Kiswahili P3 Questions and Answers - Butula Sub-County Post Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

Maagizo

 1. Jibu maswali manne pekee.
 2. Swali la kwanza ni la LAZIMA.
 3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani: tamthilia, Riwaya, hadithi Fupi, shairi na Fasihi Simulizi.
 4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
 5. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

Kwa matumizi ya Mtahini

SEHEMU

ALAMA

1

 

 

 

 

 

 

 

JUMLA

 MASWALI

SEHEMU A: USHAIRI
SWALI LA LAZIMA

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
  Ulimwengu ulimwengu, ulimwengu naratibu
  Yaliyo kichwani mwangu, nataka kuyatubu
  Wayasome ndu zangu, wa mbali na wa karibu
  Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

  Ulimwengu ni kiwanja, cha wenye raha na tabu
  Wengine wanajikonja, kwa wengine ni adhabu
  Kucha na kutwa twahanja, kutafuta matulubu
  Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

  Ni uwanja wa balaa, aliniusia babu
  Mna mambo yamejaa, ya faraja na kusibu
  Na machache ya kufaa, ila mengi ya udubu
  Cha wenye raha na tabu,ulimwengu ni kiwanja.

  Ni kiwanja cha Amina,Saidi Ali Rajabu
  Wengine kitu hatuna, tunaishia kababu
  Wale wamejaza sana, wanashindwa kuhesabu
  Cha wenye raha na tabu, Ulimwengu ni kiwanja.

  Ni uwanja wa urongo, na kweli pia ajabu
  Kichwa hudanganya shingo, tumbo kiuno chasibu
  Usitumai ubongo, wa nduguyo na swahibu
  Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

  Ni uwanja wa walevi, pombe kwao ni dhahabu
  Mara vile mara hivi, wakilewa majudhubu
  Maneno ya kiujuvi, hujipaka hata shabu
  Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

  Ni kiwanja wenye dini, wamtiio wahabu
  Mashekhe msikitini, humo humfanya muhibu
  Mapadiri kanisani, huvihubiri vitabu
  Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

  Ni uwanja wa malofa, lofa mtu mwenye tabu
  Kusema sana kashifa na moyo kisebusebu
  Tunakaribia kuja, kwa kushindwa kujimudu
  Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.

  Ni uwanja wa faraja, alowajali habibu
  Na wengine sitotaja, msinambe ninagubu
  Ni uwanja wa viroja, vigumu kuvikutubu
  Cha wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
  Maswali
  1. Lipe shairi hili anwani ifaayo. (alama 1)
  2. kwa kutoa mfano, eleza mbinu zozote mbili za lugha zilizotumika katika shairi.(alama 2)
  3. Eleza jinsi uhuru wa mshairi ulivyotumika katika shairi. (alama 2)
  4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi. (alama 4)
  5. Taja na ueleze bahari zozote mbili zilizotumika katika shairi hili.(alama 2)
  6. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
  7. Eleza toni ya shairi hili. (alama 1)
  8. Fafanua dhamira ya mshairi. (alama 2)
  9. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi.(alama2)
   1. Malofa:
   2. Udubu:

SEHEMU B: RIWAYA
CHOZI LA HERI
JIBU
2. “Nyamaza wewe! Nyinnyi ndio mnaoturudisha nyuma miaka yote hii!”

 1. Eleza muktadha wa dondoo (alama 4)
 2. Kwa kurejelea hoja saba, eleza jinsi msemaji alivyorudishwa nyuma (alama 7)
 3. Eleza umuhimu wa msemaji katika riwaya (alama 6)
 4. Eleza toni ya dondoo hili (alama2)
 5. Toa sifa moja ya msemaji katika dondoo hili. (alama1)
  AU

3. Jadili nafasi ya sehemu zifuatazo katika riwaya ya Chozi la Heri:

 1. Hotuba (alama 10)
 2. Uozo katika jamii (alama 10)

SEHEMU C:TAMTHILIA
KIGOGO
JIBU
4. “ Sitaki kazi za uchafu hapa …”

 1. Eleza muktadha wa dondoo (alama 4)
 2. Kwa kurejelea hoja kumi, onyesha jinsi kinaya inajitokeza katika tamthiliya (alama 10)
 3.  Fafanua sifa sita za msemaji (alama 6)
  AU

5.“ Do!Do!Si mameni !Si mameni ! leo kutanyesha mawe!“

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili ( Alama 4)
 2. Fafanua mbinu za lugha zilizotumika katika dondoo hili ( alama 4)
 3. Huku ukitoa mifano jadili hoja sita zinazodhihirisha jinsi mwanamke alivyasawiriwa katikaTamthilia ya Kigogo ( alama 12)

SEHEMU D: HADITHI FUPI
TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
JIBU
(Tulipokutana Tena)
6. “Mnaruka tu hewani kama ndege mkitumia uchawi wenu…
Nani kakuambia upuuzi huo?”

 1. Eleza muktadha wa dondoo (alama 4)
 2. Eleza mbinu moja katika dondoo hii (alama 2)
 3. Dondoa maudhui moja kutoka kwa dondoo hii (alama 2)
 4. Jadili matatizo nane yanayomkumba mhusika Bogoa (alama 8)
 5. Fafanua umuhimu wa mhusika Bogoa katika hadithi (alama 4)
  AU

7. Mame Bakari
“Una nini ? Umeshtuka mwanangu !Unaogopa?Unaogopa nini?”

 1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (al.4)
 2. Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo. (al.2)
 3. Eleza sifa za mrejelewa. (al.6)
 4. Eleza umuhimu wa msemaji. (al.4)
 5. Tambua maudhui yanayojitokeza katika kifungu hiki. (al.1)
 6. Fafanua maudhui katika swali la (e)kwa kurejelea hadithi nzima. (al.3)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI.
8. Soma makala yafwatayo kisha ujibu maswali yafwatayo
Hapo zamani za kale, paloindokea mtu mmoja kwa jina mzee Kata. Mzee Kata alikuwa na wake wawili. Mke wa kwanza aliitwa Neema na wa pili aliitwa Nduli. Kila mmoja wa wake hawa alikuwa na mtoto mmoja. Neema alikuwa na mtoto wa kike kwa jina Majaliwa. Majaliwa alikuwa ameumbwa akaumbika.Uso wake ulihimili macho meupe mfano wa theluji. Meno yake ya juu yalipangika kwa njia ambayo iliyafanya kuacha mwanya ambao ulifanya tabasamu yake kuwa ya mvuto wa sumaki. Urembo wa Majaliwa, kama walivyosema wengi, ungemtoa nyoka yeyote pangoni.
Kwa upande mwingine Kutu, bintiye Nduli, alikuwa mwenye sura mbaya ya kutisha.Uso wake usiopendeza ulimfanya kuonekana kama ajuza wa miaka mia moja! Tabia yake ya ukorofi ilikoleza mvuto wake hasi. Vijana wa kijijini walimfanyia inadi kila mara kwa kumkumbusha kuwa hakufaa kuringa. “Sura kama kiboko”, wangemtania
Tofauti za kiumbo kati ya Majaliwa na Kutu zilizua uhasama mkubwa kati ya ndugu hawa, sikwambii mama zao. Hali hii ilizidishwa Zaidi na nongwa za kila siku zilizotokana na ukewenza. Familia yam zee Kata ikawa medaniya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hali ya mtafaruku iliendelea kuikosesha nyumba yam zee kata amani. Asubuhi moja, Mzee Kata aliamka kama kawaida yake, alijikohoza kama isharaya kutangaza kufika kwake. Daima hakupenda kuzungumza na wakeze asubuhi na mapema. Aliamini kuwa wangemletea nuksi. Kinyume na siku nyingine, mzee Kata hakuitikiwa. Ilibidi kujikaribisha nyumbani mwake. Mara tu alipovuka kizingiti cha kijumba hicho, alitupa macho yake juu yakitanda cha mayoweambapo mke wake alijinyosha twaa kakauka kama ukuni; hanapumzi. Weupe wa macho yake na mapovu yaliyomtoka kinywani yalimhakikishia Mzee Kata kuwa Neema kampungia mkono. Harufu kali ya sumu ilihanikiza hewa kumwarifu kuwa Mzee kata kuwa mkewe kafa kwa kutendwa na mkemwenza
Maisha ya Majaliwa yalichukua mkondo mpya baada ya tanzia hii. Mama wa kambo sasa alipata mwanya wa kumhini majaliwa. Kazi zote za nyumbani aliachiwa yeye.Huku Kutu akiachwa huru kucheza. Majaliwa alipewa chakula hapa; wengine wakila biriani yeye alipewa wali wa kawaida. Mavazi yake yaligeuka matambara.Siku zilivyozidi kusonga ndivyo mateso yalivyoongezeka. Mama wa kambo alizidisha wivu wake kwa majaliwa. Hata Majaliwa alipovunja ungo na wachumba kuja kumposa, mama wa kambo aliwafukuzia mbali. Wenine walihimizwa kumposa Kutu. Wachumba waliochachawa kutaka kumuoa majaliwa wakidai kuwa hawamtaki Kutu kwa sababu ya kiburi chake, walinyeshewa matusi, wakahizinika na kujiendea zao.
Siku moja alitokea kijana mmoja makini .alikuja amavalia gwanda jeusi lililojiinamia kwa uchovu. Viatu alivyovaa vilikuwa vimejichokea kwa kupiga lami. Kofia iliokuwa kichwani pake ilitosha kumhakikishia mama wa kambo kuwa huyu alikuwa fakiri. Mama mtu alikubali mara moja posa ya kijana huyu kwa Majaliwa akijua kuwa angeadhibika. Aliamini amemtokomeza Majaliwa ndani ya lindi la ulitima. Mzee Kata naye hakusita kumwoza Majaliwa kwa kiajana huyu maana aliiona hii kama fursa ya pekee ya kumwepusha vitimbi vya mama wa kambo
Majaliwa aliandamana na mume wake hadi Kijiji cha peponi ambako kijana huyu allishi. Wallingia katika nyumba ya msonge ambamo Majaliwa alitarajia kuanza Maisha ya ndoa. Walitayarisha chajio, wakala na kulala.
Asubuhi, Majaliwa aliamshwa na nyimbo za ndege. Alipofunguamacho, alijikuta kalala ndani mya chumba chenye sakafu ya vigae. Ukuta wa chumba hicho ulikuwa wa rangi wa zari. Mapambo ya dhahabu yalitundkwa ukutani. Kumbe kijana aliyemuoa hakuwa maskini kama ilivyodhaniwa! Alikuwa mwana wa mfalme! Na hili lilikuwa kasri hasa! Majaliwa hakueza kuamini! Alikuwa ameamkia Maisha ambayo hakuwahi yawazia.
Alipoingia sebuleni alimpata mama yake mpenzi, akiwa na tabasamu ya milele usoni. Walikumbatiana kwa shauku kuu. Kumbe kijana huyo alikuwa ametumwa na mamake Majaliwa! Mumewe majaliwa alishuhudia kwa umbali. Machozi ya mama mtu na mwanawe yakilovya vifua vyao na kuyeyusha simanzi na kuyeyusha simanzi iliyokuwa imeyaandama Maisha yao. Tangu siku hiyi, watu hawa wallishi kwa raha mstarehe. Hadithi yangu inaishia hapo.

MASWALI

 1. Taja na utolee mifano mbinu sita za kimtindo zilizotumiwa katika utungo huu (al.3)
 2. Utungo huu unaweza kuainishwa kama ngamo, toa sababu (al.1)
 3. Fafanua umuhimu nne wa formula ya kumalizia katika utungo huu (al. 4)
 4. Taja shughuli moja ya kijamii katika jamii ya utungo huu (al. 1)
 5. Jadili tatizo moja la ukewenza katika utungo huu (al.1)
 6. Taja na ufafanue dhima tano ya utungo huu katika jamii yake (al.5)
 7. Taja mambo mawili ambayo fanani anaweza kutekeleza ili kuufanya utungo huu uwe wa kuvutia Zaidi (al. 1)
 8. Miviga ni nini? (al.1)
 9. Taja hasara tatu za miviga (al.3)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.                        
  1. Swali la Lazima – USHAIRI
   Ulimwengu ni kiwanja
   Changamoto ulimwenguni 1 x 1 = alama 1
  2. Istiara/ jazanda – ulimwengu ni kiwanja
   Msemo – kutwa kuchwa
   Ukinzani/tanakuzi – wenye raha na tabu
   Uhuishaji – Kichwa kudanganya shingo (zozote 2x1 = alama 2)
  3. Inkisari – naratibu – ninaratibu
   Ndu zangu – ndugu zangu.
   Kuboronga lugha – wenye kitu hatuna – wengine hatuna kitu
   Utohozi – shehe – sheikh
   Padre – padre (2x1 = 2)
  4. babu alimshauri kuwa ulimwengu ni uwanja wa balaa ulionjaa mambo ya faraja na kusibu. Pia alisema kuwa kuna machache ya kufaidi na mengi ya kuudhi. Kwa hivyo ulimwengu ni kiwanja kwa walio na raha na walio na taabu. (4x1 = alama 4)
  5.                      
   1. Tarbia – mishororo minne kwa kila ubeti
   2. Mathnawi – vipande viwili kwa kila mshororo
   3. Pindu – sehemu ya mwisho kuanzia ubeti unaofuata.
   4. Ukara – vina vya mwisho vinatirirka na vya kati havitiririki. (2x1 = alama 1)
  6.                      
   1. Mishororo minne kwa kila ubeti
   2. Vipande viwili kwa kila mshororo – ukwapi na utao.
   3. Lina beti tisa.
   4. Vina vya mwisho vinatiririka na vya kati vinabadilika
   5. Lina kibwagizo – che wenye raha na tabu, ulimwengu ni kiwanja.
   6. mizani ni 8,8 kwa kila mshororo
    4x1 = 4
  7. masikitiko (alama 1)
  8. Kufahamisha watu hali ilivyo ulimwenguni. Kwamba kuna mazuri na mabaya ili wajihadhari. (1x2= 2)
   1. Malofa – maskini
   2. Ndubu – upumbavu (alama 2)
 2.                                    
  1. Msemaji- Kijana mwenye fulana iliyoandikwa ’Hitman’ mgongoni
   Msemewa- Mmoja wa wasafiri/kiongozi aliyekuwa ndani ya gari/Mbwenyenye ndani ya gari
   Mahali- Barabarani
   Kiini- Hasira kutokana na uhaba wa kazi hata baada ya kuhitimu
   4x1
   TANBIHI: Hakuna mhusika anayeitwa Hitman
  2.                                    
   1. Vishahada vya vyuo haviwasaidii kupata ajira k.m mate yawakauka vinywani wakifunga bahasha za kutafuta kazi.
   2. Wanafunzwa kukariri nadharia bila kuwazia umilisi, stadi,kufungiwa njuga za kujitegemea
   3. Mtu anapata digrii tatu na kula lami kwa miaka kumi
   4. Kukosa mtaji wa kuanzisha biashara – ujasiriamali
   5. Unyakuzi wa ardhi
   6. Tume za kuchunguza kashfa za unyakuzi wa ardhi hazitoi ripoti baada ya uchunguzi-ripoti zinakuwa Rafiki wa rafu makavazini.
   7. Unafiki wa viongozi wanaojifanya kuwahurumia vijana- kumbe ni machozi ya mamba
   8. Kuhongwa kwa vijana wakati wa kura- kuhadaiwa kwa vihela vya kushikilia uhai
   9. Njama za kifisadi -kudanganywa kwa ajuza wazee kutia alama ya makasi kwenye kura kuonyesha hamtaki kiongozi na hivyo kumpigia kura pasi na kujua
   10. Uwezo wa kuzalisha mali haupo nchini
   11. Ukabila- k.m katika hazina ya vijana
   12. Unasaba-k.m katika hazina ya vijana  7x1
    Za kwanza saba
  3.                            
   1. Mwenye hasira k.m ‘”nyamaza wewe!”
    Lazima atoe mfano, la sivyo apewe nusu alama
    1x1
  4. Uchungu/huzuni/masikitiko/majonzi   2x1
  5. Kupitia kwake tunapata kujua kuhusu:
   1. Hadaa za viongozi kuhusu ajira
   2. Udanganyifu wa viongozi wakati wa kupiga kura
   3. Upungufu/ sera mbovu ya elimu chuoni
   4. Ufisadi katika miradi ya kusaidia vijana-ukabila na unasaba
   5. Ukosefu wa kazi
    Anaendeleza maudhui yafuatayo:
   6. Elimu
   7. Kutamauka
   8. Ukatili (mauaji)
   9. Unyakuzi wa ardhi
   10. Uharibifu wa mali (kuchoma magari) 6x1
    Mwalimu akadirie hoja za mwanafunzi
 3. Jadili nafasi ya sehemu zifuatazo katika riwaya ya Chozi la Hari:
  1. Hotuba (alama 10)
   Hotuba ni maelezo maalumu yanayotolewa na mtu mmoja mbele ya watu. Pia huitwa hutuba. Mwandishi wa riwaya hii ametumia hutuba kwa ustadi mkuu kupitisha ujumbe mbalimbali. Hotuba hizi ni:
   1. Hotuba ya Racheal Apondi kwa maafisa waliohudhuria warsha kuhusu jukumu la vikosivya askari katika kudumisha usalama, amani na maridhiano nchini (uk 112- 113). Katika hotuba hii, Racheal Apondi anasisitiza kuwa:
    Suala la usalama haliwezi tena kupuuzwa. Usalama umekuwa moja wapoyamahitajiyakibinadamu.
    Anasema kuwa bila usalama, binadamu hawezi hata kushiriki katika shughuli za kuzalisha mali, hivyo hata mahitaji yake mengine ya kimsingi kama vile chakula, malazi na makazi haya wezi kukidhiwa.
    Kila binadamu ana jukumu la kudumisha amani na usalama.
    Wafanyakazi wa umma, hasa polisi na wanajeshi wana jukumu kubwa zaidi la kudumisha usalama na amani.
    Kila mmoja wetu anastahili kuhakikisha kuwa ameepuka vitendo vya kihalifu.
    Ni vyema mtu kuwaangaza wahalifu wakati wote.
    Vikosi vya polisi na wanajeshi vimefunzwa maarifa ya kukabiliana na kadhia za Jinai na upelelezi. (4×1= 4)
   2. Hotuba ya Lunga Kiriri- Kangata kwa walimu na wanafunzi gwarideni (uk 68-69). Hotuba hiii lisisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazingira. Anasisitiza kuwa:
    Suala la uhifadhi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu.
    Misitu ilikuwa imevamiwa na viongozi wenye mate yafisi.
    Baadhi ya vinara wa taasisi mbalimbali za umma wamewaacha Wanyama kama mayatima kwa kuwap okama kazi yao.
    Maelfu ya maekari ya misitu yamefyekwa na kujengwa viwanda.
    Badala ya mibamba kofi na miti mingine inayosafisha hewa, micha iimetwaa nafasi yake.
    Wanaohusika na matendo haya wanapoulizwa hudai kuwa michaisia duiya mazingira!
    Wengine wanasema kuwa misitu haina budi kukatwa ili kupanda mimea inayotoa chakula, kwani jamii lazima ijitosheleze kwa chakula.
    La kuhuzunisha ni kwamba hawa hawa wanaosema hivyo ndio wanaokita majengo ya kifahari katika sehemu ambazo zinastahili kutengewa upanzi wa chakula!
    Wengine wamediriki kunyakua hata madhabahu kwenye Mlima wa Nasibu ili kujenga hoteli kubwa za kitalii.
    Wazee wetu hata hawana mahali pa kuchomea kafara!
    Tuna kata miti bila kupanda smingine.
    Hata mabustani ya maua tunashindwa kuyastawisha.
    Tukiendelea kuharibu mazingira sehemu yetu itazidi kuwa jangwa. (2×1= 2)
   3. Hotuba ya Umu katika hoteli ya Majaliwa siku ya key akuzaliwa.
    Umu ana washuku Mwangeka na Apondi kwa kuwa wazazi wake wema.
    Ana washukuru kwa kumsomesha.
    Anawashukuru kwa kumsaidia Dick kujiendeleza kimasomo.
    Mwangeka na Apondi wanamshukuru Umu kwa kuwapa furaha.
    Apondi anamshukuru kwa kumlea mdogo wao kwa maadili bora. (2×1= 2)
   4. Hotuba ya Dick katika hoteli ya Majaliwa siku ya kuzaliwakwaUmu.
    Dick anamshukuru Umu kwa msaada wake na ahadi ya kumlea.
    Anamkumbusha siku walipokutana katika uwanja wa ndege na ilivyokuwa muhimu kwake.
    Anamshukuru Umu kwa kumwelekeza kwa wazazi wao wale.
    Anawashukuru Apondi, Mwangeka na wanawe kwa ushauri wanaompa. (2×1= 2)
    Mtahiniwa ataje hotuba kisha aeleze masuala muhimu yanayoibuliwa na kila moja.
  2. Uozo katika jamii (alama 10)
   • Uozo ni hali ya kuzorota na kutozingatiwa tena kwa maadili mema katika jamii. Ni hali ambapo mila zote na desturi njema huvurugwa na wanajamii wanaofanya mambo yaliyo kinyume na hali hali si yamaisha. Mwandishi amejadili suala hili kwa undani kama ifuatavyo;
   • Jamii inaendeleza ubakaji. Genge la mabarobaro watano lilifululiza hadi walipokuwa maskini Lime naMwanaheri na kuwabaka mbele ya baba yao (uk 25).
   • Kuna ulanguzi wa dawa za kulevya. Dick alipotoroshwana Sauna alipelekwa kwa Tajiri mmoja aliyemwingiza katika kusafirisha dawa za kulevya kutoka nchi moja hadi nyingine (uk 119- 120).
   • Wanajamii wanaendeleza uporaji na wizi wa mali. Vijana wana wavamia watu, kuwaua na kupora katika maduka ya kihindi, kiarabu naya wa afrika wenzao.
   • Jamiii naendeleza ufuska/ ukahaba. Sauna aliiba Watoto na kuwapeleka kwa mama mmoja aliyewatumia kwa biashara yanipe ni kupe (uk 84).
   • Biashara haramu inaendelezwa. Bi. Kangara alifanya biashara ya kuwa uza Watoto na vijana- Safari yake ilipata mkondo mwingine baada ya polisi kupata fununu kuhusu njama ambazo yeye na Bi. Kangara walikuwa wakiendesha. Mabibi hawa walikuwa na mtandao ambao kazi yake ilikuwa kuwauza Watoto na vijana (uk 84).
   • Kuna tatizo la mimba za mapema. Vijana wana mazoea ya kukumbatia mtafaruku wa kuhisia unaowapatana mara hujipata wameambulia ujauzito kama alivyofanya Zohali (uk 98).
   • Baadhi ya wanajamii wanaendeleza uavyaji mimba. Sauna alijaribu awezavyo kuavya mimba na mwishowe, baada ya kushindwa, anaamua kujiua.
   • Kukiuka maadili ya kikazi. Fumba (mwalimu) anakiuka maadili ya kazina kujihusisha kwa mapenzi na mwanafunzi wake, Rehema, na hatimaye kumpachika ujauzito (uk 102).
   • Wazazi wana wabaka wana wao. Babake Sauna anafanya mapenzi na mwanawe kila apatapo nafasi, na mwishowe, Sauna anapata mimba.
   • Starehe na anasa kwa vijana. Vijana wa vyuo vikuu wameshindwa kutofautisha usiku na mchana. Tindi anasahau kumrejesha Lemi nyumbani kutokana na muziki (uk 121).
   • Wazazi wanakwepa malezi na kuwatupa wanao wakiwa wachanga. Neema anampeleka mtoto aliyemwokota kwapolisi (uk 162).
   • Vijana kuwaiga wazee. Mwangemi na Mwangeka walikuwa na tabia mbovu yakumuiga babu yao (uk 186).
    (10×1= 10)
    Mtahiniwa afafanue kwa mifano kutoka katika riwaya
 4.                              
  1.                      
   • Msemaji- Majoka
   • Msemewa- Ashua
   • Mahali- Ofisini kwa Majoka
   • Kiini- Baada ya Ashua kuoimba msaada kwa sababu wanawe walilala njaa
    4x1
  2.                                                    
   1. Soko ni chafu-maji ya povu kwenye mtaro
   2. Anamtaka Ashua mapenzi ilhali ana mke. Huu ni uchafu wa kimaadili.
   3. Wanafunzi wa Majoka and Majoka Academy hawafuzu- kuwa makabeji kutokana na sumu ya nyoka
   4. Ngurumo kuzikwa juu ya maiti wengine
   5. Kenga kumsaliti Majoka
   6. Majoka kuwakuta watu achache kwenye lango la soko
   7. Akina Kombe na Boza kupewa makombo ya keki ilhali wao ndio wanazalisha (rasilimali inatumiwa kwingine)
   8. Kulipa kodi na kitu juu yake
   9. Majoka anaamrisha mauaji ya Jabali na raia wengine ( mikono yake ni michafu-ina damu)
   10. Mamapima kupewa kibali cha kuuza pombe haramu
    10x1
    Mwalimu akadirie kazi ya mwanafunzi
  3.                              
   1. Katili
   2. Mkware
   3. Mwenye tamaa-mali
   4. Mwenye dharau- zebe wako
   5. Mpyoro
   6. Mbinasfi
   7. Mfisadi 6x1
    Lazima mwanafunzi aeleze ndiposa apewe alama kamili.
    Mwalimu akadirie kazi ya mwanafunzi
 5. Ni maneno yaNgurumo
  Anawaambia walevi wenzake
  Wako Mangweni kwa Mamapima/Asiya
  Anayasema maneno haya anapowaonaTunu na Sudi kwa mamapima ,jambo ambalo halikuwa la kawaida. (al 4)
  1. Nidaa- Do! Do ! Do!
   Takriri- Simameni! Simameni! Simameni!
   Jazanda - Kutanyesha mawe(al 4)
  2.                          
   • Mteteziwahaki-Tununa Asha wanatetea haki za Wanasagamoyo
   • Jasiri- Tunu anamkabili Majoka bila uoga
   • Msomi- Tunu anasomea uanasheria
   • Ashua amesomea ualimu
   • Chombo cha burundani/ Kustareheka- Majoka anapomwona Ashua akiingia ofisini mwake anaona kuwa amerudi kwake kuonja asali.
   • Mbeya- Ashua anamkejeli Husda kuwa ana sifa ya umbeya iwe hadharani ama faraghani.
   • Mzalendo- Tunu analipenda jimbo anapopigania mabadiliko yatakayowafaa Wanasagamoyo .
   • Mwasherati/ Asherati- Asiya ana uhusiano wakimapenzi na Ngurumo ilhali yeye ni mke wa Boza.
   • Pia anahusishwa na Keki za Uroda.
   • Mpenda anasa na starehe- Husda hupenda kwenda kwenye hoteli ya kifahari kujivinjari.
   • Mpyoro/mwenye matusi- Husda anamtusi Ashua kwa kumwita hawara, kidudu mtu na mbeya.
    Mwenye msimamo dabiti
    (zozote 12X1=12)
    (Tulipokutana Tena)
 6.                            
  1. Msemaji- Kazu
   Msemewa- Msimulizi/ Sebu
   Mahali- Rombeko Hotel/Hotelini/Seka
   Kiini- Wanazungumza kuhusu uchawi wa Wamate
   4x1
  2.                        
   1. Tashbihi-Kuruku hewani kama ndege
   2. Balagha- Nani kakuambia upuuzi huo?
    2x1
  3. Uchawi/ Ushirikina
   1x2
  4.                        
   1. Kuchomwa moto viganjani na Bi. Sinai-maandazi yalipoungua
   2. Kufanya kazi nyingi bila hiari yake-kudondoa mchele,kupara samaki, kumenya vitunguu n.k
   3. Kutopelekwa shuleni kwa sababu yeye ni mtoto wa kimaskini
   4. Kunyimwa uhuru wa kucheza na Watoto wenzake
   5. Kupigwa vibaya na Bi. Sinai
   6. Matusi kutoka kwa Bi. Sinai
   7. Kutopewa muda wa kusema na mzazi wake ilia toe dukuduku lake
   8. Kula makombo ya chakula
   9. Kula mwisho
   10. Kula kwenye vyungu na sufuria
   11. Kutishiwa kukatwa ulimi na Bi. Sinai
    1x8
  5. Anaendeleza maudhui yafuatayo:
   1. Dhuluma kwa Watoto
   2. Ulezi
   3. Ukatili
   4. Utelekezwaji-wazazi wake kumpatiana kwa Bi. Sinai
   5. Ni kielelezo cha Watoto wanaoteswa na wazazi walezi
   6. Ametumiwa kutujuza hulka/sifa za Bi. Sinai
   7. Ni kielelezo cha vijana wanojikwamua kutoka kwa shida /minyororo ya utumwa na kujenga Maisha yao upya
    1x4
    Mwalimu akadirie kazi ya mwanafunzi
 7.      
  1.                                                  
   1. Msemaji ni Babake sara.
   2. Akimwambia sara.
   3. Walikuwa hospitali katika chumba cha daktari.
   4. Alikuwa ameenda kufanyiwa vya ujauzito na Belewa, alipowakuta wazaziwe ivv) wakisubiri katika chumba hicho.
    (4x1=4)
  2. Mbinu za lugha .
   1. swali la balagha unanini?
   2. takriri unaogopa. Zozote (2x1=2)
  3. Mrejelewa sara.
   • Mpenda masomo.
   • mwoga.
   • mwenye mapenzi ya dhati.
   • mwenye busara anamua kujiua sio suluhisho.
   • mwenye utu hakutaka kuavya mimba.
   • Msiri
   • Mvumilivu
   • Msamehevu.
   • mwenye madili
   • mwenye majuto Zozote 6 x 1= 6)
  4. BABAKE SARA.
   • Kupitia kwake tunapata athari ya ukali kupita kiasi wa wazazi kwa wanao.
   • Nikielelezo cha wazazi ambao wako tayari kubadili msimamo wao mkali kwa watoto wao.
   • Anaonyesha umuhimu wa wazazi kushirikiana katika maelezi.
   • Anaonyesha umuhimu wa kuweka siri katika masuala tata ya familia.
   • Ni kielelezo cha wazazi wanaouenzi utamaduni wa jamii yake.
    (4x1=4)
  5. Malezi /mapenzi
   1. Malezi – babake sora anakuwa mkali kwa sora.
    Babake sora anabadilika na kumwonyesha mapenzi, anamsaidia.
    Mapenzi – kuna mapenzi ya dhati kati ya sara na salina.
    Salina anamsaidia sara anapokuwa mjamzito.
    Salina aidha anamsaidia sara kuweka siri ya ujamzito na kufanyiwa vipimo na mipango ya kujifungua.
    ( 3x1=3.)
 8.                        
  1. MBINU ZA KIMTINDO
   1. Tashbihi -Sura kama kiboko
   2. msemo/nahau -Kumtoa nyoka pangoni
   3. Nidaa- Ajuza wa miaka mia moja
   4. Taswira mnuso- Harufu
   5. Usimulizi- Hapo zamani za kale
   6. Istiara- Mavazi kugeuka matambara
   7. Majazi-Neema, Majaliwa, Nduli
   8. Tashhisi- harufu kumwarifu
    ( 1/2x6= alama 3)
  2.                            
   1. kuna formula ya ufunguzi- hapo zamani za kale
   2. kuna formula ya kumalizia- Hadithi yangu inaishia hapo (1x1=alama 1)
  3. UMUHIMU WA FOMULA YA KUMALIZIA
   1. Kurudisha wasikizaji kwa hali ya kawaida
   2. Kubeba wazo au maudhui au ujumbe wa hadithi
   3. Onyesha mwisho wa hadithi
   4. Pahsa mtambali anayefuata. Pisha shughuli inayofuata
   5. Kitulizo kwa hadhira baada ya kumakinika kwa muda
   6. Kutoa changamotomkwa hadhira.
    (4x1=alama 4)
  4. SHUGHULI ZA KIJAMII
   1. Ndoa- Wake wawili, Nduli kukosa kupashashwa, Majaliwa kuolewa
    1x1= alama 1
  5. MATATIZO YA UKEWENZA
   1. Wivu- mamake majaliwa kupewa sumu
   2. Mateso kwa wana wa wake wenza- majaliwa kuteswa na mamake Nduli
    (1x1= alama 1)
  6. DHIMA YA UTUNGO
   1. Huelimisha
   2. Huburudisha
   3. Huadilisha
   4. Hukuza utamaduni
   5. huleta utangamano
   6. Hukuza ubunifu
   7. Hukuza uwezo wa kukumbusha
   8. Hutoa onyo
   9. Ni kitambulisho cha jamii
   10. Hukuza ujasiri
   11. Hukuza historia
    (5x1=alama 5)
    mwanafunzi atoe maelezo Zaidi ndiposa apewe
  7. MAMBO YA KUFANYA HADITHI KUVUTIA
   1. Kutumia Ishara kama miondoko
   2. Kutumia ala za muziki
   3. kutumia maleba
   4. Kushirikisha hadhira
   5. kuimba
   6. Kucheka
    (2x1/2=alama 1)
  8. MIVIGA- sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi au wakati maalumu wa mwaka (1x1=alama 1)
   1. HASARA ZA MIVIGA
   2. Zingine zimepitwa na wakati kama vile tohara ya wanawake. Huhatarisha Maisha ya waathiriwa
   3. Zingine hukinzana na malengo ya taifa kama vile ukeketaji wa Watoto wa kike
   4. Zingine hujaza watu hofu kama zile zinazotumia kafara ya binadamu
   5. zingine huleta uhasama kati ya koo hasa zile za kufukuza mapepo
   6. Zingine ni ghali kwani huhitaji fedha nyingi na kusababisha umaskini
    (3x1=alama 3)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P3 Questions and Answers - Butula Sub-County Post Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest