Kiswahili P3 Questions and Answers - Momaliche 4 cycle Post Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Jibu maswali manne pekee
  2. Swali la kwanza ni la lazima
  3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani Riwaya, Hadithi fupi, Tamthilia, Ushairi na Fasihi simulizi.
  4. usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja

Swali

Upeo

Alama

1

20

 

 

20

 

 

20

 

 

20

 

Jumla

80

 



MASWALI

  1. “La, Mzee…. Mbio za sakafuni zimefika ukingoni” (al 4)
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili
    2. Mbio zipi zimefika ukingoni? (al 4)
    3. Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo lenyewe. (al 4)
    4. Taja mbinu za lugha zinazojitokeza hapa. (al 4)
  2. CHOZI LA HERI
    Matatizo mengi yanayowakumba wahusika wengi katika riwaya hii ni mwiba wa kujdunga. Jadili. (al 20)
  3. “Hili lilimtia………………..uchungu, akajiona kama aliyedhalilishwa na mwanamke.”
    1. yaweke maneno haya katika muktadha wake. (al 4)
    2. Taja suala linalodokezwa katika dondoo hili. (al.1)
    3. kwa kutumia hoja kumi na tano, eleza namna suala ulilolitaja hapo juu(b) llinavyojitokeza katika Riwaya. (al.15)
  4. HADITHI FUPI
    SHIBE INATUMALIZA:
    “Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tunakula”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
    2. Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika (al 2)
    3. Eleza umuhimu wa mnenaji. (al 4)
    4. “Lakini nakwambia, kula kunatumaliza”. Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli hii. (al 10)
  5. Huku ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza namna unyanyasaji umeshughulikiwa. (al 20).
    1. Tumbo lisiloshiba
    2. Shibe inatumaliza
    3. Mame Bakari
    4. Kidege
    5. Tulipokutana tena
  6. Soma shairi hili kisha ujibu maswali
    Naingia ukumbuni,nyote kuwakariria
    Ushairi niwapeni, hoja nitawaachia
    Mnipe masikioni, shike nachoelezea,
    Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

    Naaanza kwa usalendo, nchi yetu tuipende,
    Yadhihirishe matendo, nchi yetu tuilinde,
    Wa kila mtu muwendo, usije kawa mpinde,
    Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

    Wote tuwe na umoja, tuuache ukabila,
    Kabila lisiwe hoja, mwenza kunyima hela,
    Taifa letu ni moja, Mkenya ndilo kabla,
    Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

    Linda demokrasia, uongozi tushiriki,
    Haki kujielezea, wachotaka na hutaki,
    Change naweza tetea, demokrasia haki,
    Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili 

    Tena adili usawa, mgao rasilimali,
    Bajeti inapogawa, isawazishe ratili,
    Idara zilizoundwa, faidi kila mahali,
    Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

    Tuwe na uadilifu, twache tamaa ya hongo,
    Tusiwe na uadilifu, wa kuwa watu waongo,
    Tukomeshe uhalifu, kisha tuache maringo,
    Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

    Ubinafsi si adili, ila ni kusaidiya,
    Ukiwa nayo maali, asiyenacho patiya,
    Kama mtu mswahili, ubinafsi achiya,
    Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

    Na invyoelezea, katiba ni kielezi,
    Tutii kwa mazoea, hadi kijacho kizazi,
    Kwa hayo nitawachia, hiyo ya ziada kazi,
    Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
    Maswali.

    1. Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu (al 2)
    2.                    
      1. Onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili (al 2)
      2. Bainisha umuhimu wa uhuru wa kishairi uliotaja hapo juu (i) (al 2)
    3. Bainisha kipengele kifuatacho cha kimtindo katika shairi hili (al 1)
      Usambamba
    4. Eleza toni ya shairi hili. (al 1)
    5. Bainisha nafsineni katika shairi hili (al 1)
    6. Ainisha shairi hili kulingana na:-
      1. Mpangilio wa vina
      2. Idadi ya vipande katika ubeti (al 2)
    7. Changanua muundo wa ubeti wa nne. (al 3)
    8. Eleza aina mbili za urudiaji katika shairi hili (al 2)
    9. Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari. (al 4)
  7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

    Hukuja hapa kwa wingi,
    Vitimbi vya kila namna,
    Kunambia nikuruzuku,
    Kimwana awe mwenzio,
    Hukumtwaa mwanangu,
    Kisema mno walavu,
    Vipi wangeuza ngoma,
    Mapepo wampigia?

    Siwe uloandaa,
    Harusi ya kukata na shoka,
    Masafu ya magari, yakilalama jua kali,
    Hadi kanisani kungia, mimbari wa kusimama,
    Kasema utamuenzi, hadi yenu mauko?
    Vipi jicho lageukia, mitaani vipaa mwitu? 

    Hukunabia we fidhuli,
    Mwanangu utamtunza?
    Taandamana naye daima,
    Ja chanda na pete?
    Hukumwonjesha tamu, ya ulaghai huyuno?
    Midisko wampleka, kizingizia mapenzi,
    Vipi wamtezea shere, mwangu kumliza?

    Lini taacha dhuluma hizino humfanyiazo,
    Tuchukua lini majukumu,
    Ya kumlea na vifaranga?
    Huachi kulia u waya
    Wanao kitelekeza
    Nadhiri zako za nitakipu promise,
    Zi wapi mwana balaa?

    Lini tafumbua maozi, uone huyu nduli,
    Alotwala wengi wapendi,
    Kwa jicho la nje kuwangia,
    Imeanguka miamba mingapi, nayo ngangania kufia dodani,
    Zinduka mwana zinduka,
    Ailayo waangamiza.
    Maswali

    1.  Hili ni shairi huru. Thibitisha. (al 2)
    2. Mwandishi anaibusha masuala kadhaa ya kijamii. Yadokeze (al 2)
    3. Bainisha nafsineni katika shairi hili (al 1)
    4. Eleza toni ya utungo huu. (al 1)
    5. Bainisha matumizi ya: -
      • Mistari mishata
      • Mistari kifu
    6. Eleza kwa kutoa mifano mbinu za kifasihi zilizotumika katika ushairi huu.(al 3)
    7. Eleza vile mshairi alivyotumia idhini ya kishairi katika utungo huu. (al 3)
    8. Bainisha umuhimu wa maswali ya balagha yaliyotumika katika ushairi huu.(al 2)
    9. Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi. (al 4)
      FASIHI SIMULIZI
      Soma maagizo yafuatayo kisha ujibu maswali
      (Alfajiri kuu. Vijana wanazunguka kinu, vifua wazi. Nyusoni wamepakwa masizi na aina ya tope jeupe. Wako katikati yam situ. Mzee Jando ameketi kwenye namna yam to wa nyasi.)
      Mzee Jando: (Akiwahiza) haraka! Ongezeni kasi! Zunguka! Haya imbeni, barobaro!
      Vijana: jua lachomoza!
      Muda umefika wa mbegu kuatika!
      Ichipuke na kuzalisha matunda!
      Ni leo, ni sasa!
      Mzee Jando: haya ketini sasa
      Vijana: (Vijana wanaketi katika mistari huku wameshikana mikono mabegani)
      Mzee Jando: tulisema mume nini?
      Vijana: (kwa pamoja na kwa sauti ya dhati)
      Mume ni kazi
      Sio ubazazi
      Ale jasho lake!
      Mzee Jando: Sawa kabisa, je mume ni nani?
      Vijana: Ni mlinzi wa jamii
      Ni mfano mwema wa jitihada
      Apambane na adui
      Atende wajibu na maadili
      Mzee Jando: Jambo linalovunja umoja!
      Vijana: Likumbatiwe na kufunzwa hata watoto wachanga!
      Mzee Jando: Haya, semeni wenyewe leo!
      Vijana: Leo tumkomaa, si watoto tena
      Tumetimia barobaro kamili
      Sisi ni stadi
      Sisi ni wapevu!
      Tayari kwa majukumu ya kujenga jamii
      Sisi ni tegemeo la umma
      Sisi ndio chimbuko la wema
      Maadili na upendo
      Mzee Jando: Nakubali mko tayari. Haya tuendelee na ada zetu zingine. Kijembe kukidhihaki!
      Vijana: (Wanasimama kijasiri na kurindimisha sauti) Tuko tayari
      kuingia utuuzima!
  8.                          
    1. Bainisha kipera cha maigizo kinachorelelewa. Thibitisha jibu lako kwa mifano mine. ( al 5)
    2. Fafanua matarajio sita ya utuuzima kwa mujibu wa maigizo haya. (al 6)
    3. Eleza mbinu nne za sanaa ambazo waigizaji wamezitumia katika kuwasilisha maigizo haya. (al 4)
    4. Unanuia kukusanya data kuhusu kupera hiki, fafanua mbinu sita utakazotumia kukusanyia data huku ukionyesha sababu za utenzi wako.(al 5)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. “La, la Mzee …mbio za sakafuni zimefika ukingoni”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4)
      1. Maneno ya Kenga
      2. Anamwambia Majoka
      3. Nje ya lango la soko la Chapakazi
      4. Baada ya Majoka kulalamika kuwa Kenga alikuwa ameshindwa kazi kwa kuwakubali wapinzani kufika pale sokoni.
    2. Mbio zipi zimefika ukingoni? (al 8)
      • Mbio za kusalia uongozini na kuendelea kuwanyanyasa raia wa Sagamoyo ndizo zimefikia kikomo. Wananchi sasa wameamka kudai haki zao bila hofu.
      • Wafuasi wa Majoka wamemgeuka hadi watu wake wa karibu. Tunaona Kenga, mshauri wake wa karibu akiamua kukubali kushindwa.
      • Vilevile Kingi ambaye ni kiongozi wa Polisi amekataa kutii amri ya Majoka ya kutaka awapige risasi watu waliokuwa wakimshangilia Tunu. Hii inaashiria kuanguka kwa utawala wa Majoka.
      • Matumizi ya sumu ya nyoka – mbinu mbaya na dhalimu za Majoka zinafikia ukingoni.
      • Kuendelea kunyanyaswa na vigogo kama Kenga na Majoka kunafikia mwisho
      • Soko kufungwa ili apate ardhi ya kujenga hoteli.
    3. Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo lenyewe. (al. 4)
      • Maudhui ya mabadiliko na mapinduzi: Uongozi umebadilishwa. Ingawa Majoka ni kiongozi aliyeachaguliwa na Wanasagamoyo, anapowatusi na kuwaita raia wasaliti, watu wanaotaka kumpiga wanaanza kumjongelea; ishara ya kuzinduka. Kenga, Chopi na Hudsa wanamzunguka na kumtoa jukwaani. Mapinduzi ya kuporomoka kwa utawala dhalimu yanatokea.
      • Maudhui ya Ustaliti: Kenga, mshauri mkuu wa Majoka anawasaliti Wanasagamoyo. Kenga anampa Majoka ushauri mbaya wa kufunga soko la Chapakazi. Hata hivyo anapoona mambo yameharibika anamsaliti Majoka na kujiunga na wanaharakati.
      • Uongozi mbaya wa vigogo kama Majoka unafika mwishso.
      • Ubinafsi katika kumiliki raslimali ya umma unafika mwisho.
      • Kutoa hongo kwa vigogo kunafika mwisho.
    4. Taja mbinu za lugha zinazojitokeza hapa? (al. 4)
      • Mdokezo: kuna alama za dukuduku zinazoonyesha kwamba yapo maneno yaliyosalia.
      • Taswira: msomaji anapata taswira ya namna utawala wa Majoka unavyoanguka.
      • Jazanda: mbio zinaweza kuashiria mikakati ya majoka kusalia madarakani.
      • Methali: mbio za sakafuni huishia ukingoni. Methali madarakani imefikia ukomo.
  2. CHOZI LA HERI
    Matatizo mengi yanayowakumba wahusika wengi katika riwaya hii ni mwiba wa kujidunga. Thibitisha. (al 20)
    • RIWAYA
      • Wahusika katika riwaya ya Chozi la Heri wanakumbwa na matatizo mbalimbali. Matatizo hayo ni ya kiuchumi na kijamii.
      • Vyanzo vya matatizo yenyewe ni tofauti, kuna yale yanasababishwa na wahusika wenyewe ilhali mengine yanaletwa na watu wengine.
      • Tunaweza kusema kuwa matatizo mengine ni mwiba wa kujindunga huku mengine yakiwa ya kudungwa na wengine.
        1. Jumba moja la Ridhaa linabomolewa kwa kuwa alilijenga katika ardhi iliyotengewa ujenzi wa barabara katika mtaa wa zari. Hakuchunguza uhalali.
        2. Terry mkewe Ridhaa anapuuza maonyo na maneno ya mumewe kuhusu mkasa ambao ungetokea hivyo anateketea alipoenda kuwasaidia watu waliokuwa wanateketea.
        3. Ami wamwangeka anaagamia katika mkasa wa moto alipoenda kuwasaidia wastu waliokuwa wanateketea.
        4. Walioteketea katika moto wa lori walijiigiza matatani wenyewe kwani walikuwa wameonywa kulikuwa na hatari.
        5. Uhasama, migorogo na ukosefu wa mahitaji muhimu unaoikumba familia ya Mwimo Msubili hii ni kwa sababu ya yeye kuwaoa wake wengi.
        6. Kufutwa kazi kwa Lunga Kangata Kiriri baada ya kutataa kukubali mahindi ya jano kuuziwa wananchi ni mwiba wa kujidunga.
        7. Mauti yanayokumba vijana waliokuwa wakiandamana baada ya sherehe za kuapishwa kwa kiongozi mpya.
        8. Tendo la Subira kuondoka nyumbani na kumwacha mumewe na watoto ni mwiba wa kujindunga kwa mumewe.
        9. Pete anapokubali kuolewa na Nyangumi bila kufanya uchunguzi wa kina.
        10. Tukio la Zohali kupata mimba na kutumbukia katika mateso mengi
        11. Tendi la Mwangeka na Mwangemi kufanyia babu yao mzaha, kwa kuwa usiku mmoja aliamua kuwalipua viboko.
        12. Kifo cha Lemi chatokana na mapuuzo ya Tindi ya ushauri wa mamao
        13. Pete kujihusisha na ukware na baadaye kupata watoto wengi
        14. Pete kujaribu kuavya mimba na baadaye alazwa hospitali
        15. Mamake Sauna kumwacha Bwana Kero na kuolewa na Bwana Maya ambaye anamdhulumu na kumpiga na kumtusi.
        16. Mwangeka anakubaliana na Tila kuigiza maombolezi ya Dedan Kimathi ambayo yanamfanya babake kumwadhibu kwa kutowajibika.
        17. Kukamatwa kwa Sauna n mwajiri wake Bi. Kangara kwa kujihusisha na Biashara ya ulanguzi wa watoto.
        18. Tuama anaathirika vibaya baada ya kupashwa tohara na kulazwa hospitalini nit endo alilolitenda kinyume na mapenzi ya baba yake.
        19. Walevi wenza wa Shamsi ambao wanapoteza uwezo wa kuona au uhai wao kwa kubugia vileo.
        20. Mumewe Selume anamfukuza mkewe kwa kuwa si wa kabila lake baadaye anamlea mtoto peke yake.
        21. Mandu anapouawa katika vita akiwa ughaibuni ni mwiba kwani huenda hangepoteza maisha kama hangeenda huko mapema.
        22. Fujo zinazosababishwa na uhafidhina baada ya uchaguzi ambapo wanapoteza uhai na mali.
        23. Wakimbizi waliohamia katika msitu wa mamba na kupanda mimea na baadaye kufukuzwa ulikuwa mwiba kwani si halali kulima msituni.
        24. Naomi kumwacha mumewe Lunga Kiriri na watoto na baadaye kuwatafuta baada ya kifo cha bwanake ullikuwa mwiba wa kujindunga.
        25. Mwangeka kujiunga na kikosi cha majeshi licha ya kukatazwa na mkewe na kisha anaporudi anakuta waliangamia motoni 1 x 20 = 20
  3.                  
    1. Maelezo ya mwandishi
      • Anamrejea Bwana Kimbaumbau
      • Ni baada ya Naomi kukataa kushiriki mapenzi naye
      • Wote wawili walikuwa Kazini 1 x 4
    2. Ubabedume/Taasubi ya kiume. 1 x 1
    3.                            
      1. Jamaa za Kangata kupinga elimu ya mabinti zake
      2. Kimbaumbau kumdhulumu Naomi anapokataa kujihusisha kimapenzi naye
      3. Mwimo Msubili kutotaka kukutana na mwanamke asubuhi kwa madai kuwa ni Mkosi
      4. Lime na Mwanaheri kunajisiwa na vijana wahuni
      5. Bwana Maya anamdhulumu mamake Sauna kwa mapigo na matusi aulizapo swali lolote lile.
      6. kuuzwa kwa Pete kwa Fungo ili wazazi wake wapate pesa za kuwaelimisha ndugu zake watano wa kiume.
      7. Pete anabakwa na mlevi anapolewa chakari
      8. Mamake Zohari kuridhia kila asemalo mumewe na kushindwa kumtetea anapopata himila.
      9. Mamake Mwengeke aliwahi kumwonya kulia kama msichana. Hii ni ishara kuwa jamii yamwona mwanamke kama mnyonge.
      10. Mwanzi anakataa kukubali matokeo ya uchaguzi madhali anashindwa na mwanamke, Mwekevu.
      11. Wahafidhina kuamini kwamba mtoto wa kiume ndiye pekee anayestahili kuwa mrithi wa mali ya babake
      12. Ushindi wa Mwekevu unaonekana kama kutoheshimiwa kwa mwanaume.
      13. Mwekevu kusingiziwa wizi wa kura anapomshinda Mwanzi.
      14. Kutishwa, kutusiwa n ahata kutengwa kwa Mwekevu anapojitosa katika siasa zilizoaminiwa kuwa ni za wanaume
      15. Fungo anamharibia Pete maisha anapomwoa kisha kumfukuza anapojifungua mtoto.
      16. Fungo anamharibia Pete maisha anapomwoa kisha kumfukuza anapojifungua mtoto
      17. Mwanamke kuonekana kama mnyonge anayestahili kulia akabiliwapo na vizingiti au changamoto maishani. Mwanaume hafai kulia.
      18. Wanafunzi wa vyuo kufa kutokana na matumizi ya pombe haramu.
      19. Selume kudhulumiwa na mumewe
      20. Sauna kunyanyaswa na babake wa kambo
      21. Kaizari kumtetea mkewe anapodhulumiwa na mama mkwe
        1x15
  4. HADITHI FUPI: Shibe inatumaliza
    1. Mnenaji ni Mbura.
      Mnenewa ni Sasa
      Wakiwa nyumbani kwa mzee Mambo
      Walikuwa wamehudhuria sherehe kwa Mambo bila ualishi katika siku ya kusherehekea siku ya kuingia darasa la chekechea kwa mtoto wa Mzee Mambo na mwingine kutoa vijino viwili. Wanafika shereheni kula, hata hivyo wanakula kilafi mpaka Mbura anaanza kujilaumu pamoja na mwenzake Sasa kwamba wanakula vyovyote wavipatavyo bila kuvichunguza na hata kuvila vya wenzao waliowatuangulia na watakaozaliwa.
      1 x 4
    2. Istiari/Jazanda – Wanakula lakini hawawezi kumaliza kula – wanakula kila leo na bado wanaendelea kula – kuendelea kunyakua mali ya uma
      kutaja = 1
      kufafanua = 1
    3. Umuhimu wa Mbura
      • Ni mfano mzuri wa watu walafi katika jamii
      • Kielelezo cha ubadhirifu wa mali ya umma
      • Ni mfano wa watu walio na mapuuza. Wanafahamu uzembe uliopo miongoni mwa wafanyikazi wa serikali na unyakuzi wa mali ya umma, lakini hawachukui hatua mwafaka
      • Kielelezo cha viongozi wasio ajibika
      • Ni mfano wa watu wanaojitolea kulihudumia taifa lao hata kama wametengwa mbali na hawatambuliwi katika taifa lao.
      • Anaendeleza maudhui ya ufisadi wakiwa na Sasa wanafanya kazi moja.
        1 x 4
    4. “lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza”.
      • Viongozi wa mataifa yanayoendelea kutowajibika katika kazi zao. Wanakubli bidhaa duni kurudidikwa katika mataifa yao: mchele ya basmati.
      • Mali ya umma kunyakuliwa. DJ anafungua duka la dawa zilizotolewa katika bohari ya serikali huku wanyonge wakiteseka.
      • Serikali kuwalipa watu ambao hawafanyi kazi mishahara kubwa hinyo kudhoofisha uchumi wa nchi – Mzee Mambo.
      • Kituo cha Televisheni ya taifa kutumika kupeperusha matangazo ya sherehe ambazo hazina umuhimu wowote katika ujenzi wa taifa.
      • Wananchi wengine badala ya kuchukua hatua mwafaka dhidi ya wanyakuzi, hungojea wakati wao ili nao wanyakue: Sasa na Mbura” …na sisi tuende – tusogee.
      • Viongozi wananyakua mali ya mabilioni kwa hila na hawajali: Mzee Mambo anaandaa sherehe kubwa kwa sababu mtoto wake wa kwanza ameingia shule ya chekechea na yule wa mwisho ameota vijino viwili.
      • Sasa na Mbura kula tena na tena bila kushiba
      • DJ anapata huduma za kimsingi kama vile maji, matibabu na kadhalika kwa vile alijuana na mzee Mambo
      • Magojwa ya sukari, presha, saratani, obesiti kutokana na kula
      • Kunyongana kwa sababu ya kula.
  5. Majibu
    1. Tumbo lisiloshiba
      1. jitu lenye tumbo linakula chakula chote katika mkahawa wa Mzee Mambo bila kuwajali wateja wengine
      2. jitu lenye tumbo linarejelea madongoporomoka na mabuldoza kubomoa vibanda vya wakazi
      3. wanamadongoporomoka wananyanyaswa kisheria kwani hawapati haki kwa kuwapata wanasheria adimu kama haki yenyewe
      4. wakubwa wa jiji wako tayari kuchukua ardhi ya wakazi wa madongoporomoka kwa upanuzi wa jiji bila kujali watakapohamia
    2. Shibe inatumaliza
      • DJ anamiliki duka kubwa la dawa ambalo mtaji wake ni bohari ya dawa za serikali
      • DJ anapata maji, umeme, matibabu na huduma zote za kimsingi za serikali ilhali wanainchi waliojawa na dhiki na ufukara wakizilipia
      • Baadhi ya viongozi kama Mzee Mambo wanapewa mishahara mikubwa na serikali kwa kufika kazini wala sio kwa kufanya kazi huku wananchi wengine wakiishi na ufukara.
      • Viongozi wengine hutumia rasilmali za nchi kwa manufaa yao kibinafsi badala ya kufaidi umma, kama vile Mzee Mambo kutumia vyombo vya habari kupeperusha sherehe aliyoandalia wanawe.
    3. Mama Bakari
      • Sara amabakwa na janadume katili alipokuwa akirudi darasa la ziada “twisheni” na kuhimili
      • Wasichana wa shule wanaambulia ujauzito hufukuzwa shule kulingana na mawazo ya Sara
      • Sara anaona akinyanyaswa na jamaa zake, majirani na wanafunzi wenziwe kwa kutengwa kama mgonjwa wa ukoma.
      • Sara anawaza jinsi babake angemfukuza nyumbani kwa kuwa mjamzito akiwa angali shuleni
      • Majirani wa Sara walimtesa kisaikolojia kwa kumsemasema baada ya kugundua kuwa alikuwa mjamzito.
    4. Kidege
      • Mose ambaye anapinga kuchukuliwa kwa samaki wa kidimbwi cha bustani ya Ilala anajipata akibanwa na mbawa za ndege wawili wakubwa.
      • Samaki wa kidimbwi cha Ilala wanaliwa na ndege wakubwa.
      • Videge vilikuwa vikinyanyaswa na midege kiasi cha kushirikiana ili kuiangamiza.
      • Hii inaonyesha jinsi viongozi wanaotawala katika jamii (midege) huwanyanyasa wananchi walio chini yao (videge)
      • Mose anapoipa midege iliombana chakula ili imwachilie aende zake, midege hiyo inakula chakula lakini haimwachilii huru kamwe
    5. Tulipokutana tena
      • Bogoa anatenganishwa na jamaa zake anapopelekwa kwenda kuishi na Bi. Sinai
      • Bogoa anafanyishwa kazi nyingi na ngumu na Bi. Sinai kama vile kumenya vitunguu, kukuna nazi, kupara samaki na kutoa matumbo na kadhalika.
      • Bogoa ananyanyaswa na Bi. Sinai kwa kuamshwa mapema kuliko wengine ili kuchoma mandazi ya kuuza shuleni.
      • Bogoa ananyimwa elimu na Bi. Sinai
      • Bogoa ananyimwa lishe bora kwa kupewa mabaki
      • Bogoa ananyanyaswa kwa kuchomwa viganja vya mikono anapouguza mandazi aliyokuwa akichoma 5x4
  6. Shairi la kwanza
    1. Tarbia. Lina mishororo mine katika kila ubeti (al 2)
    2.                              
      1. Aina mbili za uhuru wa kishairi
        1. Inkisari – nachoelezea - ninachoelezea
        2. Kuboronga sarufi
          • ya ziada kazi – kazi ya ziada
          • wa kila mtu mwende – mwende wa kila mtu
        3. Tabdila – kusaidiya – kusaidia
          • patiya – patia
          • achiya – achia
        4.  Mazida: maali - mali
          • Muwendo – mwendo 1x2
      2. Umuhimu wa uhuru wa kishairi uliotajwa hapo juu.
        1. Inkisari – kupata urari wa mizani
        2. Kuboronga sarufi – kupata urari wa vina
        3. Kuboronga – kuleta mahadhi katika shairi
        4. Tabdila – kupata urari wa mizani
        5. Mazida – kupata urari wa mizani
          1x2
    3. Usambamba
      1. Taifa sio taifa
      2. Pasi kuwa maadili 1x1
    4. himiza/ nasihi / shawishi = 1x1
    5. mwananchi / raia / mzalendo / mkereketwa =1x1
    6. kuanisha shairi kulingana na:
      1. mpangilio wa vina
        Ukaraguni.
      2. Idadi ya vipande katika ubeti
        Mathnawi 1x2
    7. Muundo wa ubeti wan ne.
      1. Vina vya kati ni ‘a’ na vya nje ni ‘ki’
      2. Mizani ni kumi na sita katika kila mshororo
      3. Vipande ni viwili, ukwapi na tao
      4. Mishororo ni minne
      5. Kibwagizo ni taifa si taifa, pasi kuwa maadili 1x3
    8. Aina mbili za urudiaji
      1. Neno – mf taifa, maadili
      2. Sauti – mf u, a
      3. Silabi – mf nde, a, li, ngo
      4. Sentensi / mshororo – taifa sio taifa, pasi kuwa maadili. 1x2
        1. Ninaanza kwa kuwaelezea kuwa tuwe wazalendo na matendo yetu yaonyeshe tunailinda nchi yetu kwa mienendo mizuri kwa sababu nchi haikamiliki bila kuwa na matendo mema
  7.                          
    1. Shairi la pili Majibu
      1. Hakuna urari wa mishororo katika kila ubeti
      2. idadi ya vipande hailingani katika kila mshororo
      3. Hakuna mpangilio maalum wa vina.
      4. Hakuna urari wa mizani katika kila mshororo 1x2
    2. Masuala yanayoibuliwa na mwandishi.
      1. Dhuluma katika ndoa
      2. Ukosefu wa uaminifu katika ndoa
      3. Kutowajibika kwa waume
      4. Tatizo la ukimwi. 1x2
    3. Nafsineni katika ushairi.
      1. Mtaalam katika masuala ya ndoa;
      2. Mzazi
      3. Mshauri
      4. Mlezi 1x1
    4. Toni ya utungo huu.
      1. Malalamishi
      2. kushauri
      3. Kuzindua
      4. Huzuni, hasira (ghadhabu)
    5. Mistari mishata
      1. Hukuja hapa kwa wingi
      2. Siwe uloandaa.
        • Mistari kifu.
          1. kusema hapa kwa wingi
          2. Huachi kulia u waya
    6. Mbinu za kifasihi
      1. maswali ya balagha
        1. Hakuja hapa kwa wingi?
        2. Vipi wangeuza ngoma, mapepo kunipigia?
        3. Vipi wamtezea shere, mwanangu kumuulizia?
      2. Tashbihi
        Taandama naye daima ja chanda na pete
      3. Utohozi
        • Walavu
        • midisko
        • Nitakipu promisi
      4. Sitiara / jazanda
        • Vipaa mwitu – wasichana wengine
        • Nduli – ugonjwa hatari
        • Kifaranga – watoto
        • Miamba – watu mashuhuri
      5. Kuchanganya ndimi; - nitakipu promise
      6. Tashihisi / uhuishaji
        • Masafu ya magari yakilalama jua kali
        • Vipi jicho lagoukia mitaani vipaa mwitu?
        • Nadhiri zako za nitakipu promisi, zi wapi mwana
      7. Nahau / msemo
        Kufia kidondani – kupata hasara unapofuata kitu unachokiona cha thamani.
        - Kukata na shoka, kucheza shere. 1x3
    7. Idhini ya kishairi iliyotumika.
      1. kuboronga sarufi / kufinyanga sarufi
        • Hadi kanisani kuingia – kuingia hadi kanisani
        • Hadi yenu mauko – hadi mauko yetu
        • Mwanangu kumuliza – kumuliza mwanangu.
      2. Insksari.
        • Kunambia – ukaniambia
        • Wanao – wanawako
        • Tachukua – utachukua
      3. Lahaja
        • Huyuno
        • Mauko
        • Nitakupiku
        • Nduli
        • Maozi
        • Kuwangia
      4. kikale
        • Tezea
        • Huyuno
        • Mauko
        • Nitakupiku
        • Kuwaingia
        • Maozi
      5. Tabdila
        Twala twaa
        Inkisari – taacha 1x3
    8. Umuhimu wa maswali ya balagha
      • Kuleta msisitizo wa ujumbe unaoangaziwa
      • Kumfanyia tashtiti mwanaume kwa yale anayotenda
      • Kumzindua mwanamume aweze kutekeleza majukumu yake ya ndoa =
        1x2
    9. Wewe mjeuri uliniahidi ungemtunza mtoto wangu na ungeishi naye daima mapenzi ya dhati lakini ulimwingiza kwenye mapenzi ya hila kwa kumpeleka disko. Kwa nini unamchezea shere mwanangu kwa kumliza = 1x4
  8. SEHEMU E FASIHI SIMULIZI
    majibu
    1. Kipera – Miviga
      Sifa za miviga
      1. Maleba maalum huvaliwa na wahusika – Vijana vifua wazi. Nyusoni wamepakwa masizi na aina ya tope jeupe
      2. Huongozwa na watu maalum – mzee Jando
      3. Huhusisha vitendo maalum kama kula viapo, kuimba, kushikana mikono
      4. Haundamana na utoaji wa mawaidha – vijana wanafunzwa majukumu yao katika jamii
      5. Mwanajamii anaingizwa katika kundi Fulani kutoka jingine – vijana wanaingizwa utuuzimani.
      6. Hufanywa mahali maalum sherehe hiyo inapofanyika kama katikati yam situ
      7. Hufanywa wakati maalum sherehe hiyo inapofanyika kama alfajiri kuu
      8. Wahusika huweka ahadi za kutenda wema. Vijana wanaahidi kutena kama waume.
      9. Huwa na mpangilio wa shughuli kuanzia mwanzo, kati hadi mwisho. Himizo, mafunzo kisha kijembe. = 1x4
    2.                                    
      1. kufanya kazi na kula jasho lako
      2. Kuwaelisha vijana – Mzee Jando
      3. Ulinzi wa jamii / kupambana na adui
      4. Mfano mwema wa jitihada
      5. Kutenda wajibu na maadili
      6. Kufunza umoja na upendo katika jamii
      7. Ustadi na upevu
      8. Kujenga jamii
      9. Tegemeo la umma
      10. Chimbuko la wema, maadili na upendo 1x6
    3.                                  
      1. Nidhaa / siahi – Haraka! Ongezeni kasi! Zunguka! Haya imbeni, barobaro!
        Kushajiisha vijana.
      2. Jazanda – kijembe kukidhihaki – tohara / ujasiri.
      3. Taswira – picha ya vijana na vitendo katika sherehe ya tohara
      4. Balagha – mume ni nani? Majukumu ya mume yanajulikana katika jamii
      5. Usambamba / takriri muundo – sisi ni stadi
        Sisi ni wapevu
    4.                                
      1. Kusikiliza – mtafiti anaweza kuwasikiliza vijana wakiwa shereheni. Mtafiti atapata ujumbe asilia na halisi kwa sababu atapata kubaini panapotatiwa chuku.
      2. Kushiriki – mtafiti anaweza kujiunga na vijana katika sherehe hii na kujirekodia kuaminika moja kwa moja.
      3. Kurekodi – mtafiti anaweza kutumia vinasasauti, kanda za video, filamu au upigaji picha. Mtafiti hupata habari za kutegemewa na anaweza kuzirejelea baadaye / kumbukumbu
      4. Uchanzaji / kutazama – mtafiti anashuhudia kwa macho mvigha huu unapoendelezwa, Mbinu hii ni bora kwani utendaji hautaathiriwa kwani washiriki hawatajua kuwa wanatazamwa.
      5. Kutumia hojaji – mtafiti anaweza kutayarisha hojaji ambayo ataipelekea mhojiwa ambaye anapaswa kuijaza. Mbinu hii ni bora kwani mtafiti anaweza kuwafikia watoaji wengi wa habari kwa wakati mmoja.
      6. Mahojioano – mtafiti anaweza kukabiliana ana kwa ana na wahusika anaonuia kupata maarifa kutoka kwao.
        Mbinu hii inamwezesha mtafiti kupata ufafanuzi wa papo kwa papo.
        Za kwanza 5x1 = 5 tanbihi, Mtahiniwa atoe mbinu aifafanue kisha atoe sababu ili apate alama moja katika kila hoja.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P3 Questions and Answers - Momaliche 4 cycle Post Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest