Kiswahili Paper 3 Questions - Mumias West Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe.
  2. Jibu maswali Manne pekee
  3. Swali la kwanza ni la Lazima
  4. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Riwaya, Tamthlia, Hadithi fupi na Fasihi simulizi
  5. Usijibu maswali Mawili kutoka Sehemu Moja
  6. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba maswali yote Nane yamo. 
  7. Majibu yote yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

Kwa Matumizi ya Mtahini Pekee

Swali

Upeo

Alama

1

20

 
 

20

 
 

20

 
 

20

 

JUMLA

80

 


MASWALI

1. LAZIMA SEHEMU A : SHAIRI
Soma shairi lifuatalo kwa makini, halafu ujibu maswali yanayofuatia

Hakika yamekithiri, ni asoyajua?
Wazazi wayahubiri, na hivyo kutubagua
Hayana kamwe fahari, ila kweli yatua.
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Mwanamke siyo huyo? Baba mtu anasema
Mwanamke kwani huyo? Anateta naye mama,
Sababu waitoayo, haina nguvu wima,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Kabila letu ni hili, sharuti uoe huko,
Unazomewa ukali, kuoa nje ni mwiko.
Hivyo twafanywa dhalili, viumbe tuso mashiko
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Wanachunguza tabaka, ndipo wazushe wahaka
Wauliza kwa haraka, wajue lake tabaka,
Wasioridhika wafika, arudi alikotoka,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Waichuja yake dini, ndo ndoa ibarikiwe
Lazima yake imani, iwe sawa na yakuwe
Huu kweli ni uhuru, wataka uondolewe,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Japo mwanipa elimu, uhuru ninautaka,
Na mie muniheshimu, nipate nilomtaka
Kuoa kitu adhimu, so mchezo kwa hakika
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Nawashauri wazazi, twahitaji kupumua,
Wawili ndo waamuzi, haa Mungu anajua,
Wasifu pasi ajizi, kwa yao njema hatua,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Ndoa akivunjikana, wawili wajisakeni
Isije kusemekana, wazazi ndio kiini,
Ndiposa hata Rabana, situtie lawamani,
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Aliye na masikio, mesikia kwa makini,
Tusitamani kilio, mtihani tulo vitani,
Wakioa sema ndio, Mola asikulaani
Uhuru wa kuoana, ni lini tutaupata?

Maswali

  1. Lipe shairi hili anwani mwafaka. (al.1)
  2. Shairi hili laweza kuwekwa katika bahari mbili. Zitaje huku ukitoa mifano. (al.2)
  3. Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili. (al.2)
  4. Eleza ujumbe unaojitokeza katika shairi hili. (al.4)
  5. Jadili muundo wa shairi hili. (al.4)
  6. Taja aina mbili za urudiaji katika shairi. (al.2)
  7. Ukizingatia shairi ulilopewa, eleza jinsi mshairi alivyotumia uhuru wake. (al.2)
  8. Taja toni ya shairi hili. (al.1)
  9. Eleza maaana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika kwa shairi.
    1. Wahaka
    2. Yamekithiri (al.2)

SEHEMU YA B :
RIWAYA A. Matei: chozi la heri Jibu Swali la 2 Au la 3

2. Alikuwa ameumwa na nyoka. Bafe hasa na bila shaka mwenyewe kuumwa na nyoka akiona ung’ongo hushtuka.

  1. Eleza muktadha wa kauli hii. (al.4)
  2. Fafanua sifa tatu za mrejelewa. (al.3)
  3. Thibitisha namna wahusika kadhaa walivyoumwa na nyoka katika riwaya. (al.13)

3.

  1. Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo. (al.10)
    Hata hivyo, tulijipa kuamini kwamba haya ndiyo yaliyokua majaliwa yetu, tuliikuwa wenye haja, maiti hasa na tangu hapo maiti hachagui sanda wala jeneza.

    Tulivumilia tukidhani hali itatengenea, tukiamini kwamba tungerudi kwetu lakini, lo! Wanasema wajuao kuwa msitu ni mpya ila nyani ni wale wale uongozi mpya haukuleta ahueni yoyote katika maisha yetu! Kilicho badilika nikikwamba tulipwa ardhi zaidi ya kujengua mabanda zaidi ili kupunguza msongamano katika mabanda ya awali. Bado tu pale pale…sioni kama pana nyumbani pema zaidi ya pale kambini. Vumilia mwenzangu zingatia masomo yako kwani ndiyo yatakayokuvusha kutoka kwenye lindi hili la huzuni. Baada ya kusema haya, Kairu alitulia kwa muda kama mtu anayevuta fikra.
  2. Jadili jinsi maudhui ya ndoa yamejitokeza katika riwaya ya chozi la heri.

SEHEMU YA C: TAMTHILIA
Bembea ya Maisha.
Jibu swali la 4 au 5.

4. Basi usijipandishe presha mama! (al.10)

  1. Eleza muktadha wa dondoo. (al.4)
  2. Bainisha vipengele viwili vya kimtindo vinavyojitokeza katika dondoo. (al.2)
  3. Eleza sifa za msemewa. (al.4)
  4. Jadili jinsi maudhui ya utamaduni yanavyojitokeza katika tamthilia. (al.10)

5. Basi tu! Wenzenu ndio walioniingiza kwenye mkondo huu. Kama unakumbuka nilikuwa miongoni mwa vijana wa kwanza kuingia kwenye dini.

  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (al.4)
  2. Eleza toni inayojitokeza katika dondoo. (al.2)
  3. Jadili mbinu mbili za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo. (al.4)
  4. Jadili umuhimu wa mzungumzaji katika dondoo hili. (al.10)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI
Mapambazuko ya machweo na hadithi nyingine Jibu swali la 6 au 7.

6. Fadhila Za Punda
Alimfungulia mlango akitetema kama unyasi upeo uvumapo. Mara akashika nywele karibu zing’ooke kisha akabururwa hadi kwenye chumba cha malazi. Si kipigo hicho, si makofi, si ngumi, si mateke tena ya mtu aliyevaa buti.

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
  2. Bainisha taswira zinazojitokeza katika dondoo hili. (al.2)
  3. Eleza sifa nne za mrejelewa. (al.4)
  4. Kwa kurejelea hadithi hii eleza jinsi maudhi ya nafasi ya mwanamke yalivyojitokeza. (al.10)

7. Ukombozi wa wanawake unakumbwa na vizingiti vingi sana. Jadili ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi ya Sabina. (al.20)
SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
8. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Zamani sana Paka na Mbwa waliishi peponi. Mungu alikuwa amewatunukia mapenzi si haba. Nyumba yao ilikuwa imepambwa kwa vyombo vya dhahabu na vito vingine. Bustani kubwa lilizunguka nyumba hiyo ya fahari. Matunda ya kila aina: si matikiti, si maembe, si matufaha, si machungwa; yote yalijaa kochokocho mitini. Alimuradi Paka na Mbwa hawakupungukiwa na lolote. Wanyama wengine hawakuisha kuwaonea kijicho wanyama hawa.
Siku moja, Malaika Mkuu mbinguni alikuwa na ujumbe kwa Mungu. Aliamka asubuhi na mapema na kuwaita Paka na Mbwa ambao walikuwa wamejipambanua kama watumishi waaminifu na kuwaambia, “Ndugu zangu, nina salamu muhimu ambazo ningependa kuwakabidhi mmpelekee Mungu. Kwa vile ujumbe wenyewe ni mrefu, nimeuandika na kuutia ndani ya bahasha hii. Basi nitakukabidhi ewe ndugu yangu Mbwa bahasha hii. Ni sharti uitunze isije ikakuponoka njiani”. Mbwa akachukua bahasha na kuitia ndani ya mfuko wa shati lake.
Kabla ya Paka na Mbwa kupondoka, Malaika Mkuu aliwaambia, “Pana jambo ambalo ningependa kuwatahadharisha nalo. Msizungumze na yeyote wala chochote hadi mtakapofika kwenye kasri la Mungu.”
Maneno haya ya mwisho yalimwia Mbwa vigumu. Alijua kuwa yeye hakuwa mzungumzaji kiasi hicho lakini kuambiwa asile chochote na hali safari hiyo ingewachukua kutwa mzima! Alichojua, kama alivyojiwazia, ni kwamba hata Malaika Mkuu asingeweza kuwa na stahamala wa kiwango hicho!
Safari ilianza saa moja asubuhi baada ya staftahi. Paka na Mbwa wakaandamana guu mosi guu pili. Jua la utosi liliwapata hata kabla ya kufika nusu ya safari. Njaa ilikuwa imeanza kuwauma, uchovu ukawa unawang’ata kama nge. Hata hivyo, walijipa moyo, wakajiambia kuwa subira yao itavuta heri baada ya muda mfupi.
Ghafla kama ajali, sungura alitokea katika kichaka kilichokuwa karibu. Macho ya Mbwa ndiyo yaliyokuwa ya kwanza kumtua sungura huyo. Moyo wake ukamzaini kukitwaa kisungura hicho na kukonga roho yake. Mara alikumbuka onyo ambalo walikuwa wamepewa na Malaika Mkuu. Mvutano mkali ulizuka katika nafsi yake, “Bwana wewe una njaa, vipi utatakiacha kitoweo ambacho kwa kweli kinakunyooshea mkono?” kwa upande mwingine dhamiri yake ilimuasa na kumwambia, “Mwenye pupa hadiriki kula tamu, tuliza moyo wako, usikaidi amri ya mtumishi wa Mungu usije ukauma dole.”
Basi mjukuuu wangu, Mbwa akawa hajifai kwa mgogoro huu wa nafasi. Mara uhayawani wake ulimvaa, akafyatuka kama mshale na kumhujumu Sungura. Akamla asimbakize chochote! Kwisha kumla, akamwambia Paka, “Ndugu, tuendelee na safari, huenda hata wewe ukabahatika kuambulia angaa buli la maziwa.”
Hatua chache mbele, Panya alitokea. Akajishaua mbele ya marafiki zetu hawa kama kwamba alitarajia posa kutoka kwa mmoja wao. Moyo wa Paka ulimpapa kwa tamaa ya kutaka kulipiza kisasi kwa kiumbe huyu ambaye daima alizoea kuyahujumu maghala ya mahindi. Paka akamtazama Panya kwa jicho la hasidi, akatayarisha mafumba yake kwa vita. Lakini ghafla akakumbuka maneno ya Malaika Mkuu na kujiasa. Alimnyoshea Panya kidole na kumwambia, “Laiti Malaika Mkuu asingekuwa amenionya dhidi ya kula chochote, ningekufunza funzo la maisha.” Basi Panya akanusurika.
Sasa walikuwa wakitazama kasri la Mungu. Kwa mbali, mbwa alikaza mboni zake zaidi na kumwona Swara akija kwa madaha. Ziraili akamwingia, “Kaka Mbwa, natumai unakumbuka walivyotwambia wahenga kuwa ngojangoja huumiza matumbo. Je, una hakika gani kuwa baada ya kufikisha ujumbe utapewa hata tone la maji? Hamadi kibindoni Bwana. Faida chajio ukionacho sasa. “bila nadhari, Mbwa alimtwaa Swara na kumla shibe yake.
Jua lilipozama Paka na Mbwa walijipata nje ya lango la kasri. Mungu akatoka kwenye chumba chake cha maongezi na kwenda kupokea salamu zake. Akamwuliza Mbwa, “Je, safari ilikuaje?” Mbwa akajibu, “Safari ilikuwa ndefu, lakini yenye mafanikio makubwa. Niliweza kuwashika sungura na Swara na kuwala. Njaa haikunidhili mno, ila bahasha niliyopewa ilipotea njiani. “Mungu akamjibu, “Subiri hapo nje ya lango. Nitakuita baada ya kuzungumza na Paka. “Paka alipoulizwa, alijibu kwa sauti hafifu, “Safari ilikuwa ndefu mno. Sikuweza kuzungumza na yeyote. Nilitaka kulipiza kisasi kwa Panya niliyekutana naye ila sikuweza kwani Malaika Mkuu alikuwa ametuonya dhidi ya hayo.” Mungu alimpa pole kwa hayo. Akamkaribisha ndani ya kasri na kumpa sharubati kwanza. Mbwa akabaki nje akisubir. Tangu siku hiyo, Mbwa daima husubiri nje naye Paka huishi ndani ya nyumba. Hadithi yangu inaishia hapo.

Maswali

  1. Hiki ni kipera cha aina gani? Thibitisha. (al.2)
  2. Changanua mbinu za kimtindo katika utungo huu. (al.10)
  3. Eleza namna hadhira inavyoweza kushiriki katika uwasilishaji wa utungo huu. (al.4)
  4. Jadili jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza Fasihi simulizi. (al.4)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions - Mumias West Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?