NIZIKENI PAPA HAPA - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Muhtasari

Nizikeni papa hapa. Haya yalikuwa maneno ya otii mwenyewe. Otii alikuwa akisakatia kandanda timu ya Bandari FC Kwenye uwanja wa manispaa na kote inchini. Wakati huo alikuwa na siha yake na aliishi Mombasa.

Anakutana na Rehema Wanjiru msichana aliyekuwa mrembo Zaidi. Rehema alimwambukiza Otii ugonjwa. Akawa anaendesha akakonda sana na akawa na kikohozi kisichokoma. Ugonjwa huu unampeleka hadi kaburini.

Kabla ya kifo chake, wanachama wa chama cha nyumbani wananza kukutana kwake kupanga mipango ya mazishi. Walihitaji kuchangisha fedha za kukondisha magari yakuchukua maiti na waombolezi kutoka Mombasa hadi sidindi karibu na Kisumu. Otii hakuona umuhimu wa safari hii ya kutoka Mombasa hadi sidindi.

Anapendekeza azikwe hapo Mombasa. Hakuna anayesikiza ombi la Otii. Wanasisitiza lazima {azikwe]maiti ya Otii angepelekwa Kisumu kulingana na mila na desturi zao. Jamaa na marafiki na watu wa nyumbani lazima waandamane kupeleka maiti Kisumu.

Walipofika mtito Andei wanakabiliana na Lori refu ambalo lilikuwa likija kasi huku linayumbayumba barabarani. Dereva wa matatu iliyokuwa imebeba maiti alijaribu kukikwepa kichwa cha lori lakini hakufanikiwa. Watu arubaini walifariki hapo papo . Wengine kumi na watatu walijeruhiwa, baadhi yao vibaya sana.


Yote haya yalisababishwa na kupuuza. wangemsikiliza otii mambo hayangeishia vile;

 Anwani

Anwani ya hadithi hii nizikeni papa hapa inaoana na yale yaliyomo. Hili lilikuwa ni pendekezo la Otii kuwa akifa maiti yake isisafirishwe hadi Kisumu lakini azikwe papo hapo Mombasa.Dhamira (Lengo)

 1. Mwandishi anakusudia kuonyesha umuhimu wa uhusiano katika kufanya mambo
 2. Anadhamiria kukashifu mapenzi ya kiholela na kutuonyesha athari zake. Mf uhusiano kati ya Otii na Rehema Wanjiru.
 3. Mwandishi alidhamiria kuonyesha ukweli wa methali asiyesikia la mkuu huvunjika guu.


Maudhui

Mila na desturi

Wananchama cha watu cha nyumbani wanasisitiza kuwa lazima otii(maiti) ipelekwe Kisumu kulingana na mila na desturi. Wanasema katika mila na desturi zetu kauli ya marehemu si chochote, si lolote, muhimu ni kwamba sharti mtu wa kwetu azikwe nyumbani.

Ushirikiano/Umoja

Wanachama wa chama cha watu wa nyumbani wanatangamana na kupinga mipango ya mazishi ya oti. Baada ya kifo cha otii, jamaa na marafiki wa watu wa nyumbani ya mazishi walijumuika kwa wingi, katika kitongoji duni cha Kisumu ndogo kupanga mazishi. Kwa pamoja wanachangisha fedha za kununua jeneza, mavazi ya kumvalisha maiti pamoja na fedha za kukodisha magari ya kuchukua maiti nyumbani, siku ya kupeleka maiti nyumbani wanajitokeza kwa wingi.

Ujeuri na athari zake

Wanachama wa chama cha watu wa nyumabani walipoanza mipango ya mazishi na hata kufanya michango ili kugharamia mipango ya kupeleka maiti nyumbani. Otii aliwaambia mara kadhaa wamzike papo hapo Mombasa laikini hawakumsikiza.

Walipokuwa safarini kuelekea Kisumu, kunatokea ajali mbaya ambayo inawaangamiza wengi na wengine wanapata majeraha mbaya. (uk100)

Rafikiye Otii anamtahadhirisha Otii dhidi ya kuwa na uhusiano na wasichana wazuri Zaidi kama Rehema Wanjiru. Otii hakutilia makini hayo. Alisema "pana hasara gani nzi kufia
kidondandani?''Aliendelea na uhusiano huu. Akapata ugonjwa uliompleka kaburini.Sifa za wahusika

Otii

Otii ndiye mhusika mkuu

Mchezaji hodari.

Aliyechezea timu ya Bandari FC kwenye uwanja wa manispaa na kote nchini. Alichezea timu ya taifa Harambee stars wakati alipotambaa jijini Mombasa. UK98 anakumbuka mataifa mengi ya kigeni alikosafiri kwenda kusakata Kabamba kwa niaba ya taifa lake na jukumu la kupeperusha bendera ya nchi yake. Alipokuja tamko la michezo lililonukuliwa gazeti lilikisi fikira za wengi. Pengo la Otii haliwezi kuzibwa.

MBADHIIFU

Wanachama wa chama cha watu wa nyumbani walipokutana kupanga mipango ya mazishi, walikusudia kuchangisha fedha za kununua jeneza, mavazi ya kumvalisha maiti pamoja na fedha za kukodisha magari ya kuchukua maiti na waombolezaji hadi sindindi yeye hakutaka hayo alisema, ' gharama zote hizo za kunipelka sidindi za nini? Lakini wenzake wakasisitiza kuwa gharama hizo ni zao si zake{UK97]

Ujeuri/mwenye mapuuza

Alipotahadharisashwa dhidi yakuwa na uhusiano na huyo msichana mrembo Rehema Wanjiru alipuuza. Hatimaye akaambukizwa ugonjwa uliompeleka kaburini.

Chama cha watu wa nyumbani

Umoja/ushirikiano

Wanashirikiana kuanzia mwanzo hadi mwisho katika kupanga mazishi ya Otii wanachanga pesa, wanakutana kwa Otii na wanafuatana kuelekea sidindi kuhudhuria mazishi ya Otii.

Wanamapuuza

Otii alisisitiza kuwa yeye angetaka azikwe palepale Mombasa lakini wakapuuza. Hatimaye wakapata ajali mbaya sana wakiwa safarini kwenda sidindi kuhudhuria mazishi.

Watamaduni

Wanasisitiza lazima wamzike otii nyumbani kulingana na mila zao. Ni kinyume cha mila na ada zao kumwadia mwenzao kutupiliwa mbali kana kwamba hana kwao.

Wakarimu

Wanahakikisha wamechanga pesa za kutosha kugharamia mazishi ya otii.

Rehema Wanjiru

Ni msichana wa aina yake, mwenye urembo wa kutikisa jiji zima, urembo wa kulikausha bahari, urembo uliompa wasichana wenziwe husuda na wanaume mshawasha Fulani.

Mzinifu

Kuna uwezekano kuwa ugonjwa huu aliupata kupitia tabia ya uzinifu.Mbinu za Uandishi

Chuku(hyperbole)

Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani au kusifu.
Uk 96…. kituamepotelea kwenye kitanda chake( mdogo Zaidi)
Uk 97…..Alipokua anakanyaga ardi mpaka inatetemeka( kwa nguvu kutokana na afya nzuri)
Uk 100.. urembo wa kulitikisa jiji zima( mrembo sana)
Uk 101.. pengo aliloacha otii haliwezi kuzibwa( mchezaji stadi)
Uk 102.. wanahabari waliotiwa mbinu ya kupiga picha hawakuweza kula nyama tena mazishini mwao.

Istiara

Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja.
Uk 96….. kabakia sindano (ameendelea sana)
Uk 96 wanamwita mbu ( mdogo Zaidi)

Tashbihi (simile)

Ni mbinu ya lugha unayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha, kama mithili ya, sawa na ja;
Uk 98. Hakuweza kunyanyuka pale chini alikoabwagikie kama gunia la chumvi.
Uk 99…. Alikuwa ametupwa kama masimbi yabuzaa
Uk 102…. Akajaribu kukwepa kichw acha hari kilichokua kimemkodolea macho kama simba wa Hifadhi ya Wanyama ya Tsavo.

Jazanda:

Kutumia maneno yaliyo na maana fiche.
Uk 96…jamaa zake si watu wa kusubiri mvua kunyesha ndipo waanze kutafuta pahali pa kununua mwavuli..(jeneza)
Uk 98…. Alikua mwibe.
Uk 97,,, mbwa( kitu kisicho na thamani)
Uk 100… pana hasara gani nzi kufia kidondani.

Utohozi

Ni mbinu ya kuwahilisha maneno ya lugha yatamkike kama ya
Kiswahili.
Uk 98…. Manispaa(Municipal)
Uk 98…..mechi(march)
Uk 99 eksirei(xray)
Uk 99… klabu (club)
Uk 96 fremu

Msemo

UK 97… Anapiga chafya.
Uk 99…. Akichungulia kaburi.
Uk 99…..Hawakujali hawakubali.
Uk 99….kufumba na kufumbua.
Uk 100..akapigwa na butwaa.

Tashhisi/Uhuishaji.

Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye
UK100 urembo wa kulikaulisha bahari.
Uk.101.sifa za kibroda waombolezaji na kutapika wengine.
102 akajaribu kukikwepa kic hwa c ha lori kilic hokuwa kimemkondolea macho.

Methali

Uk.99. Mwacha kile hanacho na chema kimpotele.
Uk.99.aliyeumwa na nyoka akiona ungongo hushtuka.

Tabaini

Ni tamathali ya semi ambayo kwayo maneno/mawazo yanayokinzana hutumiwa katika sentensi ili kuleta msisitizo wa wazo.
UK99.si barabara ya mlango wa papa ,si barabara ya Nkrumah, si barabara ya jomo Kenyatta, si ya Digo
UK100..Si kuendesha, si kukonda, si vipele si si kukichwa kukikokome….

Mbinu rejeshi

UK96….Ukutani kumetundikiwa fremu yenye picha yake alipokuwa bado na siha yake alipokuwa akisakatia kandanda timu ya bandari FC.
Uk95…anakumbuka jinsi alivyokuwa akiwala chenga wachezaji wa timu pinzani.Maswali

 1. Anwani Nizikeni papa hapa ni mwafaka kwa hii hadithi. Fafanua.[al 20]
 2. Anzeni mapema kuchangisha fedha za kusafirisha maiti.
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. [al 4]
   Haya ni maneno ya mwenyekiti wa chama watu wa nyumbani walikuwa kwa Otii kando ya kitanda cha Otii ili kupanga mikakati ya mazishi. Hii ilitokea baada ya daktari kuwaeleza wamrejeshe Otii nyumbani kwa kuwa hakukuwa na matumaini ya kupata afueni.
  2. Walihitaji pesa za nini? [al 4]
   Walipaswa kununua jeneza,mavazi ya kumvisha maiti pamoja na fedha za kukodisha magari ya kuchukua maiti na waombolezaji kutoka hapa Mombasa hadi Kisumu asilia.
  3. Kwa kurejelea hadithi ya nizikeni papa hapa , eleza maafa yanayotokana na ujeuri na mapuuza.
   Wanachama wa chama cha watu wa nyumbani walipoaanza mipango ya mazishi na kufanya michango ili kugharamia mipango ya kupeleka maiti ya Otii nyumbani. Otii alipendekeza azikwe pale Mombasa lakini hawakumsikiza kabla ya Otii kukata roho.
   Pia aliwakumbusha pendekezo lake la kuzikwa pale Mombasa, lakini bado hawakutilia pendekezo lake maanani. Walipokuwa safarini kuelekea Kisumu walipata ajali mbaya ambayo iliangamiza wengi na wengine wakapata majeraha mabaya. Wangemsikiliza Otii hawangepanga safari ya kwenda Kisumu na basi hakungekuwa na ajali hii ambayo ilileta maafa Zaidi.
   UK100….Rafikiye Otii anamtahadharisha Otii dhidi ya kuwa na uhusiano na wasichana warembo kama Rehema Wanjiru lakini Otii alipuuza.
   Aliendelea na ule uhusiano akaambukizwa ugonjwa uliompeleka kaburini.
 3. Methali ni nini? Taja na ufafanue methali zilizotumwa katika hadithi ya mama bakari.
Join our whatsapp group for latest updates

Download NIZIKENI PAPA HAPA - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest