Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

MAAGIZO KWA MTAHINIWA:

  • Karatasi hii ina maswali manne.
  • Jibu maswali mawili pekee. Kila swali lina alama ishirini.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Chagua swali jingine lolote kutoka kwa matatu yaliyosalia.
  • Majibu yote yaandikwe katika karatasi ya majibu uliyopewa.
  • Majibu yote yaandikwe katika lugha ya Kiswahili.

 

  1. SWALI LA LAZIMA.
    Gari unalosafiria limehusika katika ajali mbaya barabarani. Japo kuna walioaga dunia, wewe hujadhurika kwa njia yoyote.
    Andika mahojiano kati yako na mwandishi wa gazeti la Mwangaza ambaye amekuja kukuhoji kuhusu ajali hiyo.
  2. Pendekeza njia mbalimbali zinazoweza kutumiwa ili kuleta utangamano wa kitaifa.
  3. Sitapiki nyongo harudi haramba.
  4. Malizia kwa maneno haya… hapo ndipo nilipogundua umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

Mwongozo wa Kusahihisha

USAHIHISHAJI

  • Katika hii karatasi mawasiliano yatategemea ukwasi wa lugha ya mwanafunzi kwa mfano, sentensi sahihi, zenye UTIR1RIKO MZURI KIMAWAZO, LUGHA YA KUVUTIA NA YENYE MAWAZO ASILIA. Ubunifu mwingi na hati nadhifu. Kutegemea maagizo ya swali lenyewe au umahiri wa lugha. ni lazima katika mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo. Mtahini ni lazima asome insha yote ili aweze kukadiria viwango mbalimbali vilivyopendekezwa yaani A, B, C ama D kutengeneza mahali popote pale pafaapo kuikadiria insha ya mtahiniwa.

KIWANGO CHA D

  • Maki 01 -05
    1. Insha ya aina hii haieleweki kwa vyovyote ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana, hivi kwamba mtahini ni lazima afikirie kila anachojaribu kuandika.
    2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia mane no ya Kiswahili kwa njia inayofaa,
    3. Lugha imevungika, uakifishaji usiofaa, ina makosa ya kila aina ya kisarufi, kimaendelezo, mtindo mbovu n.k.

VIWANGO TOFAUTI VYA D

  • D- (KIWANGO CHA CHINI)*
    Maki 01 -02
    Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile kama vile kunakili maswali au kujitungia swali na kulijibu
  • D (WASTANI)*
    Maki 03
    Utiririko wa mawazo haupo, na insha haieleweki Makosa ni mengi.
  • D+KIWANGO CHA JUU
    Maki 04-05
    Ingawa insha ina lugha dhaifu ya Kiswahili ina makosa mengi ya kila aina, unaweza kutambua kile ambacho anajaribu kuwasilisha

KIWANGO CHA C
MAKI 06 -10

  1. Mtahiniwa anaweza kuwasilisha mawazo yake lakini kiwango kisichoeleweka kikamilifu.
  2. Hana uhakika wa matumizi ya lugha
  3. Mada huwa haikukuzwa na kuendelezwa kikamilifu.
  4. Mtahiniwa anaweza kupotoka hapa na pale
  5. Kujiru diarudia ni dhahiri
  6. Mpangilio wake wa kazi ni hafifu na haina mtiririko.
  7. Hana matumizi mazuri ya lugha
  8. Mtahiniwa ana athari ya lugha ya kwanza ambayo huonekana dhahiri kama vile'papa1 badala yo "'baba1' karamu badala ya 'kalamu n.k

 

  • C- (KIWAANGO CHA CHINI*
    Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha mawazo yake
    Hana muundo wa sentensi ufaao
    Ana makosa mengi ya msamiati, hijai na matumizi mabaya ya sarufi.
  • C (WASTANI)
    Maki -08
    Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia isiyo sarufi
    Hufanya makosa mengi ya sarufi.
    Hana ubunifu wa kutosha.
    Katika sentensi ndefu uakifishaji wake ni mbaya.
    Ana makosa kadha ya hijai na msamiati.
  • C+ (KIWANGO CHA JUU) Maki
    09-10
    Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri lakini kwa njia isiyo na mvuto sana.
    Dhana tofauti tofauti hazijitokezi kikamilifu.
    Hutumia misemo, methali, tashbihi, tanakaliza sauti n.k. kwa njia isioyofaa.
    Utiririko wa mawazo bado haujtokezi wazi

KIWANGO CHA B Maki 11-15

  1. Katika kiwango hiki. mtahiniwa anaonyesha kuimudu lugha vilivyo
  2. Mtahiniwa hudhihirisha kwamba anaweza kutumia lugha kwa urahisi katika kujieleza.
  3. Hutumia miundo tofauti ya sentensi vizuri.
  4. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha kama sentensi kuandikwa kwa njia tofauti na ikaleta maana sawa.

 

  • B- KIWANGO CHA CHINI
    11 – 12
    Mtahiniwa huwasilisha ujumbe wake kwa kuonyesha hoja tofauti tofauti
    Kuna utiririko mzuri wa mawazo.
    Ana uwezo wa kutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi
    Makosa machache ya hapa na pale.
  • B (WASTANI)
    Maki 13
    Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kumudu lugha.
    Anawasilisha ujumbe wake waziwazi kwa mawazo yanayodhihirika.
    Matumizi ya lugha ya mnato huweza kudhihirika
    Anatumia mifano michache ya msamiati mwafaka
    Matumizi ya tamathali za usemi yanaanza kudhihirika
    Makosa machache yaweza kutokea hapa na pale
  • B+ (KIWANGO CHA JUU)
    Maki 14 – 15
    Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika
    Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa njia inayovutia na kwa urahisi
    Kuna makosa ya hapa na pale ambayo mtahiniwa hakudhamiria kuyafanya
    Uteuzi wake wa msamiati ni mzuri
    Sarufi yake ni nzuri.
    Uakifishaji wake ni mzuri.

KIWANGO CHA A
Maki 16 - 20
Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato. Ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka.
Ana uwezo wa kutumia tamathati za lugha ili kutoa hisia zake kwa njia iliyo bora na kwa urahisi.
Anadhihirisha ukakamavu wake kimawazo na mpangilio mzuri na hali ya kumvutia msomaj wake.

  • A- (KIWANGO CHA CHINI)
    Maki 16 -17
    Mtahiniwa anadhihirisha ukakamavu wa lugha. Ana mtiririko mzuri kulingana na mada.
    Huipamba lugha kwa kutumia tamathali za semi.
    Huzingatia matumizi mazuri ya msamiati na sarufi.
    Makosa ni machache
  • A (WASTANI)
    Maki 18
    Mawazo yanadhihirika zaidi.
    Makosa ni machache mno.
    Hutumia lugha ya mnato.
    Hutumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia.
    Sarufi yake ni nzuri.
    Hutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.
    Hujieleza kikamilifu.
  • A (KIWANGO (HA JUU) Maki 19-20
    Mtahiniwa huwasilishaujumbe kulingana na mada.
    Hutiririsha mawazo yake vizuri zaidi.
    Hujieleza kikamilifu bila shida
    Hutoa hoja zilizokomaa, Makosa ya kawaida ni nadra sana kupatikana
    Msamiati wake ni wa hali ya juu

JINSI MTAIHINI ANAVYOWEZA KUTUZA INSHA MBALIMBALI
Mtahiniwa asipozingatia sura ya insha aondolewe maki 4 baada ya kutuzwa.

  • Mitindo ya kuandika herufi tofauti tofauti isiingilie sana utahini.
  • Hati ya mtahiniwa isitiliwe maanani mno.

SARUFI

  1. Kuakifisha vibaya: Mifani:- vikomo, vituo alama ya kuuliza n.k.
  2. Kutumia herufi ndogo au kubwa mahali si pake.
  3. Matumizi mabaya ya ngeli na viambishi, nyakati, vihusiano, muundo mbaya wa sentensi na mnyambuliko wa vitenzi na majina.
  4. Kuacha au kuongeza neno katika sentensi k.m. kwa kwa
  5. Matumizi ya herufi kubwa

Tazama: Matumizi ya herufi kubwa

  1. Mwanzo wa sentensi
  2. Majina ya pekee
  3. Majina ya mahali miji, nchi n.k.
  4. Siku za juma. miezi n.k.
  5. Mashirika. masomo. vitabu n.k.
  6. Makabila, lugha n.k.
  7. Mungu

Makosa y a Hijai.
Haya ni makosa ya maendelezo - sahihisha huku ukionyesha yanapotokea. Makosa ya tahajia kuwa katika:

  1. Kutenganisha neno kama vile 'aliye kuwa'
  2. Kuunganisha maneno kama vile 'kwasababu'
  3. Kukata si labi vibaya kama vile 'ngan-o'
  4. Kuandika herufi isiyofaa katika neno kama mahari badala ya mahali.
  5. Kuacha herufi katika neno kama 'aliekua' badala ya 'aliyekuwa'
  6. Kuongeza herufi isiyofaa katika neno kama 'piya' badala ya 'pia'Kuacha alama inayotarajiwa kuwepo katika herufi.
  7. Kutoandika. kistari cha kuunganisha neno ufikiapo pambizo au mwisho, au kuandika mahali si pake.
  8. Kukiandika kistari pahali pasipofaa.
  9. Kuacha ritifaa au kuiweka pasipofaa
  10. Kuandika maneno kwa kifupi. Mfano k.m. n.k. v.v.

Mtindo
Mambo yatakayochunguzwa

  1. Mpangilio wa kazi kiaya
  2. Utititiko wa mawazo
  3. Hati nzuri inayosomeka kwa urahisi
  4. Namna anavyotumia methali, misemo, tamathali na mengineyo
  5. Unadhifu wa kazi
  6. Kuandika herufi nzuri k.m. Jj Pp, Uu
  7. Sura ya insha.

Msamiati
Jumla ya maneno yaliyotumiwa kuafikiana na mada au kichwa kilichopendekezwa, Maudhui na msamiati.
Baada ya kusoma mtungo utafikiria na kukadiria maudhui na msamiati uliomo kwa jumla. Alama za kusahihisha
= Hupigwa chini ya sehemu ambayo kosa la sarufì limetokea
_ Hupigwa chini ya sehemu au neno ambalo kosa la hijai limetokea

√ Hutumiwa kuonyesha msamiati bora

X Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa

Λ Hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno.

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
KARATASI YA 1 - 2013

  1. Mahojiano
    1. Mwanafunzi aandike kichwa kikamilifu, kwa kutaja mahojiano ni baina ya nani na nani.
    2. Ahusishe maelezo kwenye mabano.
    3. Asiwache mhusika mmoja kutawala mahojiano.
    4. Maswali yasiwe ya kumwelekeza mhojiwa.
    5. Mane ya wazungumzaji yaandikwe upande wa kushoto.
  2. Utangamano wa kitaifa.
    Mwanafunzi ashughulikie kila hoja katika aya yake.
    • Elimu
    • Michezo/spoti
    • Michezo ya kuigiza(drama)
    • Dini
    • Ugatuzi wa rasilimali katika kila jimbo/kaunti
    • Kuhimiza ndoa baina ya makabila tofauti.
    • Kupitia kwa vyombo vya habari (magazeti, redio, televisheni)
    • Mikutano ya kuhubiri amani n.k.
    • Kutafuta mbinu ya kupunguza jumbe za chuki kupitia mtandao.
    • Ikiwezekana kutolewe nafasi sawa za kazi kwa jamii zote.
  3. Methali: mwanafunzi athibitishe methali katika masimulizi
    • Sitabiki nyongo harudi haramba.
    • Nyongo – utomvu au maji machungu yaliyomo katika kibofu kidogo juu ya ini.
    • Maana yake – siwezi kutapika nyongo kisha nikarudi nikairamba. Jambo ambalo mtu alilisema hawezi tena akalikana au mtu hawezi kuwa ameiasi tabia fulani kisha airudie.
  4. Insha ya kumalizia. (Mdokezo)
    • . . . Hapo ndipo nilipogundua umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.
    • Yaliyomo kwenye mwili yaoane na maneno yaliyomalizia insha.
    • Mada ikuzwe kikamilifu ili kuibua taharuki.
    • Mbinu za uandishi kama vile methali, tashbihi n.k. zitumiwe kwa njia ifaayo.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest