Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Sukellemo Joint Pre Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI
SEHEMU A: FASIHI SIMULIZI

  1. LAZIMA Alama 20
    1. Taja hatua tano za kufanya utafiti (alama 5)
    2. Eleza kwa hoja tano, umuhimu wa kushiriki kama njia ya kukusanya data (alama 5)
    3. Kikundi cha Tamasha Bora kiliwasilisha maigizo katika ukumbi wa shule yenu. Fafanua kwa hoja tano sababu za uwasilishi wao kufanikiwa. (alama 5)
    4. Eleza msamiati ufuatao (alama 5)
      1. ulumbi
      2. mbazi
      3. lakabu
      4. matambiko
      5. rara nafsi 

SEHEMU B: TAMTHILIA
KIGOGO PAULINE KEA
Jibu swali la 2 au la 3

  1. ‘Wewe ni popo: Kwa ndege hupo na kwa wanyama hupo.’
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
    2. Taja na ueleze tamathali za usemi katika dondoo hili. (al 4)
    3. Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (al 6)
    4. Huku ukitoa mifano sita mwafaka, fafanua maudhui ya usaliti kama yalivyojitokeza katika tamthilia hii. (al 6)
      Au
  2.    
    1. Kwa kutolea hoja kumi, onyesha matumizi ya kinaya ili kufanikisha maudhui mbalimbali katika tamthilia ya Kigogo . (al 10)
    2. Jumuiya ya Sagamoyo inakumbwa na udhalimu chungu nzima. Thibitisha kwa hoja kumi. (al 10)

SEHEMU C: RIWAYA
ASSUMPTA MATEI: CHOZI LA HERI
Jibu swali la 4 au la 5

  1. Eleza ufaafu wa anwani “Chozi la Heri” (al20)
    AU
  2. "Kuukata mkono niliostahili kuubusu yalinifika ya kunifika”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (Alama 4)
    2. Eleza tamathali ya usemi inayoojitokeza katika dondoo hili. (alama.2)
    3. Msiba huandamwa na msiba mwingine. Thibitisha kauli hii ukirejelea msemaji wa maneno kwenye dondoo (alama 4)
    4. Eleza jinsi haki za watoto zimekiukwa katika riwaya ya Chozi la Heri. (alama 10)

SEHEMU D: HADITHI FUPI
Chokocho na Kayanda (Wah) Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 6 au la 7
Tulipokutana Tena

  1. Ingawa mimi nilikuwa kitoto cha miaka mitano, nilihisi siku ile ilikuwa mbaya kwangu.
    1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Eleza toni ya dondoo hili. (alama 2)
    3. Eleza sifa sita za mzungumzaji wa kauli hii. (alama 6)
    4. Fafanua umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuijenga hadithi ya Tulipokutana Tena. (alama 8)
      Au
  2. Huku ukirejelea hadithi ya Tumbo lisiloshiba na Shibe inatumaliza, Fafanua madhui yaliyoonyeshwa kwenye mabano;
    Tumbo lisiloshiba ( ukiukaji wa haki.) (alama 10)
    Shibe inatumaliza (ubadhirifu) (alama 10)

SEHEMU E: USHAIRI

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki
    Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki
    Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki,
    Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Wenginea watakuua, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo
    Hizo kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakizifuata nyago
    Hadi kwenye wako au, pasipo hata kupesa, walakukupa kisogo
    Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Pindi kinunua kitu, hafurahi shaitani, bali tajawa chukizo
    Mtu kiwa mtukutu, tanuna mtimani, kwato ako tekelezo
    Tamko lake ‘subutu’, kuondoa tumaini, na kukuliza wazo
    Mtu kuwa tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Aliye na taraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kujidai
    Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui
    Hana faida nyumbani, ni mtu akichimbaye, mradi usitumai
    Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Kwa hakika ni baka, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo
    Bahati ina hadaa, kukupa alo sodawi, aibarili rowoyo
    Mipangayo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza kuvunja kaniyo
    Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    Ninacho changu kilio, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa
    Ningetoa azinio, lakini uwezo sina, kwa mazito kuambiwa
    Ama nitimue mbio, fuadinininanena, akilini nazuiwa
    Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    1. Jadili dhamira ya shairi hili. (Alama 1)
    2. Eleza sababu za mtungaji kulalamika katika shairi hili. (Alama 3)
    3. Eleza umbo la shairi hili. (Alama 4)
    4. Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari/ tutumbi. (Alama 4)
    5. Taja na utoe mifano ya aina nne za tamathali za usemi zilizotumika katika shairi hili (Alama 4)
    6. Toa mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi hili . (Alamfa 2)
    7. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi. (Alama 2)
      1. Zani
      2. Faraghani 


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. LAZIMA
    1. Taja hatua tano za kufanya utafiti (alama 5)
      • Maandalizi
      • Utafiti na ukusanyaji data
      • Rekodi ya data
      • Kuchunguza data na kunakili ili kuchanganua baadaye
      • Uchanganuzi na kufasiri data.
        1×5=5
    2.    
      • Kupata habari za kuaminika
      • Njia bora kwa wasiojua kusoma
      • Rahisi mtafiti kuuliza maswali kuhusu kipera
      • Mtafiti anaweza kunakili anayotazama au kusikiliza na hivyo kuhifadhi kiimbo, toni na ishara.
      • Mtafiti anaweza kuthibitisha aliyokusanya
      • Kushiriki hukuza utangamano
        Zozote 5×1=5
    3.  Ujasiri wa waigizaji
      • Ubunifu wa waigizaji - kutumia mbinu mbalimbalu ili kufanya uihizaji kuvutia
      • Ujuzi wa kutumia ishara za uso,mwili na miondoko inayooana na yanayoigizwa
      • Ujuzi na ufasaha wa lugha na waigizaji
      • Kuielewa hadhira na kubadili mtindo ipasavyo
      • Matumizi ya maleba mwafaka
      • Kushirikisha hadhira kwa kuuliza maswali
      • Kuelewa utamaduni wa hadhira
      • Ufaraguzi wa wahusika
        Zozote 5×1=5
        1. Ulumbi
          Uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee/ utumiaji lugha kwa mvuto wa kipekee
        2. Mbazi
          Hadithi fupi yenye mafunzo na inayotolewa kama kielelezo wakati wa kumkanya au kumwelekeza mtu.
        3. Lakabu
          Jina la msimbo/kupanga ambalo mtu hujibandika au hubandikwa kutokana na sifa zake za kimaumbile, kitabaka, kitabia au kimatendo
        4. Matambiko
          Sadaka au ada inayotolewa kwa Mwenyezi Mungu, miungu, pepo au mizimu moja kwa moja ili kutatua matatizo ya kijamii ama kwa shukrani.
        5. Rara nafsi
          Ushairi wa kinafsi ambao hutungwa na mtu kuelezea hisia, matatizo na fikra zake mwenyewe
          1×5= 
  2. ‘Wewe ni popo: Kwa ndege hupo na kwa wanyama hupo.’
    1. Maneno ya Boza
      Anamwambia Kombe
      Wako katika karakana yao katika soko la chapa kazi.
      Wanazungumza kuhusu Hali ilivyobadilika Sagamoyo.
    2.    
      1. sitiari - wewe ni popo.
        Boza anamrejelea Kombe kama popo kwa kuonekana kutokuwa na msimamo wa ni nani anayemuunga mkono.
      2. Kejeli- Boza anamrejelea Kombe kama popo. Huku ni kumdunisha kwa kukosa msimamo.
        Kutambua tamathali al.1
        Kueleza al.1 1×4
    3.      
      1. Mbinafsi
        Anapopewa keki na Kenga, anasema kuwa ni ndogo sana hivi kwamba hangeweza kuwapelekea jamaa zake.
      2. Mjinga
        Habaini maovu yoyote ya uongozi wa Majoka. Anautetea na kmuunga mkono licha ya hali Sagamoyo kuendelea kuwa mbaya.
      3. Mwenye kiburi
        Sudi anapoizima redio ya rununu yake anaikejeli kwa kuirejelea kama kijiredio cha pesa nane.
      4. Mlevi
        Anashiriki ulevi na walevi wengine kule Mangweni.
      5. Mwenye tamaa
        Hawaelezi Sudi na Kombe kuhusu mradi wa kuchonga kinyago akitarajia kuchonga yeye ili ajifaidi.
      6. Mwenye mapuuza.
        Hakung'amua uhusiano wa kimapenzi ulioendelzwa baina ya Ngurumo na mkewe.
      7. Huku ukitoa mifano sita mwafaka, fafanua maudhui ya usaliti kama yalivyojitokeza katika tamthilia hii. (al 6)
    4.    
      1. Kupigwa na kuumizwa
        Ngurumo aliyesoma na Tunu darasa moja anakubali kutumiwa na Majoka kumpiga na kumvunja muundi wa mguu.
      2. Kufungulia biashara ya ukataji miti.
        Majoka anasaliti wajibu wake wa kulinda rasilmali za nchi kwa kufungulia biashara ya ukataji miti.
      3. Kufunga soko la Chapa kazi.
        Majoka anasaliti raia anaowaongoza kwa kufunga soko hivyo kuwahini kipato chao cha kila siku.
      4. Kutosafisha soko.
        Majoka anasaliti raia wanaolipa Kodi sokoni kwa kutosafisha soko. Wanafanyia biashara katika mazingira machafu yanayowasababishia ndwele zisizo majina.
      5. Kutawanya raia kwa fujo.
        Polisi wanasaliti wajibu wao wa kuhakikishia raia usalama wao kwa kutawanya kwa risasi na vitoza machozi kila wanapoandamana kutetea haki
      6. Kumwaga taka sokoni.
        Serikali ya Majoka inasaliti raia kwa kumwaga kemikali na majitaka sokoni na kuwasababishia uvundo na ndwele.
        Au
  3.      
    1.    
      • Habari zinazotolewa na mjumbe katika rununu ni za kinaya, kuwa wanasagamoyo wasirudishe maendeleo nyuma bali wafurahie ufanisi ambao umepatikana katika kipindi cha miaka sitini baada ya uhuru.- uongozi mbaya
      • Ujumbe huu ni kinaya kwa vile Sagamoyo hakuna maendeleo wala ufanisi. Watu wana njaa na wanakosa mambo ya kimsingi kama vile maji, elimu na matakwa mengine mengi -umaskini
      • Boza anadai kuwa kulipa kodi ni kujenga nchi na kujitegemea. Kauli hii ni kinaya kwa vile kodi wanayolipa wanasagamoyo haitumiki kujenga nchi kwa vyovyote vile. ubadhirifu
      • Sudi anasema kuwa katika kipindi cha mwezi mzima wa uhuru wale mali walizochuna kwa miaka sitini. Ni kinaya kwa kuwa hakuna walichovuna, viongozi hujilimbikizia mali. Ubadhirifu/ umaskini
      • Boza anamwambia Sudi kuwa wanatia doa kwa kila jambo nzuri. Ni kinaya kwa vile hakuna mambo mazuri ambayo Majoka amefanya Sagamoyo. (uk5) mapuuza
      • Wanasagamoyo kusherehekea miaka sitini ya uhuru ni kinaya kwani hakuna cha muhimu kusheherekewa, hakuna maendeleo Sagamoyo. Uongozi mbaya
      • Boza anadai kuwa kinyago chake chapendeza na kufanana na shujaa Marara Bin Ngao, ni kinaya kwani kinyago hicho hakifanani na shujaa huyo. ubinafsi
      • Mzee Majoka kudai kuwa anamheshimu sudi ni kinaya. Majoka hana heshima kwa raia wake, nia yake ni kutaka Sudi amchongee kinyago. (uk13) ubinafsi
      • Kenga kumwambia Sudi kuwa ipo siku atamtafuta mzee Majoka ni kinaya kwani Sudi hana haja naye. ulaghai
      • Majoka kudai kuwa takataka za soko zitaharibu sifa nzuri za jimbo la Sagamoyo ni kinaya kwa vile hakuna sifa nzuri Sagamoyo. Viongozi wanaendeleza maovu na hata kupanga mauaji. 25unyakuzi wa ardhi
      • Ni kinaya kwa polisi Sagamoyo kutawanya waandamanaji. Polisi wanapaswa kulinda na kutetea haki za wananchi. udhalimu
      • Majoka kusema kuwa Sagamoyo wanajiweza ni kinaya. Watu wana matakwa mengi, ni maskini, wana njaa na hata kupata ufadhili kutoka nje kwa miradi isiyo muhimu.mapuuza
      • Ni kinaya Kenga anapomwambia Majoka aache moyo wa huruma, kwa sababu Majoka hana hata chembe cha huruma. Anapanga mauaji na kunyanyasa raia. 34 ukatili
      • Majoka anaposema kuwa juhudi za Tunu kuandaa migomo hazitamfikisha mahali ni kinaya kwa vile Tunu wanafanikiwa katika maandamano yao na hata kuungwa mkono na wengi. Utetezi wa haki
      • Ni kinaya kwa Ashua kumwambia Sudi kuwa ni kosa lake kutiwa ndani. Kosa ni la Majoka na njama yake ya kutaka kuchongewa kinyago. uchochezi
      • Ashua anasema kuwa katika jela kuna amani na amechoshwa na Sudi. Ni kinaya kwani Ashua anapata maumivu akiwa jelani. Mabadiliko/ ukatili
      • Uvumi unaoenea kuwa Sudi na Ashua ndio wanaowinda roho ya Tunu ni kinaya kwani wote hawa ni wanamapinduzi wanaopigania haki Sagamoyo. Ulaghai/ propaganda
      • Madai ya Ngurumo ni kinaya kuwa tangu soko kufungwa Sagamoyo ni pazuri mno. Eti mauzo ni maradufu ilihali watu hawana mahali pa kuuzia bidhaa zao, kifungwa kwa soko kunawaangaisha raia hata zaidi.60 mapuuza
      • Ngurumo kusema kuwa pombe ni starehe ni kinaya kwani watu wanaangamia kutokana na pombe, wengine kuwa vipofu.mapuuza
      • Watu wengi wanatarajiwa kufika katika uwanja wa ikulu ya Majoka kusherehekea uhuru siku ya sherehe lakini ni kinaya kwa kuwa ni watu kumi tu ambao wanafika. Mabadiliko/ mapuuza
      • Mamapima kusema pombe inaondoa karaha ilhali inasababisha karaha kwa kuua, kupofusha, uzembe, kufuja familia. Tamaa/ ubinafsi/mapuuza
      • Raia kuimba nyimbo za kusifu Ngao badala ya kumkashifu kwa udhalimu wake. mapuuza
      • Mzee Majoka kudai kuwa anamheshimu sudi ni kinaya. Majoka hana heshima kwa raia wake, nia yake ni kutaka Sudi amchongee kinyago. (uk13) unafiki
        Mifano mingine yoyote mwafaka ya kinaya na maudhui
    2. Dhuluma
      1. Kumwaga kemikali sokoni - serikali ya Majoka inamwaga taka za kemikali sokoni zinazowasababishia ndwele zisizo majina.
      2. Matumizi ya vitisho
        Bi. Hashima anasema kuwa serikali ya Majoka imewajaza hofu. Wanaishi kwa woga.
      3. Kubebeshwa mzigo wa madeni.
        Serikali ya Majoka inakopa pesa nyingi wanazotumia vibaya huku wananchi wakilazimika kulipa.
      4. Kufunga soko la chapa kazi.
        Majoka anafunga soko la chapa kazi bila kuwazia maslahi ya wanasagamoyo wanaolitegemea kwa riziki.
      5. Kuongeza Kodi. Baada ya kuwaongeza walimu na wauguzi mishahara, majoka anapandisha Kodi na hivyo kuwahini.
      6. Kutokuwa na bima ya matibabu.
        Babake Tunu anapofia kazini Majoka aliwanyima fidia kwa madai kuwa hakuwa na bima ya afya.
      7. Kupandisha bei ya bidhaa.
        Wafanyakazi kiwandani wamegoma kudai haki baada ya bei ya bidhaa kuongezwa huku soko likiwa limefungwa.
      8. Kufunga vyombo vya habari na kuwanyima wanasagamoyo haki ya kupata taarifa.
      9. Kukusanya kodi pasi na kusafisha soko.
        Wanasagamoyo wanaofanyia kazi katika soko la chapa kazi wanatozwa kodi ilihali haitumiki kulisafisha soko.
      10. Kufungwa jela bila hatia km Ashua.
        Hakiki majibu mengine sahihi
  4. Majibu ya ufaafu wa anwani
    1. Familia ya mzee Mwimo Msubili inateseka kutokana na udogo wa ardhi lakini hali inakuwa nzuri babake Ridhaa anapowahamisha wake zake wawili wa mwisho, katika Msitu wa Heri. Mmoja wa hawa ni mamake Ridhaa.
    2. Ridhaa anadhulumiwa na wanafunzi wenzake shulenina kutukanwa kuwa yeye ni mfuata mvua lakini hali inakuwa nzuri baada yamamake kwenda na kuzungumza na mwalimu mkuu na hali nii kusitishwa.
    3. Eneo la Msitu wa Heri lilikuwa kame (Kalahari) lakini inageuka kuwa nzuri baada ya Ridhaa kuwaletea maji ya mabomba na eneo hilo kutwaa rangi ya kichani kiwiti.
    4. Hali inakuwa nzuri kwa Mzee Kedi Ridhaa anapoyathamini masomo ya wapwa zake wawili.
    5. Mwekevu anapoingia kwenye siasa anatusiwa na watu lakini hali hii inabadilika na kuwa bora baada ya kushinda uchaguzi.
    6. Familia ya Kaizari inapata taabu anapovamiwa na wahuni lakini anapata heri wakati jirani yake Tulia anapomsaidia kutorokea palipo salama.
    7. Kaizari anapovamiwa na mkewe Subira kujeruhiwa na wananwe Lime na Mwanaheri kubakwa, anapata heri Tulia anapojitolea kumlindia nyumba isije ikaharibiwa na wahuni.
    8. Wakimbizi wanapoteseka kambini kutokana na ukosefu wa chakula, misikiti na makanisa yana waletea chakula na kuwafanya kuona heri.
    9. Wakimbizi wanapoteseka kwa kulala vibandani, shirika la Makazi Bora linajitolea kuwajengea makao bora.
    10. Selume anapotaabika baada ya kukataliwa na mumewe Mwanzi, anakutana na Ridhaa anayemsaidia kupata kazi ya uuguzi katika hospitali ya umma.
    11. Kuchomwa kwa familia ya Ridhaa kunamletea ugojwa wa shinikizo la damu lakini anasaidiwa kudhibiti hali hiikutokana na huduma za ushauri na uelekezaji kutoka kwa wataalamu.
    12. Lime na Mwanaheri wanabakwa lakini wanapata heri abaada ya kutibiwa na wauguzi waliotumwa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
    13. Ridhaa anafuraha kupatana na mwanawe Mwangeka vita vya baada ya uchaguzi vilivyozuka na kusababisha wanawe wengine pamoja na mkewe Terry kuangamia.
    14. Usalama unazorota katika nchi ya Wahafidhina lakini wanapata heri jamii ya kimataifa inapowasaidia kurejesha Amani.
    15. Kiriri anamsaidia mfanyikazi wake Kangata kuyadhamini masomo ya binti zake wawili.
    16. Riziki Immaculata, kitoto kinachotupwa na mamake kwenye biwi la taka linapata heri kinapookolewa na Neema anayekipeleka katika kituo cha watoto cha Benefactor.
    17. Umulkeri amekuwa akilia kwa kukosa wazazi lakini hali inakuwa bora kwake Apondi na Mwangeka wanapomchukua na kuishi naye kama mwana wao wa kupanga.
    18. Chanda Chema anataabika kwa kukosa malezi lakini Bwana Tenge na Bi. Kimai wanamchukua na kumlea kama mwanao.
    19. Mwaliko anatekwa nyara na nyumbani kwa Bi.Kangara lakini anaokolewa na polisi na kupelekwa katika kituo cha Benefactor.
    20. Mwangeka anafiwa na mkewe Lily Nyamvula lakini anapata heri anapowoa Apondi.
    21. Apondi anafiwa na mumewe aliyeenda kudumisha amani lakini anapata nafuu anapoolewa na Mwangeka.
    22. Hazina anataabika barabarani kama ombaomba lakini anapata heri Umu anapompa pesa.
    23. Umulkheri anapoteseka mjini anabahatika kumpata Hazina aliyempa pesa miaka mingi iliyopita. Hazina anamsaidia Umukheri.
    24. Dick anapata heri anapojinasua kutoka kwenye biashara ya kuuza dawa za kulevya na kuanza biashara yake ya kuuza vifaa vya elekroniki.
    25. Tuama anapoteza damu nyingi baada ya kupashwa tohara lakini anapata heri anapotibiwa na kupona.
    26. Neema anataabika kwa kukosa mtoto lakini hali yake inaimarika anapofaulu kupewa Mwaliko na Mtawa Anastacia kutoka kituo cha watoto cha Benefactor na kumlea kama mtoto wa kupanga
    27. Kadiria majibu ya mwanafunzi
      AU
  5.      
    1. Haya ni maneno ya Lunga. Maneno/maelezo ambayo lunga angempa yeyote ambaye angemuuliza/ kumkumbusha kuhusu jadhiba yake ya uhifadhi mazingira. Hii ni baada ya lunga kufutwa kazi ya ukurugenzi katika shirika la Maghala ya Fanaka baada ya kukataa kuidhinisha ununuzi wa mahindi aliyodai yalikuwa hatari kwa binadamu. Lunga anarejea katika msitu wa mamba na kuanzisha kilimo chenye natija jambo (uk74)
    2. Jazanda-kuukata mkono aliostahili kuubusu-kuwapinga wakubwa wake.
    3. Msiba huandamwa na msiba mwingine. Thibitisha kauli hii ukirejelea msemaji wa maneno kwenye dondoo (alama 4)
      Kufutwa kazi katika shirika la maghala ya fanaka
      Kutimuliwa katika msitu wa mamba
      Kuachwa na mkewe, Naomi
      Kupatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu
    4. Kutekwa nyara. Sauna anateka nyara Dick na Mwaliko
      Kuuzwa. Wasichana wanauzwa madanguroni na Bi. Kangara nao wavulana kwa matajiri wanaowatumia kulangua dawa za kulevya na kuwatumikisha katika mashamba na makasri yao.
      Kuavyawa. Sauna anaavya baada ya kubakwa na baba mlezi. Pete alijaribu pia kuavya.
      Kutishwa. Dick anatishwa na Buda kuwa alikataa kuuza mihadarati atasingiziwa wizi ili auawe.
      Ajira ya watoto. Kuchuma majanichai katika shirika la Chai la Tengenea km Chanda chema akiwa darasa la tano. Sauna anafanya katika machimbo ya mawe na pia kuuza pombe.
      Ndoa za lazima. Pete kuozwa na wajomba na mamake kwa Fungo aliye na wake watatu tayari.
      Kukatiziwa masomo. Pete alikuwa darasa la saba. Wototo walioajiriwa katika shirika la Chai la Tengenea.
      Kutupwa. Mtoto aliyeokotwa na Neema ametupwa jaani na aliyetupwa langoni la Kituo cha watoto cha Benefactor.
      Kudhulumiwa kimapenzi. Fumba kuhusiana kimapenzi na mwanafunzi wake Rehema na kupachika mimba.
      Dhiki za kisaikolojia. Tenge kufanya mapenzi na makahaba machoni pa wanawe na Chandachema.
      Kutumikishwa. Zohali anapopata mimba na kufukuzwa shuleni anafanyishwa kazi za nyumbani na kudhalilishwa badala ya kushauriwa hadi anatoroka.
      Kubakwa. Lime, Mwanaheri na Sauna.
      Kuchomwa. Becky, Mukela na Tila wanachomwa na Kedi naye Lemi anachomwa na umati uliodhani ameiba simu.
      Kutelekezwa
      Kupigwa
      Kunyanyaswa. Umu anaulizwa maswali magumu na polisi aliporipoti kupotea kwa nduguye badala ya kumsaidia.
      Kunyimwa malezi ya wazazi.
  6. Ingawa mimi nilikuwa kitoto cha miaka mitano, nilihisi siku ile ilikuwa mbaya kwangu.
    1.      
      1. Haya ni maneno ya Bogoa Bakari.
      2. Anawaambia mkewe Sakina , Sebu na mkewe Tunu , Kazu na mkewe Bi. Temu.
      3. Wamo katika Club Pogopogo.
      4. Bogoa anawasimulia hadithi kuhusu jinsi alivyotolewa nyumbani kwao na kupelekwa kwa Bi. Sinai aliyemtesa sana.
        4x1=4
    2. Toni ya huzuni- Bogoa anahuzunika anapokumbuka mateso yake mikononi mwa Bi Sinai
    3.      
      1. Mpenda anasa – Sebu anasema kwamba yeye na Bogoa walikuwa wakienda mjini kucheza densi wakiwa na miaka kumi na minane.
      2. Karimu – anashirikiana na Kazu kuwanunua chakula Sebu, Bi.Tunu , Bi.Temu na Sakina.
      3. Mwenye mapenzi – Baba yake alipotaka kumpeleka mjini akaishi huko alilia kwa maana hakutaka kutengana na mama, baba, ndugu , kaka na dada zake.
      4. Mtiifu – anatii kila analoambiwa na Bi.Sinai . Kwa mfano , Bi. Sinai anapomtisha kuwa angemkata ulimi iwapo angefichua chochote kuhusu maisha aliyoyapitia nyumbani kwa Bi.Sinai.
      5. Msiri – aliteseka sana nyumbani kwa Bi. Sinai ila hakumwambia rafikiye Sebu licha ya kucheza naye. Aidha, hakuwahi kumtolea mkewe hadithi kuhusu masaibu aliyoyapitia nyumbani kwa Bi.Sinai.
      6. Mwongo – Bi. Sinai anapomchoma viganja kwa sababu ya kuacha mandazi kuungua anamhadaa Sebu kuwa aliungua akiepua maji moto.
      7. Mwoga – anaseama kwamba alimwogopa Bi. Sinai kwa sababu ya kumtisha kwamba angemkata ulimi kama angesema chochote kuhusu maisha yao ya ndani.
      8. Mwenye mawazo mapevu – Sebu anapomuuliza kwa nini hakumueleza masaibu yake nyumbani kwa Bi. Sinai, anamwambia kwamba hangeweza kufanya chochote kwa maana yeye alikuwa mtoto kama yeye.
      9. Mwenye kisasi - anapotoroka nyumbani mwa Bi. Sinai anaamua kurorejea nyumbani kwao na pia kutotaka kumwona mtu yeyote kwa sababu anaona kuwa masaibu aliyoyapitia nyumbani kwa Bi. Sinai yalisababishwa na wazazi wake.
        6x1=6
    4.      
      1. Inachimuza saula la umaskini – Wazazi wake Bogoa hawana uwezo wa kununua sabuni / Bogoa na baba yake wanatembea kwa miguu , bila ya viatu hadi mjini.
      2. Inaonyesha masaibu ya wanakijiji - Walikuwa na tatizo la maji kwa maana yalikuwa hayapatikani karibu . Walitembea masafa marefu kuyatafuta.
      3. Imemfumbulia Sebu fumbo alilotaka kufumbua – Amejua sababu ya Bogoa kutoroka nyumbani kwa Bi. Sinai.
      4. Kusawiri maudhui ya mapenzi – Mapezi ya Bogoa kwa nduguze na wazazi wake yalimfanya kutotaka kutengana na familia yake.
      5. Kusawiri maudhui ya elimu - Baba yake Bogoa anamwambia kwamba angepelekwa shuleni kusoma.
      6. Kuendeleza maudhui ya ajira ya Watoto – Bi. Sinai alimtumia Bogoa kufanya kazi za Nyumbani.
      7. Kuonyesha suala la ukiukaji wa haki za Watoto – Bi. Sinai anamtumia Bogoa kufanya kazi za nyumbani badala ya kumpeleka shuleni.
      8. Kuonyesha maudhui ya utabaka – Bi. Sinai anawaambia wanawe kwamba Watoto wa maskini hawastahili kusoma; kazi yao ni kutumwa.
      9. Kuonyesha maudhui ya uwajibikaji – Wazazi wake Bogoa walimtembelea ili kumjulia hali.
      10. Kuendeleza maudhui ya siri – Bogoa aliteseka sana mikononi mwa Bi. Sinai ila hakuwahi kumwambia rafikiye Sebu.
      11. Unajenga ploti/ msuko wa hadithi – Usimulizi wake unachimuza masuala kadhaa kama vile ukiukaji wa haki za Watoto umaskini n.k.
      12. Kubainisha masaibu ya Bogoa – Bi. Sinai hakumruhusu kutangamana na wazazi wake walipomtembelea, alikula makombo, anatusiwa, anasimbuliwa, anakatazwa kucheza na Watoto wengine.
        xiii. Unajenga sifa za wahusika. Kwa mfano, ukatili wa Sinai unabainika kutokana na usimulizi huu. Sinai anamchoma Bogoa mandazi yalipoungua.
        8x1=8
        Au
  7.    
    1. Viongozi kuweka vitego na vikwazo vya sheria ili watu wadogo wasiweze kutetea mali zao kama vile Mzee Mambo na Wanamadogoporomoka wengine wanajadiliana.
    2. Kutowahusisha maskini katika maamuzi muhimu yanayoathiri maisha yao.Mwansishi anaeleza kuwa maskini huonwa kama takataka na walio wakubwa hivyo basi hawawashirikishi katika maamuzi.
    3. Kunyakua ardhi ya madongoporomoka ambapo watu maskini waliishi.Kabwe analalamika kuwa hawajui watakapoenda baada ya ardhi yao kutwaliwa na wakubwa.
    4. Kupanga jama za kuwapatia wanyonge visenti vichache ili waondoke madongoporomoka.Visenti hivi havingeweza kuwapatia mahali pa kuishi ndiposa kabwe,Mzee Mago na wengine wanapinga kufurushwa kwao.
    5. Jitu la miraba minne kula chakula chote bila kubakishia wateja.Jitu linaagiza chakula chote katika mkahawa mshenzi wa Mzee Mago bila kujali waliokuwepo awali kama vile Kabwe,Bi. Suruta na wengine.
    6. wanamadongoporomoka kubomolewa vibanda vyao na mubuldoza.Hawakuwa wamepewa hata notisi ya kuondoka ilhali wanaamshwa na milio wakati mabuldoza yanafanya kazi.
    7. Askari wa baraza kutimua watu waliokuwa wanabomolewa.Askari wa jiji badala ya kuwalinda wanamadongoporomoka wanasaidia kuwafurusha huku wengine wakionekana na Rungu.
    8. Askari kuwapiga virungu watu. Wanamadongoromoka wanapigwa rungu na askari wa jiji ili waondoke kwenye ardi yao.
    9. Kukosa kupewa notisi ya kuhama; Wanamadongoporoka hawakupewa taarifa ya kufurusha.Wanaamshwa asubuhi kwa milio na buldoza kubomoa vibanda vyao.
    10. Uchafu na mashonde kupatikana katika madongoporomoka.Mwandishi anatueleza fika kuwa ardhi iliyopatikana ili jiji kupanuka ilipatika ktika sehemu hii ambapo kulisheheni uchafu na mashond ishara ya kuteleezwa kwa haki ya mazingira safi ya wenyeji.( zozote 10 x 1 = 10)
      • Kuvuja rasilmali za umma.Wafanyikazi vivuli wanaolipwa mshahara mkubwa. km Mambo.
      • Dawa za serikali kuuzwa katika duka la DJ na anazitoa kwenye bohari ya serikali
      • Sherehe ya kibinafsi kugharamiwa na pesa za serikali.
      • DJ kutolipia huduma ili acheze nyimbo za kejeli katika sherehe.
      • Matajiri kuwalipa wafuasi wao wakitumia pesa za umma. DJ analipwa mabilioni ya pesa kwa kucheza mziki katika sherehe yake
      • Wachache ndio wananufaika na jasho la watumishi wa umma
      • Sasa na Mbura kupakua chakula kingi na hata kurejea foleni mara zaidi ya tatu kupakua tena. Ishara ya kunyakua mali ya umma popote fursa inapatikana.
      • Watu wako tayari kuuana ili waendelee kujilimbikizia mali. Uk 44.
      • Viongozi kupakua mishahara.
      • Vyakula na vinywaji vya aina mbalimbali katika sherehe ya Mzee Mambo. Pesa zilizotumika kununua zingetumika kufanya jambo muhimu.
      • Kutumia magari ya serikali kwa sherehe ya kibinafsi.
      • Kuwafanya watu wa karibu kufaidi mali ya umma pasipo kutolea jasho. DJ ana duka la dawa ambalo mtaji wake ni bohari ya dawa za serikali.
      • Kuajiri viongozi wawili wenye nyadhifa sawa katika mataifa mengi ya Kiafrika. Sasa na Mbura ni mawaziri wawili wa wizara moja ya mipango na mipangilio.
      • Sherehe ya kibinafsi kupeperushwa katika runinga ya kitaifa moja kwa moja. Kwa kawaida jambo kama hili lafaa kulipiwa.
        Maelezo ya mwanafunzi yaafiki.
  8.    
    1. Kuonyesha vile tamaa ni hatari.
    2. Mtu mwenye tamaa ni hatari kama nyoka
      Mwenye tamaa ana unafiki / masengenyo
      Mwenye tamaa anaweza kuua
      Mwenye tamaa ni mchoyo
    3. Mishororo minne katika kila ubeti
      Migao/ vipande vitatu – ukwapi / utao / mwandamizi /Vina vitatu
      Mizani 8, 8, 8.
      Lina Kibwagizo- Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
      Lina beti sita (hoja zozote 4x1=4)
    4. Mwandishi anasema kuwa mwenye tamaa atakuwa na chuki iwapo utanunua kitu na anakuwa kama shetani kwani hafurahi. Mtu kama huyo atakasirika moyoni kwa kile ulichokifanya.
      Atakuonya ili akuvunje matumaini ya kutekeleza ulichonua. Anamalizia kw akusema kuwa mtu mwenye tamaa ni hatari kama nyoka.
    5. Takriri – kibwagizo
      Tashibihi – hatari kama nyoka
      Tashihisi – Bahati ina hadaa
      Nahau – Kinyesi kimetupiwa
    6. Inkisari – Ukweliwe, tajawa, asosema, alo, mpangoyo
      Mazida sheitani (Kurefusha she/ta/ni)
      Kufinyanga sarufi- Ninacho changu kilio badala ya ninacho kilio change nk
    7.        
      1. Zani = baa/ janga /balaa
      2. Faraghani – kwa siri
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Sukellemo Joint Pre Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest