Kiswahili P1 Questions and Answers - Momaliche 4 cycle Post Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. Andika barua kwa mhariri wa gazeti la sauti ya mzalendo kuhusu madhara ya janga la korona nchini Kenya.
 2. Vyama vya wanafunzi shuleni vina manufaa ya kuhusudiwa.Jadili.
 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
  Mwenye kovu sidhani kapona.
 4.  Tunga kisa cha kusisimua na kumalizika kwa …..hivyo ndivyo ukurasa mpya katika kitabu cha maisha yangu ulivyofunguka.

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.  Andika barua kwa mhariri wa gazeti la sauti ya mzalendo kuhusu madhara ya janga la korona nchini Kenya.
  • Mwanafunzi azingatie muundo wa barua kwa mhariri kikamilifu.
   • Madhara ya janga la korona nchini Kenya.
    • Kukatizwa kwa elimu
    • Vifo
    • Kufutwa kazi
    • Kudorora kwa uchumi
    • Ndoa za mapema
    • Mimba za mapema
    • Gharama kubwa ya matibabu
    • Woga miongoni mwa wananchi
    • Kudorora kwa mila na tamaduni za jamii.
    • (Mwalimu akadirie maudhui ya wanafunzi)
 2. Vyama vya wanafunzi shuleni vina manufaa ya kuhusudiwa.Jadili.
  Manufaa ya vyama vya wanafunzi shuleni.
  • Hukuza vipawa na kuimarisha stadi za kujieleza
  • Huhimiza utangamano miongoni mwa wanachama
  • Husaidia mwanafunzi kukabiliana na changamoto za maisha
  • Humfunza mwanafunzi maadili ya kijamii na kidini
  • Majukumu ambayo mwanafunzi hupewa hupalilia uwajibikaji,uaminifu na kipawa cha uongozi
  • Kupitia vyama hivi mwanafunzi anaweza kuwahamasisha wenzake dhidi y tabia hasi k.v mapenzi ya kiholela n.k
  • Shughuli na miradi ya vyama hivi humwezesha mwanafunzi kutumia nishati zake kwa njia ya kunufaisha na kuepuka maovu.
  • Vyama vya michezo humwezesha mwanafunzi kuimarisha afya na kujenga misuli.
  • Vyama vya michezo huweza pia kuwa msingi wa kupata chanzo cha riziki baadaye.
  • Vyama vya wanafunzi ni msingi wa mshikamano na maridhiano.
   (Mwalimu akadirie maudhui ya wanafunzi.)
 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
  Mwenye kovu sidhani kapona.
  • Msimulizi asimulie kisa kitakachoonyesha ukweli wa methali hii.
  • Maana-Mtu ambaye amewahi kuwa mbaya hata akionekana kubadili mwenendo huenda akarudia maovu yake.
  • Mtahiniwa aonyeshe:
   1. Makosa ambayo mhusika alifanya.
   2. Jinsi makosa hayo yalimfanya kubadili mwenendo wake.
   3. Kurudia makosa yale au mengine mabaya zaidi.
  • Kisa ndicho muhimu si utangulizi
 4. Tunga kisa cha kusisimua na kumalizika kwa …..hivyo ndivyo ukurasa mpya katika kitabu cha maisha yangu ulivyofunguka.
  • Mtahiniwa asimulie kisa kitakachoonyesha mabadiliko yaliyotokea katika maisha yake.mabadiliko haya yaweza kuwa mazuri au mabaya.
  • Mtahiniwa atumie wakati uliopita ; aonyeshe matukio yaliyomfikisha katika mabadiliko haya.
  • Kisa kioane na mdokezo aliopewa.
   maudhui yasipungue 6 x 2 =12
   Muundo –alama 4
   Lugha -4
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P1 Questions and Answers - Momaliche 4 cycle Post Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest