Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - MECS Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO:

 • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
 • Kisha chagua insha moja nyingine kutoka hizo tatu zilizobaki.
 • Kila insha isipungue Maneno 400.
 • Kila insha ina alama 20.
 • Karatasi hii ina kurasa 2 zilizopigwa chapa.
 • Watahiniwa ni lazima wahakikishe kuwa kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

Kwa matumizi ya mtahini pekee

Swali

Upeo

Alama

1

20

 

 

20

 

Jumla

40

 MASWALI

SWALI LA LAZIMA.

 1. Shuleni mwenu kumekuwa na visa vingi vya matumizi ya mihadarati. Wewe ni katibu wa chama kilichobuniwa kuchunguza sababu za wanafunzi wengi kutumia mihadarati- Chama cha Wapekuzi. Andika kumbukumbu za mkutano ulizoandika kuhusu sababu za vijana wengi kutumia mihadarati nchini.
 2. Teknolojia ya kisasa ni kama sarafu yenye sura mbili; ina faida na hasara. Jadili.
 3. Tunga kisa kitakachooana na methali ifuatayo;
  Asante ya punda ni mateke.
 4. Andika kisa kitakachomalizia kwa maneno yafuatayo;
  ...nilipozinduka kutoka usingizini, nilijipata bado nikiwa katika hali yangu ya umaskini hohehahe. Kumbe ilikuwa ni ndoto!


MWONGOZO

VIWANGO MBALIMBALI KATIKA UKADIRIAJI
KIWANGO CHA D KWA JUMLA MAKI 01-05

 1. Insha haieleweki kwa vyovyote vile ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana, hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile mtahiniwa anachojaribu kuwasilisha.
 2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahiuli kwa njia inayofaa.
 3. Lugha imevurugika, uakifishaji haufai na insha ina makossa ya kila aina.
 4. Kujitungia swali na kulijibu.
 5. Kunakiri swali au kichwa tu.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA D
D- (D YA CHINI) MAKI 01-02

 1. Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile.
 2. Kujitungia swali tofauti na kulijibu.
 3. Kuandia kwa lugha isiyo ya Kiswahili au kuchanganya ndimi.
 4. Kunakili swali au maswali na kuyakariri.
 5. Kunakiri swali au kichwa tu.

D WASTANI MAKI 03

 1. Mtiririko wa mawazo haupo.
 2. Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.
 3. Matumizi ya lugha ni hafifu mno.
 4. Kuna makossa mengi ya kila aina.

D+ (D YA JUU) MAKI 04-05

 1. Insha ya aina hii huwa na makosa mengi ya kila aina, lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha.
 2. Hoja hazikuelezwa kikamilifu/ mada haikukuzwa vilivyo.
 3. Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha.
 4. Mtahiniwa hujirudiarudia.
 5. Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa.

KIANGO CHA C KWA JUMLA MAKI 06-10

 1. Mtahiniwa amejaribu kushughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.
 2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia/ hana ubunifu wa kutosha.
 3. Mtahiniwa naakifisha sentensi vibaya.
 4. Mtiririko wa mawazo unaanza kujitokeza japo kwa njia hafifu.
 5. Insha ina makossa mengi ya sarufi, msamiati na tahajia (hijai)
 6. Insha ya urefu wa nusu ikadiriwe hapa.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA C
C- (C YA CHINI) MAKI 06-07

 1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.
 2. Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.
 3. Mtahiniwa anafanya makossa mengi ya sarufi, ya hijai nay a msamiati na insha yake haieleweki kwa urahisi.

C WASTANI MAKI 08

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
 2. Dhana tofautitofauti hazijajitokeza wazi.
 3. Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.
 4. Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi unaofaa.
 5. Amejaribu kuishughulikia mada aliyopewa.
 6. Mtahiniwa ana shida ya uakifishaji.
 7. Mtahiniwa anafanya makossa mengi ya sarufi, hijai nay a msamiati lakini bado insha inaeleweka.

C+ (C YA JUU) MAKI 09-10

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyo na mvuto.
 2. Dhana tofautitofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu.
 3. Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.
 4. Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.
 5. Ana shida ya uakifishaji.
 6. Kuna makossa ya sarufi, msamiati na ya hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

KIWANGO CHA B KWA JUMLA MAKI 11-15
B- (B YA CHINI) MAKI 11-12

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofautitofauti akizingatia mada.
 2. Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.
 3. Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia.
 4. Makosa yanadhihirika kiasi.

B WASTANI MAKI 13

 1. Mtahiniwa adhihirisha hali ya kuimudu lugha.
 2. Mawazo ya mtahiniwa yadhihirika akizingatia mada.
 3. Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
 4. Sarufi yake ni nzuri.
 5. Makosa ni machache.

B+ (B YA JUU) MAKI 14-15

 1. Mawazo ya mtahiniwa yadhihirika na anajieleza waziwazi.
 2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
 3. Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.
 4. Sarufi yake ni nzuri.
 5. Uakifishaji wa sentensi zake ni mzuri.
 6. Makosa yake ni machache ya hapa na pale.

KIWANGO CHA A KWA JUMLA MAKI 16-20

 1. Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka akizingatia mada.
 2. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.
 3.  Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemi ili kutoa hisia zake kwa njia bora na kwa urahisi.
 4. Umbuji wake unadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake wa kimawazo.
 5. Insha ina urefu kamili.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA A
A- (A YA CHINI) MAKI 16-17

 1. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.
 2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anaishughulikia mada.
 3. Ana mtiririko mzuri wa mawazo.
 4. Sarufi yake ni nzuri.
 5. Anatumia miundo tofautitofauti kiufundi.
 6. Makosa ni machache yasiyokusudiwa.

A WASTANI MAKI 18

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kulingana na mada.
 2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato.
 3. Anatoa hoja zilizokomaa.
 4. Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia Zaidi.
 5. Anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi kiufundi.
 6. Makosa ni nadra kupatikana.

A+ (A YA JUU) MAKI 19-20

 1. Mawazo yanadhihirika Zaidi na mada imeshughulikiwa vilivyo.
 2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato.
 3. Hoja zake zimekomaa na zinashawishi.
 4. Msamiati wake ni wa hali ya juu na unavutia Zaidi.
 5. Sarufi yake ni nzuri Zaidi.
 6. Anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi kiufundi.
 7. Makosa yote kwa jumla hayazidi matano.

1. SWALI LA LAZIMA.
Shuleni mwenu kumekuwa na visa vingi vya matumizi ya mihadarati. Wewe ni katibu wa chama kilichobuniwa kuchunguza sababu za wanafunzi wengi kutumia mihadarati- Chama cha wapekuzi. Andika kumbukumbu za mkutano ulizoandika kuhusu sababu za vijana wengi kutumia mihadarati nchini.

 • Muundo wa kumbukumbu uzingatiwe.
 • Kichwa kitaje jina kumbukumbu, jina la kikundi, mahali, saa na tarehe ya mkutano huo.
 • Kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa, kipigiwe mstari na kisitoneshwe.
 • Majina ya waliohudhuria na vyeo vyao vionyeshwe vikianza na mwenyekiti, naibu mwenye kiti, katibu, mwekahazina kasha wanachama.(baada ya kuandika cheo asitoneshe)
 • Alama ya majina ya waliohudhuria isiwe refu mno.
 • Agenda ziorodheshwe vilivyo zikianza kwa kufunguliwa kwa mkutano, kusomwa na kudhibitishwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia, yaliyotokana na kumbukumbu hizo kasha maudhui manane au Zaidi.
 • Maudhui/ Hoja zijitokeze kikamilifu.

Baadhi ya hoja ni;
Sababu za kutumia mihadarati miongoni mwa vijana

 1. Kutokana na shinikizo la rika/ kushawishiwa na marafiki miongoni mwa vijana.
 2. Ukosefu wa ushauri dhidi ya kutumia dawa hizo.
 3. Ukosefu/ upungufu wa vielelezo bora katika jamii.
 4. Vijana wengine hutumia ili kujipa burudani/ raha.
 5. Tamaa ya kujaribu.
 6. Kuwepo kwa dawa hizi kila mahali.
 7. Msongo wa mawazo kutokana na shinikizo la kijamii.
 8. Sheria hafifu zinazowafanya wauzaji na watumiaji kuendeleza shughuli bila wasiwasi wowote.
 9. Kuvunjika kwa muundo wa mshikamano wa wa jamii/ uozo katika jamii (watu wako huru kufanya watakavyo)
 10. Kuporomoka kwa maadili ya kijamii.
 11. Kupuuzakwa vijana wengi wanaojua madhara yake.
 12. Kushindwa kwa wazazi kudhibiti watoto wao.
 13. Shida na umaskini- wengine hutumia ili wasahau matatizo yanayowakabili.
 14. Kuwa na pesa/ mali nyingi hufanya wengi kutumbukia katika lindi hili.
 15. Wengine hutumia ili wapate sifa kama vile ujasiri, kujiamini, kuwa huru.

2. Njia za kupambana na ufisadi

 1. Hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wanaoshiriki ufisadi.
 2. Kuwaelimisha wananchi kuhusu hasara za ufisadi.
 3. Kuwaachisha na kuwafuta kazi wafisadi.
 4. Kuarifu polisi au mashirika ya kupambana na ufisadi kuhusu visa vya ufisadi.
 5. Kuwalipa wafanyikazi mishahara inayolingana na hali ya kiuchumi.
 6. Viongozi kutangaza mali zao hadharani.
 7. Kujifunza kutosheka na kile mtu alichonacho na kuishi maisha ya kiwango chake.
 8. Kumcha Mungu.
 9. Watu kunyang’anywa pesa/ mali waliopata kwa njia ya ufisadi.
 10. Majina ya wale wafisadi kuanikwa hadharani.
 11. Mashirika ya kupambana na ufisadi yachunguze washukiwa wa ufisadi.
 12. Hakuna msiba usiookuwa na mwenziwe
 13. Matokeo mabaya mara nyingine humjia mtu ghafla kwa mfululizo, mmoja baada ya mwingine.

2. Teknolojia ya kisasa ni kama sarafu yenye sura mbili; ina faida na hasara. Jadili.
Faida za teknolojia

 1. Kusafiri kwenda kila mahali ulimwenguni kumerahisishwa.
 2. Afya na matibabu zimeimarika.
 3. Uhusiano wa nchi umeboreshwa.
 4. Uchukuzi wa haraka umeimarika k.v kutumia ndege.
 5. Usalama umeimarika.
 6. Mawasiliano yamerahihishwa na kuharakishwa.
 7. Biashara imeimarika.
 8. Mwingiliano wa tamaduni umeboreka.
 9. Nafasi za kazi ng’ambo zimetangazwa na kuongezeka.
 10. Utangamano kwa jumla umeimarika.
 11. Mapishi jikoni yamerahisishwa kutumia vifaa kama tanuri.
 12. Uvumbuzi wa aina nyingi ya nishati badala ya kutegemea umeme- mvuke, nguvu za upepo. Nk
 13. Kutumia kanda za video kujiburudisha.
 14. Masomo yamerahisishwa- kufunza na kufanya utafiti kutumia mitandao.
 15. Shughuli za kitaifa kama vile kuhesabu kura.
 16. Nafasi za ajira zimeongezeka- kuna watu wanauza simu na vifaa vyake.
 17. Biashara kupitia kwa mtandao.

Hasara za teknolojia

 1. Kupoteza muda mwingi mtandaoni.
 2. Wahalifu wanaweza kusikiliza mawasiliano ya watu na pia kupanga maovu
 3. Kuna uundaji wa silaha hatari zinazotishia kuangamiza watu- mabomu
 4. Uzembe kutokana na uraibu hivyo watumiaji wanasahau kuwajibika vilivyo kwa kazi zao.
 5. Kupotoka kwa maadili pamoja na utovu wa nidhamu hasa kupitia kutazama ngono, lugha chafu, wavazi yasiyofaa nk.
 6. Husababisha magonjwa ya macho.
 7. Matatizo ya kiafya kutokana na vyakula vinavyosemekana kukuzwa kiteknolojia zenye kemikali nyingi.
 8.  Ajali ya gari moshi stima zinapoanguka watu wengi hufa.
 9. Kuongezeka kwa uhalifu, kama vile wizi wa mtihani.
 10. Ubadhirifu wa pesa kwani gharama yake iko juu kununua na kutumia.
 11. Uozo katika jamii hasa miongoni mwa vijana kwa maana mitandao inaonyesha mambo ambayo ni miiko kwa jamii.
  (Kadiria majibu ya mwanafunzi)

3. Tunga kisa kitakachooana na methali ifuatayo;
Asante ya punda ni mateke.

 • Lazima mtahiniwa atafsiri maana ya methali katika kisa cha kusisimua.
 • Afahamu kwamba lazima pande zote mbili za methali zijitokeze.
 • Kisa chenyewe kiweze kidhihirisha hali ambapo mhusika atapuuza fadhili aliyotendewa na mwenzake ama pia alipe wema aliotendewa kwa kumtendea mabaya.
 • Usaliti ujitokeze katika kisa.
 • Anwani ya insha iwe ni methali yenyewe

4.  Andika kisa kitakachomalizia kwa maneno yafuatayo, ………..nilipozinduka kutoka usingizini, nilijipata bado nikiwa katika hali yangu ya umaskini hohehahe. Kumbe ilikuwa ni ndoto!

 • Kisa lazima kimalizie kwa maneno hayo bila kubadilisha.
 • Mtahiniwa aweza kuongea kuhusu kisa chake mwenyewe.
 • Lazima kisa kiwe ni ndoto ya kusisimua iliyohusu maisha ya kifahari kinyume na hali yake ya kawaida.
 • Insha irebeshwe vilivyo kwa kutumia tamadhali zote za usemi na iwe na lugha ya mnato.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - MECS Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?