Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Chogoria Murugi Zone Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani; tamthilia, riwaya, hadithi fupi na fasihi simulizi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  • Andika nambari ya maswali uliyoyajibu.

SEHEMU YA A: USHAIRI
SWALI LA LAZIMA

  1. MBELE YA SAFARI
    1. Ilipoanza safari , ilianza kwa dhiki
      Tulishikana kwa ari, kwenda safari ya haki
      Tukawa ni majabari, nyoyo zisitaharuki
      Tukajizatiti
    2. Njaa ikawa dhabiti ,na kiu kutamalaki
      Nasi tulitia dhati tusijali kuhiliki
      Ingawa mbele mauti ,dhila na mingi mikiki
      Tukajizatiti
    3. Huu mwisho wa safari, tukaambiwa ni haki
      Shangwe kwetu na fahari,utumwa hatuutaki
      Kuwa mbele ya safari , juhudi iliyobaki
      Tukajizatiti
    4. Ile ilikuwa ndoto , mwisho wake mafataki
      Nguvu zimechomwa moto,sahala ‘mekuwa dhiki
      Wagombanio kipato,utashi haukatiki
      Nakutabakari
    5. Msafara ukasita , kwenye mlima wa haki
      Kijasho kinatuita , mlima haupandiki
      Basi sote ‘kijipeta, kukikwea kima hiki
      Twataka hazina
    6. Tukiwa migongo wazi ,tukainama kwa shaki
      Tukawa’chia ukwezi , kialeni wadiriki
      Wakapanda bila kazi ,Kuteremsha miliki
      Wakaitapia
    7. Wakafikia makazi,ya pumbao na ashiki
      Huko wakajibirizi, kwenye raha lakilaki
      Wakaisahau ngazi, ya umma ulomiliki
      Mbele ya safari
    8. Na hazina yetu sote, kuishusha hawataki
      Wamo wanatema , kwa umati halaiki
      Imezima nia yote ,kiza hakitakasiki
      Mbele ya safari
      1. Eleza safari inayolejelewa katika shairi hili. (al 2)
      2. Onyesha kinaya cha safari inayozungumziwa. (al 6)
      3. Taja na ueleze bahari mbili za shairi ukizingatia : (al 4)
        1. Mizani ;
        2. Vina
      4. Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (al 4)
      5. Eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika ubeti wa sita. (al 4)
      6. Eleza umbo/ muundo wa shairi hili. (ala 2)

SEHEMU YA B: TAMTHILIA
Timothy Arege
BEMBEA YA MAISHA

  1. Hiyo ndio ajabu! Kizazi hili hakitaki kufanya kazi. Kinataka kuja kazini kwa sababu ya mshahara tu. Wachapa kazi hodari ni njozi iliyopotea.
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
    2. Eleza sifa za msemaji wa dondoo hili. (ala 4)
    3. Fafanua imuhimu wa msemewa katika kazi ya Bembea ya Maisha. (ala 4)
    4. Taja na uonyeshe mbinu za uandishi zilizotumika katika dondoo. (ala 4)
    5. Eleza maudhui yanayokuzwa katika muktadha wa dondoo. (ala 4)
  2. Kila binadamu hukabiliana na mabadiliko katika maisha yake. Jadili kauli hii ukirejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha. (ala 20)

SEHEMU YA C: Riwaya
Assumpta Matei
Riwaya ya Chozi la Heri
Jibu swali la 4 au 5

  1. “Siku moja nitakuwa mtetezi wa haki za kibinadamu, hususan haki za watoto.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
    2. Jadili sifa tano za mzungimzaji. (ala 5)
    3. Kwa kutumia hoja kumi na moja . Onyesha jinsi jamii ya wahafidhina inavyokiuka haki za watoto.
      (al 11)
      Au
  2. Onyesha jinsi maudhui ya usaliti yanavyojitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri. (al 20)

HADITHI FUPI
D.W Lutomia na Phibbian Muthama: Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 6 au la 7

  1. “Isije ikawa mwenye nyumba kuja na yeye mpangaji akachelewa kumfungulia mlango; itakuwa balaa bin beluwa”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili (ala 4)
    2. Jadili umuhimu wa mwenye nyumba anayerejelea (ala 6)
    3. Maisha yalikuwa balaa bin beluwa kwa mpangaji. Thibitisha ( ala 10)
  2.  
    1. Machoka alikumbuka kauli ya jirani yake, Zuhura, aliyeishi kumkumbusha, “wetu ni wetu, hata akiwa mbaya … wetu. Hatuna budi ila kumchagua yeye. Lisilobudi hubidi. Awe amesoma ama hajasoma, angali wetu.”leo hii hata Zuhura mwenyewe alikuwa anajutia kumchagua huyo wetu.

      Kwa muda mrefu, Machoka na Zuhura walikuwa kama fahali wawili hawakai katika zizi moja. Kisa na maana, ni wafuasi wa watu wawili tofauti. Leo hii kinachowaleta pamoja Machoka na Zuhura ni udhikinifu, hali ngumu ya maisha, mfumuko wa bei za bidhaa muhimu na kutozwa ushuru wa kiwango cha juu na serikali hiyo hiyo ya ‘watu wao’. Zuhura alisuta nafsi yake.

      Alikuwa akiitazamia nchi nzuri na maisha bora baada ya uchaguzi. Alitazamia ‘watu wake’ wangezitimiza ahadi walizozitoa wakati wa kampeni zao. Leo hii imebakia kujuta. Kujuta ghya ya kujuta! Tayari alikuwa amekwishafanya kosa. Kosa ambalo alifahamu lilikuwa la kujitakia. Ulikuwa mwiba wa kujidunga usiokuwa na kilio wala kuambiwa pole. Maji yalikuwa yashamwagika, katu hayangeweza kuzoleka…”
      Chambua maudhui katika dondoo hili. (ala 12)
    2. Eleza sababu nne zinazochangia jimbo la Matopeni kutoshuhudia maendeleo ya kisiasa tangu nchi kupata uhuru . (ala 8)

SEHEMU YA E
FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1. Eleza maana ya misimu. (al 2)
    2. Taja mambo manne ya kimsingi yanayochangia kuchipuka kwa msimu. (al 4)
    3. Eleza umuhimu wa misimu katika jamii. (al 10
    4. Taja sifa nne za misimu. (al 4)

MARKING SCHEME

  1. USHAIRI
    1.  
      • Kupigania uhuru /haki /kujiendeleza kiuchumi
      • Washiriki /walisimama /walitaka milki pamoja.    (2 x1)
    2. Kinaya
      • Viongozi kujinufaisha -raia maskini.
      • Viongozi kudharau raia -kuwatemea mate.
      • Raia kupigania uhuru -kutofaidika
      • Kutoafikia maazimio -milki ya haki
      • Walianza safari pamoja -mwishowe wanabaguliwa.   (4 x 1=4)
    3.  
      1. Mizani -msuko -mshororo wa mwisho wa kila ubeti umefupishwa.
      2. Vina-ukara -vina vya kati vinabadilika vya tamati vinatirirka. (2x2=4)
        (Kutaja 1 na kueleza 1)
    4. Mshairi analalamika kuwa viongozi walipofikia hali nzuri ya Maisha tamaa ilizidi huku wakiwa na starehe za kila aina huku akiwasahau waliowapa nafasi za uongozi ili kufikia hali yao ya sasa. (4x1=4)
    5.  
      • Inkisari-Tukawa’chia -Tukawachia-kutosheleza mizani.
      • Kuboronga sarufi -kialeni wadiriki -wadiriki kialeni -urari wa vina.
      • Tabdila -shaki-shaka-urari wa vina
      • Lahaja /kikale -kialeni-kialeni-upekee wa msamiati /mapigo ya kimziki.    (za kwanza 2x2)
    6.  
      • Lina beti nane.
      • Mishororo minne kwa kila ubeti.
      • Mshororo wa mwisho umefupishwa katika kila ubeti.
      • Msishororo wa kwanza hadi wa tatu katika kila ubeti vina vipande viwili.
      • Kila mshororo una mizani kumi na sita na wa mwisho una mizani sita katika kila ubeti .
      • Vina vya ndani havifanani ilihali vile vya nje vinafanana.( 4 x ½ = 2)
  2. BEMBEA YA MAISHA (T. AREGE)
    1. Eleza muktadha wa dondoo. (al 4)
      • Haya ni maneno ya Sara akimwambia Yona kuhusu majukumuwakiwa nyumbani mwao. Ni baada ya kuvutanna kuhusu majukumu ya pale nyumbani na namna Neema aliwasaidia.
    2. Eleza sifa za msemaji. (al 4)
      • Mwenye huruma
        • Anamhurumia Neema kwa majukumu yake na kwa wazazi wake.
      • Mwajibikaji
        • Anamwalika Dina ili aje kumpikia mumewe Yona.
      • Mvumilivu
        • Anavumilia kusutwa, kudharauliwa na hata kuchapwa na mumewe.
      • Mchangamfu
        • Uso wake umejaa tabasamu
      • Mshawishi
        • Anamshawishi Asna aolewe.
      • Mshauri mwema
        • Anawashauri mabinti zake kuhusu maisha. (1x4)
          Mwanafunzi afafanue sifa ili pate alama.
    3. Fafanua umunhimu wa msemewa
      • Ni kielelezo cha watu wenye bidii katika jamii.
      • Anaendeleza maudhui ya athari za ulevi.
      • Ni klielelezo cha watu wanaowajibika.
      • Anawakilisha watu wasiowazia matendo yao na kuishia kujuta.
      • Anakuza ploti. (1x 4)|
        Mwanafunzi athibitishe kila umuhimu.
    4. Taja na uonyeshe mbinu za uandishi katika dondoo. (ala 4)
      1. Nidaa – Hiyo ndiyo ajabu!
      2. Isitiara – wachapa kazi hodari ni njozi iliyopotea.
    5. Eleza maudhui yanayokuzwa katika muktadha. (ala 4)
      1. KAZI
        • Vijana siku hizi hawapendi kufanya kazi.
        • Vijana hawafurahii kazi bali mishahara tu.
      2. MABADILIKO
        • Zamani vijana walikuwa wenye bidii na walipenda kazi lakini siku hizi wao huthamini mshahara tu.
        • Yona alipokuwa mwalimu alifika shuleni alfajiri.
  3. Kila binadamu hukabiliana na mabadikliko katika maisha yake. Jadili kauli hii ukirejelea tamthilia ya Bembea ya Masiha.
    Zozote (20 x1) ( alama 20)
    Majibu
    1. Kutoka ujana hadi uzee – Yona
    2. Sheria kubadilika – katika Elimu. Huwezi kumnyoosha mtoto kwa Kiboko.
    3. kubadilika kwa mtazamo. Yona anabadilisha mtazamo wake kwa sara na kumwelewa kuwa alikuwa mgonjwa.
    4. Kubadilika kwa hisia.- Yona analalamikia Sara kwa kutopika lakini baadaye Anamhurumia.
    5. Yona anabadilisha hali yake ya zamani na kuamua kufuata mkondo mpya wa maisha.
    6. Yona anasawiriwa kama mtu mzuri mwanzoni, lakini baada ya kusutwa na kudharauliwa.
    7. Yona anabadilika na kujutia ulevi wake kuwa pombe ilimchezesha kama mwanasesere.
    8. Kuna mabadiliko kuhusiana na mila na desturi – kuhusiana na mtoto wa kike na wakiume.
    9. Katika kizazi cha leo mtoto wa kike anaweza kurithi na kushughulikia wazazi wao.
    10. Ndoa inakumbwa na mabadiliko – mtu hujichagulia wakati wa kuoa/ kuoelewa kinyume na hapo awali msichana alipolazimishwa.
    11. Majukumu vilevile yanabadilika Yona anaingia jikoni kumpikia Sara.
    12. Mbeleni wazee walifunzwa na dunia lakini kizazi cha leo kinategemea vitabu tu ili kufahamu lolote.
    13. Hali ya uchumi inabadilika – wanaotegemea mifuko yao watakabiliana na kipindi kigumu.
    14. Mitindo ya nyimbo-
    15. Burudani – watoto wa kisasa hupenda kupelekwa out.
    16. Elimu ya sasa haina mafundisho kwa vijana kuhusu ndoa.
    17. Mbeleni watoto walifunzwa na kuzishikilia mila na desturi ila sasa wamwezitupa mila na desturi zao.
    18. Watoto walitumia lugha asilia, leo hawajui hata neno moja.
    19. Zamani wasichana hawakuendelea na masomo.
    20. Safari za kwenda kijijini hazibughudhi kama zamani kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia.
      (zozote 20 x 1)
  4. RIWAYA
    Siku moja nitakuwa mtetezi wahaki za kibinadamu, hususan haki za watoto.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili
      • Maneno ya Chandachema
      • Anawaambia Kairu, Umu, Zohali na Mwanaheri.
      • Wamo katika shule ya Tangamano.
      • Chandachema ana azma ya kutetea haki za watoto kutokana na dhiki alizopitia maishani mwake.
      • Alikuwa akisimulia dhiki alizopitia maishani mwake.
    2. Jadili sifa tano za mzungumzaji
      • Ni chandachema. Ana sifa zifuatazo.
      • Mvumilivu- anavumilia dhiki nyingi maishani tangu kifo cha nyanyake hadi aliposaidiwa na makao ya watoto mayatima.
      • Msiri- wahisani wake Bwana Tenge na Bi. Kimai wanahamishiwa shamba jingine lakini hakuwahi kumwarifu mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya kilimo, Bi. Tamasha.
      • Mzalendo – anataka akamilishe masomo yake kisha arudi kwao kupajenga upya.
      • Mwenye bidii – Anachuma majani chai alfajiri kabla ya kwenda shuleni.
      • Mwenye matumaini – Anatumai kwamba siku moja atakamilisha masomo yake na kurudi nyumbani kwao na kupajenga upya.
      • Mwerevu/mwenye mawazo mapevu- Satua anapoanza kulalamikia matumizi mabaya ya sabuni na kuishia haraka kwa sukari anang’amua kwamba ni yeye anayelengwa na kuhama.
      • Mwenye shukrani – Analishukuru shirika la kidini la Hakikisho la Utulivu kwa kumpeleka katika makao ya watoto mayatima anakosaidiwa.
      • Mdadisi – Anauliziaulizia kuhusu kitovu cha mamake kutoka kwa majirani ilA hakupata habari ya kumsaidia kukijua.
    3. Kwa kutumia hoja kumi na moja onyesha jinsi jamii ya Wahifidhina inavyokiuka haki za watoto.
      • Kutengwa na mama – Sara ananyimwa malezi ya mamake Selume anapotalakiwa na mumewe Mwanzi.
      • kinyimwa tiba – madaktari katika kituo cha afya kilichofunguliwa na mzungu ili kuwatibu wafanyakazi vibarua wanakataa kuwatibu watoto wa wafanyakazi hao.
      • Kuuliwa kwa wazazi – vita vya wenyewe kwa wenyewe vinapozuka katika msitu wa Mamba, walinda usalama wanawaua wazazi wakimbizi na kuwaacha watoto wakiwa mayatima.
      • Kuajiriwa – Chndachema anaajiriwa na shirika la chai la Tegemea akiwa darasa la tano. Sauna akiwa mtoto anaajiriwa katika machimbo yaa mawe, kuuza pombe kwenye baa na kuuza maji.
      • Kuuza mihadarati – Dick anatumiwa kulangua dawa za kulevya na Buda.
      • Kuchomwa - Umati unamchoma Lemi kwa kumkisia kuiba simu.
      • Mzee Kedi anawachoma Becky, Mukala na Tila.
      • Kubakwa – Sauna anabakwa na babake wakambo. Wahuni wanawabaka Lime na mwanahabari.
      • Kuuzwa – Bi Kangara anawauza wasichana anaowateka nyara mandanguroni.
      • Kutupwa – Neema anamwokota mtoto aliyetupwa kwenye biwi la taka.
      • Kuavya – Pete anajaribu kwavya mimba ya mtoto wake nawa pili na watatu.
      • Mama Sauna anamsaidia sauna kuavya kitoto chake.
      • Kukataliwa na wazazi – Pete, kipanga.
      • Kukatiziwa masomo – Sauna anamkatizia Dick masomo akiwa darasa la kwanza.
        . Rehema, Pete
      • Kutumikishwa – Zohali
      • Kuzini machoni pao- Tenge kufanya ukahaba machoni pa watoto wake; hivyo kuwaathiri kisaikolojia.
      • Kuibwa – Sauna anawaiba Dick na Mwaliko na kuwapeleka kwa Bi Kangara.
      • Kutelekezwa na baba zao Kairu, Chandachema.
      • Kutishwa – Buda anamtisha Dick anapokataa kulangua dawa za kulevya.
  5. Jadili jinsi maudhui ya usaliti yanavyojitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.
    • Naomi na subira wanawasaliti wanao kwa kuwaacha wakitaabika.
    • Serikali inawasaliti raia kwa kuwauzia mahindi ambayo yameharibika.
    • Fumba anamsaliti mwanafunzi wake Rehema kwa kuhusiana naye kimapenzi na kumpachika mimba.
    • Mzee Kedi anamsaliti Ridhaa kwa kuichoma familia pamoja na nyumba yake.
    • Wauguzi wAnawasaliti wagonjwa kwa kutowatibu. Mfano, madaktari hawatibu watoto wa wafanyakazi vibarua.
    • Wazazi wa Zohali wanamsimanga na kumtumikisha anapopachikwa mimba.
    • Mama Sauna anamsaliti mumewe,Bw. Kero kwa kumtoroka na kuolewa na Maya.
    • Wanawake kwa kuwazaa watoto na kuwatupa kwenye mabiwi ya taka.
    • Bwana Maya kwa kuhusiana kimwili na Sauna bintiye.
    • Wahafidhina wanaosaliti wajibu wao wa kuboresha uongozi kwa kupokea homgo na kuwachangua viongozi wasiostahili.
    • Annette anamsaliti mumewe kiriri anapomwacha na kwenda kuishi ughaibuni.
    • Halmashauri inayotoa mikOpo ya masomo inawasaliti wanafunzi maskini kwa kutoa mikopo na kuwaacha wale maskini.
    • Bw. Tenge anamsaliti Mkewe Bi Kimai kwa kuzini na makahaba anapoenda mashambani.
    • Tenge anawasaliti watoto wake pamoja na Chandachema anapofanya mapenzi machoni pao.
    • Mwanzi anamsaliti mkewe Selume kwa kumkataa na kuoa msichana wa kwao.
    • Baba Kipanga kwa kumkana Kipanga.
    • Fumba kwa kumtelekeza mwanawe Chandachema.
    • Wanafunzi kwa kumtenga Ridhaa michezoni na kumsimanga.
    • Wasimamizi wa hospitali za umma wanaiba dawa za hospitali na kuziuza kwenye maduka yao.

SEHEMU YA HADITHI FUPI
D.W Lutomia na Phibbian Muthama
Mapambazuko ya Machweo na hadithi nyingine.

  1. “Isije Ikawa mwenye nyumba kuja na yeye mpangaji akachelewa kumfungulia mpangaji itakuwa balaa bin beluwa.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
      • Maneno ya msimulizi
      • Anarejelea Lilia
      • Lilia alikuwa nyumbani
      • Lilia anamngojea mumewe Luka huku akiwa na mawazo mengi kutoka mateso ambayo amepitia kutoka kwa Luka.
    2. Jadili umuhimu wa mwenye nyuMba anayerejelea. (alama 6)
      • Anabainisha maudhui ya unyanyasaji wa kijinsia – Luka anamchapa Lilia.
      • Anaendeleza maudhui ya uongozi mbaya kwa kutotimiza ahadi alizowapa wananchi.
      • Pia anachimuza maudhui ya usaliti kwani analiuza kanisa aliloachiwa na babamkwe Lee Imani.
      • Pia anaendeleza maudhui ya elimu kwa kuwa yeye na mkewe Lilia wanasoma katika chuo kimoja.
      • Anaendeleza maudhui ya ukandamizaji hasa katika kituo cha polisi. Ana marafiki kituoni wanaomjuza kuhusu kwenda kwa mkewe pale.
      • Ni kielelezo cha wanaume katili licha ya mkewe kuwa na ujauzito, Luka anataka waandamane naye katika siasa.
      • Ni kiwakilishi cha viongozi wanaotumia mamlaka yao vizivyo. Baada ya kuwa gavana anasema kuwa ana uwezo wa kufanya haki kuwa batili na batili kuwa haki.
        (zozote 6 x 1)
    3. Maisha yalikuwa balaa bin beluwa kwa mpangaji.Thibitisha.
      • Ana mawazo na wasiwasi – mumewe harejei nyumbani.
      • Kutusiwa na mumewe anamfananisha na nguruwe anapokataa kuandamana naye katika siasa.
      • Anakanwa na mumewe kuwa akiwa kazini yeye si mumewe.
      • Kupigwa – Luka anampiga Lilia si mara moja tu. Anamshika nywele na kumbururura, anapopigwa teke tumboni….
      • Kuharibikia kwa mimba – Mimba yake inaharibika na hili linamliza sana.
      • Anakatazwa kufika ofisini.
      • Ana hofu ya kutochukua simu inapopigwa.
      • Wakati alipigwa na kuanguka chini, alikuwa anashindwa ampigie nani.
      • Baada ya kufiwa na wazazi wote anahisi hana mtetezi.
      • Lilia alikuwa na wasiwasi wakati Luka aliingia kanisani na kuketi karibu naye.
      • Alikuwa na wasiwasi kwa wale waliomtembelea Luka hospitalini kwani hakukuwa na jamaa yeyote.
      • Lilia alikuwa na wasiwasi kuhusu yule mgonjwa,”Luka’ aliyetambulika na mamamkwe lakini yeye hakumjua.
        (zozote 10 x1)
  2.  
    1. Maudhui katika dondoo
      • Mgogoro- Machoka na Zuhura walikuwa fahali wawili hawakai zizi moja.
      • Ukabila – “Wetu ni wetu, ata akiwa mbaya….wetu.
      • Umoja – Leo hii kinachowaleta pamoja Machoka na Zuhura ni udhikinifu, hali ngumu ya maisha.
      • Hali ngumu ya masiha – mfururiko wa bei za bidhaa muhimu na kutozwa ushuru wa kiwango cha juu.
      • Majuto – Leo hii hata Zuhura mwenyewe alikuwa anajutia kumchagua huyo wetu.
      • Utamaushi – Maji yalikuwa yashamwagika, katu hayangeweza kuzoleka…
      • Usaliti- waliochaguliwa kama watu wao walikosa kuendeleza uongozi wenye manufaa.
      • Unafiki – Ahadi zilizotolewa kwa kampeni hazikutimizwa.
        (zozote 6 x 2)
    2. Sababu za matopeni kutoshuhudia maendeleo.
      • Usaliti – Jimbo la Matopeni linawachagua viongozi kwa matumaini ya kuboresha maisha ya wananchi.
      • Viongozi wanapochagulia wanatupikia mbali ahadi walizotoa kama vile kuimarisha sekta ya afya, kutengeneza barabara, kuimarisha ukulima n.k.
      • Ukabila na unasaba- Wakati wa kampeni Zuhura anamwambia Machoka kuwa wanastahili kumchagua mtu wao. Matopeni imetawaliwa na familia moja; Sugu Senior na Sugu Junior.
      • Ujinga – kutoshuhudia maendeleo ndiyo malipo ya kumpigia kura kiongozi kwa kutumia matumbo yao badala ya akili.
      • Ufisadi – Wanamatopeni wanawachagua viongozi kwa sababu wakati wa kampeni, wanaowania wanawanunulia unga, khanga, sukari na mafuta.
      • Viongozi kuendeleza udikteta na ukoloni mamboleo. Kahindi Mlalama anadai kuwa vizingiti hivi haviishi daima matopeni licha ya kuwa bado wana ndoto ya kesho njema.
      • Ubadhirifu wa mali ya umma, mali ya umma inayotumiwa kugharamia safari za ndege za viongozi wa majimbo jirani.
      • Utabaka – Viongozi kwenye hafla ya kuapisha Sugu Junior wameketi vyema kwenye hema zilizotandikwa vyema, ilhali wananchi wameketi kwenye jua kali.
      • Uvunjaji wa sheria- kupiga kura si kazi, kazi ni kuhesabu kura.
      • Wanasiasa kukosa sera za kimaendeleo.
      • Wananchi kutuwazia sera za wanasiasa.
      • Propaganda – Wananchi kushindwa kufikiria ahadi za wanasiasa.
        (zozote 8 x 1)

FASIHI SIMULIZI
MAJIBU

  1.  
    1. Misimu -Semi za muda ambazo hubuniwa na kutumiwa katika mazingira maalum na katika kipindi maalum cha wakati. (al 2)
    2.  
      • Rika na umri wa matumizi k.m vijana,wazee.
      • Mazingira-sokoni ,shule,bandarini
      • Mada husika -mavazi,mtu
      • Jinsia husika
      • Sababu za kutumia -kuficha siri nk
        (al 4x1)
    3.  
      • Ni kitambulisho cha kundi fulani la watu.
      • Huhifadhi siri za wanaotumia.
      • Kuibua hisia fulani miongoni mwa watumiaji.
      • Hukuza ushirikiano.
      • Huongeza haiba na ladha katika lugha.
      • Huhifadhi utamaduni na historia ya jamii.
      • Ni kielelezo cha mpangilio wa jamii Fulani kijamii na kiuchumi.
      • Hutumiwa kuondoa urasmi katika mazungumzo.
        (Zozote 5x2)
    4.  
      • Ni semi za muda
      • Hutumiwa na kundi fulani la watu kufanikisha mawasiliano.
      • Baadhi ya misimu hudumu na kukubalika kama semi au msamiati sanifu wa lugha husika.
      • Misimu si semi sanifu, hivyo haipaswi kutumiwa katika miktadha rasmi.
      • Misimu huundwa kwa mbinu mbalimbali kama vile kutoa maneno au kubadili mpangilio wake.
      • Misimu hupata maana yake kutoka kwa watumiaji pamoja na muktadha wa mahali na wakati.
        (Zozote 4x1)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Chogoria Murugi Zone Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?