MWALIMU MSTAAFU - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Muhtasari

Mwalimu Mesi ndiye mhusika mkuu katika hadithi hili. Anwani hii inafaa kwa sababu hadithi inaelezea kuhusu maisha ya Mwalimu Mesi Kabla na baada ya kustaafu.

Kutokana na kuwajibika kama mwalimu,Mwalimu Mesi alipewa sifa chungu nzima. Aliweza 'kuwafinyanga' wanafunzi wake mpaka hatimaye wakawa watu wa kutajika. Wengine wakawa mawaziri, wabunge, marubani, wahandisi, madaktari na wengine wahasibu.

Siku ya sherehe ya kumuaga shuleni,wazazi wa wanafunzi wa zamani na wampya walihudhuria na kumletea zawadi za aina tofauti tofauti. Hotuba zilizotolewa zilisheheni sifa isipokuwa hotuba ya Jairo iliyokuwa ya kumlaumu tu Mwalimu Mesi.

Jairo alikuwa zuzu hata darasani , anamlaumu mwalimua eti alimpotezea muda wake na ndio kwa sababu yeye ni maskini.

Mwalimu anampa Jairo zawadi zote lakini Jairo hana shukrani. Anakiona hicho kitendo cha kupewa zawadi kama kuaibishwa na Mwalimu. Jairo anawaleta mke na watoto wake kwa mwalimu kama zawadi. Mke wa Jairo alipewa nyumba kwenye kichumba cha mwalimu na akakaa na watoto wake.

Jairo hakuwapitia kwa Mwalimu Mesi kuwaona jamaa yake hadi siku alipofikiwa na tetesi kuwa mwalimu amemwoa bintiye. Kumbe ilisadifu kuwa mwalimu na kile kisichana walipoandamana kwenda kununua kitabu mjini, mwalimu akawa mgonjwa na Yule msichana akapelekwa shule ya bweni. Ilikua ni sababu tosha ya wenye umbeya kueneza uvumi kwa mwalimu na bintiye Jairo. 

Hawakuonekana na ni kwa sababu wameanza kuandika kurasa mpya za maisha yao pamoja.



Anwani

Anwani hii MWALIMU MKUU inafaa kwa sababu hadithi mzima inazungumza kuhusu maisha ya Mwalimu mstaafu Mesi.



Dhamira

  1. Mwandishi alikusudia kuonyesha umuhimu wa kuwajibika kazini kama alivyowajibika Mwalimu na mazao ya kazi yake yanaonekana.
  2. Mwandishi pia anadhamiria kuonyesha tofauti ya watu wa elimu maishani. Kuna tofauti ya watu waliosoma na wale ambao ni zuzu kama Jairo.


Wahusika

Mwalimu Mesi

Amewajibika

Kutokana na kule kuwajibika, anapewa sifa chungu nzima. Wanafunzi wanaishia kuwa madaktari,, mawaziri, marubani n.k. Wengi wanahudhuria sherehe yake ya kumuaga na kumletea zawadi nyingi kama ishara ya shukrani.

Karimu

Anampa Jairo zawadi Zote alizoletewa katika sherehe ya kumuaga.
Anakubali mke na watoto wa Jairo waishi kwake.
Kisichana cha Jairo kilipofukuzwa shuleni kwa kukosa kitabu, waliandamana hadi mjini kukinunulia kitabu.

Mwenye utu/ubinadamu

Anaamini watu wote ni sawa, hakuna mtu nusu mtu.
Anasisitiza watu ambao hawakuja kwa magari mazito pia wapewe nafasi ya kutoa hotuba walivyopewa wengine wa tabaka la juu.
Jairo anapotoa hotuba yake, alimlaumu tu Mwalimu lakini hilo halikumkera Mwalimu. Anampa Jairo zawadi zote, anaamini jairo alizihitaji zaidi.

Mwenye sifa tele

Uk 120…Wanafunzi wake wote hao hawamsahau kwa nasaha zake, kwa insafu yake, kwa huruma yake, kwa hekima yake,kwa ustaarabu wake,kwa uadilifu wake ,kwa uwajibikaji wake, kwa nemsi yake,kwa ucheshi wake.
Hotuba zao zilijaa sifa tele.

Jairo

Alikua mwanafunzi wa Mwalimu msaafu ambaye mambo hayakumwendea vizuri.

Mwenye Kulaumu

Jairo alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Mwalimu Mstaafu. Yeye ni tofauti na wengine wengi, aliishia kuwa mtu ovyo. Hali yake ya umaskini inamfanya amlaumu Mwalimu eti alipotezea wakati kwa kumueka darasani na kumpa tumaini za uongo.

Zuzu

Hata baada ya kuwa shuleni kwa miaka yote ile hakuweza kuunga moja na moja. Pia alipata sufuri masomoni.

Mcheshi

  1. Haelewi kwa nini Mwalimu alimshauri asilewe ilhali anaamini tembo inampa raha ya kuishii. Alisema kuwa alipolewa hata akitembea bila viatu na kujikwaa au kudungwa na miiba, hakuhisi kitu.
  2. Hakuelewa pia kwa nini kuepukana na ulevi, kusubiri hadi ndoa ndipo 'kuchana ngazi.'
  3. Anapeleka mkewe na wanawe kwa Mwalimu na kumpa kama zawadi.

Mke wa mwalimu

Mwenye utu

Anakubali mke wa Jairo na wanawe waishi kwao. Anamtunza kama bintiye. Anamwambia , “Hapa paite nyumbani. Upaone hapa kwenu kama si nyumbani pako. Ukae upumzike. Ukae uone raha ya kuishi.”

Mwenye bidii/Anauhusiano mzuri na watu

Wanaandamana na mke Wa Jairo kwenda kondeni kupanda mbegu, kupalilia, kumwagia mazao kondeni mbolea. Pia walienda kuteka majina kutafta kuni . Walichuma kunde na
mchacha, mabenda kondeni wakiziambua na kuzikata mboga hizo pamoja pale uani.

Mke wa jairo

Mvumilivu

Mwandishi anaeleza maisha ambayo mkewe Jairo ameyapitia. “Katika maisha yake na Jairo, ameonja ladha zote za dhiki, thakili, bughudha na kero. Hakuna mwanamke anayejua kumezamate machungu kama Mke wa Jairo.”

Mtiifu

Anapopelekwa kwa Mwalimu kama zawadi, Mwalimua anamshauri arudi kwake lakini anakataa. Anasema “sharti ni mtii mume wangu. Mume ni mume hata akiwa gumegume.” Mwalimu aliposisitiza, mke wa Jairo alimweleza kuwa hawezi kwenda kinyume na amri ya Jairo mume wake.

Mwenye bidii

Waliandamana na mke wa Mwalimu kondeni kupanda, kupalilia, kuteka maji vijitoni na kutafta kunikuni.

Wanafunzi na wazazi

Ni wenye shukrani

Wanafika katika sherehe ya kumuaga Mwalimu kwa wingi wakiwa na zawadi chungu nzima.

Karimu

Wanamletea Mwalimu zawadi chungu nzima. Wanaendesha magari makubwa na ni waadilifu kwa sababu walifuata ushauri wa walimu wao. Wale ambao hawakupata elimu wameishia kuwa maskini , walevi ambao hawana mbele wala nyuma. Pia hawana maadili mema.

Uzuzu/Ujinga

Hata baada ya kuhudhuria shule ya msingi, Jairo hawezi kuunga moja na moja. Haoni umuhimu wa elimu. Anamlaumu Mwalimu Mesi eti alimpotezea muda wake bure shuleni kwa kumwambia kila uchao kwamba ataimarika na hakuwahi imarika.

Anamlaumu Mwalimu kwa kumshauri asinywe tembo ilhali anaamini hiyo tembo ndio humpa raha ya kuishi. Anaamini kinyume cha nasaha za Mwalimu ndio utamu na uhondo wa maisha.

Uzuzu unamfanya awapeleke mke na watoto wake kwa Mwalimu kama zawadi. Anaona soni kupokea zawadi kutoka kwa Mwalimu. Haelewi mbona akapewa zile zawadi ilhali alizihitaji zaidi.



Maudhui

Kuwajibika

Hii inadhihirika zaidi siku ya sherehe za kumuaga Mwalimu Mesi pale shuleni.
Waliohudhuria sherehe hii walikua wengi mno. Mwandishi asema “walifika kwenye kiambo cha shule kama mashabiki wa mchuano wa soka wa kuwania kombe la dunia kutokana na kazi nzuri ya Mwalimu, wanafunzi wake waliishia kuwa madaktari, wabunge n.k.

Hotuba zilizotolewa zilisheheni sifa kwa Mwalimi Mesi.

Elimu

Mwandishi anatuonyesha umuhimu wa Elimu. Watu waliomakinika katika elimu hatimaye walikuwa 'watu' , wakawa mawaziri,wabunge, marubani n.k. Wakawa pia wanaendesha magari ya nguvu.

Elimu unawafanya watu kuwa watu wa maana, watu bora kwa hadafu. Lakini wale ambao hawakumakinika, hutumia yao duni, maisha ya umaskini. Pia wana mitazamo hasi
kuhusu maisha.

Utabaka

Utabaka unasababishwa na kupata au kukosa elimu. Waliosoma na kufaulu katika elimu, wanaishi kama 'watu'. Wanapata kazi nzuri, zinawapa mshahara.

Ukarimu

Ukarimu unajitokeza wakati Mwalimu Mesi anampa Jairo zawadi zake zote, anasema “mimi nimeamua kwa hiari yangu kukupa wewe zawadi hizi.”

Mwalimu na mkewe (Bi Sera) ni karimu,wanawakaribisha mke na watoto wa Jairo kwao.



Mbinu za Lugha

Kuorodhesha

Mwandishi anatumia mbinu ya kuorodhesha mfano;
Uk 120: Wanafunzi waje wote hao wanafunzi wake hawamsahau kwa nasaha zake,kwa insafu yake, kwa huruma zake, kwa hekima zake, kwa ustaarabu wake, kwa uadilifu wake…
Uk 121:Wanafunzi wake waliokuwa bado wanasoma kwenye shule hiyo waliimba tele, nyimmbo za jamii mbalimbali, wakacheza zeze,mariamba, lelemama, mdundiko, violoni.
Uk 122:…sikwambii haya madude makubwa waliokuja kututisha nayo akina Bariki,Festo, Mshamba ,Nangeto na hali kadhalika.

Tabaini

Uk 124:Si matoroli,si vijiko vikubwa vya kuzola mchanga,si makubadhi ,si meza na samani aina aina, si fedha
Uk 124:Si matoroli,si vijiko vikubwa vya kuzolea mchanga,si makubadhi,si meza na samani aina aina,si fedha.

 

Takriri/Uradidi

Uk 126:Wanafunzi wako wote hao wanafunzi wake.
Uk 128:Jairo aliambiwa , akaambiwa na kuambiwa na wajuao.

Tashbihi

Uk 120:…mvi zimemkaa kwa haiba kama theluji kwenye mlima Kilimanjaro.
Uk 121:…walifurika kwenye kiambo cha shule kama mashabiki wa mchuano.
Uk 122:Kichwa chake chenye upana killing'aa utosini kama sufuria kwenye duka la Buniani.
Uk 125:…wakapokeza hotuba hio kama huizi kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Uk 129:…kimenawiri kama ua linalotimbuka kudamu.
Uk 129:Aliona madodo yamesimama kifuani kama kanzi mbili za mwanamasumbwi.
Uk 129:…kiuno kimechukua umbo mduara kama cha nyigu.

Tashhisi

Uk 120:Alijaaliwa mvi nyeupe zilizojianika kwenye kichwa chake kidogo.

Methali

Uk 121: Anayo maneno ya kuweza kumtoa nyoka pangoni.
Uk 123: : Kuwashia pofu taa si kuharibu mafuta.
Uk 128:Alikuwa ametuma jongoo na mti wake.

Jazanda

Matumizi ya maneno yenye maana fiche.
Uk 121:…wenzao hao waliokuwa wamekua watu.
Uk 121:…lakini nadhani ni jambo la busara kutotia mchanga kitumbua.
Uk 129:Walitafuta kitabu cha maisha na kuanza kuandika kurasa mpya za maisha yao pamoja.
Uk 124:…kusubiri hadi ndio ndipo kuchuna ngozi.

Kinaya

Kinyume cha matarajio
Uk 123: Ni kinaya kwa Jairo hakuona sifa nzuri ya Mwalimu Mesi. Yeye anamuona kama kikwazo kikubwa kwake. Kama yeye Jairo anaishi maisha duni kwa sababu ya Mwalimu Mesi.
Uk 126:Ni kinaya Mwalimu Mesi kumpongeza Jairo kwa hotuba yake kumhusu ambayo ilijaa kumlaumu Mwalimu kisha Mwalimu Mesi anamueleza akifa mwanzo azungumze siku ya mazishi yake.
Uk 126:Ni kinaya Jairo anapopeleka mke wake na watoto kwa Mwalimu Mesi kama zawadi.
Uk 127:Ni kinaya kwa mkewe Mwalimu Mesi (Bi Sera)kumkaribisha mke na watoto wa Jairo kwao “Mwachie akae huyu binti na watoto wake, tutawatunza.”

Msemo

Uk 121:Wanafunzi wake wa zamani waliopewa kisogo na dunia
Uk 126:Hakuna mwanamke anayejua kumeza mate machungu.

Mdokezo/Kauli isiyokamilika

uk 120:kisa na maana ni huyo Mwalimu Mesi.
uk 123:kwamba kuwashia pofu taa si kuharibu mafuta.
UK 125:…umefanya makosa makubwa sana.
Uk 125:…hamna mwendawazimu wala mahaka kati yetu.
Uk 126: “Badala ya ngojera nyingi za huyo anayemwita si siri au siri sijui.

 

Sadfa(matukio mawili yanayotokea kwa pamoja).

Inasadifu kuwa baada ya Mwalimu kuondoka na kile kisichana kununua kitabu hakuonekana tena. Watu wakafikiri eti Mwalimu alikua amekioa kile kisichana.

Kumbe wakati huu Mwalimu alikua akiugua na alikua ndani(nyumbani) wakati wote huo na ndio sababu hakuonekana.



Maswali

  1. Onyesha umihimu wa wahusika wafuatao katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu.
    1. Mwalimu Mesi
    2. Jairo
    3. Mkewe Jairo
    4. Wanakijiji
      (al 20)
  2. Fafanua maudhui yoyote manne katika hadithi hii. (al 20)
Join our whatsapp group for latest updates

Download MWALIMU MSTAAFU - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest