Kiswahili P2 Questions and Answers - Momaliche 4 cycle Post Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MASWALI

1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata:
“Hamjambo wananchi nyote? Ni fursa kubwa kwangu kusimama hapa kwa niaba ya wachukuzi , makuli, wakulima, waashi, masonara na wengine wote wanaokandamizwa ili kufahamishana kwamba tumeamua kugoma kuanzia kesho kutwa. Madhila yanayotusakama hayahitaji mtaalamu ili kutuchambulia. Watoto wetu wamebaki nyumbani tangu kufunguliwa kwa shule kwa sababu ya kukosa kutimiza mahitaji ya kimsingi kwa ajili ya masomo yao. Haina haja wazazi kukumbushana kuhusu adha za wenye nyumba kwa sababu ya kulimbikizwa kodi pasi na kujali maslahi ya wapangaji. Si hanikizo la uvundo, si mlundiko wa taka, si majitaka yaliyovavagaa, si ukuukuu wa majengo na rangi zinazoning’inia, si maji ya kubahatisha- ilmradi hali si hali hapa. Malalamishi yetu ama yanaangukia masikio yenye nta au yaliyozibwa kwa komango. Mwisho wa mwezi hawachelewi kunyoosha mkono kudai kodi. Alfajiri unasikia mgongo mlangoni mradi mwezi umeisha; hawajali kwamba hujalipwa na huna kibaba cha kuikimu aila yako. Milungula waliyolishwa wakuu wa kutetea maslahi ya wapangaji katika Wizara ya Nyumba ilifanya kazi yake barabara- hawajali hawabali yote yasemwayo na wenye nyumba. Ni dhahiri kwamba tumetekwa kikamilifu- mbele simba, mgongoni fisi.
Bahati alitongoa hoja zake akisikizwa na wenzake, kisha akaendelea:

‘ Kule mashambani wakulima wanalazimishwa kupeleka mifugo yao kupigwa sindano maalum eti kuzuia magonjwa ambayo hawajaambiwa. Ni wazi kwetu kwamba mifugo wakipigwa sindano watakufa. Hapana anayejua faida ya ng’ombe kupigwa sindano maana ng’ombe wetu wamekuwa wakiumwa na kujiponea bila hiyo chanjo yao. Wanataka wawapige ng’ombe sindano tu, ikiwa watakufa au kupona, si hoja kwao. Tumejifunza kutoka kwa majirani zetu kwamba upigaji ng’ombe sindano umeteketeza ng’ombe. Ni lazima wafugaji wachukue tahadhari kwa jambo kama hili kabla ya kuharibikiwa kabisa. Kumbuka wakati ule walipotaka kujenga uwanja wa ndege waliwafurusha wakulima kutoka kwa ardhi yao na kuvunja nyumba zao. Madai yao yalikuwa kwamba uwanja wa ndege ulikuwa na manufaa ya kiuchumi kwa taifa kuliko harakati za zaraa. Si hoja kwamba wenye ardhi walipewa fidia. Hatujui ndege zinazoruka na kutua zina maslahi gani kwetu kama sio kelele za kuudhi masikio na kubughudhi usingizi wa wanetu?’
Mzee Gae, licha ya umri wake, alitafakari mtimani mwake kuhusu mawazo fyongo ya namna hii yaliyomdondoka Bahati kutoka kinywani bila sumile. Labda kuhusu yale malalamishi ya kwanza kulikuwa na nafuu ya kukubalina nayo lakini haya ya chanjo na uwanja wa ndege yalikuwa na taksiri hasa. Lau yangetoka kinywani mwa mzee kama yeye, msamaha ungeweza kufikiriwa. Mzee hangeweza kutabiri kama miaka iendeleavyo ndivyo binadamu anaimarika au anasambaratika kimawazo. Akiwa angali mawazoni hivi, Simali naye akadakizia usemi wa Bahati kwa hotuba yake fupi. “Heri waache tulime mashamba yetu ndege zibaki hukohuko angani au kule zitokako!’
Stahamala za Mzee Gae zikafika mwisho sasa akaja juu kwa ukakamavu wa ghafla na kuanza…“ Simali unasahau jambo moja. Mgalla muue lakini haki yake usimhini. Angatua unayoikejeli imetufaa si haba. Lile gonjwa sugu lilipolipuka na kuzua taharuki, madaktari na wauguzi walifikishwa hapa haraka kwa ndege kupitia anga hiyo. Vyakula vya msaada kwa walioathirika na njaa iliyozuka miaka mitano iliyopita, vilisafirishwa haraka kwa sababu ya kuwepo kwa muundo msingi huu. Wakati wa mafuriko ya mwaka jana daraja la kutuunganisha na mji mkuu lilisombwa na maji ikawa vigumu kupata mahitaji ya kila siku. Kama sio uwanja huu, nusura yetu ingetoka wapi? Mwanao aliyekuwa mtahini wa mwaka jana hapa petu anaelewa jinsi uwanja huu ulivyomfaa yeye na watahiniwa wenzake vinginevyo karatasi za mtihani zingebaki kuko huko kashani. Mengi yaliyowezeshwa na kuwepo kwa uwanja huu yanaonekana sio nuruni tu bali hata penye giza totoro. Ni kweli kuwa kujengwa kwa uwanja huu kulitatiza malisho na uzalishaji wa mazao ya kilimo lakini kama ilivyo ada shughuli huvunja nyingine. Binadamu yu mbioni kufanya uvumbuzi usiku na mchana ili maisha yake na ya vizazi vya usoni yawe bora zaidi. Anapovumbua kitu bora kuliko kile alichonacho, hana budi kuvunja ili kujenga! Si lazima mbegu izikwe ndipo imee.
‘Ni kweli kuwa amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga. Hata hivyo, amani ijayo kwa njia hii ina gharama kubwa na huwaachia majeraha mengi wahusika kisha makovu yake hudumu milele. Majuto na chuki hukalia viti vya mioyo ya wahusika ya wahusika bila kubanduka. Makuruhu tunayokumbana nayo jinsi Bahati alivyochambua mwanzoni yanadhihirika na kupinga kuwepo kwake ni hujuma kwa jamii yetu. Lakini katika ulimwengu wa sasa, kunazo mbinu mbadala za kuyasuluhisha. Ulimwengu mzima umesheheni visa vya mizozo baina ya jamii mbalimbali lakini wangwana hufanya vikao vya kimataifa kama njia ya kukumbatia umuhimu wa mashauriano mahali pa kushika zana za vita. Kumbuka hata sasa kuna zana bora sana za kivita zilizobuniwa lakini hakuna taifa lililo na haraka ya kuzitumia kero zinapozuka. Mgomo hautasuluhisha migogoro yetu vyema. Heri tung’ang’anie mazungumzo kwa kuwatuma wajumbe wetu kwa wakuu wetu. Hata hivyo, wajumbe wasijihasiri kwa kupinga suala la chanjo ya ng’ombe dhidi ya maradhi ya miguu na midomo ambayo yamefagia mifugo katika taifa jirani. Maneno hayo!
Akatamatisha mzee Gae na kuketi akitazamwa kwa meno na Bahati na Simali na wote waliokuwa pale. Avuliwapo nguo, muungwana huchutama.
Maswali

 1. ' … tumetekwa kikamilifu- mbele simba, mgongoni fisi.` Kwa kuzingatia hali ya wapangaji, rejelea mifano sita kuthibitisha kauli ya ‘fisi mgongoni.’ (alama 6)
  ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
 2.  Andika mawazo manne kwenye makala yanayoonyesha mawazo fyongo. (alama 4)
  ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
 3. Thibitisha kuwa walimwengu wa sasa wametawaliwa na hekima zaidi ya nguvu katika kusuluhisha migogoro. (alama 2)
  ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
 4. Tumia visawe vya maneno yafuatayo katika muktadha wa makala haya: (alama 2)
  1. tumeamidi ………………………………………………………………………………………………………
  2. yaliyovavagaa ......................................................................................................................................
 5. Nomino ‘mgongo’ imetumiwa na msimulizi kuleta maana gani? (alama 1) ………………………………………………………………………………………………………

2. UFUPISHO (Alama 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Bila shaka, umewahi kusikia kuwa afya ni taji. Hakuna ajuaye haya vyema kama anayeugua. Wanaoelewa usemi huu huthamini na kudumisha siha yao kwa kila njia. Licha ya lishe bora, michezo ni muhimu katika kudumisha afya njema. Mtu asiposhiriki katika michezo au unyoshaji wa viungo, mwili hunyong’onyea na kunenepa. Mwili mnyonge ni windo rahisi la maradhi. Kushiriki katika michezo hukuepusha na kutingwa na shughuli za maisha ya kileo. Shughuli hizi zisipodhibitiwa huweza kumdhuru mtu kiafya.
Maradhi hatari ya moyo, akili na shinikizo la damu husababishwa na shughuli katika maisha yetu. Hapa ndipo michezo inaingilia. Michezo huyeyusha mafuta mwilini na kutukinga dhidi ya maradhi yanayosababishwa na unene wa kupindukia.
Kushiriki katika michezo vilevile hujenga ushirikiano na umoja. Michezo hutufundisha uwajibikaji. Mathalani, mlindalango atalenga kulilinda lango na kuhakikisha kuwa hamna bao linaloingia langoni. Washambulizi nao watalenga kushambulia lango la wapinzani huku waking’ang’ania kwa udi na uvumba kufunga bao.
Wachezaji ni sharti watii kanuni na sheria zinazotawala mchezo. Aidha, lazima wakubali amri za refa, kocha na waamuzi wengine ili kuimarisha nidhamu michezoni.
Watu hujipatia riziki kwa kushiriki michezo. Sasa hivi, kuna wanamichezo ambao wamesifika sana duniani. Baadhi yao wamevuka bonde la uchochole na kuwa wakwasi kutokana na talanta zao michezoni. Bila shaka, majina kama vile David Rudisha, Vivian Cheruiyot, Jason Dunford, Colins Injera na Dennis Oliech yakitajwa, kila awajuao huwavulia kofia.
Tangu jadi, michezo imekuwa kitegauchumi kote duniani. Wagiriki, kwa mfano walianzisha michezo ya Olimpiki karne nyingi zilizopita, takribani miaka 776 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Michezo hii ilipoanza ilishirikisha Wagiriki kutoka himaya zote za Ugiriki. Baadaye, watu wengine waliposhuhudia faida zilizotokana na michezo hii, walikubali kushirikishwa. Michezo ya Olimpiki ikawa si ya Wagiriki tu, bali dunia nzima. Baada ya hapo pamekuwa na michezo mingine ambayo inashirikisha watu kutoka kila pembe ya dunia. Mchezo wa kandanda wa kuwania Kombe la Dunia, michezo ya raga na riadha ni baadhi tu ya michezo ya kimataifa.
Watu kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni wanapokutana kwa michezo, nchi na watu wake hufaidika sana kiuchumi. Wenyeji hupata soko la kuuza bidhaa zao. Wakulima hufaidi kuuza vyakula wanavyokuza. Mikahawa nayo hujaa wageni tele huleta fedha za kigeni. Wafanyabiashara katika sekta ya usafiri na wenye hoteli nao huchuma kutoka kwa washiriki na mashabiki. Nchi inayoandaa mashindano hayo, aidha hupata sifa kimataifa.

 1. Bila kupoteza maana, fupisha aya tano za kwanza. (Maneno 80-90) (Alama 8, 1 ya mtiririko)
  Matayarisho
  ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  Jibu
  ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
 2. Kwa mujibu wa taarifa hii, michezo huwafaidi vipi wasioshiriki michezo yenyewe? (Maneno 40-50) (Alama 5, 1 ya mtiririko)
  Matayarisho
  ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  Jibu
  ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Kanusha: Osuma alipoanza mtihani alikuwa na kikokotoo kipya. (al. 2)
   ………………………………………………………………………………………………………
  2. Onyesha matumizi mawili tofouti ya kiambishi ‘e’ katika sentensi moja. (al. 2)
   ……………………………………………………………………………………………………..’……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………
  3. Tunga sentensi yenye mpangilio ufuatao wa maneno: Kiwakilishi nomino, kitenzi kisaidizi chenye urejeshi, kitenzi kikuu. (al. 2) ………………………………………………………………………………………………………
  4.                              
   1. Taja sifa bainifu za konsonanti. (al. 1)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………
   2. Tofoutisha irabu zinazotamkwa ulimi ukiwa juu. (al. 1)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………
  5. Onyesha miundo mitatu ya nomino katika ngeli ya LI-YA. (al. 3)
   ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………...………………………………………………………………………………………………………………………………….…………………………………………………………………………...………………………………………………………………………………………………………
  6. Tunga sentensi moja kudhihirisha maana ya: Enda nguu (al. 2)
   ………………………………………………………………………………………………………
  7. Ainisha neno: litumbukizalo
   1. Kimuundo (al. 1)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………
   2. Kimajukumu (al. 2)
    …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  8.                    
   1.  Andika neno lenye muundo ufuatao: (al. 2)
    1. Kipasuo ghuna cha kaakaagumu, irabu ya nyuma wastani, kikwamizo ghuna cha ufizi, irabu ya juu mbele.
     ………………………………………………………………………………………………………
    2. Sauti mwambatano ya ufizi, irabu ya nyuma wastani, irabu ya kati chini.
     ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
  9. Tunga sentensi yenye masharti yasiyowezekana kamwe. (al. 2)
   ………………………………………………………………………………………………………
  10.                            
   1. Kirai ni nini? (al. 1)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………
   2. Tambua aina ya kirai katika sentensi hii;
    Kabla ya uchaguzi mkuu viongozi walikuwa waadilifu. (al. 2)
    ……………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………
  11. Tunga sentensi changamano yenye kiwakilishi kirejeshi. (al. 2)
   ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………
  12. Taja yambwa katika sentensi hii: Mjomba hakupikiwa mlo wa leo kwa gesi. (al. 2)
   ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………
  13. Changanua kwa kielelezo cha matawi. (al. 4)
   Juma alizawidiwa ila Aisha aliyekata tamaa hakutuzwa.
  14. Eleza maana tatu zinazojitokeza katika sentensi hii. (al. 3)
   Maara, babake Ishumaeli na Maulidi wameenda Mombasa.
   ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….…………………………………………………………………………
  15. Tasfidi sentensi hii kwa wakati ujao hali timilifu. (al. 2)
   Mama alizaa mtoto msichana.
   ………………………………………………………………………………………………………
  16. Andika kwa usemi taarifa. “ Unaitwa nani?” Mwalimu alimuuliza. “Naitwa Mahat.” Akajibu. (al. 2)
   ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….……………………………………
  17. Akifisha: Mjomba alinunua mbuzi kifaa cha kukunia nazi na mayai. (al. 1)
   ………………………………………………………………………………………………………
  18. Andika kinyume cha kitenzi kilichopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo: (al. 1)
   Mwafrika anapenda kutii maagizo.
   ………………………………………………………………………………………………………

ISIMUJAMII (ALAMA 10)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
“Naona ‘Horse Power’ mwenyewe ndiye atakayepiga,….. atakayecheza foul hiyo. Wachezaji wa …….”

 1. Tambua sajili inayorejelewa. (al.2)
  …………………………………………………………………………………………………………………………………………………….………………………………………………………
 2. Tambua sifa zinazobainisha sajili yenyewe. (al.8)
  …………………………………………………………………………………………………………………………………………………….…………………………………………………………………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

MWONGOZO WA MOMALICHE

 1. UFAHAMU (alama 15)
  1.                        
   1. Kulimbikiziwa kodi
   2. Hanikizo la uvundo katika nyumba
   3. Mlundiko wa taka
   4. Majitaka yaliyovavagaa
   5. Ukuukuu wa majengo
   6. Rangi zinazoning’inia/zilizobambuka
   7. Maji ya kubahatisha/uhaba wa maji Za kwanza 6
  2. Mawazo fyongo/ yasiyokwenda sawa
   1. Wakulima kulazimishwa kupeleka mifugo kupigwa sindano/ kuchanjwa
   2. Mifugo wakipigwa sindano watakufa/ wakichanjwa watakufa/ upigaji ng’ombe sindano umeteketeza ng’ombe.
   3. Ng’ombe wamekuwa wakiumwa na kujiponea bila chanjo.
   4. Ndege zinazoruka na kutua zina kelele/ hazina manufaa.
   5. Heri kulima mashamba ndege zibaki angani au kule zitokako/ badala ya kujenga uwanja wa ndege.
   6. Migomo/ kugoma kuwa njia ya kusuluhisha migogoro. Za kwanza 4
  3. Hufanya vikao (mikutano ) maalumu ya mashauriano/mazungumzo badala ya kushika zana za vita (kupiigana)
  4.                            
   1. Limeamidi- tumeamua/ tumeazimia/tumedhamiria
   2. Yaliyovavagaa-yaliyotapakaa/yaliyoenea/yaliyosambaa/yaliyowamba/yaliyoshamiri
  5. Mlio(sauti) unaotokana na kugonga.
 2. UFUPISHO
  1.  Bila kupoteza maana, fupisha aya tano za kwanza. (Maneno 80-90)
   1. Afya ni taji.
   2. Anayeugua hujua umuhimu wa afya.
   3. Wajuao huthamini na kudumisha siha yao kwa kila njia.
   4. Michezo ni muhimu katika kudumisha afya njema.
   5. Mtu asiposhiriki michezo mwili hunyong’onyea na kunenepa.
   6. Mwili mnyonge ni windo rahisi la maradhi.
   7. Maradhi hatari husababishwa na shughuli katika maisha ya binadamu.
   8. Kushiriki katika michezo hujenga ushirikiano na umoja.
   9. Michezo hufunza uwajibikaji.
   10. Watu hujipatia riziki kwa kushiriki michezo. (Hoja zozote 8x1=8, 1 ya utiririko=9)
  2. Kwa mujibu wa taarifa hii, michezo huwafaidi vipi wasioshiriki michezo yenyewe (Maneno 40-50) (Alama 6, 1 ya mtiririko)
   1. Wenyeji wa michezo hupata soko la kuuza bidhaa zao.
   2. Wakulima hufaidi kuuza vyakula wanavyokuza.
   3. Mikahawa hujaa wageni tele huleta fedha za kigeni.
   4. Wafanyabiashara katika sekta ya usafiri huchuma kutoka kwa washiriki na mashabiki.
   5. Wenye hoteli huchuma kutoka kwa washiriki na mashabiki.
   6. Nchi inayoandaa mashindano hayo hupata sifa kimataifa.(Hoja zozote 5x1=5, 1 ya utiririko=6)

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (AL 40)

 1. Osuma alipoanza mtihani hakuwa na kikokotoo kipya. (alama 2)
 2.                      
  1. Kwenye michezo kuna mshindi na mshinde, teua- teule (Kuunda nomino)
  2. Cheza- chezea, chora- chorea (mnyambuliko) (alama 2)
 3. Yeye/ yule aliyepigwa amefariki. (alama 2)
 4.                          
  1. Hewa huzuiliwa mahali mahususi/ hutamkiwa mahali fulani.
  2. Huwa na jinsi / namna hewa inavyozuiliwa zinapotamkwa.
  3. Husepetuka/ zingine hazisepetuki, hutoa mrindimo/ hazitoi mrindimo katika nyuzi za sauti/ huwa ghuna/sighuna. (alama 3)
 5. O- ma (tunda-matunda, gari- magari),
  Ji- me (jino-meno, jiko- meko),
  Ji- ma (jina –majina, Jicho- macho)
 6. Enda nguu- fika kileleni/upeoni.
 7. Kimuundo (li-kiambishi awali, tumbukiz-mzizi, a-lo –kiambishi tamati)
  Kimajukumu( li- ngeli ya LI-YA, tumbukiz- mzizi, a- kiishio, lo- kirejeshi) (alama 3)
 8.                          
  1. Jozi
  2. Ndoa (alama 2)
 9. Makweche angalisoma kwa bidii angalifaulu. (alama 2)
 10.                      
  1. Kipashio cha kisarufi kisichokuwa na muumdo wa kiima na kiarifu/ kipashio cha kisarufi kisichokuwa na maana kamilifu (isipokuwa kirai kitenzi) (alama 1)
  2. Kirai kihusishi (kabla ya uchaguzi mkuu), Kirai nomino (uchaguzi), Kirai kitenzi (walikuwa waadilifu) (alama. 2)
 11. Aliyeapishwa juzi ameanza kazi rasmi. (alama 2)
 12. Mjomba- yambwa tendewa, mlo- yambwa tendwa, gesi- yambwa ala (alama 2)
 13.                                                    
  mmmmmm hjgaytda
   (alama 4)
 14.                                    
  1. Maara ambaye ni babake Ishumaeli wameenda Mombasa na Maulidi. (alama 3)
  2. Watu walioenda Mombasa ni watatu, Maara mwenyewe, babake Ishumaeli na Maulidi.
  3. Watu walioenda Mombasa ni wawili; Maara na baba ya Ishumaeli na Maulidi
 15. Mama atakuwa amejifungua mtoto msichana. (alama 2)
 16. Mwalimu alimuuliza alikuwa anaitwa nani naye akajibu kwa alikuwa anaitwa Mahat. (alama 2)
 17. Mjomba alinunua mbuzi; kifaa cha kukunia nazi na mayai.
  Mjomba alininua mbuzi-kifaa cha kukunia nazi na mayai. (alama 1)
 18. Mwafrika anapenda kukiuka/ kukaidi maagizo. (alama 1)

3. ISIMUJAMII

 1. Sajili ya michezo/ kandanda / kabumbu. 1x2 = 2
 2. Matumizi ya lugha changamfu / ucheshi.
  Matumizi ya chuku.
  Utohozi.
  Matumizi ya kuchanganya ndimi.
  Matumizi ya tamathali za usemi – takriri.
  Matumizi ya msamiati teule.
  Huchanganywa na nyimbo.
  Hutumia sentensi fupifupi.
  Matumizi ya lakabu. Zozote 8 x 1 = 8
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P2 Questions and Answers - Momaliche 4 cycle Post Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest