Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lugari Constituency Joint Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika insha mbili.
  • Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua Insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila Insha isipungue maneno 400
  • Kila insha ina alama 20
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya kiswahili

MASWALI

  1. LAZIMA
    Katika karne hii ya kiteknolojia, ni dhahiri kuwa mabadiliko ya kiteknolojia yamechangia pakubwa kuboresha maisha. Wewe ni Mhariri wa Gazeti La Zinduka, andika tahariri ukieleza jinsi teknolojia ya kisasa ilivyochangia kuboresha maisha.
  2. Serikali ni ya kulaumiwa kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini. Jadili.
  3. Andika Insha itakayothibitisha ukweli wa methali:
    Usipoziba ufa utajenga ukuta.
  4. Andika Insha itakayoanza kwa maneno haya:
    Baada ya kusafiri mwendo wa kilomita mbili hivi, watu wawili waliokuwa wamefunika nyuso zao kwa barakoa na bunduki mikononi...
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA (SIRI)
  1. Swali la lazima 
    • Hii ni Insha ya kiuamilifu
    • Ni tahariri
    • Sura ya Insha ya tahariri izingatiwe. 
    • Asiyezingatia sura aondolewe alama 4.
    • Kichwa kianze kwa neno tahariri
    • Utangulizi utoe maelezo machache kuhusu mada.  Mtahiniwa atoe hoja kikamilifu

      Hoja 
    • Imerahisisha kufikisha ujumbe kwa watu wengi kwa haraka mfano runinga, radio, rununu
    • Imeimarisha biashara kote ulimwenguni
    • Imeimarisha huduma za afya kote ulimwenguni
    • Imeboresha kilimo nchini .
    • Imeboresha usalama kwa mfano kamera za siri
    • Imeboresha uwajibikaji kazini
    • Imerahisisha usafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine.
    • Imerahisisha masomo shuleni kwa mfano kudurusu vitabu kwenye maktaba mbalimbali bila kusafiri.
    • Imeimarisha utangamano wa kimataifa
    • Imerahisisha shughuli za kitaifa k.v  usajili wa wapiga kura.

      Hitimisho ijitokeze
  2. Serikali ni ya kulaumiwa kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini. Jadili. 

    Kuunga 
    • Uchache wa maafisa wa usalama nchini.
    • Ukosefu wa ajira nchini.
    • Uchochole uliokithiri miongoni mwa wanajamii.
    • Kutotekeleza sera kuhusu mpango wa uzazi ambapo kuongezeka kwa idadi ya watu kunasababisha kung’ang’aniwa kwa rasilimali kama mashamba na nyinginezo.
    • Kuwepo kwa silaha haramu mikononi mwa raia.
    • Wachache kuruhusiwa kumiliki bunduki bila kufanyiwa uchunguzi wa sawa.
    • Askari kuzembea kikazi au kukosa kutekeleza majukumu yao kama inavyotarajiwa. ⮚ Kutokuwa na sera faafu kuhusu usalama wa mwanainchi.

      Kupinga 
    • Serikali inafanya msako wa kitaifa kuwasaka na kuwatambua magaidid wanaojificha miongoni mwa wananchi.
    • Serikali ina mpango wa kuwasajili upya wananchi.
    • Serikali imeanzisha mpango wa nyumba kumi.
    • Ukiwa na fadhaa huwasukuma watu kufanya maovu.
    • Kuwapo kwa misimamo mikali ya kidini ambayo baadhi yayo huhimiza mauaji.
    • Vijana kukosa maelekezo faafu kutoka kwa wazazi.
    • Kuvunjika kwa asasi za kijamii ambapo hapana uelekezi kwa wana.
    • Jukumu la ulezi wa wana limeachiwa familia husika badala ya jamii nzima kama ilivyokuwa awali.
    • Mazingira wanamokulia na kulelewa wanajamii (watoto wa mitaani)yanafunza uhalifu.
      ⮚ Kutokuwa na msimamao sawa kuhusu suala zima la usalama miongoni mwa viongozi.

      Tanbihi 
    • Mtahiniwa anaweza kuwa na hoja nyingi za kuunga mkono na moja au zaidi za kupinga.
    • Mtahiniwa anaweza kuwa na hoja nyingi za kupinga na moja au zaidi za kuunga.
    • Mtahiniwa atoe msimamo wake. 
    • Katika hali zote mtahiniwa asiwe na chini ya  hoja nane.
    • Anayekosa kushughulikia pande zote mbili asipite alama 10.
    • Mtahiniwa anaweza kutoa hoja sawa pande zote ilimradi atoe msimamo.
      Hakiki hoja zingine za mtahiniwa. 
  3. Hii ni Insha ya methali 
    • Ina maana kuwa tusipuuze tunapoona kitu fulani kitu fulani kinaanza kwenda vibaya au kuharibika .
    • Tufanye bidii kurekebisha  hali hiyo mapema kabla athari mbaya zaidi haijatokea.
      Mtahiniwa atoe kisa kinachoafiki methali hii. 

      Mfano: 
    • Mwanafunzi anayezembea shuleni na baadaye kufeli mtihani wa kitaifa baada ya kupuuza ushauri.
    • Mzazi anayekosa kurekebisha tabia za mwanawe mwishowe mwanawe  anaathirika zaidi.serikali inayopuuza matatizo ya wananchi mwishowe nchi inaharibika kiuchumi zaidi kutokana na migomo au ukosefu wa usalama.

      Tanbihi:
    • Mtahiniwa azingatie pande mbili za methali
    • Kuwepo kisa kinachosababisha ushauri / hali ya kutaka marekebisho ya haraka yanayopuuzwa na mwishowe athari ijitokeze.
    • Atakayeshughulikia upande mmoja tu asizidi alama 10 (C+)
  4. Andika Insha itakayoanza kwa maneno haya: 
    Baada ya kusafiri mwendo wa kilomita mbili hivi, watu wawili waliokuwa wamefunika nyuso zao kwa barakoa na bunduki mikononi... Hii ni insha ya kiubunifu.  Mtahiniwa abuni kisa ambacho chaangazia mambo kama vile
    • wizi
    • ugaidi
    • utekaji nyara
    • uharamia n.k
    • Mtahiniwa  aonyeshe walichotendewa, walivyokabiliana na tukio hilo, walivyojinasua na hatima ya waathiri  na waathiriwa.
    • Mtahini ahakikishe ukomavu wa lugha ya mtahiriwa na hoja alizotoa.

      UREFU
    • Robo  maneno   1  -  174 asizidi alama 5
    • Nusu   maneno  175 – 274  asizidi alama 10
    • Robo tatu  maneno  275 – 374  asizidi  alama 15
    • Kamili  maneno 375 na zaidi asizidi alama 20 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lugari Constituency Joint Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?