Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - MECS Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Jibu maswali yote.
  2. Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
  3. Usitoe ukurasa wowote kutoka kwenye kijitabu hiki.

Kwa matumizi ya mtahini pekee

Swali

Upeo

Alama

1

15

 

2

15

 

3

40

 

4

10

 

Jumla

80

 



MASWALI

1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Zamani wanadamu wa kwanza ambao ni mababu wa vizazi vingi vilivyopita waliishi duniani. Habari kuhusu maisha na maumbile yao haikujulikana kwa hakika kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kuandika. Lakini mara kwa mara shughuli za wanaakiolojia kama Louis Leakey na wengine hugundua mifupa yao ardhini na michoro yao katika mapango. Wataalamu hawa hufukua mafuvu, vyombo na silaha zao za zamani. Kwa kuchuguza vitu hivi tunaweza kubahatisha viumbe hawa walivyokuwa na jinsi walivyoishi.
Moja ya mambo yanayofahamika sasa ni kuwa wanadamu hawa wa awali walifanana na sokwe. Aidha, walitembea kwa kupinda mgongo kama kibiongo. Chakula na uhai wao ulitegemea kukusanya matunda, kokwe, majani ya miti na mayai ya ndege. Vilevile, walitegemea wanyama wadogo, kufukua mizizi na kubambua magamba ya miti walipokabwa na njaa.
Maisha yao yalikuwa ya hatari. Walikuwa wakiwindwa na wanyama wakubwa. Hii ni kwa sababu mwanzoni hawakuwa na silaha za kujihami. Hivyo iliwabidi kujificha katika miti na vilima kuepuka uvamizi. Lakini usalama wao ulitegemea kwa kiasi kikubwa kudura za Mungu au pengine miungu.
Kwa taratibu wanadamu hawa walijifunza kutengeneza silaha. Walianza kwa kutumia fimbo nene zenye ncha au mawe ya kutupia. Baadaye walichonga mawe ili kufanya kuwa visu, nyundo au vigumba vya mikuki. Hatimaye, walivigomoa au kupasua vipande vya mawe na kuvitumia kama mishale. Hapa ndipo walipoanza kuwinda wanyama wakubwa mithili ya swara, nguruwe, nyati na ngiri. Pia waliweza kutumia mikuki kudunga samaki majini.
Mababu zetu hawakuwa na nyumba. Kwanza walikuwa wakijisitiri kwa kukaa chini ya vivuli vya miti au kujenga vibanda vya matawi na majani ya miti. Hawakuweza kuingia mapangoni asilani kwa kuchelea wanyamapori wakali kama chatu, simba na mamba waliokaa humo. Kwa bahati, siku moja mmoja wao aligundua moto alipokuwa akipekecha vijiti. Kabla ya ugunduzi huu, wao pia hawakujua kazi ya moto na walikuwa wakiogopa na kukimbia moto jinsi wafanyavyo wanyama wa mbugani mpaka leo.
Ujuzi wao wa kutumia moto ulileta mabadiliko makubwa. Baada ya hapo waliweza kukaa mapangoni na kukoka mioto milangoni mwa mapango ili kuwaogofya adui. Hali kadhalika, waliweza kuota moto, kumulikia maskani yao mapya na kuchoma nyama badala ya kuila mbichi.
Wanadamu wa awali hawakuwa na mavazi. Waliwezaje kuzuia baridi? Inadhaniwa kwamba nywele nyingi walizokuwa nazo kwenye mwili zilisaidia kuwapa joto. Uvaaji wa nguo ulianza walipoanza kutumia ngozi kutoka kwa wanyama waliowawinda. Walizisafisha ngozi kwa kuzipaa kwa kombe za mawe na kuzianika juani. Zilipokauka walizifunga na kuzishikanisha kwa mifupa au mikanda ya ngozi.
Wanadamu hawa hawakuweza hata kuongea. Waliwasiliana kwa kupiga mayowe, kutoa milio au kuguruma jinsi wafanyavyo wanyama. Polepole walianza kutumia sauti na baada ya muda walipanga sauti kuibua mfumo wa maneno yenye maana za kipekee. Umilisi wa kutumia lugha uliwawezesha kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Lugha pamoja na matumizi ya moto na silaha viliwarahisishia maisha na kuwawezesha kupata muda wa kupumzika mapangoni jioni wakiota moto. Kutokana na hali hii waliweza kutekeleza jambo moja kuu waliloturithisha. Walitupokeza Sanaa. Kutoka kwao tulirithi fasihi simulizi na kupata nakshi za michoro yao kwenye mapango. Michoro hii inapatikana katika mapango hata leo hii nchini Ufaransa, Uhispania, Afrika Kusini na hata Afrika Mashariki.

MASWALI

  1. Msemo “Kudura za Mungu au pengine miungu” inadhihirisha hali gani ya wanadamu wa kwanza. ( alama 2)
  2. Kwa nini wanadamu hawakuishi mapangoni mwanzoni? (alama 1)
  3. Fafanua mambo matano yaliyomwezesha mwanadamu wa kwanza kupiga hatua kimaendeleo. (alama 5)
  4. Taja sifa zilizotofautisha wanadamu wa awali na wa siku hizi? (alama 2)
  5. Eleza maana ya? (alama 3)
    1. walipokabwa
    2. kujihami
    3. maskani

2. UFUPISHO( ALAMA 15)
Uwazaji tunduizi ni tendo ambalo huhusisha matumizi ya akili. Uwazaji huu umekitwa kwenye matumizi ya michakato kama makini, upangiliaji, uteuzi na tathmini. Hata hivyo, uwazaji huu si mchakato mwepesi bali ni mchakato changamano.
Mchakato wa uwazaji tunduizi unahusisha stadi na mikabala tofauti. Mathalan, kuweza kutambua na kubainisha misimamo ya watu wengine, hoja wanazozua na uamuzi waliofikia kutathmini au kupima ushahidi uliopo ili kubainisha mitazamo tofauti. Vilevile, uwazaji tunduizi hushirikisha kupima hoja za upinzani na ushahidi uliopo kwa njia ya haki pamoja na kutambua yaliyofichwa au ukweli uliofunikwa na taswira ya juu juu. Hali kadhalika, uwazaji tunduizi hujumisha kutambua mbinu zinazotumiwa kufikia misimamo fulani kwa mvuto zaidi na kwa matumizi ya mbinu za kishawishi. Aidha, uwazaji huu huhitaji kutathmini masuala kwa mtindo ulio wazi, kufikia uamuzi kama hoja zinazotumiwa zina mashiko au zinakubalika kuwa nzuri. Zaidi ya hayo, uwazaji tunduizi unahusisha kuwasilisha mtazamo kwa njia yenye uwazaji mzuri na inayoshawishi.
Uwazaji tunduizi una manufaa anuwai. Mosi, unasaidia kujenga makini ya utendaji. Pili, hupevusha uwezo wa usomaji kwa kuufanya usomaji huo uwe na malengo wazi. Fauka ya hayo unamsaidia mtumiaji kutambua hoja kuu katika matini au ujumbe fulani ya kuzongwazongwa na hoja duni za pembeni. Uwazaji huu unasaidia kuuchonga uwezo wa kuikabili au kuiitikia hali fulani na kukuza stadi za uchanganuzi. Mwanadamu huwa mtu tofauti na bora anapoujenga na kuuimarisha uwazaji tunduizi wake.

Maswali

  1. Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha aya mbili za mwanzo. (maneno 70-80) (alama 8, 1 utiririko)
    Matayarisho

    Jibu
  2. Andika kwa muhtasari mambo muhimu katika aya ya tatu. (maneno 35-40) (alama 5, 1 ya utiririko)
    Matayarisho

    Jibu

3. MATUMIZI YA LUGHA( ALAMA 40)

  1. Tofautisha sauti zifuatazo. (alama 2)
    1. /ny/ na /m/
    2. /a/ na /u/
  2. Andika neno lenye muundo ufuatao wa silabi. (alama 1)
    K-KKI
  3. Ainisha nomino katika sentensi hii.
    Kuuza sukari kwa Rehema kulimfanya awe na utajiri. (alama 2)
  4. Geuza sentensi ifuatayo iwe katika hali yakinishi.
    Mtoto hakupatiwa chakula wala nguo. (alama 1)
  5. Kwa kutoa mifano, ainisha aina mbili za mofimu. (alama 2)
  6. Andika katika hali ya ukubwa wingi. (alama 2)
    Mwanamke alibeba kiti chake.
  7. Ainisha yambwa katika sentensi hii. (alama 3)
    Mtoto alipikiwa chakula kizuri kwa mwiko.
  8. Tunga sentensi yenye kivumishi cha pekee chenye dhana ya kutojali. (alama 2)
  9. Kwa kutunga moja sentensi tofautisha kati ya vitate hivi. (alama 2)
    Mzazi na msasi.
  10. Eleza maana ya kiambishi “ji” katika sentensi hii.
    Mchezaji alijikata kwa kisu. (ala1)
  11. Taja ngeli za nomino zifuatazo. (alama 1)
    Kiwete

    Maji
  12. Tunga sentensi ukitumia neno vile kama kitenzi na kivumishi. (alama 2)
  13. Ainisha virai tofauti katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
    Mwalimu yule mzuri sana alikuja darasani mapema sana.
  14. Onyesha matumizi ya viakifishi vifuatavyo; (alama 2)
    1. kibainishi
    2. vifungo
  15. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi. (alama 4)
    Kitabu kilichonunuliwa ni hiki.
  16. Sahihisha kwa njia mbili tofauti. (alama 2)
    Mwanafunzi alifika katika nyumbani
  17. Eleza maana ya nahau kula mwata. (alama 1)
  18. Tambulisha hali katika sentensi hii. (alama 1)
    Mtoto acheza.
  19. Andika kulingana na maagizo. (alama 2)
    Mtoto alipoenda Mombasa alijawa na furaha. (anza kwa: Kwenda…) 

4. ISIMU JAMII (ALAMA10)

  1. Umeteuliwa kama mtangazaji wa mashindano ya michezo baina ya shule katika eneo gatuzi ndogo lenu. Eleza sifa tano za lugha utakayotumia. (alama 5)
  2. Jadili mambo matano yanayoathiri matumizi ya lugha katika jamii. (alama 5)


MWONGOZO

UFAHAMU

  1. Hawakuweza kujikinga na haieleweki walivyookoka uvamizi hali ya unyonge – kuonyesha hawakuwa na uwezo mwa kujikinga kutokana na hatari. (yoyote 1x2)
  2. Wanyama hatari waliishi humo. (1x 1)
  3.                        
    1. Uwezo wa kutumia silaha kujikinga na kupata chakula.
    2. uvumbuzi wa moto uliomwezesha kuishi pangoni.
    3. Uwezo wa kutumia lugha kuwasiliana.
    4. mavazi ili kuzuia baridi
    5. kujenga nyumba ili kujisitiri (zozote 5x1)
  4.                      
    1. Walitembea kwa kuinama
    2. Walikuwa na nywele nyingi mwilini
    3. Walifanana na sokwe
    4. Hawakuwa na uwezo wa kuandika
    5. Hawakuweza kuongea/ waliwasiliana kwa mayowe na kupiga duru ( zozote 4x1)
      ( kadiria hoja nyingine zozote kutoka kwenye kifungu)
  5.                        
    1. Walipohisi, walipoona, walipokumbwa (1/0)
    2. Kujilinda, kujitetea (1/0)
    3. Makaazi, makao, nyumbani (1/0)

UFUPISHO

  1.                    
    1. Uwazaji tunduizi nitendo ambalo huhusisha matumizi ya akili.
    2. Umekitwa kwenye mizizi ya michakato kama makini, upangiliaji, utenzi na tathmini/ Umekitwa kwa mizizi ya michakato mbalimbali.
    3. Uwazaji si mchakato mwepesi/ Uwazaji ni mchakato changamano.
    4. Uwazaji tunduizi unahusisha stadi na mikabala tofauti.
    5. Hushirikisha kupima hoja za upinzani na ushahidi uliopo kwa njia ya haki/ukweli uliofunikwa na taswira ya juu juu.
    6. Hujumuisha kutambua mbinu zinazotumiwa kufikia msimamo fulani kwa mvuto zaidi na ka matumizi ya mbinu za kishawishi.
    7. Huhitaji kutathmini masuala kwa mtindo ulio wazi kufikia uamuzi.
    8. Huhusisha kuwasilisha matazamo kwa njia yenye uwazaji mzuri na inayoshawishi.
      ( hoja 8, 1 utirirko = 9)
  2.                        
    1. Unasaidia kujenga makini ya utendaji
    2. Hupevusha uwezo kutambua hoja kuu katika matini.kutambua ujumbe fulani bila kuzongwazongwa na hoja duni za pembeni.
    3. Unasaidia kuuchonga uwezo wa kuikabili hali Fulani/unasaidia kuitikia hali Fulani.
    4. Unasaidia kukuza stadi za uchanganuzi.
    5. Binadamu huwa mtu tofauti na bora anapojenga na kuuimarisha uwazaji tunduizi wake.
      ( hoja 5, 1 utiririko = 6)

MATUMIZI YA LUGHA

  1.                          
    1. /ny/ ni ya Kakaa gumu
      /m/ ni ya midomoni (1/0)
    2. /a/ Chini/kati/tandaze
      /u/ juu/ nyuma/viringe ( 1/0)
  2. M-bwa, m-pwa, m-chwa, m-kwe ( zingatia silabi) (1/0)
  3. Kuuza – kitenzi jina
    Sukari – wingi
    Rehema – pekee
    Utajiri – dhahania (½ x 4 )
  4. Mtoto alipatiwa chakula na nguo
  5. Mofimu huru – baba
    Mofimu tegemezi – a-li-som-a (kadiria majibu) (lazima atenge mofimu zenyewe)
    ( kutaja ½, mfano ½ )
  6. Majanajike yalibeba majikiti yayo. (2/0) (sahihisha sentensi moja, ya kwanza)
  7. Mtoto – tendewa/ kitondo
    Chakula (kizuri) – tendwa/kipozi
    Mwiko – tumizi ( asichanganye shamirisho na yambwa) ( 3x1)
  8. O-ote ( atunge sentensi moja) (2/0)
  9. Mzazi – aliyekuzaa
    Msasi – mwindaji (sentensi moja na maana idhihirike wazi) ( 2 x 1)
  10. Mchezaji – unominishaji/mazoea/uundaji wa nomino
    Alijikata – kirejeshi/kijitendea ( ½ x 2 )
  11. A/WA
    YA/YA ( ½ x 2)
  12. Vile vyakula vile
    (T) (v) ( 2 x 1)
  13. mwalimu - RN
    Mwalimu yule
    Mwalimu yule mzuri sana RN
    Yule mzuri sana RV
    Alikuja darasani RT
    Darasani mapema sana RE
    Mapema sana RE ( vyovyote 3 x 1)
  14.                      
    1. Kuonyesha ung’ong’o – ng’ombe
      Kufupisha – usiseme ’siseme
    2. Kuzungira herufi (a)
      Maelezo ya ziada
      (Kadiria majibu) ( 2x 1)
  15.                        
    16 siuhauihda
  16. Mwanafunzi alifika nyumbani
    Mwanafunzi alifika katika nyumba
    Mwanafunzi alifika ndani ya nyumba
    Mwanafunzi alifika kwa nyumba. ( zozote 2x 1)
  17. Kupata shida ( 1/0)
  18. Hali isiyodhihirika (1/0)
  19. Kwenda kwa mtoto Mombasa kulimfanya awe na furaha ( afurahie). (kadiria majbu mengine sahihi)

ISIMU JAMII

  1.                    
    1. msamiati maalum – mpira, mchezaji, uwanja
    2. lugha yenye misimu – sare,
    3. lugha ya uradidi – anakwenda anakwenda
    4. lugha ya ucheshi –
    5. matumizi ya chuku –
    6. utohozi
    7. kuchanganya / kuhamisha msimbo –
    8. kauli fupifupi –
    9. matumizi ya vihisishi-
    10. kauli zisizokamilika (mdokezo)
      ( kadiria siafa zaidi) (zozote 5x1 )
  2.                        
    1. Umri
    2. Mazingira
    3. Uhusiano
    4. Tabaka
    5. Jinsia
    6. Mada
    7. Wakati ( zozote zilizofafanuliwa 5x 1)

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - MECS Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?