Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA
MUHULA WA 1 2021
KIDATO CHA NNE
KARATASI YA 2
MUDA SAA 2

MAAGIZO

  • jibu maswali yote
  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

    Tangu opresheni ya Usalama kuanza kutekelezwa na maafisa wa usalama katika mtaa wa Eastleigh, kumekuwa na propaganda kuwa inalenga watu wa jamii na dini Fulani.

    Harakati hizi za kuwasaka magaidi sharti ziendelee na zichangiwe na kila raia ili zizae matunda tatunayoazimia kupata; kuwanasa wote wanaohusika.

    Wakenya tumeishi kwa miaka mingi bila kubaguana katika misingi ya dini na ukabila. Iweje tuanze sasa miaka zaidi ya hamsini baada ya uhuru? Ndiposa tunawasihi Wakenya wote wenye nia njema kukumbuka kwamba hatuna njia ya mkato katika suala hili la ugaidi. Sharti tupambane nao. Hawa ni watu; ni ndugu zetu, rafiki zetu na watoto wetu.

    Hakuna mzazi atakayejitokeza hadharani na kukiri kuwa mtoto wake ni gaidi! Hata kama atajua wazi mwanawe ni gaidi na amelipua Wakenya na ataendelea kufanya hivyo akizidi kupewa nafasi. Atanyamaza na kumtetea kwa hali na mali.

    Madhara ya mashambulizi hayo ya kigaidi tayari yameanza kuonekana ambapo wamiliki wa mahoteli ya kifahari wanalalama kuwa idadi ya wageni imepungua maradufu. Hali kama hii ni hatari kwa uchumi wa nchi.

    Sisi tukiwa Wakenya wapenda amani hatuna budi kuungana mkono katika oparesheni hiyo na kushirikiana na maafisa wa usalama kwa kutoa habari muhimu kuhusu washukiwa wa ugaidi. Hakuna operesheni dhidi ya wahalifu ambayo inaweza kuendeshwa bila jamii ambapo wamejificha kuathiriwa. Heri nusu shari kuliko shari kamili; magaidi wana madhara makubwa kuliko operesheni ya usalama.

    Sisi Wakenya kwa sasa tuko katika hali hii tatanishi ya kushindwa kuamua; tupambane na magaidi tuumize na Wakenya wachache wasio na hatia ama tuache tu magaidi wakae kwa sababu tunaogopa kuwasumbua hao wachache.

    Kadhalika, badala ya kuangazia maeneo yenye visa vingi vya mashambulizi ya ugaidi operesheni ya usalama inafaa kuelekezwa pia katika maeneo mengineyo ambayo yamekuwa yakikumbwa na visa vya utovu wa usalama mara kwa mara.

    Vikosi vya usalama vinafaa kuhakisha kuwa magenge ya aina hii hayasazwi katika operesheni hiyo. Aidha, serikali inapaswa kutoa makataa kwa kila Mkenya ambaye anamiliki bunduki kinyume cha sheria kusalimisha silaha hizo mara moja katika vituo vya polisi, la sivyo wachukuliwe hatua kali za kisheria.

    Wakenya wote wafaa kuonyesha ushirikiano kwa kuwa makini zaidi. Wajiepushe na maeneo hatari ambayo yaweza kuwa makazi ya magaidi ama ya washukiwa wa ugaidi. Aliye kando haangukiwi na mti ama mshausahau huo maarufu.

    Maswali
    1.    
      1. Eleza uongo unaosambazwa kuhusu operesheni ya usalama mtaani Eastleigh. (alama 1)
      2. Operesheni hii ina lengo lipi? (alama 1)
    2. Eeleza jinsi Wakenya wamekuwa wakiishi tangu uhuru. (alama 1)
    3.    
      1. Magaidi wana uhusiano upi nasi kwa mujibu wa kifungu? (alama 1)
      2. Eleza namna wazazi wanavyochangia kuwepo kwa ugaidi nchini. (alama 2)
    4. Fafanua athari mbili zinazokumba nchi kutokana na ugaidi. (alama 2)
    5. Wakenya wamepewa changamoto ipi ili kusaidia katika kuangamiza ugaidi? (alama 2)
    6. “Wakenya wako kwenye njia panda.” Tetea kauli hii ukirejelea kufungu. (alama 2)
    7. Serikali inapaswa kuchukua hatua ipi dhidi ya wamiliki haramu wa bunduki? (alama 2)
    8. Eleza maana ya methali hii kulingana na taarifa. (alama 1)
      Aliye kando haangukiwi na mti.

  2. MUHTASARI.
    Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.

    Lugha imekuwa kikwazo kikubwa katika kukuza tecknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) barani Afrika . Lugha ambazo zimekuwa zikitumiwa ni za kimagharibi kama vile kijerumani , kifaransa na kiingereza. Idadi kubwa ya waafrika ,hasa wanaoishi vijijini hawazifahamu lugha hizi.

    Uamuzi wa shirika la Microsoft wa kutumia lugha ya kiswahili katika program za kompyuta kuanzia mwaka 2005 ni mchango mkubwa. Kuzinduliwa kwa mradi huu ni tukio la kipekee kuimarisha tecknolojia sehemu za mashambani.

    Mradi huu umewawezesha wananchi takribani milioni 150 wa janibu za Afrika Mashariki kufaidika na huduma za tarakilishi.

    Utekelezaji wa mradi halikuwa jambo jepesi. Kwanza, ilibidi shirika la microsoft chini ya uongozi wa Bill Gates kulishawishi Bodi lake la wakurigenzi. Bodi liliposhawishika kuwa Kiswahili ni lugha inayo tumiwa na mamilioni ya watu liliidhinisha kuzinduliwa kwa mradi. Hatua iliyofuatia ilikuwa kuteua maneno 700,000 ya kimsingi ya kiiingereza ambayo yangetafsiriwa kwa kiswhili.

    Hatua iliyofuata ilikuwa ya kutafuta ushirikiano na dola pamoja na mashirika ya kibiashara na taasisi za elimu ulimwenguni. Ilipobainika kuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili yangehanasisha

    Uwekaji katika vituo vya mtandao vijijini, ushirikiano katika kuendesha mradi huu uliafikiwa bila shida. Mradi huu ulichukua muda wa miezi 18 kukamilika.Uliwashirikisha wahisika katika uwanja wa tecknolojia ya habari mawasiliano, elimu biashara na idara za Kiswahili katika vyuo vikuu vya Africa Mashariki. Vyuo –vikuu ni pamoja na Dar es Salaam . Nairobi, Kenyatta na Makerere.

    Waatalamu walioshirikishwa walisaidia katika kubuni faharasa ya istilahi za Kiswahili 3,000. Hizi ni zile ambazo zinafaa kwa matumizi ya kompyuta ya kawaida na ya kila siku.

    Mradi huu umeshangiliwa na wakereketwa na wapenzi wa Kiswahili katika nyanja zote. Wasomi, wanariadha , wanamuziki, watalii, wafanyabiashara , wanasiasa ,wafuasi wa dini mbalimbali na wakulima ; wote wamefurahia hatua ya Kiswahili kuingizwa kwenye mtandao.

    Watu ambao walikuwa hawawezi kutumia tarakilishi kwa sababu ya kutojua Kiingereza sasa hawana kisingizio. Matumizi ya kiswahili yatapanua na kuimarisha mawasiliano baina ya watu wanaoishi vijijini na pembe zote za ulimwengu.

    Jambo la kutia moyo zaidi ni kuwa sasa vyuo vikuu vinavyotoa masomo kwa kutumia mitandao vimepewa idhini ya kutumia programu hizi. Walimu na wanafunzi wanapata habari moja kwa moja kwa kiswahili bila kutafsiri . Kuna uwezekano sasa wa kusambaza mafonzo katika nyanja na viwango vyote kwa mfumo wa elimu ya mbali.

    Katika ulimwengu wa utandawazi,tukio kama hili lina manufaa makubwa. Wananchi wa vijijini wanaweza kupata habari na maarifa kutoka pembe zote za dunia na kuhusu masuala tofauti tofauti kwa lugha wanyoielewa barabara.

    Kusambaa kwa matumizi ya ngamizi vijijini kutaimarisha biashara inayofungamana na tecknolojia na mawasiliano .Haili hii itainua maendeleoya teknolojia na kiwango cha maisha vijijini. Bila shaka mwachano uliopo baina ya sehemu za mijini na vijijini utapunguwa.

    Haya ndiyo maendeleo anayokamia kila mja wa siku hizi . Lililopo ni serikali kupania kupanua na kusambaza muundo mbinu kama –umeme na simu katika sehemu zote za nchi. Pamoja na haya , kuna haja ya kupunguza bei ya ngamizi na vipuri vyake ili kuwatia motisha watu kununua kompyuta kwa wingi. Ikumbukwe – kuwa lengo la kuanzisha mradi huu ilikuwa kuisaidia serikali kupanua na kusambaza matumizi ya huduma za kompyuta na mtandao katika shule, vituo vya kijami na maeneo ya makaazi. Huduma hizi ni msigi wa elimu, biashara na mawasiliano ya makaazi.

    Maswali.
    1. Bila kubadilisha maana, fupisha aya tatu za kwanza. (Maneno 45-55) (al.6)
      Matayarisho :
      Jibu :
    2. Fupisha faida za mradi wa kutumia Kiswahili katika program ya kompyuta. (Maneno 45-55) (al.6)
      Matayarisho :
      Jibu :
    3. Eleza kwa ufupi serikali inahitaji kufanya nini ili kufanikisha maradi huu? (Maneno 15 -20)
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Eleza tofauti kati ya sauti za vipasuo na vikwamizo (al 2)
    2. Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifuatavyo. (al.2)
      1. Kitenzi kishirikishi kipungufu
      2. Kitenzi kishirikishi kikamilifu
    3. Unda nomino ya dhahania kutokana na vitenzi vifuatavyo (al.2)
      1. Cheza
      2. Pika
    4. Tambulisha aina ya virai vilivyotumika katika sentensi zifuatazo
      1. Walisomba changarawe (al.1)
      2. Kwa hofu alimkabidhi matokeo (al.1)
    5. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia matawi.
      Simba waliojeruhiwa jana walikimbia vichakani (al.4)
    6. Taja aina tatu kuu za sentensi kwa kuzingatia muundo. (al.3)
      1. -
      2. -
      3. -
    7. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendewa
      1. Paka alimla panya mkubwa jana jioni (al.2)
      2. Mwalimu mkuu amenisamehe kosa langu (al. 2)
    8. Kanusha sentensi zifuatazo kwa umoja
      1. Nywele zenu hukatika mnapochana (al 3)
      2. Nyinyi ndio mnaopenda kuchezea mbeleko za mtoto (al.2)
    9. Tunga sentensi ukitumia viungo vifuatavyo ili kudhihirisha maana ya dhana katika mabano. (al 2)
      1. Kwa(umilikaji)
      2. Ku(Nafsi)
    10. Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii (al 2)
      1. Walichukua pesa waliporudi
    11. Andika katika usemi wa taarifa.
      “ Lazima ufike leo asubuhi na mapema ama sivyo hutanipata” Juma alimwambia mamake. (al.4)
    12. Onyesha tofauti kati ya sentensi hizi: (al 2)
      1. Amefika.
      2. Amefika!
    13. Eleza matumizi mawili ya “ ki” kisha utunge sentensi moja moja kuonyesha matumizi hayo (al 4)
    14. Tumia kirejeshi tamati katika sentensi hii. (al 2)
      Malipo ambayo anapewa ni yale ambayo yanaridhisha
  4. ISIMU JAMII
    1. Maenezi ya Kiswahili Afrika mashariki punde baada ya uhuru yalikuwa na chagamoto tele. Fafanua zozote tano. (al 10)

MAAKIZO

  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    Maswali
    1.    
      1. Eleza uongo unaosambazwa kuhusu operesheni ya usalama mtaani Eastleigh. (alama 1)
        • Eti operesheni hii inalenga watu wa jamii na dini Fulani

      2. Operesheni hii ina lengo lipi? (alama 1)
        • Kuwanasa magaidi wote

    2. Eeleza jinsi Wakenya wamekuwa wakiishi tangu uhuru. (alama 1)
      • Kwa umoja/bila kubagwana katika wingi ya dini na ukabila

    3.    
      1. Magaidi wana uhusiano upi nasi kwa mujibu wa kifungu? (alama 1)
        • Ni ndugu zetu, rafiki zetu na watoto wetu

      2. Eleza namna wazazi wanavyochangia kuwepo kwa ugaidi nchini. (alama 2)
        • Wanawafika/wana wanyamazia na kuwatetea watot wao magaidi kwa hali na nchi

    4. Fafanua athari mbili zinazokumba nchi kutokana na ugaidi. (alama 2)
      • Uchumi kuzoroteka/kuthjirika k.m
      • Idadi ya wageni/watalii kupungua
      • Ukosefu wa susalama kwa raia/wananchi

    5. Wakenya wamepewa changamoto ipi ili kusaidia katika kuangamiza ugaidi? (alama 2)
      • Kushirikiana na maafisa wa usalama kwa kutoa habari muhimu kuhusu washukiwa wa ugaidi

    6. “Wakenya wako kwenye njia panda.” Tetea kauli hii ukirejelea kufungu. (alama 2)
      • Wanashindwa kuamua iwapo watapmabna na magaidi waqaumize na wakenya wenzao wachache wasio na hatia au waache tu magaidi waendelee na mashambulizi

    7. Serikali inapaswa kuchukua hatua ipi dhidi ya wamiliki haramu wa bunduki? (alama 2)
      • Kutwa makataa ya kuzisalimisha silaha hizo mara moja kaitka vituoo vya polisi

    8. Eleza maana ya methali hii kulingana na taarifa. (alama 1)
      Aliye kando haangukiwi na mti.
      • Wakenya washuriwa wajiepushe na maneno hatari

  2. MUKHTASARI.
    Maswali.
    1. Bila kubadilisha maana, fupisha aya tatu za kwanza. (Maneno 45-55) (al.6)
      Matayarisho :
      Jibu : Lugha za kimagharibi ambazo wafrika wengi hawazifahamu ni kikwazo kwa kukuza Mawasiliano. Mradi wa Microsoft wa kutumia Kiswahili utasaidia kuimarisha technolojia vijijini. Idhini imetolewa na shirika hili limeletwa maneno laki saba ya kiingereza ili yatafsiriwe kwa Kiswahili.

    2. Fupisha faida za mradi wa kutumia Kiswahili katika program ya kompyuta. (Maneno 45-55) (al.6)
      Matayarisho :
      Jibu :
      • Kuimrisha uwekezaji
      • Kuimarisha mafunzo
      • Kufahamisha habari kutoka pembe zote.
      • Kuinua maendeleo ya kiteknolojia.
      • Kupanua mawasiliano.
      • Kusambaza mafunzo.
      • Kuinua kiwango cha maisha

    3. Eleza kwa ufupi serikali inahitaji kufanya nini ili kufanikisha maradi huu? (Maneno 15 -20)
      • Kupanua na kusambaza miundo mbinu.
      • Kupuunguza bei ya tarakilishi na vipuri vyake.

  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Eleza tofauti kati ya sauti za vipasuo na vikwamizo (al 2)
      • Vipasuo - Hewa huzuiwa kabisa na kuachiliwa kw ghafla kwa mpasho k.m p& b
      • Vikwamizo – Ala za kutamkia hukaribiana na kutoa sauti ya mkwaruzo wa hewa au msuguano k.m.(f/v/lt gh)

    2. Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifuatavyo. (al.2)
      1. Kitenzi kishirikishi kipungufu
        • ni /si /yu

      2. Kitenzi kishirikishi kikamilifu
        • agali/likuwa /kwamba/anaonekana

    3. Unda nomino ya dhahania kutokana na vitenzi vifuatavyo (al.2)
      1. Cheza - uchezaji
      2. Pika - upishi
    4. Tambulisha aina ya virai vilivyotumika katika sentensi zifuatazo
      1. Walisomba changarawe (al.1)
        • walisomba (kirai kitenzi)
      2. Kwa hofu alimkabidhi matokeo (al.1)
        • Kirai kihusishi(kwa)

    5. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia matawi.
      Simba waliojeruhiwa jana walikimbia vichakani (al.4)
           S
         KN KT  
      S   T  E
      Simba Waliojeruhiwa Jana walikimbia  vichakani
    6. Taja aina tatu kuu za sentensi kwa kuzingatia muundo. (al.3)
      1. Sahili
      2. Ambatano
      3. Changamano

    7. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendewa
      1. Paka alimla panya mkubwa jana jioni (al.2)
        • Panya mkubwa aliliwa na paka jana jioni

      2. Mwalimu mkuu amenisamehe kosa langu (al. 2)
        • Nimesamehewa na mwalimu mkuu kwa kosa hilo

    8. Kanusha sentensi zifuatazo kwa umoja
      1. Nywele zenu hukatika mnapochana (al 3)
        • Unywele wako haukatiki unapochana

      2. Nyinyi ndio mnaopenda kuchezea mbeleko za mtoto (al.2)
        • Wewe siye unayependa kuchezea ubaleko wa mtoto

    9. Tunga sentensi ukitumia viungo vifuatavyo ili kudhihirisha maana ya dhana katika mabano. (al 2)
      1. Kwa(umilikaji)
        • Aliaenda kwake jana jioni
      2. Ku(Nafsi)
        • Anakutaka (nafsi ya pili)

    10. Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii (al 2)
      1. Walichukua pesa waliporudi
        • Walienda halafu wakarudi baadae kuchukua pesa
        • Waliochukua pesa walichukua baada ya watu watu waliokuwa wanangoja kurudi
    11. Andika katika usemi wa taarifa.
      “ Lazima ufike leo asubuhi na mapema ama sivyo hutanipata” Juma alimwambia mamake. (al.4)
      • Juma alimwambia mamake kuwa lazima afike siku hiyo asubuhi na mapema ama sivyo hangempata

    12. Onyesha tofauti kati ya sentensi hizi: (al 2)
      1. Amefika.
      2. Amefika!
        Sentensi ya kwanza inasemwa kwa njia ya kawaida ilhali ya pili inasemwa kwa njia ya mshangao, labda luonyesha ni kitu kisichotarajika.

    13. Eleza matumizi mawili ya “ ki” kisha utunge sentensi moja moja kuonyesha matumizi hayo (al 4)
      • Ki ya masharti K.M. ukicheza K.M.kinyama
        ״ ״ namna /jinsi /mfano K.M. kinyama
        ״kiambishi cha ngeli K.M.KI-Viumoja kimepotea
        ״kishirikishi kipungufu K.M kikulacho ki
        ״ kuonyesha wakati K,M .Niliwakuta wakiimba odogo/kulisha K.M kijili

    14. Tumia kirejeshi tamati katika sentensi hii. (al 2)
      Malipo ambayo anapewa ni yale ambayo yanaridhisha
      • Anapewa malipo yaridhishayo

  4. ISIMU JAMII
    1. Maenezi ya Kiswahili Afrika mashariki punde baada ya uhuru yalikuwa na chagamoto tele. Fafanua zozote tano. (al 10)
      • Uhaba mkubwa wa wataalamu wa Kiswahili
      • Athari kutoka kwa lugha ya kwanza.
      • Watu kuchangamka lugha nyinginezo ka vile kiingereza, kijerumani.
      • Imani potovu – lugha ya Kiswahili ni duni
      • Uhaba wa walimu wa Kiswahili.
      • Uhaba wa vitabu vya Kiswahili.
      • Kutokuwepo kwa sera ya lugha kutoka kwa baadhi ya serikali za mataifa ya Afrika mashariki.
      • Uhaba wa pesa za kutafikia
      • Nchi za Afrika za kukuza na kuendeleza Kiswahili
      • Zozote 5 x 2 = 10
      • Lazima afafanue.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest