Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lainaku 1 Joint PreMock Exams 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

 • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima
 • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya tatu zilizobakia
 • Kila insha isipungue maneno 400
 • Kila insha ina alama 20
 • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
 • Watahiniwa wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
 1. Lazima
  Umepata tangazo la nafasi ya kazi ya ualimu katika shule moja maarufu nchini kwenye gazeti la Pambazuko. Andika barua ya kuomba nafasi hii na uiambatanishe na wasifukazi wako.
 2. Wanafunzi wa shule za kutwa wanakabiliwa na changamato nyingi katika juhudi zao za kupata elimu wakilinganishwa na wa shule za bweni. Jadili.
 3. Tunga kisa chenye kudhihirisha ukweli wa methali; Mchumia juani hulia kivulini.
 4. Andika kisa kitakachokamilika kwa maneno haya;
  … tulifumukana huku nyuso zetu zikiwa na tabasamu la matumaini ya kuneemeka kwa maisha yetu ya baadaye.

                                                              MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA

 1. Insha ya Lazima
  Ni insha ya barua rasmi
  Sura
  1. Muundo wa barua rasmi uzingatiwe
   1. Anwani mbili; ya mwandishi na ya mwandikiwa.
   2. Tarehe iandikwe chini ya anwani ya kwanza.
   3. Maamkizi; Bwana/Bi.
   4. Mada /kichwa
    Mwili wa barua
    1. Utangulizi- Aeleze kwa kifupi alipolisoma au kuliona tangazo
    2. Mwili- ufaafu wake katika hiyo nafasi.
    3. Hitimisho
     • Ataje kuwa ameambatanisha barua yake na wasifukazi.
     • Taratibu za kutamatisha barua zidhihirike kv. Wako mwaminifu, sahihi na jina lake
      Wasifukazi / Tawasifu kazi / wasifutaala
      1. Habari za kibinafsi
       • Jina
       • Jinsia / uana
       • Umri / Tarehe ya kuzaliwa
       • Hadhi katika ndoa
       • Anwani – barua pepe/nambari ya simu
       • Dini
       • Lugha azijuazo
      2. Elimu
       • Orodha ya shule alizohudhuria masomo – aanze kwa kiwango cha juu zaidi kwenda chini.
       • Abainishe kipindi cha masomo kwa kuandika miaka kv. 1974 – 1980.
       • Ataje cheti alichohitimu katika kila daraja ya masomo yake.
      3. Tajriba – ujuzi wa kikazi/maarifa.
      4. Ufanisi – Aeleze ufanisi wake – popote alipokuwa akifanya kazi hii anayoitafuta.
      5. Uraibu – Aorodheshe mambo anayopenda kufanya nje ya mazingira ya kazi rasmi.
      6. Wadhamini / warejelewa wawili au zaidi
       • Jina la mdhamini.
       • Vyeo / cheo chake.
       • Anwani.
       • Nambari ya simu.
       • Barua pepe.
        Tanbihi: Ni insha moja iliyo na vipengele viwili vikuu;
       • Sehemu ya barua rasmi.
       • Tawasifukazi / wasifukazi
        Kadiria kazi ya mwanafunzi ipasavyo ukizingatia muundo na maudhui.
  2. Ni insha ya mjadala wa kuunga au kupinga.
   Hoja za kuunga
   • Kusafiri safari ndefu za kuelekea shuleni asubuhi na nyumbani jioni.
   • Kukosa wakati wa kutosha kufundishwa saa za ziada.
   • Kukubwa na changamoto za kifamilia nyumbani.
   • Uwepo wa kuingizwa kwa matumizi ya mihadarati.
   • Wasichana kutungwa mimba na baadaye kuingizwa katika ndoa za mapema.
   • Makini yao kutekwa na vyombo vya kitekinolojia kama vile runinga na rununu, hivyo kukosa wakati murwa wa kudurusu.
   • Kupewa majukumu mengi nyumbani baada ya kutoka shule.
   • Athari za hali ya anga kv. Kunyeshewa na kutembea kwenye matope.
   • Uchovu wa kutembea masafa marefu; kwenda shule na kurudi nyumbani.
   • Kukosa kawi kama mafuta taa ama umeme kwao nyumbani – hivyo hawawezi kusoma jioni au usiku.
   • Wengine kulazimika kufanya ajira ya watoto wakiwa nyumbani.

    Hoja za kupinga
   • Hutangamana na wazazi kila siku – hivyo hawawezi kupotoka kwa urahisi.
   • Wanakula vyakula wavipendavyo nyumbani wakilinganishwa na wenzao katika shule za bweni.
   • Uhuru wa kusoma wakati wowote wakiwa nyumbani.
   • Si rahisi kuathirika na shinikizo la rika kama wenzao katika mabweni.
   • Wana nafasi ya kusaidia wazazi nyumbani; hivyo huwajibika.
   • Gharama ya masomo katika shule za kutwa si kubwa kama ya shule za bweni.
    Tanbihi: kadiria hoja nyingine sahihi.
  3. Ni insha ya methali
   Atunge kisa chenye kudhihirisha maana na matumizi ya methali husika.
   Pande zote mbili za methali zibainike
   • Kuchumia juani
   • Kulia kivulini
    Atakayeshughulikia upande mmoja tu, maki zake zisizidi (C+ 10)
  4. Insha ya mdokezo tamatishi
   • Aandike kisa chenye kuafiki mwisho aliopewa.
   • Utungo wake ukamilike kwa maneno aliyopewa.
   • Kisa kijikite katika nafsi ya kwanza wingi.
   • Asipotamatisha kwa maneno aliyopewa lichukuliwe kuwa kosa la kimtindo tu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Lainaku 1 Joint PreMock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?