Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Arise and Shine Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Andika insha mbili.  Insha ya kwanza ni ya lazima kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  2. Kila insha isipungue maneno 400.
  3. Kila insha ina alama 20.
  4. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  5. Karatasi hii ina kurasa 2 zilizopigwa chapa. 
  6. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

Kwa Matumizi ya Mtahini Pekee

SWALI

UPEO

ALAMA

1

20

 
 

20

 

Jumla

40

 


MASWALI

  1. Umetangazwa kuwa mwanafunzi bora katika mtihani wa kitaifa.  Mwalimu Mkuu wa shule ya upili ya Tuamke amekualika katika shule hii yake kuwahutubia  wanafunzi kuhusu kilichochangia ufanisi wako.  Andika hotuba yako.
  2. Fafanua hatua ambazo jamii imechukua kuimarisha maisha ya wanawake katika jamii.
  3. Andika kisa kinachodhihirisha maana ya methali; Mui huwa Mwema.
  4. Andika insha itakayomalizia kwa:  Nilijitazama na kujidharau kwa nini sikuwafahamisha walimu jambo hilo mapema.

MTIHANI WA MUUNGANO WA ARISE AND SHINE (KCSE) JARIBIO LA KWANZA, 2023.
UTANGULIZI.



MWONGOZO WA KUDUMU

Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi,akizingatia mada aliyopewa. Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa, kwa mfano, kutunga sentensi sahihi zenye mtiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asilia, ubunifu mwingi na hati nadhifu. Kwa kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo. Mtahini lazima aisome insha yote huku akizingatia sarufi, hijai, hoja, msamiati na mtindo ili aweze kuikadiria kwa kurejelea viwango mbalimbali vilivyopendekezwa. Viwango vyenyewe ni A, B, C na D kutegemea uwezo wa mtahiniwa.

VIWANGO MBALIMBALI.
KIWANGO CHA D KWA JUMLA MAKI 01-05.

  1. Insha haieleweki kwa vyovyote vile ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana, hivi kwamba mtahinilazima afikirie kile mtahiniwa anachojaribu kuwasilisha.
  2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.
  3. Lugha imevurugika, uakifishaji haufai na insha ina makosa ya kila aina.
  4. Kujitungia swali na kulijibu.
  5. Insha ya urefu wa robo ikadiriwe hapa.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA D.
D-(D YA CHINI) MAKI 01-02.

  1. Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile.
  2. Kujitungia swali tofauti na kulijibu
  3. Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya ndimi.
  4. Kunakili swali au maswali na kuyakariri.
  5. Kunakili swali au kichwa tu.

D WASTANI MAKI 03.

  1. Mtiririko wa mawazo haupo.
  2. Mtahiniwa amepotoka kimaudhui. 
  3. Matumizi ya lugha ni hafifu mno.
  4. Kuna makosa mengi ya kila aina.

D+ (D YA JUU) MAKI 04-05.

  1. Insha ya aina hii hukuwa na makosa mengi ya kila aina, lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha.
  2. Hoja hazikuelezwa kikamilifu/ mada haikukuzwa vilivyo.
  3. Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha.
  4. Mtahiniwa hujirudiarudia.
  5. Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa.

KIWANGO CHA C KWA JUMLA MAKI 06-10.

  1. Mtahiniwa anajaribu kuishughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.
  2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia
  3. Mtahiniwa anaakifisha sentensi vibaya.
  4. Mtiririko wa mawazo unaanza kujitokeza japo kwa njia hafifu.
  5. Insha ina makosa mengi ya sarufi, ya msamiati na ya tahajia (hijai). 

C-(C YA CHINI) MAKI 06-07.

  1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.
  2. Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.
  3. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati na insha yake haieleweki kwa urahisi.

C WASTANI MAKI 08.

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
  2. Dhana tofauti tofauti hazijitokezi wazi.
  3. Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.
  4. Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.
  5. Anajaribu kushughulikia mada aliyopewa.
  6. Mtahiniwa ana shida ya uakifishaji.
  7. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati lakini bado insha inaeleweka.

C+ (C YA JUU) MAKI 09-10.

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyo na mvuto.
  2. Dhana tofauti tofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu.
  3. Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.
  4. Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.
  5. Ana shida ya uakifishaji.
  6. Kuna makosa ya sarufi, ya msamiati na ya hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

KIWANGO CHA B KWA JUMLA MAKI 11-15

  1. Mtahiniwa anaonyesha hali ya kuimudu lugha.
  2. Mtahiniwa anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.
  3. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha.
  4. Mada imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.
  5. Insha ya urefu wa robo tatu ikadiriwe katika kiwango hiki.
    Ngazi mbalimbali za kiwango cha B.

B- (B YA CHINI) MAKI 11-12

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofauti tofauti akizingatia mada.
  2. Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.
  3. Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia.
  4. Makosa yanadhihirika kiasi.

B WASTANI MAKI 13

  1. Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
  2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika akizingatia mada.
  3. Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
  4. Sarufi yake ni nzuri.
  5. Makosa ni machache/ kuna makosa machache.

B+(B YA JUU) MAKI 14-15

  1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anajieleza waziwazi.
  2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
  3. Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.
  4. Sarufi yake ni nzuri.
  5. Uakifishaji wa sentensi zake ni mzuri.
  6. Makosa ni machache ya hapa na pale.

KIWANGO CHA A KWA JUMLA MAKI 16-20

  1. Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka akizingatia mada.
  2. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.
  3. Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemi ili kutoa hisia zake kwa njia bora na kwa urahisi.
  4. Umbuji wake unadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake kimawazo.
  5. Insha ina urefu kamili.

USAHIHISHAJI NA UTUNZAJI KWA JUMLA.
Mtahini ni sharti aisome insha yote akizingatia vipengee muhimu. Vipengee hivi ni maudhui, msamiati, mtindo, sarufi na hijai.

MAUDHUL
Maudhui ni hoja au mambo yanayozungumziwa, kuelezewa au kuhadithiwa kwa mujibu wa mada iliyoteuliwa. Maudhui ndio hasa uti wa mgongo wa insha yoyote ile. Ubunifu wa mtahiniwa hukisiwa kwa kutathmini uzito wa maudhui yake kulingana na mada teule.

MSAMIATI.
Msamiati ni jumla ya maneno yatumiwayo katika lugha husika. Mtahiniwa anatarajiwa kutumia msamiati unaooana na mada teule. Kutegea ukwasi wa lugha alionao, mtahiniwa anatarajiwa kuikuza mada kwa kuifinyanga lugha kiufundi. Ni muhimu kuelewa kwamba kutokana na maendeleo na ukuaji wa teknolojia na mawasiliano, maneno mapya yanaibuka kila uchao.

MTINDO.
Mtindo unahusu mambo yafuatayo:

  • Mpangilio wa kazi kiaya.
  • Mtiririko na mshikamano wa mawazo kiaya na katika insha nzima.
  • Hati nzuri na inayosomeka kwa urahisi.
  • Matumizi ya tamathali za usemi, kwa mfano methali, misemo, jazanda na kadhalika.
  • Kuandika herufi vizuri kwa mfano Jj, Pp, Uu, Ww na kadhalika.
  • Sura ya insha.
  • Unadhifu wa kazi ya mtahiniwa.

SARUFI.
Sarufi ndio msingi wa lugha. Ufanisi wa mawasiliano hutegemea uwezo wa mtahiniwa wa kutunga sentensi sahihi zenye uwiano wa kisarufi. Mtahini ataonyesha makosa yote ya sarufi yaliyo katika insha anayosahihisha. Makosa ya sarufi huweza kutokea katika:
Matumizi ya alama za uakifishaji.

  1. Kutumia herufi kubwa na ndogo mahali pasipofaa.
  2. Matumizi yasiyofaa ya ngeli na viambishi, viunganishi, nyakati, hali, vihusiano na kadhalika.
  3. Mpangilio wa maneno katika sentensi.
  4. Mnyambuliko wa vitenzi na majina.
  5. Kuacha neno linalohitajika au kuongeza neno lisilohitajika katika sentensi.
  6. Matumizi ya herufi kubwa katika:
    1. Mwanzo wa sentensi.
    2. Majina ya pekee.
      1. Majina ya mahali, miji, nchi, mataifa na kadhalika.
      2. Siku za juma, miezi n.k
      3. Mashirika, masomo, vitabu n.k
      4. Jina la mungu.
      5. Majina ya kutambulisha hasa wanyama wa kufugwa, kwa mfano yale ya mbwa- Foksi, Jak, Popi, Simba, Tomi na mengineyo.

MAKOSA YA HIJAITAHAJIA.
Haya ni makosa ya maendelezo. Mtahini anashauriwa asahihishe huku akiyaonyesha yanapotokea kwa mara ya
kwanza tu.
Makosa ya tahajia huweza kutokea katika:
Kutenganisha neno kwa mfano aliye kuwa
Kuunganisha maneno kwa mfano kwasababu
Kukata silabi visivyo afikapo pambizoni kama vile_ngan-o'. Kuandika herufi isiyofaa kwa mfano_ongesa' badala ya _ongeza Kuacha herufi katika neno kwa mfano aliekuja' badala ya aliyekuja' Kuongeza herufi isiyohitajika kama vile _piya' badala ya pia'
Kuacha alama inayotarajiwa katika herufi kama vile j i
Kukosa kuandika kistari cha kuendelezea neno afikiapo pambizoni au kukosa kukiandikia mahali pasipofaa. Kuacha ritifaa au kuiandikia mahali pasipofaa, kwa mfano ngombe, ngom'be, n'gombe, ngo'mbe n.k Kuandika maneno kwa kifupi kama vile k.v, k.m, v.v, n.k na kadhalika.
Kuandika tarakimu kwa mfano 27-08-2010.

UKADIRIAJI WA UREFU WA INSHA.
Maneno 9 katika kila mstari - ukurasa moja na nusu. Maneno 8 katika kila mstari - ukurasa moja na robo tatu. Maneno 7 katika kila mstari -kurasa mbili.
Maneno 6 katika kila mstari-kurasa mbili na nusu. Maneno 5 katika kila mstari - ukurasa mbili na robo tatu.. Maneno 4 katika kila mstari -kurasa tatu na robo tatu. Maneno 3 katika kila mstari-kurasa nne na nusu.

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Huu ni utungo wa kiuamilifu.  Mtahiniwa azingatie vipengele viwili vikuu.
    1. Muundo
      • Mtahiniwa azingatie muundo au sura ya hotuba.
      • Anwani ya hotuba.
      • Anwani itaje kuwa ni hotuba.
      • Anwani itaje mada ya hotuba.
        • Utangulizi
          • Huanza kwa salamu au mwito wa kuhamasisha hadhira inayohutubiwa.  Hatibu huanza kwa kutaja waliofika kwa vyeo vyao.  Aliye na cheo cha juu zaidi ndiye hutanguliza kwanza.  Maamkizi hufuatwa na lengo la hotuba.
        • Mwili
          • Maudhui yenyewe hutolewa.  Kila hoja hufafanuliwa kwa aya yake.  Hoja hupangwa vyema ili mawazo yatiririke vyema.  Mtahiniwa aliyejitoshelesha kimaudhui awe na hoja tano au zaidi zilizofafanuliwa vilivyo.
        • Hitimisho
          • Hatibu anaweza kurejelea aliyoyahutubu kwa muhtasari.  Anaweza pia kushukuru hadhira.
    2. Maudhui
      Mtahiniwa anaweza kuibuka na hoja zinazohusiana na mada.  Baadhi ya hoja hizo ni:
      • Kuwa na nidhamu ya hali ya juu.
      • Jitihada katika masomo.
      • Kuwaheshimu walimu, wazazi na wanafunzi.
      • Kufuata ushauri nasaha wa wakubwa .
      • Kumcha Mungu.
      • Kushughulikia kazi ya ziada na kuduruju vitabu vingi.
      • Kutopoteza wakati wowote.
      • Kuamka na kuingia darasani mapema.
      • Kukamilika kwa mtaala mapema.Kuepuka kukwa
      • ruzana na mamlaka shuleni.
      • Kufanya marudio vikundini.

        Tanbihi:  Mtahini akadiria kazi ya mtahiniwa.
  2. Mwongozo wa Swali la Pili
    1. Kuimarisha na kuongeza shule za wasichana.
    2. Hatua kali kuchukuliwa dhidi ya ukandamizaji wa wanawake.
    3. Nafasi sawa za kazi kwa wanawake na waume.
    4. Kuharamisha kwa ndoa za mapema.
    5. Katiba kuwapa wanawake nafasi sawa za uongozi katika bunge la kitaifa.
    6. Afya ya wanawake kuimarishwa wakati wa kujifungua.
    7. Mashirika ya utetezi wa haki za wanawake kama FIDA.
    8. Mashirika ya mikopo kwa wanawake kama KWFT.
    9. Kupeana visodo katika shule za wasichana.
    10. Wanawake kuhamasishwa kuhusu haki zao.
    11. Kuharamisha tohara kwa wanawake.
      Tanbihi:  Mtahini akadiria hoja za mwanafunzi.
  3. Insha ya Methali
    Mui – mtu mwovu/mbaya/tabia potovu.
    • Kisa kilenge mtu mwovu / potovu hatimaye anageuka na kuwa mtu mzuri.
    • Mtu aliyekuwa potovu anabadilika na kuwa na tabia njema za kupigiwa mfano.
    • Sehemu mbili za methali zijitoke waziwazi.
    • Umui unaweza kuhusisha tabia hasi au moja.  Vilevile, wema unaweza kuwa mwingi au aina moja.
    • Mabadiliko yaandamane na kichocheo cha aina fulani kama vile:  kushauriwa, kuadhibiwa, kufungwa jela n.k
      Mifano
      1. Mwizi sugu kushikwa, kujeruhiwa, kuponea chupuchupu na mwishowe kuacha wizi na kuanza kazi yake mwenyewe.
      2. Mwanafunzi kiburi kutosikiliza walimu shuleni, kufeli mtihani na baadaye kujirudi baada ya kudhurika, anakuwa mtiifu na kupasi mtihani wake.
      3. Msichana anayependa ukware, anaambulia uja uzito.  Anapitia machungu mengi hata kuwazia kujiua au kuavya mimba.  Anajirudi baada ya kushauriwa na kuamua kumlea mwanawe na kuasi tabia potovu za ukware.
        Tanbihi: 
        • Anayeshughulikia upande mmoja wa methali asipite alama C+ 10/20
        • Kisa kisipolenga maana batini ya methali atakuwa amepotoka kimaudhui.  Atuzwe D 03/20
        • Atakayesimulia kisa kisichomhusu binadamu (pengine myama Fulani) atakuwa amepotoka kimaudhui.  Atuzwe D 03/20
        • Atakayekariri au kunakili swali tu atuzwe D 02-01/20
  4.                      
    1. Hii ni insha ya mdokezo ambayo mtahiniwa lazima amalizie kwa mdokezo aliopewa.
    2. Kisa cha mtahiniwa sharti kioane kikamilifu na mdokezo huu.
      Mifano 
      1. Yawezekana uwe ni mkasa wa moto shuleni.
      2. Au uvamizi uliofanyika.
      3. Wizi ulifanyika wa mtihani au chochote kile anajutia kwa sababu alifahamu jambo hilo.
      4. Kutekwa nyara n.k.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Arise and Shine Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?