Kiswahili Paper 2 Questions - Mumias West Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO KWA MTAHINIWA

  1. Karatasi hii ina kurasa kumi na mbili zilizopigwa chapa.
  2. Andika jina na nambari yako katika nafasi ulioachiwa hapo juu.
  3. Jibu maswali yote.
  4. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.
  5. Majibu yote yaandikwe katika lugha ya Kiswahili.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

SWALI

UPEO

ALAMA

1

15

 

2

15

 

3

40

 

4

10

 

JUMLA

80

 



MASWALI

1. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Zaraa ndio uti wa mgongo wa taifa Ia Kenya. Viwanda vingi nchini hutegemea kilimo kama malighafi na kuwalisha wafanyakazi. Licha ya umuhimu wa sekta hii, mkulima ambaye ndiye nguzo ya zaraa anaendelea kukabiliwa na matatizo mbalimbali yanayokwamiza juhudi zake.
Mojawapo ya matatizo yanayomkabili mkulima ni ukosefu wa ushauri wa zaraa. Wataalamu wanaotarajiwa kumshauri mkulima kuhusu njia bora za kuzalisha na kuongeza pato lake ni haba ikilinganishwa na idadi ya wakulima wanaohitaji ushauri. Wachache walioko nao wanakwamizwa na mambo tofauti. Mathalani, utawapata hawaendi nyanjani ili kukutana na wakulima kwa kuwa hawana vyombo vya usafiri. Iwapo vipo, huenda petroli ikawa ni kizungumkuti. Halikadhalika, usisahau kuwa baadhi ya wataalamu hawa ni walazadamu au mafisadi. Kuna wale wanaofika ofisini na kushinda siku nzima wakisoma gazeti huku wakijaza miraba, wakicheza bao au karata. Kuna wale nao ambao hufika ofisini wakaangika koti au sweta kitini ili waonekane kuwa bado wapo na kisha kutokomea kwenda kushughulikia mambo yao ya kibinafsi yasiyohusu ndewe wala sikio kazi waliyoajiriwa kuifanya.
Ukosefu wa sera mwafaka kuhusu ardhi nalo ni tatizo jingine linalotatiza kilimo nchini. Serikali haijaweka sera mahususi kuhusu matumizi ya ardhi. Wananchi wengi huongozwa na taratibu za utamaduni za nasaba zao. Taratibu hizi hupendekeza ugawaji wa ardhi kwa minajili ya urithi kulingana na warithi waliopo. Si ajabu kuwa kote nchini, ardhi inayofaa kwa kilimo imekatwakakatwa vipande vidogovidogo ambavyo haviwezi kuwa na faida kwa zaraa.
Kushindwa kwa mkulima kuongeza virutubishi ardhini ni changamoto nyingine inayokabili kilimo nchini. Ulimaji wa kile kipande cha ardhi miaka nenda miaka rudi, bila kukipa nafasi ya kukipumzisha, huufanya mchanga kupoteza virutubishi muhimu vinavyohitajiwa na mimea. Hili nalo huchangia kupunguza uzalishaji wa mazao. Ili kutatua tatizo hili, wakulima wengi hukimbilia mbolea za kisasa ambazo badala ya kumsaidia, humwongezea madhila. Mbolea hizi zinatambulikana kuchangia uchafuzi wa mchanga na ardhi.
Mabadiliko ya hali ya anga nayo huongeza msururu wa madhila ya mkulima. Mabadiliko haya yamemfanya mkulima kushindwa kupanga wakati anaotakiwa kutayarisha shamba, kupanda, kupalilia, kunyunyizia dawa na kadhalika kwa sababu mvua imekuwa adimu. Badala yake panakuwa na vipindi virefu vya kiangazi ambavyo huathiri bidii za mkulima. Maji nayo yanaendelea kupungua na wakulima wengi hawawezi kukimu mahitaji ya unyunyizaji maji mashambani.
Maradhi pamoja na wadudu waharibifu kama vile viwavi, kupe na mbung’o ni changamoto nyingine inayotatiza juhudi za mkulima hapa nchini. Haya hupunguza uzalishaji wa mkulima au wakati mwingine kupunguza mifugo au mimea yake.
Kwa sadfa, iwapo mkulima ataweza kuzalisha mazao licha ya msururu huu wa vikwazo; ana tatizo jingine linalomngojea: ukosefu wa soko kwa mazao yake. Aghalabu, maeneo mengi yanayotoa mazao ya kilimo kwa wingi huwa na matatizo ya usafiri. Njia na barabara huwa mbovu na hazipitiki. Mazao mengi huwa hayafiki sokoni kwa wakati na huwa ni hasara kwa wakulima. Fauka ya hayo, gharama ya uzalishaji wa mazao ya kilimo hapa nchini huwa ya juu zaidi kuliko faida anayopata mkulima. Watu wengi wameacha kutegemea kilimo kama njia ya ajira kwa kuwa hakilipi. Hii ni zaidi ya ushindani wa bidhaa za kilimo kutoka nje ya nchi ambao ni tatizo jingine linalomkabili mkulima. Mara nyingune wakulima wa kutoka nje ya nchi husaidiwa na serikabi zao kuzalisha mazao kwa kufidiwa au kupewa karadha. Mazao kama haya yaingiapo sokoni huuzwa kwa bei ya chini na hayawezi kushindana na yale ya wale wasiopata mchango wowote kutoka kwa serikali kama wakulima wa hapa nchini.
Mkulima wa Kenya anahitaji msaada wa dharura ili aweze kunyanyua kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa uchumi wetu. Lau haya hayatofanyika, uchumi wetu utaendelea kudidimia. Maswali

  1. Ipe taarifa hii anwani mwafaka . (ala.1)
    ................................................................................................................................................................................................................................................................................................
  2. Kilimo kina umuhimu gani hapa nchini? (ala.2)
    ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
  3. Ni kwa nini wataalamu wa kilimo waliopo hawawafai wakulima nyanjani? (ala.4)
    ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
  4. Eleza sababu zozote nne zinazokinga mkulima kuzalisha mazao ya kutosha. (ala.4)
    ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
  5. Kwa nini watu wengi wameacha kutegemea kilimo kama njia ya ajira? (ala.2)
    ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
  6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika taarifa. (ala.2)
    1. Walazadamu
      ................................................................................................................................................................................................................................................................................................ ................................................................................................................................................
    2. Karadha
      ................................................................................................................................................................................................................................................................................................ ................................................................................................................................................

2. UFUPISHO (ALAMA 15 )
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili na maarifa fuvu tele ili kuratibu shughuli na mambo; kiumbe kilichopewa uwezo wa kuwasiliana na kutumia sauti nasibu ili kuwa na urari na muwala; kiumbe kilichopewa uwezo wa kufaidi viumbe wengine kwa njia mbalimbali na jumla jamala; hiki ndicho kiumbe kilichopewa idhini maalumu ya kuzaana na kujaza dunia. Huyu ndiye mwana wa mama ambaye sasa amegeuka ndovu kumla mwanawe.
Kwa sababu ya bongo alizonazo, binadamu ana uwezo wa kutumia teknolojia kwa manufaa yake na ithibati zipo tele. Binadamu ametumia nyambizi kuzuru chini ya bahari; amefika mwezini; amevumbua mangala; amevumbua uyoka; amevumbua tarakilishi na sasa shughuli zake ni za kutandaridhi. Mwenyewe yuasema kuwa dunia yake imekuwa kitongoji katika muumano huu.Chambilecho wavyele, akili nyingi huondoa maarifa.Binadamu amekuwa dubwana linalojenga kushoto na kubomoa kulia na tuna sababu ya kulisoza dubwana hili kidole. Rabana ndiye msanii asiye mfanowe kwani aliisawiri dunia kwa kila lililo jema kwa siku sita mtawalia na kumpa binadamu mazingira murua. Rabuka akaona yote yalikuwa mema na mazuri; akamwambia binadamu, “Haya, twende kazi!”
Viwanda vya binadamu vinatiririsha maji-taka ovyo hadi mitoni, maziwani na baharini na matokeo yamekuwa ni vifo vya viumbe vya majini kama samaki ambavyo ni urithi aliopewa na Muumba. Hakuna kiumbe kinachoweza kustahimili maisha bila maji safi. Maji yote sasa yametiwa sumu na binadamu kwa sababu ya ‘maendeleo’ yake. Joshi kutoka katika viwanda vivyo hivyo nalo limehasiri ukanda wa ozoni ambao sasa umeruhusu jua kutuhasiri kwa joto kali mno. Siku hizi inasemekana kuwa kuna mvua ya asidi inayonyesha katika baadhi ya sehemu za dunia na kuleta madhara makubwa. Labda hata mabahari yamekasirika kwa sababu hivi majuzi katika kile kilichoitwa ‘tsunami’ bahari lilihamia nchi kavu na kusomba maelfu ya binadamu na kuwameza wazima wazima. Vimbunga navyo vimetokea kwa wingi. Wataalamu wanasema kuwa viwango vya miyeyuko vitazidi kwa sababu ya joto na kiwango cha maji kitazidi pia. Binadamu atatorokea wapi?
Idadi ya binadamu imezidi hadi kiasi asichoweza kukishughulikia kwa sababu anaijaza kiholela kwa sababu anadai kuwa aliruhusiwa kuijaza. Hii ni imani potovu. Anasahau kuwa alipewa ubongo wa kuwaza na kuwazua kabla ya kufanya chochote. Dhiki, maradhi na ufukara zimehamia kwa binadamu na kumtia kiwewe.
Binadamu amefyeka misitu kwa kutaka makao, mashamba, mbao, makaa, ujenzi wa nyumba na barabara na mahitaji mengine mengi. Wanyama wamefurushwa na wengi kuangamia kwa sababu ya ukosefu wa chakula na wengine kushindwa kuhimili mabadiliko katika mazingira. Chemichemi za maji zimekauka nalo jangwa limeanza kutuzuru kwa kasi inayotisha. Kazi ya binadamu imekuwa ya kusukia kamba motoni. Itambidi aanze kujenga kwa matofali ya barafu!

Maswali

  1. Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa taarifa, fupisha aya mbili za kwanza.
    (Maneno 50-60) (alama 7)

    Matayarisho
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
    Jibu
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….......…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………........……………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………..
  2. Kwa kuzingatia aya tatu za mwisho, eleza mambo muhimu yanayoshughulikiwa na mwandishi.
    (Maneno 85 – 95) (alama 8)

    Matayarisho:
    ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
    Jibu:
    ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

3.MATUMIZI YA LUGHA ( ALAMA 40)

  1. Taja mifano miwili ya sauti mwambatano. (alama 1)
  2. Andika sentensi ifuatayo katika umoja. ( alama 1 )
    Maseremala walilainisha mbao hizo wakatutengenezea meza.
  3. Bainisha silabi zitakazowekwa shadda katika maneno yafuatayo: (alama 2)
    1. miambakofi
    2. yatazoleka
  4. Tumia neno ‘hawa’ katika sentensi kama ; (alama 2)
    Kiwakilishi

    Kivumishi
  5. Ainisha vihusishi katika sentensi ifuatayo; (alama 2)
    Babu alifika mapema kuliko wote halafu akaondoka.
  6. Andika sentensi yenye muundo ufuatao. (alama 2)
    KN (N+RH)+KT(TS+T)
  7. Tumia kitenzi “ Fa “ katika sentensi kuonyesha mazoea (alama 1)
  8. Andika neno lenye muundo ufuatao wa silabi. (alama 2)
    1. irabu,konsonanti,konsonanti,irabu,konsonanti,irabu
    2. konsonanti,konsonanti,irabu,irabu
  9. Weka maneno haya katika ngeli zake. (alama 2)
    Miwani

    vyanda
  10. Ainisha mofimu katika neno lifuatalo. (alama 3)
    Aliyesamehewa
  11. Andika kinyume cha sentensi ifuatayo kwa kuzingatia maneno yaliyopigiwa mstari
    ( alama 2)
    Punde tu alipouliza swali hilo Halima aliingia darasani
  12. Bainisha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
    Viwanda vikianzishwa mashambani idadi ya wanaohamia mjini itapunguzwa.
  13. Tambua yambwa na chagizo katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
    Juma alimtunzia Kuta watoto hao kwa upendo.
  14. Yakinisha sentensi ifuatayo (alama 2)
    Badi huwa hapitii hapa , huenda usimpate.
  15. Ainisha virai katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
    Viongozi wengine watasafiri ughaibuni kesho.
  16. Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa (alama 1)
    Mtu huyo alifuata njia iliyomwelekeza mjini.
  17. Andika katika usemi wa taarifa. (alama 2)
    “Nitamwalika kesho jioni .” Fatuma akasema.
  18. Changanua sentensi hii kwa kielelezo cha mstari (alama 2)
    Mvua imepusa na watu wameanza kuondoka.
  19. Kanusha ; (alama 2)
    Mbao hizo zilihifadhiwa ili ziuzwe mjini.
  20. Zito ni kwa jepesi,___________ ni kwa choyo, na _____________kwa kali. (alama2)
  21. Tunga sentensi moja kubainisha maana mbili za neno: zima (alama 2)

4.ISIMU JAMII ( ALAMA 10 )
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali
“Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa , mahakama hii imethibitisha bila chembe ya shaka kwamba wewe mshtakiwa, Bi. Mlachake Chauchau ndiye uliyepika pombe haramu ambayo ilisababisha vifo vya raia hamsini na kupofuka kwa wengine mia moja. Unahukumiwa kwa kosa la mauaji. “

  1. Bainisha sajili ya makala haya kwa kutoa mifano miwili kutoka kwenye makala. ( alama 2 )
  2. Fafanua sifa nyingine nane za sajili hii ambazo zingejitokeza katika makala haya ( alama.8 )
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions - Mumias West Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?