Zozote 6 ni jibu kamili kwa swali hili.)

Mtahiniwa sharti ajibu sehemu zote za swali. Vyanzo na madhara.
Madhara ya utovu wa nidhamu

 1. Kufeli mtihani.
 2. Kutowajibika maishani.
 3. Kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara na walimu.
 4. Kutaabika mustakabalini.(Maisha yabadaye)
 5. Kutamausha wazazi.
 6. Kutokamilisha masomo baada ya kufukuzwa shuleni.

Swali la 3. Methali:
Ukicheza ujanani, utalipa uzeeni.
Maana yake: Ukicheza uwapo kijana, utapokea matokeo ya mchezo wako uzeeni.
Matumizi:Hutumiwa kuwahimiza watu wajitahidi kujitengenezea maisha yao ya kesho au mustakabali wao wakiwa wangali na uwezo wa kufanya hivyo.
Tanbihi: Mtahiniwa aandike kisa kitakachodhihirisha maana ya methali.
Methali huwa na sehemu mbili. Mtahiniwa lazima abainishe sehemu zote mbili za methali katika kisa chake. Vinginevyo, hatakuwa amejibu swali ipasavyo. Asituzwe zaidi ya alama 8 (C yawastani).
Akipotoka kwa maana ya methali, hatakuwa amelijibu swali. AtuzweBk 02/20.
Si lazima aeleze maana ya methali.

Swali la 4:
Mdokezo:…waliwasili saa tatu baadaye. Uharibifu wa mali na maisha ulikuwa umeshatendeka. Kufika kwao hakukusaidia kwa lolote.

 • Kisa kioane na maneno yaliyopeanwa.
 • Mtahiniwa sharti amalizie insha yake kwa maneno aliyopewa.
 • Insha iwe na mada inayowiana na yaliyomo.

Dhana zifuatazo zinaweza kujitokeza;

 1. Uvamizi
 2. Mkasawa moto.
 3. Tukiololote la hatarik.vajali.

Katika dhana hizi zote, wanaotoa msaada hawakufika kwa wakati unaofaa.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P1 Questions and Answers - Butula Sub-County Post Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest