Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Arise and Shine Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO:

  1. Swali la kwanza ni la lazima
  2. Maswali hayo mengine yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki, yaani Riwaya, Tamthilia, Hadithi fupi na Fasihi Simulizi.
  3. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  4. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili. 

Kwa Matumizi ya Mtahini Pekee

Swali

Upeo

Alama

1

20

 

 

20

 

 

20

 

 

20

 

Jumla

80

 



QUESTIONS

SEHEMU YA A: USHAIRI
Swali la Lazima

  1. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata:

    Shimo: Ali Salim Zakwany

    1. Mwambieni kibushuti, asiruke shimo lile
      Kimo chake kama goti, kwenda ng'ambu sifikile
      Mtu haoli bahati, akasahau umbile
      Kila muwania mbele, na nyuma 'sisahawile
    2. Afanyayo ni hatari, sijitie mpulele
      Mambo yote ajasiri, shari asithibutile
      Mjalia watu kheri, shairi ni yake vivile
      Kila muwania mbele, na nyuma 'sisahawile
    3. Asambe ndiyo busara, kutenda kitendo kile
      Itamuwia hasara, na madhara kama yale
      Mola mwingi wa subira, ajapo chomwa vidole
      Kila muwania mbele, na nyuma 'sisahawile
    4. Licha na yeye nyadungo, chuya katika mchele
      Hata warefu ja pondo, hawatusi shimo lile
      Walojaribu kitendo, shimoni watumbukile
      Kila muwania mbele, na nyuma sisahawile
    5. Nimefika kituoni, nasema mumuwasile
      Mfua maji ngamani, ili kwamba sizamile
      Chombo huungia mwambani, na nahodha ni yuyule
      Kila muwania mbele, na nyuma 'sisahawile

Maswali

  1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
  2. Fafanua toni ya shairi hili. (alama 4)
  3. Taja na utoe mifano ya tamathali za usemi mbili zinazopatikana katika shairi. (alama 4)
  4. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
  5. Kwa kutoa mifano minne, eleza aina moja ya idhini ya kishairi iliyotumika zaidi katika shairi. (alama 3)
  6. Andika ubeti wa tano kwa lugha ya nathari. (alama 4) 

SEHEMU YA B: RIWAYA – CHOZI LA HERI (ASSUMPTA MATEI)
2. "Jua linalochomoza halina ule wekundu wa jua la matlai ambao huleta haiba ya uzawa wa siku yenye matumaini. Naona wingu kubwa angani likitembea kwa kedi na madaha na kulifunika jua..... Mawingu yaliyoshiba yakataka kutapika yanagooka, yanakaribiana, kupigana busu na kusababisha mwanguko wa matone mazito ya mvua..."

  1. Eleza aina za taswira zinazojitokeza katika dondoo hili (alama 8)
  2. Eleza mbinu nyingine ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
  3. Eleza sifa na umuhimu wa msimulizi wa dondoo hili. (alama 10)

3. Lakini itakuwaje 'historical injustice' nawe Ridhaa hapo ulipo sicho kitovu?

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 2)
  3. Eleza sifa nne za mzungumzaji wa maneno haya. (alama 8)
  4. Eleza mambo matatu yaliyowakumba walioishi penye kitovu kisicho chao. (alama 6)

SEHEMU YA C: TAMTHILIA - BEMBEA YA MAISHA (Timothy Arege)
4. Ukirejelea Anwani ya Tamthilia ya Bembea ya Maisha, onyesha namna wahusika wanavyobembea maishani mwao. (alama 20)

5. Maskini mke wangu! Kumbe ugonjwa haukumsaza mwaka baada ya mwaka. Umemla bila huruma. Awali niliona kuwa mchezo kumbe ilikuwa kweli yake ninaona imesimama. Ni mwele hakika. Laiti ningejua, jana ningeishi tofauti. Silezi zetu za maisha tungezila zilivyokuja kwa furaha. Siku hazigandi wala jana hairudi. Sasa jana imebaki kumbukizi baada ya kusombwa na wakati mfano wa mafuriko msimu wa masika."

  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake (alama 4)
  2. Eleza kwa mfano mbinu nne za kimtindo zilizotumika (alama 4)
  3. Barusha toni katika dondoo hili. (alama 2)
  4. Ni maudhui gani yanayojitokeza katika dondoo hili? (alama 4)
  5. Onyesha sifa za mzungumzaji zinazodhihirisha kuwa silezi zao hawakuzila kwa furaha. (alama 6)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI - MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI ZINGINE.
6.

  1. Fafanua mbinu za kimtindo katika dondoo lifuatalo. (alama 6)
    "Jimbo la matopeni lilikuwa limegeuzwa ngome ya watu fulani binafsi. Watu wenye ushawishi mkubwa serikalini! Watu wasiojali maisha ya wapiga kura kama Machoka na Zuhura. Wapiga kura walioamka siku hiyo asubuhi ya majogoo, wakastahimili baridi kali ya bukrata. Wakavumilia jua kali la mchana. Zuhura alikumbuka namna yeye na wenzake walivyotunga foleni ndefu kwenye vituo vya kupigia kura. Yote haya wakiwa na matumaini ya maisha bora ya baadaye, si bora maisha! Kumbe wajinga ndio waliwao! Mzigo mzito wa maisha haukuwatisha wala kuwakosesha usingizi viongozi wao. Ama kweli, mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi. "
  2. Onyesha namna wanamatopeni wanavyokumbwa na madhila kwa kurejelea hadithi ya "Msiba wa kujitakia" (alama 14)

7. “Katika hali ile ya uchungu, kilio na mtanziko wa mawazo, akaiona simu yake imeanguka chini ya kitanda….. Haidhuru hata kama atamuunga mkono mwanawe.”

  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
  2. Fafanua mbinu ya kimtindo inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
  3. Eleza sifa nne za anayerejelewa katika dondoo hili. (alama 4)
  4. Eleza jinsi “taasubi ya kiume” inavyoshughulikiwa na mwandishi wa “fadhila za punda”. (alama 10)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
8. Ewe Mainga wa Ndumi
Siwe uloambia akina mama
Siku tulopiga foleni
Chakula cha msaada kupata
Turudishe vifaranga kwenye miji
Wageuke vijusi tena
Njaa isiwaangamize?

Siwe ulopita
Matusi ukitema
Chumvi na sukari kuturushia ja samadi?
Uhitaji wetu ukatutuma
Kuokota vihela uloturushia
Ukatununua, kura ukapata?
Sasa miaka mitano imetimia
Waja tulaghai tena
Mainga wa Ndumi huna lolote safari hii
Ubunge umekudondoka ukitazama
Wanyonge tumeamua
Kwingine kujaribu.

  1. Eleza aina ya kipera hiki. (alama 2)
  2. Huku ukitoa mifano, tambua mbinu za lugha nne zilizotumiwa katika utungo huu. (alama 8)
  3. Tambua nafsineni katika utungo huu. (alama 2)
  4. Fafanua toni ya utengo huu. (alama 2)
  5. Fafanua umuhimu wa kipera hiki. (alama 6)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1.                        
    1.                      
      1. Nyuma sisahau vile.
      2. Muwanie mbele.
      3. Jiepusheni na balaa (alama 1)
    2. Toni ya
      1. Masikitiko - msimulizi anasikitika na tabia za mtu Pulani.
      2. Tahadhari - Mjalia watu kheri, shari ni yake pia
      3. Dharau - Licha ya yeye nyadundo. Cheya katika mchele. Hata...
      4. Ombi - nasema mumuwasile. (alama 4)
    3.            
      • Jazanda:
        1. Chombo huingia mwambani na nahodha ni yuyule
        2. Mfua maji ngamani
      • Tashbihi:
        1. kimo chake kama goti
        2. warefu ja pondo
        3. madhara kama yale (kutaja 1, mfano 1, 2x 2 = 4)
    4. Ni shairi la beti 5.
      • Kila ubeti una mishororo 4
      • Kila mshororo una vipande viwili, ulewapi na utao.
      • Vina vya ndani vimebadilika ila vya nje vimefanana
      • Shairi lina mkarara/kibwagizo. (zozote 4 x 1 = 4)
    5. mazida
      • sisahawile badala ya sisahau
      • asithubutile badala ya asithubutu
      • sifikilie - sifike
      • yuyule – yuyu (kutaja 1, mifano 4 x ½ = 2, jumla 3)
    6. Nimefika mwisho nasema mmpe wasia. Anayetoa maji chomboni akiwa katikati ya chombo hicho ni kwa sababu asizame. Na ikumbukwe kwamba huenda mrama na akawa nahodha wa kila siku. Kila anayewania yaliyoko mbele asisahau aliyowacha nyuma.
      (alama 4)
  2.                  
    1. Taswira oni – Naona wingu kubwa angani.
      Taswira mwendo – yanagooka /yanakaribiana.
      Taswira mguso – kupigana busu
      Taswira hisi – akitembea kwa kedi na madaha.
      (Kutaja – alama 1, mfano – alama 1. 4 x 2 = 8)
    2. Tashihisi/uhuishi – kama mawingu yaliyoshiba
      (kutaja – alama 1, mfano – alama 1. 2 x 1 = 2)
    3. Sifa za Kaizari
      1. Ni mtamauka – anatamauka baada ya mkewe Subira kuondoka.
      2. Ni mwenye kihoro – anajaa kihoro baada ya kuishi kwa majuto baada ya kukuta mkewe ameshafariki.
      3. Ni mwoga – anashindwa kusimama kidete kumtetea mkewe Subira ambaye anabaguliwa kwa kuwa ametoka mbari ya Bamwezi.
      4. Mwenye utu – anawahurumia wanawe Lime na mwanaheri na kusikitika kwamba walitendewa unyama.
        • Aliwapa binti zake na mkewe huduma ya kwanza baada ya kuvamiwa.
      5. Mwenye mapenzi – Alienda kumtafuta mkewe alipotoroka.
        • Alihakikisha mkewe amezikwa nyumbani.
      6. Mzalendo - Alisikita kwamba nchi yake ilikuwa imeshindwa kudumisha usalama nchini mwake.
        (zozote 3 x 2 = 6)

        Umuhimu wa Kaizari
        1. Ni kielelezo cha watu wenye utu katika jamii; alihurumia familia yake ilipovamiwa nyumbani.
        2. Ni mfano wa waume katika jamii ambao hawawasitiri wake wao wanaposubuliwa na mavyaa.
        3. Ni kielelezo cha watu ambao huthamini mabadiliko katika jamii. Alimpigia mwanamke kura.
        4. Ni kielelezo cha kuigwa na watu maana hakubagua kabila wakati wa kuoa, alitafuta mke kutoka jamii tofauti na yake.
          (zozote 2 x 2 = 4)
  3.                          
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
      1. Ridhaa anajisemea akilini.
      2. Anarejelea majadiliano yao na Tila bintiye.
      3. Baada ya kuteketezwa nyumba na mali pamoja na watoto wake.
      4. Akiwa eneo lililochomekea nyumba. (alama 4)
    2. Tambua mbinu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
      • Maswali ya balagha
      • Kuchanganya ndimi. (2 x 1 = alama 2)
    3. Eleza sifa za mzungumzaji wa maneno haya.
      1. Ana mapenzi – alisaidia jamii kupata maji
      2. Mvumilivu – alivumilia kwa kumpoteza mkewe na mali.
      3. Mwenye maadili – aliwaadhibu Mwangeka na Tila.
      4. Msomi – ana shahada ya uzamili.
      5. Mfariji – alimfariji mwanaye Mwangeka. (4 x 2 = 8)
    4. Mambo gani yaliypwakumba walioishi kitovu kisicho chao?
      • Kejeliwa kuitwa mfuata mvua k.m Ridhaa
      • Kutengwa shuleni k.m Ridhaa
      • Kuchomewa nyumba zao k.m Ridhaa
      • Kuharibiwa majimbo kwa kujengwa eneo la barabara/stima.
      • Wakimbiaji walitokea msituni
      • Watoto wao kubakwa k.m binti za Kaizari.
      • Waliotoroka kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani.
        (3 x 2 = 6)
  4. Bemba - Ukirejelea Anwani ya Tamthilia hii onyesha namna wahusika wanavyobembea maishani mwao. (alama 20)
    • Familia ya Yora na Sara inabembea katika shutuma mbalimbali kutoka kwa watu baada ya kukaa muda mrefu bila kupata mtoto. Baadaye Mungu aliwajalia watoto wa kike.
    • Watu walianza kumsonga Yona kula kuwa amepata watoto wa kike tu na kuwa amekosa mrithi. Yona akaanza kuishi kwa hofu na simanzi na akaanza kubembea maisha ya ulevi.
    • Neema anabembea katika maisha ya ndoa ambayo yana mchanganyiko wa mivutano na upendo ndani yake. Kuna mivutano ya kiutamaduni inayosababisha Neema na Bunju wasirlewane. Buju anadai tamaduni haziruhusu yeye kukaa nyumba moja na wazazi wa Neema, jambo ambalo Neema anadai zimepitwa na wakati lakini Bunju anashikilia papo hapo.
    • Bembea ya maisha ya Neema inaonekana kusukumwa na Bunju mumewe. Bunju alimsaidia alipopata ajali kwa kutumia 'flying doctors' ili aweze kupats matibabu. Bunju pia anasaidia kuisukuma bembea ya maisha ya Neema kwa kumsaidia Neema kuwasomesha dada zake na anamsaidia kuwajengea wazazi wa Neema nyumba.
    • Asha anaishi katika bembea ya maisha mjini akihangaika hapa na pale kufanya shughuli za kujikimu ingawa amehitimu masomo ya chuo kikuu.
    • Neema anabembea katika swala la malezi ya mwanawe Lemi. Hana muda kutokana na shughuli nyingi za kazini na kutoa huduma kwa mama yake.
    • Maisha ya familia ya Yona yanabadilika kutoka kuwa ya kukosa mahitaji ya kiuchumi kwani badala ya Neema kifanikiwa kupata kazi, bembea ya maisha yao inakuwa juu. Kujengewa nyumba.
    • Bembea ya maisha ya mjini huwa juu kutokana na maendeleo k.m barabara, magari, majengo n.k.
    • Maradhi ya Sara yanaifanya bembea ya maisha ya Sara kuwa kama iliyokatika na kuwa chini na anakosa matumaini ya kuishi.
    • Watu mjini wanapokea matibabu ya hali ya juu ilhali bembea ya maisha ya kijijini huwa chini kwa sababu ya matibabu ya hali ya chini, hali inayomfanya Neema kumtafutia mamake hospitali ya mjini.
    • Beni anabembea katika swala la kuelimisha watoto wa kike. Aidha anayumbayumba kuhusu thamani ya watoto wa jinsia ya kike au kiume.
      (zozote 10 x 2 = 20)
  5.                      
    1. Ni maneno ya Yona akijisemea akiwa sebuleni kwake nyumbani anapoamua kuacha unywaji pombe na kuanza maisha mapya. (alama 4)
    2. Nidaa - wangu?
      Tashihisi - ugonjwa kumla
      Tashbihi - mfano wa mafuriko.
      Takriri - mwaka baada ya mwaka (4 x 1 = 4)
    3. Majuto - laiti ningejua. (1 x 2 = alama 2)
    4. Madhara ya ulevi
      Athari za maradhi. (2 x 2 = alama 4)
    5. Sifa za Yona
      Ni hodari - Ni mwalimu wa shule ya msingi aliyefaulisha wanafunzi na kupewa zawadi.
      • Huenda shuleni alfajiri.
      • Ni katili - alimpa Sara kichapo cha mbwa akiwa mlevi.
      • Mwenye majuto - Anajutia uraibu wa pombe na kujiletea hasara.
      • Ni mtamaduni - Anaamuru kuwa watoto wa kike hawapaswi kuwa warithi.
      • Mwenye msimamo thabiti - Hakushawishika na watu aoe mke mwingine.
        (zozote 3 x 2 =6)
  6.                        
    1.                                      
      1. Takriri - watu, wapiga kura.
      2. Nidaa/siyahi - hawajui leo wala kesho!
      3. Tashbihi - Maisha ya Wanamatopeni yalikuwa kama mchezo wa karata.
      4. Msemo - asubuhi ya majogoo.
      5. Mbinu rejeshi - Zuhura anakumbuka namna yeye na wenzake walivyotunga foleni ndefu.
      6. Methali - Wajinga ndio waliwao.
        • mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.
      7. Jazanda - Mzigo mzito wa maisha. (zozote 6 x 1 =6)
    2.                    
      1. Maisha ya udhikifu
      2. Mfumuko wa bei
      3. Kutozwa ushuru wa kiwango cha juu na serikali.
      4. Uamuzi wa mpiga kura hauheshimiwi.
      5. Kupewa mishahara duni.
      6. Mishahara inachelewa kulipwa
      7. Wanatawaliwa na viongozi wasio na sera bora.
      8. Shughuli za uchaguzi zinaendeshwa kwa njia isiyo huru wa haki.
      9. Ndoto na nia za vijana zimebanwa, zikafinywa na kuzimwa.
      10. Njaa - Machoka hajatia chochote kinywani tangu asubuhi kiasi matumbo yake kushindwa kuhimili makali ya njaa.
      11. Ukosefu wa ajira - Machoka anatafuta kibarua mchana kutwa bila mafanikio.
      12. Ukabila – Zuhura anampigia kura Sugu Junior kwa sababu ni wa kabila lao.
      13. Viongozi waliochaguliwa hawawatimizii raia ahadi walizotoa.
      14. Ufisadi - wapiga kura wanahongwa kwa kupewa khanga, sukari, unga wa sima, mafuta na visenti vya kununua tembo.
        (zozote 7 x 2 = 14)
  7.                            
    1. Msemaji ni mwandishi.
      • Anayerejelewa ni Lilia
      • Mahali ni nyumbani kwa Luka/Lilia.
      • Ni baada ya kupigwa na mumewe kwa kumripoti katika kituo cha polisi. (alama 4)
    2. Taswira (hisi) - hali ya uchungu/ kilio /mtanziko
      • Nahau/msemo - unga mkono (alama 2)
    3. Sifa za Lilia
      • Mwenye mapenzi ya dhati - anampenda mumewe
      • Ni mtiifu - anawacha kazi baada ya kushauriwa na mumewe.
      • Ni mwaminifu - mbele ya mumewe
      • Ni mwenye heshima - anamwita mama mkwe kwa heshima.
      • Ni mwenye huruma - anamtetea mumewe kupewa ufadhili.
      • Mtulivu - hapendi ugomvi.
      • Mwenye bidii - anasoma hadi chuo.
        (za kwanza 4 x 1 =4)
    4. Taasubi ya kiume
      • Luka anampiga mkewe Lilia kwa ngumi, teke, kofi na hata kumfokea.
      • Baada ya kuanza uzinzi na hawara zake, Luka anakuwa mkali kwa mkewe.
      • Luka anashinikiza Lilia kuacha kazi kwa madai kuwa anamhitaji kudhibiti fedha za kanisa.
      • Lilia hana usemi nyumbani mbele ya Luka.
      • Luka anampuuza Lilia anapomshauri asiingilie siasa.
      • Luka analiuza kanisa lao bila kumshauri wala kumwuliza mkewe Lilia.
      • Luka kurithi mali ya babake Lilia badala ya bintiye (Lilia)
      • Luka haoni umuhimu wa kuandamana na mkewe; anamwacha kijijini.
      • Luka kutaka miadi kabla ya kutembelewa na mkewe.
      • Wanawake hawafai kuwastaki waume zao. Lilia anahofia kujulikana kwamba alikuwa na nia ya kumshtaki mumewe.
      • Luka kuwa na hawara. Kitendo hiki kinamkosesha Lilia hadhi yake katika ndoa.
        (zozote 5 x 2 = 10)
  8.                        
    1. Wimbo wa kisiasa
      • Kimetaja kura na ubunge. (alama 2)
    2. Sitiari - vifaranga - watoto
      • Maswali ya balagha - njaa isiwaangamize?
      • Kura ukapata?
      • Tashbihi - chumvi na sukari kuturushia ja samadi?
      • Tashihisi - uhitaji ukatutuma - uwezo wa kutuma.
      • Usambamba - siwe uloambia akina mama
      • Siwe ulopita. (4 x 2 = alama 8)
    3. Mpiga kura/mnyonge/mpiga kura mwanamke. (alama 2)
    4. Toni ya kusuta/kulalamika. (alama 2)
    5. Kukashifu uongozi dhalimu.
      • Kutangaza kauli mbiu za vyama vya kisiasa.
      • Kusifu viongozi waadilifu.
      • Kuimarisha uzalendo miongoni mwa wanajamii.
      • Kukuza umoja miongoni mwa wanajamii.
      • Huonyesha matarajio ya watawaliwa kwa viongozi.
      • Huonyesha historia ya jamii husika.
      • Huburudisha. (zozote 6 x 1 =6)

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Arise and Shine Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?