KISWAHILI
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA
MUHULA WA 1 2021
KIDATO CHA NNE
KARATASI YA 1
MUDA SAA 2
MAAGIZO
- Jibu maswali mawili
- Swali la kwanza ni la lazima
- Chagua swali moja kati ya matatu yaliyobaki
- Kila insha isipungue maneno 400
-
Swali la LAZIMA
Ukiwa Gavana Mtajika wa Kaunti yako umealikwa kuwazungumzia wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Mafanikio. Andika Tawasifu utakayowasilisha. (alama 20) -
Eleza jinsi udanganyifu katika mitihani utaathiri maisha ya kizazi kijacho. (alama 20)
-
Andika kisa kitakachothibitisha maana ya methali: Mtenda mema kwa watu atendea nafsiye. (alama 20)
-
Kamilisha tukio kwa maneno yafuatayo:
“…waliwasili saa tatu baadaye. Uharibifu wa mali na maisha ulikuwa umeshatendeka wala kufika kwao hakukusaidia kwa lolote.”(alama 20)
MAAKIZO
- Muundo
Zingatia lugha ya mtiririko.- KujitambulishaJina
- Kuzaliwa/Eneo/Kaunti n.k
- Malezi yake
- Elimu
- Msingi
- Sekondari
- Vyuo mbalimbali alivyosomea.
- Tajriba
- Kazi aliyofanya/alizofanya kabla ya kuwa Gavana.
- Siasa – kiwango/viwango gani?
- Anatajika kwa jambo/mambo gani
- Mifano: - Elimu ya juu – shahada kadha
- Miradi ya maendeleo
- Ziara alizofanya.
- Uwajibikaji wake/maadili kazini
- Falsafa yake ya maisha.
- Malengo yake
- Changamoto alizopitia.
- Ruwaza/maazimio yake.
- Lugha – mtahiniwa atumie nafsi ya kwanza.
- Usemi ya taarifa.
- Lugha rasmi itumiwe.
- KujitambulishaJina
- Hoja.
- Maadili yatazorota
- Njia za mkato maishani
- Uzembe kazini
- Ukosefu wa uwajibikaji
- Mapuuza
- Kutothamini mitihani
- Elimu kudorora
- Kuathirika kwa taaluma mbalimbali
- Utendekazi utaathirika
- Nidhamu kutoweka
- Mtenda mema kwa watu atendea nafsiye
- Maana: Kuwafanyia wema watu ni sawa na kujiwekea akiba. Huenda nao wakakutendea wema utakapouhitaji.
- Funzo: Usidhani unafanya kazi ya bure unapomfaa mtu Fulani.
- Matumizi: Inaweza kuhimizwa anayefikiria kuwa wema uatendao ni wa bure na kuwa hatafaidika hata akiendelea.
- Mtahiniwa aandike kisa kitakachodhihirika pande zote mbili.
- Mambo ya kuzingatiwa
- Kisa kinafaa kuwa katika wakati uliopita.
- Mtahiniwa azingatie kumaliza kisa chake kwa maneno yote yaliyodokezwa.
- Mahali pa tukio patajwe.
- Baadhi ya matukio;
- Moto
- Wizi
- Ugaidi
- Baharini/majini
- Ajali barabarani.
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2021.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students