Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Lugari Constituency Joint Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp
 1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
  Boka alijishika tama, akaangalia viambaza vya seli ile. Matumaini yake yakazidi kudidimia. Lililompotezea matumaini zaidi ni vile vikuku vilivyokuwa viwikoni mwa mikono yake. Hiyo ilikuwa ni siku ya kukatwa kwa kesi yake. Alikuwa katika seli ya mahakama chini ya ulinzi mkali. Kwa miaka miwili mtawalia, alikuwa katika rumande. Siku hiyo hakutarajia mageni. Iwapo angebahatika, basi angeepuka na kifungo kirefu au hata cha maisha gerezani. Na iwapo asingebahatika basi, angehukumiwa kula kitanzi kutokana na kosa la wizi wa mabavu. Kwa miezi ishirini na minne, mawakili wake walijaribu juu chini kumtetea bila kufanikiwa. Jaribio lao la kutaka mteja wao aachiliwe kwa dhamana halikadhalika liligonga mwamba. Licha ya kuwa na njenje chungu nzima, alizochuma kwa njia za haramu, alishindwa kuupata uhuru wake.

  Hapo ndipo alipong’amua kuwa pesa si kila kitu. Ingawa pesa huvunja milima na nguu kulala, mara kwa mara, nguu nyingine hughairi pesa. Wazo la kujiona pale kizimbani huku hakimu akitoa hukumu lilimsababishia Boka tumbo la kuendesha. Alinyanyuka polepole hadi pale ndooni. Kwa ugumu mwingi aliweza kwenda haja kisha akarejea pale pale pembeni. Alizivuta nyuma fikra zake na kujuta jinsi alivyopotoka. Kimzaha tu, alianza kuwa kichwa maji pale shuleni. Polepole akawa mtoto asiyelika wala kutafunika. Aliwatesa na kuwachapa maghulamu wa rika lake kiasi cha kupata msimbo ‘Moto’. Alikumbuka jinsi alivyoanza uraibu wa kutumia sigara kimchezo tu kisha akahitimu na kujiunga na chuo cha uvutaji bangi. Nao uvutaji bangi ukampatia msisimko wa ajabu. Mambo yote kwake akayaona ni mboga.

  Akapata ujasiri wa ajabu kiasi cha kuhisi kuwa angepigana na bila shaka amshinde yeyote yule. Hata simba mfalme wa nyika! Machozi yalimdondoka alipokumbuka jinsi elimu yake ilivyokatika. Akakumbuka jinsi kipaji chake katika mchezo wa soka kilivyoangamia. Kiamboni nako wakawa hawasikizani na yeyote. Si wavyele si umbu zake. Shuleni mambo yakawa ni yayo hayo. Mambo yaliwafika walimu kooni alipogeuka na kuwa tisho kwa usalama na maisha ya walimu. Alikumbuka kwa masikitiko tele jinsi alivyojaribu kumdunga kwa kisu mwalimu wake wa Kiswahili. Kisa na maana, maskini mwalimu alipojaribu kufafanua methali “mkataa ya mkuu huona makuu”. Boka alidai mwalimu wake alikuwa akimpiga vijembe. Kwa nyota ya jaha, mwalimu yule aliupata upenu na kusema mguu niponye na kuyaokoa maisha yake.

  Alipotimuliwa shuleni, alielekea mjini. Huko alipatana na wenzake masikio ya kufa. Kwa miaka minne, waliwasumbua wananchi wapenda amani. Walivuna kule ambako hawakupanda wala kupalilia. Kutokana na matendo yao, wakachuma pesa vilivyo na wakaishi maisha ya anasa. Siku za mwizi ni arobaini. Siku moja walifumaniwa wakiiba katika dukakuu moja. Wanne walisalimu amri mbele ya bunduki. Boka alipoona hayo, alibwaga silaha na kujisalimisha.
  Maswali
  1. Tambua mtindo uliotumika katika kifungu hiki.            (alama 3)
  2. Kitendo cha kujishika tama kinaashiria hali ipi ya mhusika?        (alama 10)
  3. Ingawa pesa huvunja mlima na nguu kulala,mara kwa mara nguu nyingine hughairi pesa. Eleza maana ya msemo huu.   
   (alama 2)                                                                                 
  4. Eleza migogoro inayojitokeza katika kifungu hiki.                (alama 4)
  5. Kwa nini mhusika hakutarajia mageni?                     (alama 2)
  6. Eleza maana ya misemo hii kama ilivyotumiwa katika kifungu.         (alama 3)
   1. Akimpiga vijembe.
   2. Yaliwafika kooni.
   3. Akayaona ni mboga.
 2. Ufupisho
  Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Ubongo wa mwanadamu hutekeleza shughuli hii kwa namna tatu. Kwanza, ubongo hunasa jambo kisha hulihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilichohifadhiwa. Ubongo ukiathirika kwa namna yeyote katika mojawapo ya njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika.

  Ingawa inaaminika kuwa uwezo wa kukumbuka hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine, wataalamu wa masuala ya kiakili wanabaini kuwa uwezo huu unaweza kuimarishwa. Uimarishaji huu huhitaji mikakati madhubuti.

  Njia mojawapo ya kustawisha uwezo wa kukumbuka ni kupitia kwa lishe. Vyakula vilivyosheheni vitamini B na amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka. Vyakula kama hivi ni mboga, nyama (hasa maini), bidhaa za soya, matunda, maziwa, bidhaa za ngano, samaki, pamoja na mayai. Vyakula vingine muhimu katika ustawishaji huu ni vile vyenye madini ya chuma. Madini haya huwezesha usambazaji wa hewa katika ubongo kwa wepesi. Vyakula ambavyo vina madini haya ni mboga za kijani, mawele, dengu, soya, matunda kama maembe, ufuta (simsim), pamoja na nyama, hasa maini, na mayai.

  Ubongo wa mwanadamu aliye hai hufanya kazi kila wakati; awe macho au amelala. Utendaji kazi wake huendeshwa na glukosi mwilini. Kwa hivyo, vyakula vyenye sukari ni muhimu kuliwa. Hata hivyo, lazima mtu awe mwangalifu na kuhakikisha kuwa mwili una kiwango cha sukari kisichohatarisha maisha. Haya yanawezekana Kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mboga na matunda.

  Njia ya pili ni kupiga marufuku vileo kama pombe na nikotini. Vileo hivi huathiri utaratibu wa kunasa, kuhifadhi na kutoa yaliyo ubongoni.

  Iwapo mtu ana tatizo la kuyakumbuka majina ya watu, ni muhimu kufanya mazoezi ya kusikiliza kisha kurudia majina hayo wakati wa mazungumzo. Ni bora kulihusisha jina na sura ya mtu. Kwa njia hii ubongo utanasa na kuhusisha jina na kile kinacholengwa.

  Woga na kuvurugika kiakili ni mambo mengine tunayopaswa kuepuka kila wakati. Ni kawaida mtu kupata woga wakati anapokabili jambo asilokuwa na uhakika na matokeo yake kama mtihani au mahojiano. Lakini anapaswa kuwa makini. Woga huo usikiuke mpaka na kumvuruga kiakili. Vurugu hizi huathiri kilichohifadhiwa ubongoni na pia namna ya kukitoa.

  Halikadhalika, mwili wenye siha nzuri huhakikisha kuwa ubongo ni timamu. Wataalamu wengine wa siha wanakubali kuwa mazoezi ya kunyoosha viungo hustawisha ubongo na hivyo huhakikisha kuweko Kwa uwezo wa kukumbuka mambo. Ni muhimu kuwa na ratiba ya kunyoosha viungo kila wakati. Fauka ya hayo, mazoezi ya kiakili, kama vile kusoma makala yanayovutia, kujaza mraba na michezo mingine kama mafumbo, vitanza ndimi na kadhalika ni muhimu katika kustawisha uwezo wa kukumbuka.

  Jamii ya watu wenye uwezo wa kuyakumbuka mambo ni jamii iliyopiga hatua kimaendeleo. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuimarisha uwezo wa kukumbuka kila wakati.
  Maswali
  1. Kwa maneno 60 - 65, fupisha mchango wa chakula katika uimarishaji wa uwezo wa kukumbuka.         (alama 6)         
   Matayarisho
   Nakala safi
  2. Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 80 - 90.               (alama 9)
   Matayarisho
   Nakala safi
 3. Matumizi ya lugha                                                    (Alama 40)
  1. Andika sauti zifuatazo:                   (alama 2)
   1. Mtuo ghuna wa midomo
   2. Kikwamizo sighuna cha meno na ufizi
  2. Bainisha panapotiwa shadda katika neno lifuatalo:       (alama 1)
   Sentensi
  3. Ainisha mofimu katika maneno haya:        (alama 3)
   1. Gari 
   2. Ujumbe
  4. Tolea mifano mitatu ya sentensi kimuundo.       (alama 3) 
  5. Andika katika hali ya udogo. 
   1. Jijiko like lilipakua chakula vizuri.     (alama 2)
   2. Jiti lile linapendeza.           (alama 2)
  6. Badilisha sentensi hii iwe katika umoja.
   Watu watahojiwa tu iwapo watatuma maombi.        (alama 2)
  7. Andika muundo wa sentensi hizi:
   1. Kiatu kilichoraruka sana kitatupwa shimoni kesho.  (alama 2)
   2. Mtoto alijikwaa akaanguka.      (alama 2)
  8. Eleza dhana zinazojitokeza katika sentensi hii.
   Mama ameniletea taa.             (alama 2)
  9. Zingatia maagizo yaliyo mabanoni kuandika upya sentensi hizi:
   1. Mpira mweupe ulitobolewa na mtoto wangu jana. (Anza kwa kiima)        (alama 1)                                                             
   2. Yeye alienda shuleni. ( Tumia kielezi cha kiasi badala ya kile kilichotumiwa)     (alama 2)                                                 
  10. Andika sentensi ifuatayo upya huku ukitumia visawe vya maneno yaliyopigwa mstari.  (alama 3)                                     
   Mama alimwagiza afunge jeraha lililokuwa linatoa damu kwa kitambaa.
  11. Bainisha virai katika sentensi hii kisha uandike miundo yake.     (alama 2)
   Mbuzi wetu ana madoa meusi sana.
  12. Kwa kutolea mifano eleza matumizi mawili ya alama ya nukta na kituo.  (alama 2)                                                             
  13. Badilisha sentensi hii iwe katika usemi wa taarifa.
   "Kwa nini unamrudi mtoto mdogo?" Mzazi aliuliza.           (alama 2)
  14. Tumia misemo ifuatayo katika sentensi ili maana yake ijitokeze:
   1. Alifu kwa kijiti.       (alama 1)
   2. Beba wazazi.            (alama 1)
  15. Tambua matumizi ya kiambishi ‘ka’ katika sentensi hii.
   Dada alikimbia akashinda.            (alama 1)
  16. Andika nomino mbili zinazotokana na vitenzi hivi:       (alama 2)
   1. Funza
   2. Soma
  17. Andika sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali timilifu.
   Askari atamkamata mhalifu.       (alama 2)
 4. Isimujamii                   (Alama 10)
  Matumizi ya lugha yoyote ile hudhibitiwa na mambo fulani. Fafanua mambo haya.

                                                                                  MWELEKEZO WA KUSAHIHISHA

 1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
  Boka alijishika tama, akaangalia viambaza vya seli ile. Matumaini yake yakazidi kudidimia. Lililompotezea matumaini zaidi ni vile vikuku vilivyokuwa viwikoni mwa mikono yake. Hiyo ilikuwa ni siku ya kukatwa kwa kesi yake. Alikuwa katika seli ya mahakama chini ya ulinzi mkali. Kwa miaka miwili mtawalia, alikuwa katika rumande. Siku hiyo hakutarajia mageni. Iwapo angebahatika, basi angeepuka na kifungo kirefu au hata cha maisha gerezani. Na iwapo asingebahatika basi, angehukumiwa kula kitanzi kutokana na kosa la wizi wa mabavu. Kwa miezi ishirini na minne, mawakili wake walijaribu juu chini kumtetea bila kufanikiwa. Jaribio lao la kutaka mteja wao aachiliwe kwa dhamana halikadhalika liligonga mwamba. Licha ya kuwa na njenje chungu nzima, alizochuma kwa njia za haramu, alishindwa kuupata uhuru wake.

  Hapo ndipo alipong’amua kuwa pesa si kila kitu. Ingawa pesa huvunja milima na nguu kulala, mara kwa mara, nguu nyingine hughairi pesa. Wazo la kujiona pale kizimbani huku hakimu akitoa hukumu lilimsababishia Boka tumbo la kuendesha. Alinyanyuka polepole hadi pale ndooni. Kwa ugumu mwingi aliweza kwenda haja kisha akarejea pale pale pembeni. Alizivuta nyuma fikra zake na kujuta jinsi alivyopotoka. Kimzaha tu, alianza kuwa kichwa maji pale shuleni. Polepole akawa mtoto asiyelika wala kutafunika. Aliwatesa na kuwachapa maghulamu wa rika lake kiasi cha kupata msimbo ‘Moto’. Alikumbuka jinsi alivyoanza uraibu wa kutumia sigara kimchezo tu kisha akahitimu na kujiunga na chuo cha uvutaji bangi. Nao uvutaji bangi ukampatia msisimko wa ajabu. Mambo yote kwake akayaona ni mboga.

  Akapata ujasiri wa ajabu kiasi cha kuhisi kuwa angepigana na bila shaka amshinde yeyote yule. Hata simba mfalme wa nyika! Machozi yalimdondoka alipokumbuka jinsi elimu yake ilivyokatika. Akakumbuka jinsi kipaji chake katika mchezo wa soka kilivyoangamia. Kiamboni nako wakawa hawasikizani na yeyote. Si wavyele si umbu zake. Shuleni mambo yakawa ni yayo hayo. Mambo yaliwafika walimu kooni alipogeuka na kuwa tisho kwa usalama na maisha ya walimu. Alikumbuka kwa masikitiko tele jinsi alivyojaribu kumdunga kwa kisu mwalimu wake wa Kiswahili. Kisa na maana, maskini mwalimu alipojaribu kufafanua methali “mkataa ya mkuu huona makuu”. Boka alidai mwalimu wake alikuwa akimpiga vijembe. Kwa nyota ya jaha, mwalimu yule aliupata upenu na kusema mguu niponye na kuyaokoa maisha yake.

  Alipotimuliwa shuleni, alielekea mjini. Huko alipatana na wenzake masikio ya kufa. Kwa miaka minne, waliwasumbua wananchi wapenda amani. Walivuna kule ambako hawakupanda wala kupalilia. Kutokana na matendo yao, wakachuma pesa vilivyo na wakaishi maisha ya anasa. Siku za mwizi ni arobaini. Siku moja walifumaniwa wakiiba katika dukakuu moja. Wanne walisalimu amri mbele ya bunduki. Boka alipoona hayo, alibwaga silaha na kujisalimisha.
  Maswali
  1. Tambua mtindo uliotumika katika kifungu hiki.            (alama 3)
   • Methali - mkataa ya mkuu huona makuu
   • Lakabu - 'moto'
   • Tabaini - Si umbu zake, si wavyele
   • Msemo - mguu niponye
  2. Kitendo cha kujishika tama kinaashiria hali ipi ya mhusika?        (alama 10)
   • Hali ya majuto
  3. Ingawa pesa huvunja mlima na nguu kulala,mara kwa mara nguu nyingine hughairi pesa. Eleza maana ya msemo huu. 
   (alama 2)  
   • Pesa alizokuwa nazo Boka hazingwezea kumtoa kwenye rumande                                                                        
  4. Eleza migogoro inayojitokeza katika kifungu hiki.                (alama 4)
   • Mgogoro kati ya Boka na mwalimu wake wa Kiswahili alipotaka kumdunga mwalimu kisu
   • Mgogoro kati ya Boka na wanafunzi wenzake
   • Mgogoro kati ya Boka na wavyele wake
   • Mgogoro kati ya Boka na umbu zake
  5. Kwa nini mhusika hakutarajia mageni?              (alama 2)
   • Kwa sababu alikua amekaa kwenye rumande kwa miezi ishirini na minne na mawakili wake walikuwa wamejaribu juu chini kumtoa bila kufanikiwa
  6. Eleza maana ya misemo hii kama ilivyotumiwa katika kifungu.         (alama 3)
   1. Akimpiga vijembe.
    • Akisema kwa kutumia fumbo
   2. Yaliwafika kooni.
    • Yaliwachosha
   3. Akayaona ni mboga.
    • Akayaona ni rahisi
 2. Ufupisho
  Uwezo wa kuyakumbuka mambo ni hazina kuu kwa mtu yeyote yule aliye hai. Uwezo huu wa kukumbuka ni mojawapo ya shughuli changamano za ubongo. Ubongo wa mwanadamu hutekeleza shughuli hii kwa namna tatu. Kwanza, ubongo hunasa jambo kisha hulihifadhi. Baadaye huanzisha mfumo wa kutoa kilichohifadhiwa. Ubongo ukiathirika kwa namna yeyote katika mojawapo ya njia hizi, basi uwezo wa kuyakumbuka mambo huvurugika.
  1. Matayarisho
   • Vyakula viliyosheheni vitamini B na amino asidi husaidia kuimarisha uwezo wa kukumbuka
   • Vyakula vyenye madini ya chuma huwezesha usambazaji wa hewa kwa urahisi katika ubongo
   • Vyakula vyenye glukosi husaidia kuendesha vyungo vya mwili na ubongo
   • Vyakula vyenye nyuzi nyuzikama mboga na matunda husaidia kuhakikisha kiwango cha sukari kiko sawa
   • Kutumia vileo na vyakula vyenye nikotini kwani huzorotesha uwezo wa kukumbuka
  2. Fupisha aya tatu za mwisho kwa maneno 80 - 90
   Matayarisho
   • Ni muhimu kuepuka woga na kuvurugika akili kulikozidi
   • Haya huathiri uwezo wa kukumbuka
   • Lazima mtu awe na ratiba ya kunyoosha viungo
   • Unyoshaji wa viungo huimarisha ubongo pamoja na uwezo wa kukumbuka
   • Haya yaandamane na michezo ya kiakili ambayo huchangia uimarishaji wa uwezo huu
   • Uimarishaji wa uwezo huu ni muhimu kwa maendeleo ya jamii
   • Unahitaji mchango wa kila mmoja, kila wakati                     (Utiririko alama 3) 
 3. Matumizi ya lugha            (Alama 40)
  1. Andika sauti zifuatazo:                   (alama 2)
   1. Mtuo ghuna wa midomo
    • /b/
   2. Kikwamizo sighuna cha meno na ufizi
    • /th/ 
     1. Bainisha panapotiwa shadda katika neno lifuatalo:       (alama 1)
      Sentensi
     2. Ainisha mofimu katika maneno haya:        (alama 3)
      1. Gari 
      2. Ujumbe
     3. Tolea mifano mitatu ya sentensi kimuundo.       (alama 3) 
     4. Andika katika hali ya udogo. 
      1. Jijiko like lilipakua chakula vizuri.     (alama 2)
      2. Jiti lile linapendeza.           (alama 2)
     5. Badilisha sentensi hii iwe katika umoja.
      Watu watahojiwa tu iwapo watatuma maombi.        (alama 2)
     6. Andika muundo wa sentensi hizi:
      1. Kiatu kilichoraruka sana kitatupwa shimoni kesho.  (alama 2)
      2. Mtoto alijikwaa akaanguka.      (alama 2)
     7. Eleza dhana zinazojitokeza katika sentensi hii.
      Mama ameniletea taa.             (alama 2)
     8. Zingatia maagizo yaliyo mabanoni kuandika upya sentensi hizi:
      1. Mpira mweupe ulitobolewa na mtoto wangu jana. (Anza kwa kiima)        (alama 1)                                                             
      2. Yeye alienda shuleni. ( Tumia kielezi cha kiasi badala ya kile kilichotumiwa)     (alama 2)                                                 
     9. Andika sentensi ifuatayo upya huku ukitumia visawe vya maneno yaliyopigwa mstari.  (alama 3)                                     
      Mama alimwagiza afunge jeraha lililokuwa linatoa damu kwa kitambaa.
     10. Bainisha virai katika sentensi hii kisha uandike miundo yake.     (alama 2)
      Mbuzi wetu ana madoa meusi sana.
     11. Kwa kutolea mifano eleza matumizi mawili ya alama ya nukta na kituo.  (alama 2)                                                             
     12. Badilisha sentensi hii iwe katika usemi wa taarifa.
      "Kwa nini unamrudi mtoto mdogo?" Mzazi aliuliza.           (alama 2)
     13. Tumia misemo ifuatayo katika sentensi ili maana yake ijitokeze:
      1. Alifu kwa kijiti.       (alama 1)
      2. Beba wazazi.            (alama 1)
     14. Tambua matumizi ya kiambishi ‘ka’ katika sentensi hii.
      Dada alikimbia akashinda.            (alama 1)
     15. Andika nomino mbili zinazotokana na vitenzi hivi:       (alama 2)
      1. Funza
      2. Soma
     16. Andika sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali timilifu.
      Askari atamkamata mhalifu.       (alama 2)
 4. ISIMUJAMI
  • Wahusika na uhusiano wao
  • Hali ya wahusika
  • Mada zinazozungumziwa
  • Madhumuni ya mawasiliano/mazungumzo
  • Jinsia ya wahusika wa mazungumzo
  • Umri wa wahusika
  • Muktadha wa matumizi au mazungumzo
  • Lugha azijuazo mzungumzaji
  • Vyeo vya wahusika katika mazungumzo
  • Tabaka/nafasi ya kijamii ya wahusika katika mazungumzo
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Lugari Constituency Joint Pre Mock Exams 2023.

Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?