Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Arise and Shine Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Tiasahihi yakokisha tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa
  • Jibu maswali yote katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha majibu.
  • Hakikisha kwamba kurasa zote zimepigwa chapa.
  • Majibu yote ni lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

Kwa Matumizi ya Mtahini Pekee

Swali

Upeo

Alama

1

15

 

2

15

 

3

40

 

4

10

 

JUMLA

80

 



MASWALI

UFAHAMU: (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Tumeshuhudia baadhi ya ndugu wa familia moja wakiishi bila maelewano na wakati mwingine kukata kabisa kabisa mawasiliano. Hivi leo kuna familia ambazo haziwezi kuketi pamoja na kumaliza matatizo yao, na badala yake huchukua njia za vita ugomvi na hata pengine mauaji kama suluhisho la migogoro yao.

Kawaida maisha sio mstari mnyoofu. Kuna milima,mabonde,kona na hata mashimo. Ndiposa migogoro ni sehemu ya maisha yetu! Mara nyingi haiepukiki, isipokuwa kuipitia na kupata suluhisho. Ipo migogoro baina ya ndugu ambayo huleta kutoelewana,kukosesha amani nahata pengine kupoteza kabisa mahusiano. Ni wazi kuwa mahali popote wanapoishi watu au kufanya kazi pamoja, hapakosekani migogoro kwani hata vikombe vinapokuwa kabatini, havikosi kugongana.

Ukweli ni kwamba sote tunazaliwa na tabia tofauti, uwezo tofauti wa kuvumilia na hata kuamua kutenda. Katika mazingira yoyote ya kutoelewana, kiasi kikubwa cha busara, upendo, amani na imani huhitajika ili kuiondoa migogoro hiyo. Isipotafutiwa suluhisho ama utatuzi wake ukatendeka kwa jazba na chuki, migogoro ya ndugu katika familia hukua na kuzaa madhara makubwa.

Kuanzia utotoni au hadi uzimani, kunaweza kuwa na sababu nyingi ambazo huweza kupelekea kuleta tofauti baina ya ndugu. Kwa ujumla, ndugu ni watu unaowaamini, ambao hawatakupa kisogo. Walakini, hii sio wakati wote. Kwa bahati mbaya ukweli umetuonyesha kuwa kuna uhusiano wa kindugu ambao huisha vibaya. Sababu kubwa zikiwa ni mazingira ambayo ndugu wameishi ambayo wakati mwingine kuna upendeleo wa mzazi kwa mtoto au watoto fulani na kuwafanya wengine wahisi wivu, kutopendwa na kutengwa.

Zipo sababu za kiuchumi ambapo ndugu wengine katika familia wanafanikiwa zaidi kuliko wengine na kuwa na maisha bora zaidi kuliko wengine. Hali hii pia inaweza kuleta mfarakano kwa wale ambao hali zao ni tofauti na wengine, hasa iwapo hakukuwa na mazingira ya utangamano katika familia tangu awali.

Ndugu wa familia moja huzaliwa wakiwa na tabia tofauti. Kila mshiriki wa familia ana haiba na mtazamo wake tofauti katika masuala mbalimbali. Wengine hukasirika mara kwa mara, wengine ni wakimya sana, wapo walio wakorofi na wengine wanaopenda amani, hivyo jambo hili ni muhimu mno kulielewa mara inapotokea migogoro ili kutamua namna ya kupata suluhisho.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba migogoro hii wakati mwingine hupelekea kuvuruga mwelekeo wa maisha ya watoto hasa wakati wa ukuaji, kwani kulingana na tofauti zao, wapo wale wanaoamua kuondoka nyumbani wakiwa bado na umri mdogo na kuhamia mitaani.

Pamoja na migogoro kuwepo katika familia zetu ni vyema wazazi ama walezi waelewe tofauti za kifamilia zinavyoweza kuchangia mfarakano baina ya ndugu wa familia moja. Kwamba mzazi ama mlezi anapompendelea mtoto mmoja na kutokuwa karibu na mwingine, anatengeneza mazingira ya tofauti baina ya watoto wake. Ni vyema kuweka uwiano sawa baina ya watoto na familia ili kuweza kupunguza tofauti zinazoweza kujitokeza.

Maswali

  1. Onyesha athari tatu za migogoro miongoni mwa ndugu katika familia. (Alama 3)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  2. Eleza mambo matano yanayochangia kuwepo kwa watoto wanaorandaranda mitaani kwa kurejelea kifungu. (Alama 5)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  3. Malezi yanachangia migogoro baina ya ndugu. Thibitisha kwa kurejelea kifungu. (alama. 1)
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  4. Taja na ueleze mbinu nne za kimtindo zilizotumika katika kifungu. (alama. 4)
    ………………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  5. Andika visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. (alama.2)
    1. haiepukiki
      ……………………………………………………………………………………………………..
    2. haiba
      ………………………………………………………………………………………………………

2. MUHTASARI
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
Migongoni mwa starehe ambazo Waswahili wamezihifadhi mpaka leo ni kutoleana hadithi na kutegeana vitendawili. Starehe hizo ambazo kwa kawaida hufanywa nje huwa njiani au uani, ama ndani chumbani au ukumbini, aghalabu hufanywa wakati wa magharibi au usiku baada ya kila mtu kumaliza kazi ya nyumbani,dukani,shambani,ofisini na kadhalika. Mambo haya yakitazamwa sana itaonekana kuwa hayakufanywa vivi hivi.

Tangu zamani wazee wa Kiswahili waliwakataza wana wao kucheza mchana. Hawakupenda vijana wajizoeshe uvivu kwa kupiga malapa. Walisadiki kuwa mwana ambaye hakukanywa dhidi ya utiriri huu hangeweza kujifaa yeye mwenyewe na wala hata watu wengine. Isitoshe nani
Asiyejua kuwa ajizi ninyumba ya njaa:Vijana walilimizwa kusaidia katika makazi mbali mbali yanayofanywa majumbani, mashambani na mahali popote palipohisiwa kuwa mtu angalifanyiwa jambo la kumpa riziki. Ndiposa ungesikia wazee wakiwaambia watoto wao, ‘ukisimulia hadithi mchana utaota mkia’. Ingawa kwa watu wazima maneno haya yangekuwa masihara,kwa watoto yaliaminika sana kwa hivyo wazazi wakapata mradi wao. Hi ndiyo maana Waswahili wanasimuliana hadithi na kutegeana vitendawili jioni au usiku.

Wazazi ambao hawataki watoto wao watembeetembee au wacheze michezo ambayo itawafanya wakimbiekimbie na kujihasiri huwatia ndani ili wawe nao kuanzia magharibi. Waswahili wana itikadi nyingi zinazohusiana wakati wa magharibi. Ni ajabu kuwasikia wakisema kuwa magharibi huwaleta pamoja na kutoleana hadithi. Na hata kama si hivyo hii ni fursa nzuri kwa wazazi kuzungumza na watoto wao ambao kutwa nzima huwa hawakupata nafasi kuwa nao.

Starehe hizi pia huongeza elimu, na kama wahenga wasemavyo, elimu ni mwanga uangazao.. Kwa mfano watoto watategewa vitendawili, jambo hili litawafanya wafikiri. Na kufikiri huku kutawafanya wavumbue mambo mengi ambayo mengine hapo awali hawakuyajua na kuyathamini. Vile vile huwafunza werevu wa kufumba na kufumbua mafumbo ambayo elimu inayohitaji kiwango kikubwa cha busara.

Kutoleana hadithi ni miongoni mwa starehe ambazo kwazo hujifunza mambo mengi sana. Katika hadithi watoto wanaweza kujifunza mambo yanayohusu mila na desturi, katika mambo haya watu hujifunza tabia nzuri, heshima na uvumilivu. Pia katika hadithi mtu anaweza kujifunza mambo ya historia na pia ya mazingira aliyoyazoea na hata mambo ambayo hayajui.

Aidha hadithi ni chombo ambacho wazee hukitumia kuwafundisha watoto mbinu za kuzungumzia. Wazee wenye busara aghalabu huwapa nafasi watoto wao wabuni na wasimulie hadithi zao. Wakati mwingine jamaa mbili jirani huweza kukutana kufanya mashindano ya kutambiana hadithi. Mazoezi kama haya huwawezesha vijana kufikia viwango vya juu vya ufasaha na matumizi ya lugha na ujasiri na ukakamavu wa kuweza kusema mbele za hadhira kubwa katika maisha yao. Baadhi ya watambaji wakubwa waliopata kusifiwa haikosi mwanzo wao ulikuwa wa namna hii. Hadithi pia huwafundisha watu kuhusu maisha duniani. Zinaweza kuwafunza jinsi ya kuishi na ndugu, majirani, marafiki, wake au waume. Ulimwenguni humu tunamoishi na mambo mengi yanoyomtatiza binadamu kwa namna mbalimbali. Hadithi zinaweza kupendekeza mambo ya kufanya na kuonyesha njia zenye mapato mema tunapofikiwa na hadhaa kadhaa. Zinaweza pia kukanya kiburi na kuonyesha faida ya kutosema uwongo ama kuishi katika maisha yasiyo muruwa, yaliyojaa kiburi na majivuno. Hapana shaka hadithi zinaweza kuongoza na kuwafanya wawe watiifu na raia wema katika nchi zao. 

Maswali

  1. Kwa nini mwandishi akaoanisha utambaji wa hadithi na wakati wa jioni? (Maneno 40)
    (alama 5, alama 1 ya mtiririko)
    Nakala chafu
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    Nakala safi
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………….…………….……………………………………………………………………………………………….……
  2. Kwa maneno kati ya 70 na 90 eleza umuhimu wa kutambiana hadithi na kutegeana vitendawili,kulingana na mwandishi. ( Alama 8, 1 ya mtiririko)
    Nakala chafu
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………..
    Nakala safi
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………….…………….……………………………………………………………………………………………….……

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

  1. Andika neno lenye kikwamizo sighuna cha ufizi, irabu ya mbele wastani, nazali ya midomo na irabu ya chini kati. (alama 2)
    …………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………….…………….……………………………………………………………………………………………….……
  2. Eleza muundo wa silabi katika neno mbilikimo. (Alama1)
    …………………………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………….
  3. Andika upya kwa kutumia ‘o’-rejeshi tamati.
    Majarida ambayo yatasomwa yameagizwa (alama. 1)
    …………………………………………………………………………………………………..………………………………………………………………………………………………….
  4. Tunga sentensi zifuatazo (alama 2)
    1. Arifu
      ………………………………………………………………………………………………………
    2. Rai
      ………………………………………………………………………………………………………
  5. Tunga sentensi moja yenye kiwakilishi cha A-unganifu,kitenzi kishirikishi kipungufu na kijalizo (alama.2)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  6. Andika sentensi zifuatayo katika hali ya udogo (Alama 2)
    Mbuzi wake amekaata kamba akaingia shambani na kula mahindi.
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  7. Andika katika usemi wa taarifa (Alama 2)
    “Wanasiasa hawa wenu wakipigana hivi wataharibu nchi” Rais alisema.
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  8. Changanua sentensi kwa jedwali. (alama.4)
    Jirani aliyenisaidia juzi ataondoka mwakani.
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  9. Onyesha yambwa katika sentensi ifuatayo
    Alawi alifumiwa mkeka mzuri na shangaziye kwa miyaa. (alama 3)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  10. Eleza tofauti ya kisarufi ya maneno yaliyopigia mstari (alama.2)
    1. Duka la mwalimu limechomeka
      ………………………………………………………………………………………………….
    2. Duka la mwalimu limechomeka
      ………………………………………………………………………………………………..
  11. Tunga sentensi kuonyesha wakati ujao, hali ya mazoea (Alama 2)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..…………………………………………………………………………………………………….
  12. Tumia neno pongezi katika sentensi kama (Alama 2)
    1. Nomino
      ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    2. Kihisishi
      ………………………………………………………………………………………………………
  13. Eleza matumizi ya ‘na’ katika sentensi ifuatayo:Ridhaa na Mwangeka walikuwa wameketi karibu na jumba lakifahari walipoitwa na Apondi. (alama.3)
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  14. Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo
    1. Mwana mwadilifu huwaletea wazaziwe fahari. (alama 1).
      ( Badilisha neno lililopigiwa mstari kuwa nomino.)
      ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    2. Nyota nyingi ziliipamba anga usiku huo. (alama 1)
      (Tumia nomino ya jamii badala ya maneno yaliyopigiwa mstari)
      ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    3. Makokha ni mkakamavua Onyango ni mkakamavu pia. (alama 1)
      (Unganisha iwe sentensi moja yenye kihusishi cha kulinganisha.)
      ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    4. ‘Kibali,nionyehse ulipoandika zoezi hilo.’Mwalimu alisema. (alama.1)
      (Tumia kiwakilishi nafasi badala ya nomino ya pekee.)
      ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  15. Kwa kutunga sentensi, onyesha ngeli mbili za neno ‘upwa’ (alama.2).
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  16. Andika maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii. (alama.2)
    Selume alimsimulia Ridhaa kisa chake.
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  17. Tunga sentensi moja kubainisha maana mbili za neno. (alama.2)
    Kina
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  18. Rubani ni kwa ndege,………….ni kwa meli na……………..ni kwa matwana. (alama 2)

ISIMU JAMII (Alama 10)
Wewe ni mtaalamu wa maswala ya usalama. Umepewa fursa kuhutubia warsha inayojumuisha maafisa wa usalama kutoka katika vikosi mbalimbali kuhusu jukumu lao katika kudumisha usalama,amani na maridhiano nchini.

  1. Taja sajili ambayo utatumia kisha ueleze sababu ya jibu lako. (alama 2)
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
  2. Andika huku ukifafanua vipengele vinane vya kimtindo utakavyotumia kufanikisha mazungumzo yako. (alama 8)
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1.                    
    1. Onyeshaatharitatuzamigogoromiongonimwandugukatikafamilia. (Alama3)
      1. Kutoelewana
      2. Kukosekanakwa Amani
      3. Kupotezamahusianokabisa
    2. Eleza mambo matanoyanayochangiakuwepokwawatotowanaorandarandamitaanikwakurejeleakifungu. (Alama5)
      1. Kukosaimanimiongonimwandugu
      2. Mazingirawanamozaliwa
      3. Mapendeleoyawazazikwamtoto au watoto Fulani yanayowafanyawenginekuwaoneawivuwenzao
      4. Kutopendwanawazazi
      5. Kutengwa
      6. Tofautizakiuchumimiongonimwandugu
    3. Maleziyanachangiamigogorobainayandugu. Thibitishakwakurejeleakifungu. (alama. 1)
      • Mzazi au mlezihupendeleamtotommojanakutokuwakaribunamwinginehivyokutengenezamazingirayatofautikatiyawatoto wake.
    4. Tajanauelezembinunnezakimtindozilizotumikakatikakifungu. (alama. 4)
      1. Takariri-kabisakabisa
      2. Nidaa’…maishayetu!
      3. Jazanda/sitiari – milima/mabonde/mashimo – kumaanisha mambo mbalimbalimagumuyamaisha.
      4. Msemo – vikombevinapokuwakabatinihavikosikugongana
      5. Nahau – hawatakupakisogo
      6. Tanakuzi – utotonihadiuzimani
    5. Andikavisawevyamanenoyafuatayokamayalivyotumikakatikakifungu. (alama.2)
      1. haiepukiki- haiepeki/hihepeki
      2. haiba- tabia/mwenendo/mzoea/desturi

1. MUHTASARI
Maswali

  1. Kwa nini mwandishiakaoanishautambajiwahadithinawakaiwajioni? (Maneno 40)
    (alama 5, alama 1 ya mtiririko)
    • Jioni watu huwa wame maliza kazi zao.
    • Kuepushauvivumiongonimwavijanawakatiwamchana
    • Mwiko kuwa mtu angeotamkia akisimuliwa hadithi mchana.
    • Kuepusha watoto kutembeatembea au kucheza jioni kwa sababu wangeathirika
    • Nafasinzurikwawazazikusemanawanao
      Hoja 5x1=alama 5,alama 1 ya utiririko
  2. Kwa manenokatiya 70 na 90 elezaumuhimuwakutambianahadithinakutegeanavitendawili,kulingananamwandishi ( Alama8, 1ya mtiririko)
    • Huletajamiitofautipamoja
    • Wazazihupatafursanzuriyakuzungumzanawatotowao
    • Huongezaelimu,hufunzawerevuwakufumbanawatotowao
    • Huongezaelimu,hufunzawerevuwakufumbanakufumbuamafumbo
    • Hufunza mambo yanayohusumilanadesturi,
    • Hufunza mambo ya historian na mazingira.
    • Hufunza watoto mbinu za kuzungumza
    • Hufanya nak uongezafaidayakutosemauwongoamakuishikatikamaishayasiyomurua
    • Huwafundishawatu mambo yadunia
    • Hupendekeza mambo yakufanyanakuonyeshanjiayakupatamapatomema.
    • Huognozanakuwafanyawatukuwanatabianjema/ watiifunaraiawema.
      Hoja 8 x 1 = 8
      (Mtiririko Alama 1)

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

  1. Andikanenolenyekikwamizosighuna cha ufizi, irabuyambelewastani, nazaliyamidomonairabuyachinikati. (alama 2)
    • sema
  2. Elezamuundowasilabikatikanenombilikimo. (Alama1)
    • Mbi-kki, li-ki, ki-ki, mo-ki
  3. Andikaupyakwakutumia ‘o’-rejeshitamati. Majaridaambayoyatasomwayameagiziwa. (alama 1).
    • Majaridayasomwayoyameagizwa√1
  4. Tungasentensizifuatazo (alama 2)
    1. Arifu
      • Mama alininunuliakitabu cha Kiswahili
    2. Rai
      • Tafadhali nipe hicho kikombe (2x1=2)
        (Kadiria jibu la mwanafunzi)
  5. Tungasentensimojayenyekiwakilishi cha A-unganifu,kitenzikishirikishikipungufunakijalizo (alama.2)
    • Wamwalimunimchoyo (manenoyawematatupekee) (2/0)
  6. Andikasentensizifuatayokatikahaliyaudogo (Alama 2)
    Mbuzi wake amekaata Kamba akaingiashambaninakulamahindi.
    • Kibuzi chake kikmekata kikakamba kikaingia kijishambani na kula vijihindi
      Au
    • Kijibuzichakekimekatakikambakikaingiakijishambaninakulavijihidni (2/)
  7. Andikakatikausemiwataarifa (Alama 2)
    “Wanasiasa hawawenu wakipiganahiviwataharibunchi” Raisalisema.
    • Raisalisemakuwa/kwamba1/2 wanasiasa hao1/2 wao1/2 wangeendelea1/2kupigana hivyo1/2wangeiharibu1/2nchi
  8. Changanua sentensikwajedwali. (alama.4)
    Jiranialiyenisaidiajuziataondokamwakani.
    • Jiranialiyenisaidiajuziataondokamwakaujao

      S

      KN

      KT

      N

      s

      T

      E

      Jirani

      Aliyenisaidiajuzi

      ataondoka

      Mwakaujao

  9. Onyeshayambwakatikasentensiifuatayo
    Alawi alifumiwamkekamzurinashangaziyekwamiyaa. (alama 3)
    • Miyaa-ala/kitumizi,Alawi-tendewa/kitendo,mkeka mzuri-tendwa/Kipozi
  10. Elezatofautiyakisarufiyamanenoyaliyopigiamstari (alama.2)
    1. Dukala mwalimulimechomeka
      • La mwalimu – nikivumishi
    2. Dukalamwalimulimechomeka
      • la __kihusishi
        (2x1)
  11. Tungasentensikuonyeshawakatiujao, haliyamazoea (Alama2)
    • Mama atakuwaakipikachakula
      (Kadiriajibu la mwanafunzi) (1x2)
  12. Tumianenopongezikatikasentensikama (Alama2)
    1. Nomino
      • AlipewapongezinyingialiposhidaTuzo
    2. Kihisishi
      • Pongezi! Mama alimwambiamwanawe. (2x1)
  13.              
  14. Andikasentensizifuatazoupyakulingananamaagizo
    1. Mwanamwadilifuhuwaleteawazazifahari. (alama 1).
      ( Badilishanenolilopigiwamstarikuwanomino.)
      • Uadilifuwamwanahuwaleteawazaziwefahari
      • Mwadilifuhuwaleteawazazifahari
    2. Nyotanyingiziliipambaangasikuhuo. (alama 1)
      (Tumianominoyajamiibadalayamanenoyaliyopigiwamstari)
      • Thureayanyotailiipambaangausikuhuo
    3. Makokhanimkakamavu pia. (alama 1)
      (Unganishaiwesentensimojayenyekihusishi cha kulinganisha.)
      • Makokhanimkakamavukama/sawana /Zaidi ya/kuliko/kumpiku/kushinda Onyango
    4. ‘Kibali,nionyehseulipoandikazoezihilo.’Mwalimualisema. (alama.1)
      (Tumiakiwakilishinafasibadalayanominoyapekee.)
      • ‘Wewe,nionyesheulipoandikazoezihilo. ‘Mwalimualisema
        (4x1)
  15. Kwa kutungasentensi, onyeshangelimbilizaneno ‘upwa’ (alama.2).
    1. Upwa (U-U):Upwa wake Mwangemiulimsalimishambeleyaamiyake.
    2. Upwa (U-ZI):UpwawaZiwaViktoriahauzurikikwakujaamajiyanayofurika
    3. Wapwa (A(yu) = WA: Wapwa wake Jumawalimnunuliagari (2x1)
  16.  Andikamaanambilizinazojitokezakatikasentensihii. (alama.2)
    SelumealimsimuliaRidhaakisachake.
    • Kisa cha Selume
    • Kisa ha Ridhaa
    • Kisa cha Mtumwingine
    • Ili Ridhaasikilize
    • Kwa niabayaRidhaa
      (zozotembili 2x1=2)
  17. Tungasentensimojakubainishamaanambilizaneno. (alama.2)
    Kina
    • Kina - Urefuwakwendachini
    • Kina - silabizasautinamnamoja
    • Kina - neno la kuelezawatuwenyeuhusianowakiukoo
    • Kadiriasentensiya mwanafunzi
  18. Rubaninikwandegenahodhanikwamelinadereva.ni kwamatwana. (alama 2)

ISIMU JAMII (Alama 10)
Wewenimtaalamuwamaswalayausalama. Umepewafursakuhutubiawarshainayojumuishamaafisawausalamakutokakatikavikosimbalimbalikuhusujukumulaokatikakudumishausalama,Amaninamaridhianonchini.

  1. Tajasajiliambayoutatumiakishauelezesababuyajibulako. (alama 2)
    • Sajiliyakitaaluma/Mazungumzorasmiyausalama (Ni hotuba kwa wataalamu,maafisa wa usalama)
  2. Andikahukuukifafanuavipengelevinanevyakimtindoutakavyotumiakufanikisha mazungumzoyako. (alama 8)
    • Nitatumiamsamiatimaalum
    • Nitatumiasentensifupifupi/ndefundefuilikutoamaelezo
    • Nitatumialugharasmiya Kiswahili
    • Nitatumialughasanifu
    • Nitatumialughayaheshima,mabibinamabwana
    • Nitatumialughashawishi
    • Nitatumialughayaushauri
    • Nitatumialughayatasfidakufichaakaliyamsamiati
    • Nitachanganya na hau kuhamishamsimbo
    • Nitatumiamsamiatiwakutoholewa/manenoyakukopwakuakisimaendeleoyakiteknolojianazanazakivita.
    • Nitatajanakunukuutakwimukwakutoaushahidi
    • Nitatumiaishara
    • Nitatumialughayakuwapamatumaini
    • Nitatumiatakririilikusisitizamabomuhimu.
    • Nitatumiakiimbokuhalisihisiatofautitofauti

Tanbihi:

  • Ama mwanafunzi atoe ufafanuzi wa kina au mfanoiliatuzwealama 1 kwakilahoja
    Jumlahoja 8 x 1 = 8

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Arise and Shine Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?