MOKASA Joint Evaluation Examination Kiswahili Karatasi ya 1 2016- Pre MOCK

Share via Whatsapp
 1. LAZIMA

  Wewe ni mhariri wa gazeti la Chanuka Uendelee. Andika tahariri kuhusu kuenea kwa tatizo la ubadhirifu wa mali ya umma katika magatuzi mbalimbali na kupendekeza njia mbalimbali za kukabil iana nalo.

  Hii ni insha ya tahariri.
  Pawe na vipengele vifuatavyo vya sura;
  (i) Kichwa kina chorejelea mada iliyotolewa kwa mfano, Ubadhirifu wa mali katika magatuzi mbalimbali.
  (ii) Uhusika wa mhariri na/au gazeti la Chanuka Uendelee, kwa mfano, sisi katika gazeti la Chanuka Uendelee tunapendekeza………
  (iii) Lugha ya kuonyesha hisia za mhariri wa gazeti kuchukizwa na tatizo la ubadhilifu wa mali ya umma.
  (iv) Jina la gazeti na la mhariri

  Majibu
  Baadhi ya hoja za kuonyesha tatizo la ubadhinifu wa mali.
  (i) Wawakilishi wa wodi kujilibikizia marupurupu ya kila aina.
  (ii) Safari za nje ya gatuzi na zisizo za manufaa yoyote kwa gazeti husika.
  (iii) Ununuzi wa vifaa kwa bei ya juu kuliko ilivyo kwenye soko.
  (iv) Ujenzi wa barabara na nyumba kwa gharama ya juu kupita kiasi kinachostahili.
  (v) Matumizi mabaya ya mali ya umma kama vile magari, magavana kuwa na misafara na kuandaa karamu za kila aina.
  (vi) Wanakandarasi kulipwa kiasi kikubwa cha pesa kuliko inavyopaswa na kuendeleza miradi duni.
  (vii) Huduma za afya kukumbwa na migomo ya mara kwa mara kwa sababu ya hela za sekta hiyo kutumiwa vibaya kwingine.
  (viii) Kuajiriwa kwa maafisa pasi na kuzingatia taaluma yao ila ukabila na unasaba hivyo wakapata mishahara isiyosaidia gatuzi kukua.

  Mapendekezo
  (i) Magavana wanaotumia mamlaka yao vibaya wachunguzwe na tume yakukabiliana na ufisadi na kufikishwa mahakamani.
  (ii) Habari kuhusu matumizi ya kibadhirifu kwenye magatuzi kuangaziwa kwenye vyombo vya habari ilikuwa aibisha mafisadi.
  (iii) Wanakandarasi kulipwa baada ya kukamilisha miradi yao.
  (iv) Sheria kuhusu uwakala na utoaji zabuni iweze kufanyiwa marekebisho ili bidhaa na huduma zitolewe kwa bei/gharama inayostahili.
  (v) Makadirio ya matumizi ya fedha katika magatuzi kuangazia maendeleo na utoaji wa huduma wala si malipo ya mishahara pekee.
  (vi) Kununuliwa kwa vifaa vya matibabu na ujenzi wa hospitali badala ya kushiriki shughuli za kibadhirifu.
  (vii) Kupigwa marufuku kwa safari na sherehe zisizoongeza chochote cha thamani kwa magatuzi.
  (viii) Kupunguzwa kwa marupurupu ya wawakilishi wa wodi na kuthibiti uwezo wao wakujiongeza marupurupu hayo.

  Tanbihi
  (i) Gatuzi linaweza kuwa la kihalisia au la kubuni.
  (ii) Matukio ya ubadhirifu yanaweza kuwa yaliyotokea au yanayofikirika kutokea.
  (iii) Wakati (Hati) – Arejelee matukio yanayoendelea kutokea.

  Utuzaji
  (i) Mtahiniwa anahitajika kueleza visa mbalimbali vinavyothibitisha kuwa kuna ubadhirifu wa mali ya umma katika magatuzi. (Pawepo na angaa visa vinnne).  Mtahini amtuze mtahiniwa pale hoja inapokamilikia kwa mkwaju pembezoni.
  (ii) Mtahiniwa atoe mapendekezo ya kukabiliana na ubadhirifu kwenye magatuzi. Mapendekezo manne yataafiki mtahini amtuze mtahiniwa kw akumpa mkwaju uliokatwa pembezoni pale hoja inapokamilikia.
  (iii) Atakayekosa visa au kuvitaja pasi na kutoa maelezo amepotoka kimaudhui. Atuzwe alama ya D 03/20
  (iv) Atakayekosa vipengele vitatu vya sura au kuandika barua kwa mhariri aondolewe alama 4S baada ya kutuzwa
  (v) Atakayekosa kutaja gazeti la Chanuka Uendelee kokote katika insha yake aondolewe alama 2G (gazeti) baada ya kutuzwa.

 2. Mradi wa serikali wa vipakatalishi kwa shule za msingi nchini utakuwa na manufaa si haba. Jadili.

  Kuunga
  Tarakilishi itarahisisha kazi ya mwalimu:
  (i) Itawezesha kutoa Makala yatakayotumiwa na wanafunzi pamoja na walimu.
  (ii) Uchapishaji wa mtihani.
  Itapunguza gharama ya mtihani.
  Ni jukwaa muhimu katika kupalilia stadi za kutafiti.
  Itarahisisha mawasiliano.
  Itawezesha utangamano na kurahisisha ubadilishanaji wa mawazo.
  Itawezesha mwalimu mmoja kufunza wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.
  Litakuwa suluhu mwafaka katika kufidia uhaba wa walimu nchini.

  Kupinga
  Mradi huu utagharimu serikali pesa nyingi kwa hivyo utakuwa mzigo kwa mlipaushuru.
  Changamoto ya kuzuia wanafunzi kuingia sehemu zisizoruhusiwa kwao-picha za ngono.
  Utapunguza nafasi za ajira kwa walimu.
  Ni mradi ambao utachukua muda mrefu kufaulu.
  Shule nyingi hazina nguvu za umeme.
  Wataalamu wakuakisi na kufaulisha mradi huu ni wachache.
  Ufundishaji kwa njia ya tarakilishi utapunguza mtagusano kati ya mwalimu na mwanafunzi.
  Uchafuzi wa mazingira kutokana na vipuli na tarakilishi zilizoharibika.
  Kuharibika kwa utamaduni.

  Muhimu
  Hii ni insha ya mjadala.
  Mtahiniwa ajadili pande zote mbili za swali hili.
  Mtahiniwa atoe hoja za kuunga na kupinga kisha atoe msimamo wake kulingana na hoja.
  Mtahiniwa asipotumia wakati ujao atakuwa amejitungia swali–atuzwe D 03/20
  Atakaye egemea upande mmoja tu atakuwa amepotoka; atuzwe C 08/20
  Ili mwanafunzi achukuliwe kuwa amelijibu swali kikamilifu aweze kuwa na jumla ya hoja saba.

 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
  Fimbo ya mbali haiui nyoka.

  (i) Fimbo iliyo mbali huwezi kuitumia kumwua nyoka aliyekukaribia.
  (ii) Huwezi kutegemea kitu kilichombali kwa mahitaji ya dharura.
  (iii) Kisa kinaweza kulenga;
  Mtu aliyenuia kutenda jambo/shughuli fulani lakini akakosa vifaa/maarifa ya kushughulikia dharura hiyo na mwishowe kukosa kufaulu.

  AU

  Mtu aliyetegemea msaada wa mbali (jirani, mtu mwingine) kutekeleza shughuli fulani na mwishowe akose kufaulu kutokana na kukosa msaada huo muhimu, chambilecho; Hamadi kibindoni, ni silaha iliyo mkononi.

  UTUZAJI
  a) Sehemu mbili za methali zijitokeze waziwazi. Yaani sehemu ya dharura (nyoka) na sehemu ya uhitaji/msaada (fimbo) ambayo inakosekana.
  b) Atakaye shughulikia upande mmoja wa methali atakuwa amepungukiwa kimaudhui asipite C+ 10/20.
  c) Atakaye buni kisa kisichoafiki maana ya methali atakuwa amepotoka kimaudhui. Atuzwe 03/20.
  d) Atakaye buni kisa kwa kutumia maana ya juu/wazi (bila kumhusisha binadamu) atakuwa amepotoka kimaudhui atuzwe D 03/20.
  e) Atakaye taja upande wa pili bila kutoa maelezo kikamilifu atakuwa amelenga ila ana udhaifu wa kimaudhui.

 4. Tunga kisa kitakacho malizika kwa maneno yafuatayo:
  ........nilishusha pumzi kwa hisia za shukrani, safari hii haikuwa rahisi na wengi hawakutarajia kuwa ningefaulu licha ya wingu la simanzi na misukosuko lililoniandama tariki nzima.

   (i) Mtahiniwa amalizie kwa maneno haya. Anaye kosa kumalizia kwayo amejitungia Swali atuzwe D 01/20 au 02/20
  (ii) Anaye ongeza maneno chini ya matano, achukuliwe kuwa na kosa la mtindo na akadiriwe ifaavyo.
  (iii) Anayekata au kusahau maneno chini ya maneno achukuliwe kuwa na kosa la kimtindo;akadiriwe ifaavyo.
  (iv) Kisa cha mtahiniwa sharti kionyeshe mhusika aliyepitia katika hali ngumu aina aina kwa majonzi/simanzi na misukosuko. Watu waliomjua au waliokuwa wakimshuhudia wakipoteza matumaini yake kunusurika, lakini baadaye akafaulu kimiujiza na kuwaacha wengi wakishangaa.

  Asiyezingatia nafsi ya kwanza atuzwe D 01/20 au 02/20.

  Mifano
  a) Mwanafunzi aliyefiwa na wazazi akiwa mdogo lakini anajibidiisha kwa shida nyingi na kufaulu mtihani wake.
  b) Mtu aliyepoteza mpenziwe na kukumbana na hali ngumu maishani lakini baadaye anafaulu.
  c) Mhusika aliyeanza safari ya mbali akakumbana na matatizo mengi njiani, lakini hatimaye akafaulu kufika alikokuwa akienda.
  d) Mhusika anaweza kuwa dereva wa mashindano ya magari, baiskeli au riadha anayekumbana na matatizo mashindanoni lakini baadaye akafaulu.
  e) Tanbihi: Yatathmini majibu mengine ya mtahiniwa.
  Kumbuka mtahiniwa sharti aonyeshe simanzi na misukosuko katika kisa chake.
  Atakayeshughulikia simanzi bila msukosuko au misukosuko bila simanzi amejibu swali nusu; asipite alama ya C+ 10/20.

  Tanbihi
  Mtahiniwa azingatie urefu.

  Atakayeandika insha robo asipite D+ 05/20
  Atakayeandika insha nusu asipite C+ 10/20
  Atakayeandika insha robo tatu asipite B+ 15/20

  Maneno
  0 – 174 insha robo
  175-274 insha nusu
  275-374 insha robo tatu
  375 na Zaidi insha kamili


Download MOKASA Joint Evaluation Examination Kiswahili Karatasi ya 1 2016- Pre MOCK.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest