Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 1 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp
MAAGIZO:
  • JIBU MASWALI YOTE
INSHA (ALAMA 20) 
Andika kisa kitakachoonyesha ukweli wa methali hii:  Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. 
 
UFAHAMU  ALAMA 10

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Mwanadamu, ingawa kawaida huumbwa akiwa na afya bora wakati mwingine haiwi hivyo.  Huenda akakumbwa na magonjwa aina mbalimbali; mengine madogo madogo na mengine makubwa.  Magonjwa yale madogo madogo hayampi mtu wasiwasi mwingi bali akijua kuwa na magonjwa ya kumfisha hupotelewa na raha kabisa, hushikwa na simanzi, hata anaweza akafa kabla ya siku zake kutimia.

Magonjwa madogo madogo (mepesi) ni kama mafua na kuumwa na kichwa, ilhali magonjwa makubwa ni kama ukimwi, kipindunpindu na kifua kikuu.

Mtu akishikwa na maradhi hupotelewa na hamu ya chakula, wengine wakikiona tu huona kichefuchefu na kutapika.  Maradhi husononesha na kumfanya mtu akonde mithili ya ng’onda.  Wagonjwa wengine hushikwa na woga hasa wakijua kuwa watakata Kamba, wengine kati ya hawa huponda mali yote waliyonayo kabla ya kuishiwa wa nguvu kabisa.  Wale ambao hupata nafuu humshukuru Mungu kwa kuwanusuru katika janga hilo kwani labda waliponea tundu la sindano.

Kila auguaye hushauriwa kwenda hospitali lakiini kuna wengine ambao hata wakishauriwa kufanya hivyo hukataa katakata na mwisho hujihasiri.  Watu wengi wakiwa na maradhi hatari kama ukimwi, tauni, ukoma, na kipindupindu hukimbiwa na marafiki.  Marafiki hao huwa hawataki kuambukizwa.  Baadhi ya wagonjwa hawa wakitengwa namna hiyo hutamani kujitia kitanzi.

Uchafu ni njia mojawapo kubwa inayowapatia watu magonjwa kama kichocho, kuhara damu, kipindupindu na hata minyoo wanaoweza kuwasumbua na kuleta safura.  Inapasa kula chakula safi na kuwa nadhifu ili kujiepushe na shida kama hizo.

Magonjwa mengine hupatikana wakati mtu anapong’atwa na wadudu kama vile mbung’o ambao husababisha ugojwa na malale.  Malaria husabibishwa na mbu.  Hata kuna aina Fulani ya mbu wasabibishao ugonjwa wa matende.

Magonjwa kama surua, kifaduro na ugonjwa wa kupooza huwapata watoto na kuwaacha na matatizo chungu nzima, hasa wakikosa matibabu mapema.  Kwa mfano, wakipooza miguu wanaweza kuwa viwete.

Magonjwa kama utapia mlo, kisunzi, ukosefu wa damu, upele, kuparara na kubambuka ngozi mwilini husababishwa na ukosefu wa chakula.

Maradhi husababisha uzoroteshaji wa maendeleo.  Mgonjwa hawezi kuzalisha mali kwa kuwa atakuwa hana nguvu ya kufanya kazi.  Isitoshe, watu wengine watakuwa wakimshughulikia na kazi zao hazitafanyika.  Mara nyingi fedha nyingi hutumika kwa kumtibu mgonjwa huyo.

Juhudi zinafanywa juu chini ili kuamgamiza magonjwa yanayomaliza watu.  Madawa chungu nzima yamegunduliwa na hospitali na zahanati zimejengwa kila sehemu ili wagonjwa watibiwe.  Hata hivyo, juhudi hizi hazitoshi.

Walimwengu wataweza tu kujiona kuwa wana maendeleo kama watafaulu kuzivumbua dawa za kukomesha magonjwa yote yanayowasumbua.  Wanatakiwa wasikate tamaa kwani huenda siku moja watafanikiwa.  Yapasa waelewe kuwa palipo na nia hapakosi njia.

Maswali
  1. Andika kichwa kinachofaa kueleza habari hii. (al. 1)
  2. Taja aina tatu za magonjwa yaliyogusiwa katika kifungu hiki.            (al. 3)
  3. Maradhi husababisha hasara gani?             (al. 3)
  4. Taja njia tatu ambazo kwazo mtu anaweza kushikwa na maradhi.            (al. 3)
  5. Andika maana ya neno hili kama lilivyotumika katika taarifa hii.            (al. 1)
    1. Akakumbwa

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA               (ALAMA 20)

  1. Tofautisha kati ya sauti hizi:
    1. /m/ na /th/    (alama 1) 
    2. /o/ na /u/    (alama 1)
  2. Tenga silabi kwenye neno hili : muhtasari                                                                                 (alama 1)
  3. Onyesha majukumu mawili ya kiimbo kisha utolee mifano.                                                   (alama 2)
  4. Akifisha sentensi ifuatayo:                                                                                                             (alama 3)                      timothy  alienda shuleni tarehe 22 10 2021 akasoma kiswahili kingereza  na hesabu
  5. Onyesha miundo yoyote miwili ya ngeli ya A-WA kisha utolee mifano.                             (alama 2) 
  6. Tambua aina za maneno kwenye sentensi hii.                                                                     (alama 2)     
    Huyu mdogo alienda shuleni.
  7. Onyesha viambishi awali , mzizi na viambishi tamati kwenye neno hili: alipikiwa   (alama 2)
  8. Nyambua vitenzi hivi kwenye kauli zilizowekwa kwenye mabano.               
    1. Kimbia (tendesha)   (alama 1)  _______________________________________________________________________________
    2. tembea (tendeana)  (alama 1) _________________________________________________________________________________
  9. Eleza maana ya sentensi. (alama 1)
  10. Taja aina zozote mbili za sentensi. (alama 1)
  11. Tambua Kundi Nomino na Kundi tenzi katika sentensi ifuatayo:    (alama 2)
    Mwanafunzi huyu mfupi atapewa zawadi kesho.

FASIHI SIMULIZI   (ALAMA 10)

  1. Eleza maana ya fasihi. (alama 1)
  2. Taja tanzu mbili kuu za fasihi. (alama 1) 
  3. Andika tofauti zozote tano za tanzu ulizotaja hapo juu. (alama 5)
  4. Taja umuhimu wa fasihi kwa jamii. (alama 3)

ISIMUJAMII    (ALAMA 10)

  1. Eleza maana ya istilahi zifuatazo:                                                                                             
    1. isimujamii                              (alama 1)
    2. sajili                    ( alama 1)
  2. Taja kaida zozote tatu za lugha                 (alama 3)
  3. Orodhesha sifa zozote tano zinazotumiwa  katika lugha ya shule.                 (alama 5) 


MARKING SCHEME

SWALI LA INSHA (ALAMA 20)

Andika kisa kitakachoonyesha ukweli wa methali hii:  Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. 

  1. Kisa kinafaa kioane na methali
  2. Mwanafunzi aonyesha sehemu zote mbili za methali.
  3. Dhana ya asiyeskia la mkuu ionekane vizuri.
  4. Dhana ya kuvunjika guu  ijitokeze hata kama ni aya chache .
    Maana : Asiyefuata ushauri huwa hana mwisho mwema.
    Mfano wa kisa : mtoto aliyelelewa vyema akaasi ushauri wa wazazi kisha mwishowe akataabika.
    Tanbihi: 
    • Anayeshughulikia upande mmoja wa methali asipite alama C+ 10/20
    • Kisa kisipolenga maana batini ya methali atakuwa amepotoka kimaudhui. Atuzwe D 03/20
    • Atakayesimulia kisa kisichomhusu binadamu (pengine mnyama fulani) atakuwa amepotoka kimaudhui. Atuzwe D 03/20
    • Atakayekariri au kunakili swali atuzwe D 02-01/20

UFAHAMU (ALAMA 10)

  1. Kichwa mwafaka – Maradhi au Magonjwa 
  2. Aina tatu za magonjwa – Utapia mlo, kisunzi, ukosefu wa damu, upele kuparara na kubambuka ngozi , surua, kifaduro, kupooza miguu, malale, malaria, mafua,kuumwa na kichwa, UKIMWI, kipindupindu, kifua kikuu,tauni,ukoma, kichocho,kuhara damu na safura.
  3. Hasara za Magonjwa: 
    • Kupoteza hamu ya kula.
    • Kichefuchefu na kutapika.
    • Kusononesha.
    • Kokonda.
    • Woga kwa kufikiria kifo.
    • Kutengwa na wagonjwa na kutamani kufa.
    • Kuzorotesha maendeleo.
  4. Njia za kushikwa na maradhi:
    • Kung’atwa na wadudu.
    • Kula chakula kichafu.
    • Ukosefu wa chakula.
  5. Atakumbwa – Atapatwa

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 20)

  1. Tofautisha kati ya sauti hizi:
    1. /m/ na /th/    (alama 1) 
      • /m/ ni king’ong’o ilhali /th/ ni kikwamizo.
      • /m/ hutamkiwa midomoni ilhali /th/ ni ya ulimi na meno.
      • /m/ ni ghuna ilhali /th/ ni si ghuna.
    2. /o/ na /u/    (alama 1) 
      • /o/ hutamkiwa nyuma kati ilhali /u/ hutamkiwa nyuma juu.
  2. Tenga silabi kwenye neno hili : muhtasari                                                           (alama 1)
    • Muh-ta-sa-ri
  3. Onyesha majukumu mawili ya kiimbo kisha utolee mifano.                                  (alama 2)
    • Swali – Unaitwa nani?
    • Taarifa - Unaitwa nani.
    • Hisia - Unaitwa nani!
  4. Akifisha sentensi ifuatayo:                                                                                (alama 3)                   
    timothy alienda shuleni tarehe 22 10 2021 akasoma kiswahili kingereza  na hesabu
    • Timothy alienda shuleni tarehe 22/10/2021 akasoma: Kiswahili,Kingereza na Hesabu.
  5. Onyesha miundo yoyote miwili ya ngeli ya A-WA kisha utolee mifano.                   (alama 2)
    • M-WA Mtu – watu
    • KI-VI Kipofu -  vipofu
    • CH – VY Chura - Vyura
  6. Tambua aina za maneno kwenye sentensi hii.             (alama 2)   
    Huyu mdogo alienda shuleni.
    • Huyu – Kiwakilishi
    • Mdogo – kivumishi
    • Alienda – kitenzi
    • Shuleni - kielezi
  7. Onyesha viambishi awali ,mzizi na viambishi tamati kwenye neno hili: alipikiwa               (alama 2)
    • Awali  a- li
    • Mzizi pik
    • Tamati iw - a
  8. Nyambua vitenzi hivi kwenye kauli zilizowekwa kwenye mabano.                                                       
    1.  Kimbia (tendesha)   (alama 1)   kimbiza
    2. tembea (tendeana)  (alama 1) tembeleana
  9. Eleza maana ya sentensi. (alama 1)
    • Sentensi ni utungo wenye kiima na kiarifa.
  10. Taja aina zozote mbili za sentensi. (alama 1)                                                             
    • Sentensi sahili
    • Sentensi ambatano
    • Sentensi changamano
  11. Tambua Kundi Nomino na Kundi tenzi katika sentensi ifuatayo:    (alama 2)
    Mwanafunzi huyu mfupi atapewa zawadi kesho.
    • Mwanafunzi huyu mfupi – Kundi nomino
    • Atapewa zawadi kesho – kundi tenzi

FASIHI SIMULIZI (ALAMA 10)

  1. Eleza maana ya fasihi. (alama 1) 
    • Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe unaomhusu binadamu.
  2. Taja tanzu mbili kuu za fasihi. (alama 1)
    • Fasihi Simulizi
    • Fasihi andishi
  3. Andika tofauti zozote tano za tanzu ulizotaja hapo juu. (alama 5)
    1. Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
    2. Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali fasihi aandishi huhifadhiwa kwa maandishi.
    3. Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishi.
    4. Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa.
    5. Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi.
    6. Uwasilishaji wa fasihi simulizi huweza kuandamana na utendaji k.v matumizi ya ishara, nyimbo, makofi, kuimba, kubeba zana katika majigambo n.k ilhali ule wa fasihi andishi hauandamani na utendaji isipokuwa inapowasilishwa mbele ya hadhira.
    7. Fasihi simulizi huwasilishwa mbele ya hadhira ilhali fasihi andishi si lazima iwasilishwe mbele ya hadhira.
    8. Fasihi simulizi huwasilishwa mahali maalum k.v jandoni, matangani, arusini, n.k ilhali fasihi andishi haina mahali maalum.
    9. Fasihi simulizi huandamana na shughuli fulani ya kitamaduni ilhali fasihi andishi haiandamani na shughuli ya kitamaduni.
    10. Fasihi andishi huhitaji muda kutunga ilhali baadhi ya fasihi simulizi huzuka papo hapo k.m. semi, maigambo.
    11. Fasihi simulizi ina uwezo mkubwa wa kubadilishwa na fanani anapowasilisha ufaraguzi) bali fasihi andishi haibadiliki isipokuwa mwandishi aiandike upya.
    12. Fasihi simulizi ina historia ndefu kuliko fasihi andishi kwa kuwepo tangu mwanzo wa maisha ya binadamu.
    13. Fasihi simulizi huwasilishwa wakati maalum k.v. usiku, kipindi fulani cha mwaka ilhali andishi haina wakati maalum.
  4. Taja umuhimu wa fasihi kwa jamii. (alama 3) 
    1. Kuburudisha-kustarehesha, kufurahisha, kuchangamsha, kutuliza, kusisimua na kupumbaza akili na kiwiliwili - nyimbo, hadithi, vitendawili
    2. Kufunza maadili kwa wanajamii kwa kuwahimiza kuiga sifa chanya na kukataa sifa hasi za wahusika.
    3. Kukuza uwezo wa kufikiri/kudadisi k.m vitendawili na chemshabongo.
    4. Kufariji k.m mbolezi na methali k.m. ‘Baada ya dhiki faraja’.
    5. Vipengele vya fasihi simulizi k.v mashairi, nyimbo, nahau, hutumiwa katika uandishi wa fasihi andishi.
    6. Kuhifadhi historia ya jamii k.m. mighani, visaviini, mapisi, tarihi n.k.
    7. Kukejeli tabia zinazokiuka matarajio ya jamii k.v soga, methali, n.k.
    8. Kuendeleza tamaduni za jamii kwani husawiri imani na desturi za jamii. k.v kitendawili ‘Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini siwezi kulichuma.’ - Mtu hawezi kumwoa dadake.
    9. Kuunganisha watu pamoja kwa kuwajumuisha pamoja wakati wa ngoma, kuimba, utambaji, n.k.
    10. Kukuza lugha k.v. misimu inapokita kimatumizi na kujumuishwa katika lugha sanifu.
    11. Kukuza uwezo wa kutumia lugha kadiri mtu anapoendelea kuwasilisha k.v. hotuba, vitanza ndimi husaidia kuboresha matamshi na kutofautisha maana za maneno.
    12. Kuza uwezo wa kubuni k.v. malumano ya utani, vitanza, ndimi ngonjera, n.k.
    13. Kukuza uzalendo kwa kufanya wanajamii kuonea fahari jamii zao na kuiga mashujaa au watu waliotendea jamii makuu.
    14. Kuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya tabia hasi k.v. ulafi, uchoyo, n.k.

ISIMUJAMII (ALAMA 10)

  1. Eleza maana ya istilahi zifuatazo:                                                                                               
    1. isimujamii                       (alama 1)
      • Taaluma inayochunguza uhusiano kati ya jamii na lugha.
    2. sajili                            ( alama 1) 
      • Matumizi ya lugha katika muktadha Fulani.
  2. Taja kaida zozote tatu za lugha                                                                   (alama 3) 
    • Jinsia/uana
    • Umri
    • mazingira
  3. Orodhesha sifa zozote tano zinazotumiwa  katika lugha ya shule.                 (alama 5) 
    • Lugha ya heshima.
    • Mazungumzo hutokea kwa zamu.
    • Msamiati maalum.
    • Matumizi ya sentensi ndefu.
    • Lugha ya kuamuru.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 1 Opener Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest