Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Mid Term 1 Exams 2023

Share via Whatsapp
Maagizo:
  • Jibu maswali yote katika karatasi hii.
SEHEMU YA A INSHA      ALAMA 20
Andika kisa kitakachomalizika kwa maneno:
….Hapo ndipo nilipong’amua kuwa watu wenye ukarimu na utu wapo licha ya kuwa ni nadra kupatikana. Mja huyo aliahidi kumtua mzigo uliomlemea.
 
SEHEMU YA ‘B’ UFAHAMU        ALAMA 10
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
 Mtaa wa Kisumu Ndogo, viungani mwa jiji la Mombasa. Mgonjwa amekuwa mgonjwa malana.  Jamaa na marafiki walikuwa wameambiwa hospitali, “Mrejesheni nyumbani.” Kwa hiyo hamna matumaini tena ya kupata ahueni.  Huyu ni wa kukatika roho dakika yoyote kuanzia sasa.  Yu tayari kukutana na Muumba wake. Wamemrejesha kwenye kibanda chake kilichotalizwa udongo na kuezekwa makuti machakavu.   Amepotelea kwenye kitanda chake cha kamba.  Sharti utazame kwa makini ndipo ubaini kwamba palikuwa na mtu pale kitandani.  Kabakia sindano kwa ukondefu. Baadhi ya watu waliozika imani na huruma zao, watu wenye kejeli zilizopindukia, wanamwita mbu.
Ukutani kumetandikwa fremu yenye picha yake alipokuwa bado na siha yake.  Alipokuwa anaikanyanga ardhi mpaka inatetemeka, wakati alipokuwa akisakatia kadanda timu ya Bandari FC kwenye Uwanja wa Manispaa na kote nchini.  Wakati alipoichezea timu ya taifa Harambee Stars wakati alipotamba jijini Mombasa.  Pale kila jicho jijini ilipomtumbulia yeye.  Wakati kila ulimi ukimsifia na kila sikio kupenda kusikia jina lake, Otii.
Jamaa zake si watu wa kusibiri mvua kunyesha ndipo waanze kutafuta pahala pa kununua mwavuli.  Wanaamini juu ya upangaji wa mikakati mapema.  Kwa hivyo, wamekutana jioni hiyo kando ya kitanda chake kupanga mikakati ya mazishi.
“Anzeni mapema kuchangisha fedha za kusafirisha maiti,” alisema mwenyekiti wa Chama cha Watu wa Nyumbani.  “Tutahitaji  kuchangisha fedha za kununua jeneza, mavazi ya kumvisha maiti pamoja na fedha za kukodisha magari ya kuchukua maiti na waombelezaji kutoka hapa Kisumu Ndogo, Mombasa, hadi Sidindi karibu na Kisumu Kubwa, Kisumu asilia.
 “Nizikeni hapa,” anasema muwele.  “Gharama zote hizo za kunipeleka Sidindi za nini?”
 Kimya kinajiri.
 “Unasikia anasema nini?” Anakumbusha mwanachama mmoja.
 “Gharama hizo ni zetu si zake,” anajibu katibu wa chama.  “Yeye atuachie tupange mambo. Anahaha nini? Yeye si mbwa wa kutupwa barabarani au mwituni akishafariki bwana. Lazima tumzike nyumbani Sidindi.  Hatuwezi kukiuka mila na ada zetu kwa kumwachia mwenzetu kutupiliwa mbali kana kwamba hana kwao.”
 “Nasema nizikeni hapa.”
 “Unaskia vile anavyosema.”
 “Kauli yake si  muhimu,”  mwenyekiti alisema.   “Katika mila na desturi zetu kauli ya marehemu si chochote, si lolote. Muhimu ni kwamba sharti mtu wa kwetu azikwe nyumbani.”
 Wanapomtazama Otii wanaona anatokwa na chozi kwenye jicho moja lililokuwa halijafunikwa na shuka. Chozi linadondoka taratibu na kuteremikia kwenye shavu lake kavu kasha kumalizikia kwenye shuka.
 Anapiga chafya na kukohoa mara kadhaa.
 “Basi kila mtu  anajaribu awezavyo kukusanya fedha za kusafirisha maiti.  Sawa?”
 “Sawa,” wanasema wote sawia.
 
Maswali.
  1. Thibitisha kuwa anayerejelewa katika makala haya alikuwa fukara. Alama 1
  2. Otii alikuwa Maarufu sana kabla ya kuwa mgonjwa.  Fafanua. Alama 2
  3. Eleza maana ya: “Jamaa zake si watu wa kusubiri mvua kunyesha ndipo waanze kutafuta pahala pa kununua  mwavuli”. Alama 1
  4. Chama cha watu wa nyumbani walifanya kinyume na matakwa ya Otii.  Eleza.  Alama 1
  5. Taja sifa zozote mbili zinazojitokeza za wahusika wanaopanga mikakati ya mazishi.    Alama 1
  6. Andika na ueleze misemo yoyote miwili iliyotumika hatika hadithi hii. Alama 2
  7. Eleza maana ya msamiati.
    1. Kilichotalizwa
    2. Muwele Alama 2

SEHEMU YA ‘C’ SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA      ALAMA 40

  1. Taja sauti zenye sifa zifuatazo
    1. Kikwamizo ghuna cha menoni
    2. Irabu ya nyuma kati
    3. Kiyeyusho cha midomo                 Alama  3 
  2. Kwa kutoa mifano tofautisha kati ya mizizi funge na mizizi huru.      Alama  2
  3. Andika kwa ukubwa wingi:
    Mji mkubwa umejengwa nyumba za kifahari.              Alama  2
  4. Yakinisha sentensi ifuatayo;
    Usipojikakamua kiume hutafaulu katika mitihani.                   Alama  1
  5. Tita ni la kuni ilhali ________________ ni kwa mizigo. Alama 1
  6. Weka nomino zifuatazo katika ngeli zake.        Alama  2
    1. Kijakazi
    2. Petroli
  7. Kwa kutoa mfano, onyesha matumizi matatu ya kiakifishi:
    Parandesi                              Alama  3
  8. Andiika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
    “Leo jioni tutamtembelea shangazi yako jijini”. Mama akamwambia                       Alama  2
  9. Changanua sentensi ifuatayo kwa mstari.
    Sisi wawili tutatuzwa tuzo.                           Alama  2
  10. Tunga sentensi katika wakati uliopita hali timilifu. Alama  2
  11. Ainisha mofimu katika neno:   Alama  3 
    Apikaye     
  12. Tunga sentensi ukitumia vivumishi vinavyotoa maana zifuatazo: Alama  2
    1. Kutobagua
    2. Kutobakiza
  13. Unda nomino dhahania kutokana na vitenzi
    1. Safari 
    2. Lima Alama 2
  14. Tunga sentensi ukitumia kivumishi kisisitizi cha mbali kidogo ukitumia nomino ya ngeli ya I-ZI                Alama  2
  15. Tunga sentensi ukitumia kihusishi chochote cha wakati              Alama 2
  16. Kamilisha jedwali.                          Alama 2
     Kutenda  Kutendesha    Kutendesha 
     Cheza    
     Lia    
  17. Banisha vitenzi katika sentensi;           Alama  2
    Babu yangu alikuwa akisafiri jana jioni
  18. Weka shadda kwenye maneno yafuatayo ili kubadilisha maana kwenye mabano.      Alama  2
    1. Walakini (dosari)
    2. Barabara (shwari)
  19. Unganisha sentensi ifuatayo ili kupata sentensi ambatano   Alama  2
    Walimu hao walipewa uhamisho.
    Walimu wengine hawakupewa
  20. Andika katika wingi
    Ndizi hili langu limeoza. Alama1

SEHEMU YA ‘D’ ISUMUJAMII           ALAMA 10

Soma kifungu kifuatacho  kisha ujibu maswali yanayofuata.
 
Niaje Wasee! Ma  likizo ndiyo hayo yameingia. Round hii tumefunga siku mob.  Mambo imebadilika.  Tukiwa ma holiday NI POA KUCHILL ili kuepukana na ball au magonjwa.
  1. Tambua sajili ya makala uliyosoma. Alama2
  2. Eleza sifa sita za sajili uliyotaja hapo juu. Alama 6
  3. Istilahi zifuatazo za isimujamii zina maana gani?   Alama  2
    1. Lahaja
    2. Uwililugha

SEHEMU YA E:  FASIHI SIMULIZI                  ALAMA 10

  1. Eleza maana ya:
    1. Ushairi simulizi Alama1
    2. Taja vipera viwili vya Ushairi simulizi Alama2
  2. Mbolezi huwa na umuhimu katika jamii.  Eleza umuhimu wake kwa hoja tatu. Alama 3
  3. Fafanua aina zifuatazo za hadithi. Alama  2
    1. Mighani
    2. Hurafa
  4. Eleza aina mbili za hadhira. Alama  2

SEHEMU YA F:  USHAIRI           ALAMA 10

Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali
 
Dunia yetu dunia, watu wanakufitini,
Dunia huna udhia, watu wanakulaani,
Dunia huna hatia, wabebeshwe kila zani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
 
Dunia umenyamaza, umetua kwa makini
Dunia vitu, watu wanataka nini?
Dunia wanakucheza, binadamu maliani,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!
 
Dunia utu akose, huvutia mdomoni.
Dunia ebu waase, hao watu mafatani,
Dunia chuki upuse, munipate afueni,
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani?
 
Dunia pewa lawama, za uongo si yakini,
Dunia wanakusema, ni manjunju si raini,
Dunia huna hasama, waja ndio kisirani
Dunia unaonewa,umetenda kosa gani!
 
Dunia kuharibika, hayo amezusha nani?
Dunia watu humaka, hao wanaokuhini
Dunia umejazia, kila tunu ya thamani
Dunia unaonewa, umetenda kosa gani?
 
Maswali
  1. Taja sifa zozote mbili za binadamu kama zinavyojitokeza katika shairi.           Alama 2
  2. Hii ni shairi ya aina gani kwa mujibu wa aina mbili kuu za mashairi.            Alama 1
  3. Eleza umbo la ubeti wa tatu                     Alama 4
  4. Shairi hili linaweza kuwekwa katika bahari mbalimbali. Zitaje bahari mbili. Alama2
  5. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulifyotumika katika shairi.
    1. Mafatani        Alama 1


MARKING SCHEME

SEHEMU YA A INSHA                              ALAMA 20

  • Hii ni insha ya mdokezo. Maneno kiini katika insha hii ni kung’amua kuwa kungali na watu wenye ukarimu na utu.
  • Mtahiniwa anaweza kutumia mbinu rejeshi na kutunga kisa ambacho kinaonana na mdokezo.
  • Anaweza kurudi nyuma na kuelezea labda shida ambazo zilikuwa zimemulemea.
  • Hali zifuatazo zinaweza kujitokeza.
    1. Mhusika anaweza  kuwa na mrudukano wa madeni ambayo ameshindwa kulipwa.  Hatimaye mtu mwenye utu akaja kusaidia.
    2. Anaweza kuwa alikuwa amelemewa na mzigo wa kukidhia familia mahitaji ya kimsingi mfadhili akajitokeza kumuauni.
    3. Anaweza kuwa katika mazingira hatari lakini msamaria mwema akajitokeza na kamsaidia.
  • Tanbihi.
    1. Mtahiniwa akitunga kisa ambacho hakionani na mdokezo,atakuwa amepotoka.
    2. Mtahiniwa akikosa kuandika mdokezo atakuwa amepungukiwa kimtindo lakini hajapotoka.

SEHEMU YA B UFAHAMU ALAMA 10

  1. Aliishi kwenye kibanda kilichotalizwa udongo na kuzekwa makuti machakavu.    Alama 1
  2.  
    1. Alisakatia kadanda timu ya Bandari F.C.
    2. Alichezea timu ya Harambee Stars
    3. Alikuwa anakanyanga ardhi inatetemeka Alama 2
  3. Walianza kupanga mikakati ya mazishi ya Otii hata kablaya kifo chake.    Alama 1
  4. Wanapanga kumzika otii Kisumu kubwa Sidindi lakini yele alitaka azikwe Kisumu Ndogo Mombasa.     Alama 1
  5.  
    1. Wenye ushirika
    2. Wenye mapuuza
    3. Watamaduni                   Alama 1
  6. Misemo
    Misemo ni
    1. pata afueni-kupata nafuu
    2. kupiga chafya-kuchemua        Alama 2
  7.  
    1. Kilichotalizwa - Kilichopakwa udongo
    2. Muwele - mgonjwa             Alama 2

SEHEMU YA C SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1.  
    1. Kikwamizo ghuna cha menoni  ‘dh’
    2. Irabu ya nyuma kati ‘o’
    3. Kiyeyusho cha midomo  ‘w’ Alama 3
  2.  
    • Mzizi huru ni ule ambao unaweza kusimama kama neno kwa mfano samehe, Sali.
    • Mizizi funge ni mzizi ambao hauwezi kusimama kama neno. Kwa mfano;   -chez-     -pig-     Alama 2
  3. Ukubwa wingi
    • Majiji makuu yamejengwa majumba ya kifahari.  Alama 2
  4. Kuyakinisha
    • Ukijikakamua kiume utafaulu katika mtihani.    Alama 1
  5. Shehena ya mizigo     Alama 1
  6.  
    1. Kijakazi  A-WA
    2. Petroli  I-I Alama   2
  7. Parandesi/mabano/vifungo
    1. Kuhifadhi maelezo ya nyongeza
    2. Kutoa maelekezo ya mwandishi
    3. Kuonyesha maneno yenye maana sawa.  Alama 3
  8. Usemi wa taarifa
    • Mama alimwambia kuwa siku hiyo jioni wangemtembelea shangazi yake jijini.  Alama 2
  9. Mstari
    Sisi wawili tutakatazwa tuzo
    • S → K N (W+V) + KT (T+N) . Alama 2
  10. Wakati uliopita hali timilifu mfano
    • Kasisi alikuwa amewahubiria waumini. Alama 2
  11. Apikaye 
    • A – nafsi/ngeli
    • PIK ] Mzizi   
    • A- Kauli/Kiishio
    • Ye-Kirejeshi    Alama 3
  12.  
    1. kutobagua – o – ote
    2. Kutobakiza  - ote  Alama 2
  13.  
    1. Usafiri
    2. Ukulima  Alama 2
  14. Sahani au Nyumba iyo hiyo ama zizo hizo  Alama 2
  15. Kabla ya, baada ya, mpaka  Alama 2
  16. Kamilisha jedwali
     Kutenda  Kutendesha    Kutendesha 
     Cheza  Chezesha  Chezeshea 
     Lia  Liza  Lizia 
  17.  
    1. Alikuwa  -  Kitenzi  Kisiaidizi Ts
    2. Akisafiri  -  Kitenzi kikuu  Alama 2
  18.  
    1. Walakini (dosari)
    2. Barabara (Shwari) Alama 2
  19. Walimu hao walipewa uhamisho lakini wengini hawakupewa. Alama 2
  20. Ndizi hizi zetu zimeoza. Alama 1

SEHEMU YA D ISIMU JAMII  Alama 10

  1. Sajili ya vijana  Alama 2
  2. Sifa za sajili ya vijana
    1. Kutumia lugha legevu
    2. Kuchanganya ndimi
    3. Kuna matumizi ya sheng
    4. Matumixi ya sentensi fupi
    5. Kuna matumizi ya misimu
    6. Huwa kuna kukatizana kauli  Alama 6
  3.  
    1. Iahaja 
      •  Ni viijilugha ya lugha moja
    2. Uwililugha
      • ni uwezo wa  mtu kuzungumza lugha mbili.  Alama 2

SEHEMU YA E FASIHI SIMULIZI ALAMA 10

  1.  
    1. Ushairi simulizi ni tungo za ushairi ambazo huasilishwa mbele ya hadhira kwa kusemwa au kwa kusemwa au kwa njia ya mdomo.
    2. Vipera vya ushairi simulizi Alama 1
      • Nyimbo
      • Maghani Alama 2
  2.  
    1. Huwafariji waliofiwa
    2. Huwapa waliofiwa matumaini
    3. Huleta utangamano baina ya waliofiwa na jama za marafiki. 
    4. Huhimiza wetu wasiogope bali wawe na ujasiri
    5. Huimbwa kama njia ya kudumisha utamaduni  Alama 3
  3.  
    1. Mighani – Hadithi za mashujaa
    2. Hurafa – Hadithi za wahusika
      Wanyama pekee Alama2
  4.  
    • Hadhira hai – hadhira inayoshirikishwa
    • Hadhira tuli – Hadhira isiyoshirikishwa Alama 2

SEHEMU YA F USHAIRI ALAMA 10

  1. Sifa za binadamu
    1. Binadamu ni haini
    2. Binadamu ni wafitini
    3. Binadamu ni waongo
    4. Binadamu ni mbaya   Alama 2
  2. Shairi la Kiarudhi Alama 1
  3.  
    • Umbo la ubeti wa tatu
    • Ubeti una mishororo minne
    • Ubeti una migao miwili – ukwapi na utao
    • vina vya ubeti huu ni
      • Se - ni
      • Se- ni
      • Se – ni
      • Wa – ni
    • Kila kipande kina mizani miine Alama 4
  4. Bahari
    1. Tarbia – kila ubeti una mishororo miine
    2. Mathinau – kila mshororo una migao miwili.
    3. Ukara – vina vya kati vinatofatiana katika kila ubeti lakini vya nje vinafanana  Alama 2
  5. Watu mafatani – wachochezi  Alama 1
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Mid Term 1 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest