TULIPOKUTANA TENA - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Muhtasari

Hadithi hii inasimuliwa na Sebu, Msimulizi akiwa mkewe pamoja na rafikiye Kazu aliyekuwa na mkewe pia, walikuwa kwenye Hoteli Rombeko. Marafiki hawa walikuwa na mazoea ya kukutana kila mara walipopata wakati, kwa lengo la kubadilisha mazingira.

Kutokana na mazungumzo yao,ni bayana kuwa marafiki hawa ni watani. Utani wao unawajumuisha wote wanne bila kuudhika huku wakijihusisha jamii zao.

Siku hiyo walizungumzia kuhusu uchawi. Vicheko vyao vilidhihirisha uhusiano mwema, hali hii inaonyesha mlahaka uliokuwepo baina wane hao.
Mazungumzo yalibadilika pale msimulizi alirejelea maisha yake ya awali ambapo alikuwa na kumbukizi ya rafiki yake wa utotoni kwa jina Bogoa.

Msimulizi anasema kuwa yeye Bogoa waliyafanya mengi ya utotoni lakini walitengana baada ya kuhitimu miaka 19 mwaka wa 1966.

Kazu anazungumzia kuhusu Bogoa aliyetoka sehemu za mate. Anaelezea kuwa Bogoa alijifuza usonari na alikuwa akikifahamu kitinya kama lugha Yake mwenyewe. Inasadifu kuwa
Bogoa wanaye mzungumzia ni yuyo huyo mmoja.

Hofu ya Sebu ilikuwa uwezekano wa Bogoa kukubali mwaliko kwa sababu anavyotueleza msimulizi ni kuwa aliipuuza nchi yake na hata kuwasahau wazazi wake. Miradi yao ilikuwa wakutane club Pogopogo,kwa watu wa kupata cha chini.

Bogoa alimtambulisha mkewe Sakina kwa rafiki yake Sebu naye akamtambulisha Bogoa kwa mkewe Tunu. Bogoa anaturejesha katika maisha yake kwa uchungu mwingi. Ilikuwa ni hadithi ambayo hakuwa amemsimulia yeyote hata mkewe.

Anayakumbuka maisha aliyoyapitia kwa mlezi wake. Alinyimwa hata uhuru wa kucheza na badala yake akafanya ngumu.
Wazazi wa Bogoa wanaonyesha hali ya kutoajibika majukumu yao kama wazazi. Hawakuwa na wakati na mtoto wao hata baada ya kumuachia mle hawakufaidia maisha yake. Bogoa anabaki kuwa na kisasi kuwa na kisasi na wakazi wake.



Dhamira

Mwandishi anawakashifu wazazi ambao hawayatekelezi majukumu yao ya uzazi. Wengi wa wazazi wanawaachia walezi majukumu yote bila kujali hisia za watoto wao.
Bogoa utotoni anayapitia maisha magumu na hakuwa na wakumwelezea madhila aliyoyapitiaila ila tu aliangalia ndani kwa ndani. Hali hii inapalilia kisasi dhidi ya wazazi wake.



Maudhui.

Ulezi

Jukumu la kila mzazi ni kumlea mtoto kwa njia ifaayo na kuyatekeleza mahitaji ya huyo mtoto. Jambo la msingi ni kumwelimisha na kumpatia mashauri. Wazazi wa Bogoa waliyakwepa majukumu yao na kumtwika mlezi ambaye alimdhulumu mwanao. Malezi hayo yanamfanya Bogoa kulipiza kisasi dhidi ya wazazi wake hata wanapoaga dunia hakuhudhuria mazishi yao.

Ukatili

Sinai alimtendea ukatili Bogoa kwa kumnyima fursa ya kucheza na wenzake. Fauka ya hayo alimpiga pindi tu alipochelewa kurudi. Babake Bogoa aliutenda unyama kwa kumpeleka
mwanawe kwa mlezi bila kufuatilia maisha yake yalivyokuwa kwa mfadhili wake.

Elimu

Elimu ni mwanga kwa kila mja. Njia moja ya kuelimika ni kwa kupelekwa shule. Hata hivyo kuna elimu inayopitishwa na wanamrika(peer);mfano:Sebu alimfunza Bogoa kusoma mpaka akaweza kusoma hadithi nzima.

Kulikuwa na mtazamo hasi kuhusu watoto wa kimaskini ambao ilisemekana kuwa hawastahili kusoma shuleni. Mtoto ambaye hakwenda shule alidhaniwa kuwa mtoro.

Umaskini

Sababu kuu ya umaskini kulingana na mwandishi ni idadi kubwa ya watoto. Wazazi wa Bogoa walikuwa na watoto takribani kumi na sababu ya kumpeleka Bogoa kwa mlezi ilikuwa ni kutowamudu.
Ishara ya umaskini inadhihirishwa na vazi alilovalia msimulizi anasema . "Kilikuwa ni kivazi pekee cha mtungini kwangu''.

Hawakuwa na fedha hata za kununulia viatu. Vile vile hakuwa na pesa za kulipia nauli ndiyo maana walitembea kutwa hadi jijini.

Urafiki

Urafiki wa marafiki haya ni wa dhati. Marafiki hawa walikuwa wanakutana si mara moja kwani anasema kuwa …….` tulipenda kuja seka kubadilisha mazingira na kuonana na marafiki zetu . ” … ( UK 104 ) . Kwa kuwa walikuwa marafiki wakubwa, waliwahusisha wake zao. Ni kutokana na mojawapo wa mikutano yao. Kazu anapomtaja Bogoa. Kutajiwa Bogoa kunaleta kumbukumbu katika mawazo ya Sebu. Anamkumbuka rafiki yake wa utotoni. Kutokana na mjadala ule ndipo wanapokutana tena.

Maudhui mengine:

  1. Ukandamizaji wa watoto
  2. Uchawi
  3. Bidii
  4. Uwajibikaji
  5. Uhuru wa watoto
  6. Nafasi ya wazazi katika malezi.


Wahusika.

Sebu

Huyu ndiye msimulizi, jina lake halisi tunalitambua kutoka kwa wahusika wengi kama Kazu na Mkewe.

Mtani

Sebu pamoja na rafikiye wanataniana kwa kiwango kikubwa bila kuudhika. Ni watani wa muda mrefu kwa sababu wanataniana kuhusu jamii zao.

Ana mlahaka mzuri

Kutokana na mazungumzo yao tunaelewa kuwa uhusiano wao ni mzuri. Anatueleza kuwa huwa wanakutana pindi wanapopata upenyo. Hali hii ndiyo iliyomfanya kuwa na uhusiano mwema.

Mwaminifu

Bogoa alimwaamini tangu wakiwa watoto.

Bogoa.

Rafiki wa utotoni wa msimulizi.

Msiri;

Hakumwelezea Sebu shida alizokuwa akizipitia kwa mlezi wake. Hakuwaelezea wazazi wake madhila aliyokuwa akiyapitia. Wanafunzi wenzake hawakujua asili yake kwa maana hakuwaelezea walibaki tu kukisia.(UK 116)

Mvumilivu;

Aliyavumilia mateso kutoka kwa mlezi wake. Katika umri wake mdogo alifanyishwa kazi nyingi zilizopita umri huo. Kama anavyoeleza ni kuwa angechelewa,alitafutwa na kupigwa vibaya sana..(UK 116).

Mwenye Bidii;

Licha ya kupitia madhila hayo, Bogoa alikuwa mwenye bidii. Alijifunza kazi ya usonara na kuajiriwa.

Amewajibika;

Aliwajibikia jamii yake na ndoa yake ilikuwa imesimama imara, zaidi ya hayo ni kuwa watoto wake walikuwa wamekomaa.

Mwenye Kisasi;

Alikasirika kiasi cha kutorudi kwao tena,Hata mazishi ya wazazi wake hakuhudhuria. Alikuwa na kisasi na wazazi wake.



Matumizi ya lugha

Tashbihi

Tamathali ya usemi ambayo msanii huvilinganisha vitu viwili au zaidi kwa kutumia maneno ya kulinganisha kama vile:Mithili
ya,sawa na,ja,na mfano wa:
· Kubadilika mara moja kama uso wa mtoto mchanga(UK 109)
· Kumtoka kama maji yanavyotiririka bombani.

Uhuishi

Uhuishi/Tashihisi/Uhaishaji ni tamathali ya usemi ambayo msanii huvipatia vitu visivyokuwa na uhai sifa walizonazo binadamu na kutenda kana kwamba vina uhai.
- Vicheko vilivyovuma na kuparamia kuta.(UK 107). Vicheko vinapatiwa sifa ya binadamu ya kuparamia kuta.

- Kuikimbiza furaha na kuileta huzuni(UK 109)

- Ukweli wenye makali yanayochinja bila huruma (UK 117)

Nidaa

Ni msemo unaoonyesha kushangazwa na jambo Fulani na huambatana na alama ya mshangao.
…….na kuwatema watu hao huko magharibi!(UK 105)
……mimi ni binadamu mwenzako!(UK 105)
…..hatukupata hata fununu ya kuwepo kwake(UK 110)

Maswali ya balagha

Haya ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika na hayahitaji majibu ya moja kwa moja.
a) …..huoni kwamba unaniumiza?(UK 105)
b) …..uchawi si sayansi?(UK 106)
c) ……kabadilika vipi? (UK 111)

Semi

Haya ni mafungu ya maneno ambayo yanapotumika,hutoa maana nyingine badala ya ile ya maneno yaliyotumika. Hutumika ili kuipamba lugha.

Kuna:

Nahau

Huu ni usemi unaotumia maneno ya kawaida kwa lengo la kuleta maana iliyo tofauti na maneno hayo yaliyotumiwa. Tofauti na msemo huwa na vitenzi.
a) Napiga funda (UK 106)
b) Kupiga funda (UK 114)

Misemo

Hizi ni semi fupi fupi zinazotumiwa mara kwa mara kwa lengo la kuleta maana maalum.
Mfano;
Pua na mdomo(UK 108)

Join our whatsapp group for latest updates

Download TULIPOKUTANA TENA - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest