Kiswahili P2 Questions and Answers - Butula Sub-County Post Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

Maagizo

 1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa
 3. Jibu maswali yote.
 4. Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
 5. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
 6. Watahiniwa wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

Kwa matumizi ya mtahini pekee;

Swali

Upeo

Alama

 1. Ufahamu

15

 
 1. Ufupisho

15

 
 1. Matumizi ya Lugha

40

 
 1. Isimujamii

10

 

Jumla

80

 


MASWALI

1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Ufisadi ni uhalifu unaohusu kuzitumia njia za ulaghai kujipatia pesa, mali au vitu hasa vya umma. Nchini Kenya ufisadi hujitokeza kwa njia mbalimbali na kila mojawapo ina athari zake. Kwa mfano, kuna maafisa wa serikali wajipatiao pesa kwa kuuza stakabadhi za serikali kama vile pasi, vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kumiliki mashamba, vitambulisho na nyinginezo kwa raia, kuna hatari
kubwa kwa sababu watu wasio raia wa Kenya wameweza kusajiliwa kama wakenya na kuendeleza uhalifu kama ugaidi, wizi na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Wengine hujipatia vibali vya kufanya kazi na kuajiriwa kazi ambazo zingefanywa na wakenya.
Hii imechangia ongezeko la uhaba wa kazi nchini. Watumizi wengine wa umma huuza mali ya
serikalikama vile magari, nyumba na ardhi na kufutika pesa za mauzo mifukoni mwao. Wengine wao hujinyakulia na kufanya vitu hivyo kuwa mali yao. Ufisadi wa aina hii umegharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha. Serikali imelazimika kununulia maafisa wake magari baada ya muda mfupi, kulipia wafanyikazi wake kodi za nyumba na kukosa viwanja vya upanuzi na ujenzi wa shule hospitali, vituo vya polisi na taasisi zingine maalumu.
Baadhi ya wataalamu kama madaktari huiba dawa kutoka hospitali za umma kupeleka vituo vyao vya afya. Pia hutumia wakati wao mwingi katika kazi zao za kibinafsi na kuwaacha wagonjwa katika hospitali za umma wakihangaika. Sio madaktari tu, kuna masoroveya, wahandisi, mawakili, walimu na mahasibu ambao hukwepa majukumu yao serikalini na kufanya kazi za kibinafsi. Wengine wasio wataalamu huendesha biashara za aina tofauti, na huku wanaendelea kupokea mishahara.
Wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo na shule bora za umma na hawakuhitimu wakati mwingine hulazimika kusalimu amri na kutoa hongo hili wapate nafasi za kusoma. Kiasi cha pesa kinachohitajika huwa kikubwa hivi kwamba ni wachache humudu hizo rushwa. Wale wasiojimudu kifedha hubaki wakilia ngoa. Kuna wazazi ambao hutumia vyeo vyao na 'undugu' kupata nafasi zilizotajwa, jambo ambalo huwanyima wanafunzi werevu kutoka jamii maskini nafasi ya kupata elimu. Matokeo huwa ni kuelimisha watu wasiostahili na ambao mwishowe hawaziwezi kazi wanazosomea wakihitimu na kuanza kuhudumia jamii.
Ufisadi umekita mizizi na kushamiri katika sekta za umma za kibinafsi kwa upande wa kuajiri
wafanyakazi. Ni vigumu kupata kazi ikiwa hujui mtu mkubwa katika shirika linalohusika au
uzunguke mbuyu. Matokeo ni kuajiri wafanyakazi wasiohitimu na wasiowajibika kazini.
Vyeo na madaraka katika baadhi ya mashirika hutolewa kwa njia ya mapendeleo na ufisadi. Kwa
hivyo, wafanyakazi wenye bidii hufa moyo kwa sababu hawasaidiwi ipasavyo. Badala yake wale
wasioleta bidii hupandishwa vyeo na kuwaacha palepale.
Hata hivyo, mbio za sakafuni huishia ukingoni. Serikali imetangaza vita dhidi ya ufisadi. Tayari
tume kadhaa zimebuniwa kuchunguza visa vya ufisadi uliotekelezwa hapo mbeleni. Mojawapo ya tume hizo ni Tume ya kuchunguza Kashfa ya "Goldenberg" ambapo pesa za umma (mabilioni) ziliporwa na mashirika na watu binafsi kwa njia siziso halali. Watakaopatikana na hatia ya kushiriki ufisadi huo watahitajika kurudisha pesa hizo.
Serikali pia imeunda kamati ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi waliohasiriwa na
mawakili walaghai ambao hupokea ridhaa kwa niaba ya wateja wao na kukosa kuwalipa au
kuwatetea mahakamani ilhali wamekwishalipwa. Ni matumaini yetu kuwa ulaghai huu
utaangamizwa kabisa kwani hakuna refu lisilokuwa na ncha.
Maswali

 1. Eleza aina nne za ufisadi zilizotajwa katika kifungu ulichosoma. (alama 4)
 2. Kulingana na kifungu ulichosoma,ufisadi umeathiri nchi yetu kwa njia gani ? (alama 2)
 3. Serikali inafanya jitihada gani ili kukomesha ufisadi ? (alama 3)
 4.  Kwa maoni yako, unafikiri ufisadi husababishwa na nini ? (alama 2)
 5. Toa msamiati mwingine wenye maana sawa na rushwa (alama 1)
 6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa kifunguni: (alama 3)
  1. shamiri ________________________________________________________________
  2. waliohasiriwa __________________________________________________________
  3. wakilia ngoa ___________________________________________________________

2. UFUPISHO ( ALAMA 15)
Soma Makala haya kisha ujibu maswali.
Umuhimu wa vyombo vya habari
Vyombo vya habari hutumika kupasha watu habari kutoka upande mmoja hadi mwingine. Vyombo hivi vina manufaa kwetu. Vyombo hivyo ni kama vile runinga, redio, magazeti, tarakilishi na vinginevyo. Umuhimu mmoja wa vyombo hivi ni kueleimisha. Watu huelimishwa kuhusu jinsi ugomvi unaweza kuepukika katika familia. Pili huelimishwa juu ya magonjwa tofauti kama vile ukimwi, kipindupindu na mengine na jinsi ya kujikinga au kupata matibabu.
Mbali na hayo, vyombo hivi hutumika kuarifu. Watu huarifiwa kuhusu serikali yao, hususan jinsi
mambo yanavyoendeshwa, uhusiano kati ya wajumbe serikalini na hapo kuwaacha watu na maarifa ya kufanya uamuzi bora utakaowanufaisha. Vyombo hivi pia huarifu kuhusu matukio kama ajali za barabarani, majumba kuchomeka na hata mashambulizi ya kigaidi pamoja na matukio mengine. Hiini muhimu kwani watu huwa na habari kuhusu yanayoendelea.
Vyombo hivi, kwa upande mwingine, huchangia kwa kiwango kikubwa umoja wa wananchi. Watu waishio sehemu mbalimbali wanaweza kufahamu vile wenzao katika sehemu nyingine waishivyo kutokana na lelemama, michezo ya kuigiza na kadhalika kutoka sehemu moja hadi nyingine. Chambilecho wahenga umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Fauka ya hayo, vyombo hivi ni muhimu kwani kupitia kwavyo watu wengi wameweza kupata
gange. Watu hawa ni kama vile waandishi wa habari, wahandisi wa mitambo, watangazaji na
kadhalika. Wao huweza kujimudu, kumudu familia zao na hata kukuza uchumi.
Vyombo vya habari ni muhimu kwa kuwa ni vyombo vya kutumbuiza vilvile. Kutokana na
kutumbuizwa, waliotoka kufanya kazi za sulubu hata kazi zingine zozote huweza kupumzika
vyema kwa kuburudishwa na hivyo kuwa wachangamfu tena. Mbali na kupumzisha wanaoandaa
burudani kama vile muziki na maigizo kupitia kwa vyombo hivi vya habari hasa vijana huweza
kupata hela za kujikimu na hivyo basi kujiepusha na visa vya uhalifu, mihadarati na hata uasherati.
Mwisho, vyombo vya habari hutumiwa na wanasiasa wakati wa uchaguzi ili kueneza manifesto zao na za vyama vyao. Kupitia kwa vyombo hivi, wananchi kote nchini wanaweza kujua kujua wanasiasa ambao wananuia kuleta maendeleo na hivyo kufanya maamuzi yao wakati wa uchaguzi.
Aidha, kupitia kwa vyombo hivi tume ya uchaguzi inaweza kuwaeleza wananchi kuhusu mambo
ambayo wanafaa kujiepusha nayo, kwa mfano kupokea hongo ili kutovunja sheria za uchaguzi.
Kwa jumla vyombo vya habari ni muhimu katika maisha ya jamii. Vyombo hivi vinafaa kutumiwa ipasavyo ili navyo viwatumikie wananchi kwa njia mwafaka. Vyombo hivi vikitumiwa visivyo vinaweza kuleta hasara kubwa na hata maangamizi.
MASWALI

 1. Kulingana na Makala, vyombo vya habari vina wajibu gani katika jamii? ( maneno 60)
  Matayarisho
  ________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
  Jibu
  ________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
 2. Mbali na umuhimu wa vyombo vya habari, vyombo hivi vinaweza kuletea jamii hasara kwa njia nyingi. Eleza ( Maneno 50) ( Alama 7, moja mtiririko. )
  Matayarisho
  ________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
  Jibu
  ________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

 1. Tambua na utolee sababu sauti ambazo hazifai kuwa miongoni mwa zile zilizotajwa hapo chini ( alama 2)
  /ch/, /g/, /j/, /k/
 2. Bainisha mofimu katika utungo ufuatayo: ( alama 3)
  Hakumjia
 3. Kwa kutolea mifano, taja matumizi manne ya kiambishi m (al 2)
 4. Eleza majukumu mawili ya sentensi ifuatayo. ( Al2)
  Panda mtini na uangue matunda kwa vile yameiva vizuri.
 5. Tunga sentensi kwa kutumia kitenzi cha silabi moja chenye maana ya kuogopa katika kauli ya kutendeka. (alama 2)
 6. Ainisha kielezi katika sentensi ifuatayo na ukibadilishe kiwe kiwe kielezi igizi (al 2)
  Mbwa yule mweusi alibweka kwa hasira
 7. Bainisha mwingiliano wa maneno katika sentensi hii (al 2)
  Wanafunzi walifanya haraka japo haraka yao iliwatia taabani.
 8. Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari (al 1)
  Naam... ameleta machache.
 9. Tunga sentensi moja kwa kutumia kihisishi cha masikitiko (al 2)
 10. Yakinisha katika udogo wingi (al 2)
  Ng’ombe yuyu huyu hajazaa ndama mkubwa
 11. Tunga sentensi moja kudhihirisha matumizi mawili ya kibainishi (al 2)
 12. Andika katika usemi halisi. (al 2)
  Mama aliwahimiza warudi siku hiyo la sivyo wangekosa tuzo.
 13. Maneno yafuatayo yamo katika ngeli zipi (al 2 )
  wembe_____________________________________________________________________
  mnyoo____________________________________________________________________
 14. Tambua kiima na yambwa katika sentensi ifuatayo (al 2)
  Daktari yule hupigiwa nguo pasi na halima
 15. Ainisha fungu la maneno lenye muundo wa kiima na kiarifa ambalo linakamilika au lisilokamilika kimaana katika sentensi ifuatayo (al 2)
  Mtoto huyu atapita mtihani iwapo atasoma kwa bidii
 16. Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu (al 2)
  Msomi hakutuzwa siku hiyo
 17. Pambanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha vishale (al 4)
  Letu lililopaliliwa limetuletea mazao mengi.
 18. Amechanjiwa kuni ina maana ya kutenda kwa niaba ya.Eleza maana nyingine mbili zinazobainishwa na sentensi hii. ( Al 2)
 19. Tia nanga ni fika na___________ ni kuwa na wivu (al 1)
 20. Andika sentensi ifuatayo kwa kufuata maagizo (al 1)
  Kupanda mchongoma,kushuka ndio ngoma
  Anza kwa Kushuka...........

4. ISIUMUJAMII (ALAMA 10)

 1. Taja mambo manne yanayopelekea kufa kwa lugha (al 2)
 2. Kwa mifano minne,elezea namna muktadha unavvyoathiri mitindo ya lugha (al 4)
 3. Ukiwa mkaguzi mwakilishi katika mashindano ya kiswahili ,fafanua na kueleza mambo yanayochangia wanafunzi kufanya makosa ya kisarufi na ya kimatamshi katika lugha ya Kiswahili ( al 4)


MWONGOZO

1.UFAHAMU

 1.                        
  • wizi wa mali ya umma
  • vyeo na madaraka kutolewa hivi hivi tu
  • uuzaji wa stakabadhi za serikali
  • kuiba dawa
  • kuhonga ili kupata nafasi za kusoma
  • kuhonga au kutumia undugu ili kupata kazi
  • kutowajibika kikazi
  • kuiba dawa zozote 4 x 1 = 4
 2.                                  
  • kufilisisha serikali
  • kunyima wagonjwa matibabu
  • kuzorotesha maendeleo na huduma muhimu
  • kuelimisha watu wasiohitimu na kuacha walio werevu
  • kupandisha vyeo watu wasiostahili
  • kazi kufanywa vibaya bila uajibikaji zozote 2 x 1 = 2
 3.                            
  • kuunda tume na kamati za kuchunguza visa vya ufisadi
  • kurudisha mali iliyoibiwa
 4.                                    
  • uhaba wa kazi
  • uozo wa maadili katika jamii
  • kuongezeka kwa umaskini
  • tamaa ya anasa na starehe
  • uongozi mbaya wa kitaifa
  • kukosa huruma na uajibikaji
  • kukosa uzalendo zozote 2 x 1 = 2
 5. hongo / chai / kadhongo / kuzunguka mbuyu
 6.                              
  1. kuenea kwa jambo au habari
  2. walioumizwa / waliodhuriwa
  3. ona wivu 1 x 3 = 3
   kuwashtaki uhalifu 3 x 1 = 3

2. UFUPISHO

 1. Ufupisho uwe na hoja zifuatazo:
  • Hueleimisha
  • Hupasha habari
  • Huburudisha
  • Huajiri
  • Huleta umoja
  • Hurahisisha utawala
  • Wananchi huweza kufanya maamuzi mema katika uchaguzi
  • Ajira kama waandishi au wahandisi
   (Zozote 7, zilizofafanuliwa x1=7 )
 2. Ufupisho uwe na hoja zifuatazo:
  • Huleta athari za kigeni
  • Hutumiwa kueneza chuki na uchochezi
  • Vinaweza kuleta hasara kubwa na hata maangamizi.
  • Migawanyiko ya kisiasa
  • Nyimbo za kisasa burudani ambazo zinapuuza maadili.
  • Kueneza habari za uongo hivyo kuleta taharuki miongoni mwa wananchi
  • Uraibu hususan runinga ambapo uzembe husheheni maisha ya vijana
   (Zozote 6x 1=6)

3.MATUMIZI YA LUGHA AL 40

 1. /ch/ ni kipasuo kwamizo al 2
 2. ha-ukanusho wa nafsi ya tatu umoja al3
  ku-ukanusho wa wakati uliopita
  m-yambwa /mtendewa
  j-mzizi
  i-kauli ya kutendea
  a-kiishio
 3. Nafsi ya tatu umoja mf atasema al 3
  umbo la nomino za ngeli ya A-WA umoja
  nafsi ya pili wingi mf mnaenda
  umbo la nomino za ngeli ya U-I umoja mf mti
  kuonyesha mahali ndani mf mle
  kuonyesha unominishaji/weledi wa mtu mf mpishi,msomi
 4. panda mtini uangue matunda –agizi al 2
  Yameiva vizuri -taarifa/kauli
 5. chika al 2
  mungu huchika wakati wote
  (lazima jibu lihusishe mungu)
 6. kwa hasira-kielezi cha namna/jinsi al 2
  bwe-kiigizi
 7. haraka-kielezi al 2
  haraka –nomino
 8. naam-kihisishi 1/2
  machache-kiwakilishi ½
 9. laiti al 2. Lazima mwanafunzi atunge sentensi
  maskini
 10. Vigombe/vijigombe vivi hivi vimezaa vidama/vijidama vikubwa al 2
 11. sauti za ving’ong’o
  kuonyesha tarakimu zilizowachwa
  kuonyesha zilizoachwa katika neno
 12. ”Mrudi leo la sivyo mtakosa tuzo.”Mama aliwahimiza. (vitahini vinane al 2)
  “Mrudi leo la sivyo mtakosa tuzo”,mama aliwahimiza.
 13. wembe U-ZI AL 2(Lazima jibu liwe kwa herufi kubwa)
  Mnyoo A-WA
 14. Daktari -yambwa tendewa/kitondo
  nguo-yambwa tendwa
  pasi-yambwa tumizi
 15. Mtoto huyu atapita mtihani- Kishazi huru
  -iwapo atasoma kwa bidii- kishazi tegemezi (alama 2)
 16. Msomi hatakuwa ametuzwa / msomi atakuwa hajatuzwa
 17. S - KN+ KT
  KN-W+ S
  W- letu
  s- lililopaliliwa
  KT- T+N+V
  T- limetuletea
  N- mazao
  V- mengi
  AU
  S- KN+ KT
  KN- W+S
  W- letu
  S- lililopaliliwa
  KT- T+ KN2
  T- limetuletea
  KN2- N+V
  N- mazao
  V- mengi
 18. Kwa sababu yake
  Kutia alama kwenye ngozi yake kutumia ukuni
  alama 2
 19. lia ngoa alama 1
 20. Kushuka mchongoma ndio ngoma sio kupanda alama 1

Halima-kiima ISIMU JAMII

 1.                          
  • Uchache wa wazungumzaji/ lugha kuwa na idadi ndogo ya wazungumzaji.
  • Ndoa za mseto
  • Kutoipa hadhi lugha na kuifanya kufifia
  • Uhamiaji
  • Majanga yanayosababisha vifo vya takriban jamii nzima
   Hoja zozote 4, alama 2
 2.                      
  • Mzungumzaji huchota msamiati kutoka mahali anapozungumzia. Mf atumie msamiati wa sokoni
  • Muktadha huathiri kiimbo . Mfano mtu akiwa hospitalini huzungumza kwa kiimbo cha chini
  • Muktadha huathiri uteuzi wa kiimbo/ lugha / lahaja ambayo mtu anatumia, mfano katika muktadha rasmi, mtu hutumia lugha rasmi
  • muktadha hudhibiti ishara anazotumia mtu- miondoko mingine ni mwiko
  • Muktadha hudhibiti mtindo nafsi wa mtu, mf. Mtu katika mnada au biashara ya rejareja huweza kujirudiarudia ili kuwavutia wateja.
   Hoja zozote 4, alama 4
 3.                          
  • Athari ya lugha ya kwanza
  • Ujuzi wa lugha nyingi/ wingilugha
  • Hali ya mtu mf, mgonjwa
  • Kutofahamu na kutotambua kanuni za sarufi ya lugha ya Kiswahili
  • Kutojimudu na kutoelewa lugha vilivyo
  • Ukosefu wa baadhi ya sauti za Kiswahili katika lugha zao asilia
  • Ulemavu/ ukosefu wa baadhi ya ala za kutamkia
  • Athari/ mwingiliano wa lugha za kigeni
  • Maksudi ya msemaji kulingana na anaozungumza nao
  • Kurithisha lugha isyo snifu kwa mfano kutoka kwa wazazi, walimu, wanasarakas
  • Umri- watoto wadogo hufanya makosa zaidi. Wazee zaidihupoteza uwezo wa kusema
   Zozote 4, alama
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P2 Questions and Answers - Butula Sub-County Post Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest