Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Term 3 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp
SEHEMU YA  A:  INSHA    (ALAMA   20)
Tunga kisha kitakachomalizika kwa maneno yafuatayo:
………………….Aliyekuwa tajiri wa kutajika amegeuka kuwa maskini hohehahe. Ni kweli kuwa aliye juu mngoje chini.


SEHEMU YA B: UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma makala haya kisha ujibu maswali yanayofuata.
Kingi alizaliwa Vuruni, kijiji kilichosifika kwa ukarimu wa wanakijiji wake. Ingawa walikuwa karimu, Wavuruni wengi walikosa elimu. Fauka ya hayo, walining’inia katika umaskini uliokithiri. Hivyo, wengi waliselea katika kazi ya kijungu jiko. Watoto wa umri wa kwenda shule walikosa elimu na kuzurura mitaani. Udhaifu huu ulimpa faida Mwakisu, tajiri mmoja aliyemiliki shamba kubwa. Aliwaajiri watoto hao.

Mwakisu alikuwa mkwasi aliyetononoka si haba. Kama ni senti, alikuwa nazo. Kilichotia doa jina lake ni kiburi. Mbali na kiburi hicho, yeye hakujaliwa moyo wa huruma na utu. Hakubarikiwa kuwa mwema. Maadili hutuongoza kila mara kuwa “wema hauozi”.

Kwa Mwakisu, wema ulioza na kuvunda. Utu uling’oka katika bawaba za moyo wake na ukawa msamiati aliochukia. Aliwatumikisha watoto wa wenzake huku wake wakisoma shule. Tabia yake hiyo ndio iliowafanya Wavuruni kumtoa orodha ya watu wema.

Mwakisu alistaajabisha! Hakutaka kununua mashine zozote za kufanya kazi shambani ingawa alikuwa na uwezo. Alistahabu kuajiri watoto wadogo na kuwadhulumu. Mkwasi huyu alifurahia kuona vitoto vikimenyana na kazi shambani kwake tangu mawio hadi machweo na hatimaye kuwapa ujira mdogo.

Siku moja Kingi alimtaka radhi, “Bosi naomba uniongezee chochote, kwani tuna shida nyumbani.” Mwakisu alimkodolea macho huku mdomo ukimcheza. Hapo alimchomolea mwajiriwa wake tusi kubwa kutoka kwenye hazina yake isiyopungua. Tusi ambalo lilimtaabisha Kingi kuisahau. Lilikaririrwa akilini mwake kwa sonono. Tangu siku hiyo Kingi akaona kuwa kuajiriwa na Mwakisu ni kufadhiliwa, na uso wa kufadhiliwa u chini.

Kiburi cha Mwakisu kilidhihirika kila mara. Kila alipomwona mtoto akilia kwa uchovu au maumivu, ungemsikia akimfokea, “chapa kazi! Unalilia nani hapa? Kama humudu kazi rudi kwa mamako ukanyonye.”

Kazi nyingi  zilikuwa ngumu na hazikuwastahili watoto wenye umri mdogo. Si kipupwe, si kaskazi, si vuli, si kiangazi, si kusi; kazi ziliongezeka na kuwaumiza watoto . Kingi , kwa mfano , alitakikana akame ng’ombe kumi na abebe maziwa hadi kwenye tangi kubwa. Kisha angewakatia ng’ombe nyasi na kuwasafisha. Hatimaye angehitajika kuzoa samadi.

Msimu wa kipupwe uliwadia. Baridi ikawatafuna watoto hao waliokosa mavazi bora.Kingi aliugua. Watoto wengi wakapatwa na maradhi. Wawili wakaaga dunia. Wazazi walipoona maisha ya watoto wao yamo hatarini, wakaandamana hadi kwa chifu. Chifu alipoyaona yamempita kimo, akafululiza hadi kituo cha polisi. Mwakisu akakamatwa, akashtakiwa na kuhukumiwa. Alipatikana na makosa ya kuwaajiri watoto wenye umri mdogo na kusababisha vifo vya wawili wao.

Serikali ikatoa amri kwa wazazi kupeleka watoto wao shuleni. Ikatoa pia misaada ya kuendeleza elimu; elimu ya bure kwa shule za msingi. Kingi akasoma hadi kuhitimu chuo kikuu. Akawa daktari.

Alfajiri moja mahabusu waliletwa hospitali kuu ya mkoa kwa matibabu. Kingi akampa huduma mzee aliyejawa mvi na kukoboka meno. Alipomtazama kwa makini akamkumbuka.

Mwakisu akabahatisha, “sura yako… ni kama ya Kingi…” Kingi akamjibu, “Mimi ndiye Kingi.” Wakakodoleana macho, huku machozi yakimtiririka Mwakisu.
 
MASWALI
  1. Pendekeza anwani mwafaka ya makala uliyosoma. (Alama 2)
  2. Wanakijiji wa Vuruni walikumbwa na shida zipi. ( Alama 2)
  3. Taja sifa mbili za Mwakisu kulingana na ufahamu. (Alama 2)
  4. Kingi alitakikana kufanya kazi zipi? Zitaje. (Alama 3)
  5. Ni majanga yapi yaliwapata watoto walioajiriwa na Mwakisu  wakati wa kipupwe. (Alama 2)
  6. Serikali ilisaidia jinsi gani baada ya Mwakisu kukamatwa, kushikwa na kuhukumiwa.    (Alama 2)
  7. Eleza maana ya msamiati ufwatao kuligana na kifungu ulichosoma. (Alama 2)
    1. Mkwasi.
    2. Kipupwe

SEHEMU YA C: SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA 

  1. Tofautisha sauti zifuatazo (alama 2)
    1. /p/   na /b/
    2. /l/    na   / r/
  2. Eleza tofauti kuu kati ya irabu na konsonanati (alama2)
  3. Ainisha sentensi ifuatayo kwa kutumia kielelezo cha mstari
    Wale werevu walituzwa zawadi (alama 2)
  4. Nomino zifuatazo zimo katika ngeli gani?
    1. teo
    2. kijakazi (alama2)
  5. Andika sentensi ifuatayo kwa ukubwa
    Miji hii ni mikubwa sana (alama2)
  6. Akifisha
    mtume dereva huyu atatuangusha (alama2)
  7. Taja vipashio vinne vya lugha (alama 4)
  8. Andika sentensi zifuatazo katika nyakati au hali katika mabano
    Mama anawapikia chakula kizuri (hali timilifu)
    Kitabu chake kitasomwa na shangazi (wakati uliopita) (alama2)
  9. Andika kwa wingi
    Ndizi hili limenunuliwa leo (alama2)
  10. Weka shadda katika maneneo yafuatayo ili kubainisha maana inayokusudiwa.
    1. barabara (shwari/sawa)
    2. ala (kihisishi) (alama2)
  11. Kanusha sentensi zifuatazo
    1. Mbwa amemuuma mtoto
    2. Musa alimnunulia babake gari (alama2)
  12. Onyesha kiambishi awali na tamati katika kitenzi:
    Aliyesomea (alama2)
  13. Onyesha vielezi katika sentensi zifuatazo
    1. Wanafunzi walimkaribisha mgeni jana
    2. Werevu sana watatunukiwa (alama2)
  14. Onyesha silabi katika neno lifuatalo
    Muktadha   (alama3)
  15. Onyesha miundo miwili inajitokeza katika ngeli ya U-ZI (alama2)
  16. Sahihisha sentensi ifuatayo kwa njia tatu
    Hapo mlimo kuna siafu (alama2)
  17. Eleza matumizi ya kiakifishi kifuatacho
    Kibainishi (alama2)
  18. Tunga sentensi ili kubainisha maana  ya vitate:
    Vua
    Fua     (alama2)
  19. Mwandani ni kwa________________________ ilhali kidosho ni kwa kipusa  (alama1)

SEHEMU YA D: ISIMU JAMII (ALAMA 10)

Soma  makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.

MHUSIKA  A: Tano kwa mia! Tano kwa mia! Leo ni leo na bei ni ya kufunga kazi

MHUSIKA  B: Utauza hii shirt kwa pesa ngapi?

MHUSIKA  A: Hiyo ni eighty bob mtu wangu.

MHUSIKA  B: Nipunguzie kidogo mtu wangu. Nina shilingi sitini pekee yake.

MHUSIKA  A: Ongeza kidogo tafadhali unataka nipate hasara. 

                       Hii shati ni ya thamani kubwa, imetoka Ujerumani

Maswali

  1.  
    1. Tambua sajili kutokana na makala uliyosoma (alama 2)
    2. Eleza sifa sita za sajili uliyotambua hapo juu (alama 6)
  2. Taja kaida mbili au masharti ya matumizi ya lugha (alama 2)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI (ALAMA 15)

  1.  
    1. Fasihi simulizi ni nini? (alama2)
    2. Eleza dhima ya fasihi simulizi (alama2)
  2. Fafanua aina zifuatazo za hadithi
    1. Hekaya
    2. Hurafa (alama 4)
  3. Ni kwa jinsi gani hadhira inaweza kushirikishwa katika fasihi simulizi (alama2)
  4. Taja vipera vyovyote vitatu vya semi. (alama 2)
  5. Eleza maana ya istilahi zifuatazo za fasihi
    1. Fanani
    2. Mandhari
    3. Hadhira (alama 3)

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SEHEMU YA  A: INSHA    ALAMA (20)

Hii ni insha ya mdokezo. Mtahiniwa aweze kutunga kisa kinachooana na mdokezo huo. Kisa kionyeshe mhusika ambaye alikuwa tajiri au mwenye mamlaka lakini baadaye akauuliwa mamlaka au akafilisika na kuwa maskini.

Mtahiniwa akikosa kuandika mdokezo atakuwa amepungukiwa kimtindo.

Mtahiniwa akitunga kisa kisichooana na mdokezo atakuwa amepotoka kimaudhui.

SEHEMU YA B: UFAHAMU ALAMA (15)

  1. Ajira ya watoto.  (alama 2)
  2. Ukosefu wa elimu.
    Umaskini.
    Kuselea katika kazi za kijungujiko. 
     (alama 2)
  3. Tajiri.
    Mwenye kiburi.
    Mwenye dhuluma .
    Mwenye matusi. 
     (alama 2)
  4. Kukama ng’ombe.
    Kubeba maziwa hadi kwenye tangi kubwa.
    Kukatia ngombe nyasi na kuwasafisha .
    Kuzoa samadi. 
      (alama 3)
  5. Kingi aliugua.
    Watoto wengi walipatwa na maradhi.
    Watoto wawili waliaga dunia.
         (alama 2)
  6. Serikali ilitoa amri kuwa watoto wote wapelekwe shuleni.
    Ilitoa msaada wa kuendeleza elimu.
        (alama2)
  7. Mkwasi – tajiri.
    Kipupwe – msimu wa baridi.
          (alama2)

SEHEMU YA C: SEHEMU YA MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1. /p/ ni sauti sighuna lakini /b/ ni sauti ghuna.
    /l/  ni kitambaza lakini  /r/ ni kimadende. 
             (alama 2)
  2. Irabu hutamkwa kwa ulaini lakini wakati wa kutamka konsonanti hewa hubanwa kwenye ala mbalimbali za utamkaji. (alama 2)
  3. KN (W + V) + KT (T + N). (alama 2)
  4. teo U-ZI
    kijakazi A-WA
      (alama 2)
  5. Majiji haya ni makubwa sana.  (alama 2)
  6. Mtume! Dereva huyu atatuangusha.  (alama 2)
  7.  
    • Sauti.
    • Silabi.
    • Neno.
    • Sentensi.   (alama 4)
  8. Mama amewapikia chakula vizuri.
    Kitabu chake kilisomwa na shangaz
    i.  (alama 2)
  9. Ndizi hizi zimenunuliwa leo.  (alama 2)
  10. Ba’rabara (shwari/ sawa)
    a’la (kihisishi)
    (alama 2)
  11. Mbwa hajamuuma mtoto.
    Musa hakumnunulia babake gari
    . (alama 2)
  12. a
    li   -nViambishi awali
    ye
    som- mzizi
    e
    a - viambishi tamati
  13. Jana
    Sana 
        (alama 2)
  14. Muk-ta-dha    (alama 2)
  15. Uzi- nyuzi u-ny
    Ulimi-ndimi u-nd
    Ukuta-kuta u-0
       (alama 2)
  16. Hapo ndipo pana siafu.
    Huku mliko kuna siafu.
    Humu mlimo mna siafu.
         (alama 3)
  17. Katika maneno ya ving’ong’o
              Ng’ombe
              Ng’ ata
    Katika ushairi kupunguza idadi ya mizani.
    Kuonyesha tawakimu zilizoachwa.
  18. Vua- kutoa nguo
            kushika samaki

    Fua- kuosha nguo      (alama 2)
  19. Rafiki/ muhiba   (alama 1)

SEHEMU YA D: ISIMU JAMII (ALAMA 10)

  1.  
    1. Sajili ya sokoni/ biashara (alama 2)
    2.  
      1. Matumizi ya msamiati wa kibiashara
      2. Hutumia misimu ili kuwavutia wanunuzi
      3. Ni lugha lengevu
      4. Huchanganya ndimi
      5. Ni lugha yenye heshima na unyenyekevu
      6. Ni lugha yenye malumbano      (alama 6)
  2.  
    1. Muktadha/ mazingira
    2. Umri
    3. Madhumuni
    4. Jinsia
    5. Mada
    6. Lugha ajuazo mtu
    7. Hali
    8. Utabaka   (alama 2)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI (ALAMA 15)

  1.  
    1. Fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo huwasilishwa kwa njia ya mdomo
    2.  
      1. Huburudisha, huliwaza na kufurahisha.
      2. Huhifadhi historia
      3. Ni nguzo ya kuunganisha watu na kuleta utangamano
      4. Hukuza lugha
      5. Hukuza ubunifu
      6. Huadilisha
      7. Huhifadhi utamaduni wa jamii
      8. Huelekeza jamii (alama 5)
  2.  
    1. Hekaya
      • Ngano zinazohusisha mhusika mjanja ambaye anatumia hila na undanganyifu ili kujinusuru au kujifaidi
    2. Hurafa
      • Hadithi za wahusika wanyama pekee ambao wanawakilisha binadamu. (alama 2)
  3.  
    1. Kuulizwa maswali
    2. Kupiga makofi
    3. Kuambiwa waimbe wimbo                   (alama 2)
  4. Vipera vya semi
    • Methali
    • Vitendawili
    • Misemo
    • Misimu
    • Lakabu
    • Mafumbo
    • Chemshabongo                  (alama 2)
  5.  
    • Fanani – Ni yule anayetunga na kuwasilisha utungo wa fasihi simulizi.    (alama 3)
    • Mandhari – ni mazingira , ni mahali,hali na wakati ambapo Sanaa ya fasihi simulizi hutendwa.
    • Hadhira – ni watazamaji au wasikilizaji wa kazi ya fasihi.
 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Term 3 Opener Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest