MTIHANI WA MAISHA - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA

Share via Whatsapp


Muhtasari

Je, Samueli alikuwa amepita mtihani wake wa Elimu? Kuanguka mtihani wa elimu ni kuanguka pia mtihani wa maisha?

Samueli ambaye ni mhusika mkuu katika hadithi anaenda shuleni kuchukua matokeo yake ya mtihani. Akiwa pale foleni nafanya moyo wake kwa kuwa alikuwa na uhakika kuwa alikuwa amepita mtihani wake vizuri.

Kule ndani ya ofisi , Mwalimu Mkuu ameketi pale na anapuuza kuwepo kwake ofisini humo. Hatimaye anamtupia Samueli stakabadhi ya matokeo yake.

Samueli anapotambua alivyokuwa amefeli mtihani wake, anamdanganya babake kuwa hakupata matokeo yake kwa dai ya kutokamilisha kulipa karo ya shule.

Samueli haoni haja ya kuishi tena. Anakata kauli kujitosa majini afe. Hakuwa tayari kupata aibu kutokana na matokeo yake mabaya. 

Mamake Samueli ana matumaini kuwa kuanguka mtihani wa elimu si kuanguka mtihani wa maisha. Anamshika Samueli mkono na wanaelekea nyumbani.Anwani

Anwani ya hadithi hii, MTIHANI WA MAISHA inaoana na yale yaliyomo. Kupitia kwa mamake Samueli, mwandishi anaonyesha kuwa kuna maisha hata baada kuanguka mtihani wa elimu. Kuanguka mtihani wa elimu sio kuanguka mtihani wa maisha.Dhamira

Mwandishi alikusudia kuonyesha;

 1. Kuanguka mtihani wa elimu sio mwisho wa maisha. Bado kuna matumaini.
 2. Umuhimu wa kumakinika katika masomo kwani athari za kuanguka mtihani ni hasi.


Maudhui

Ukatili

Samueli analinganisha babake na hayawani ambaye anaweza kumrarua mtu na kumla mzimamzima. Samueli alipofeli mtihani wake, anavunjika moyo na kuona maana ya kuishi.

Anakata kauli ya kujiangamiza kwa kujitosa majini. Babake hata baada ya kumuona mwanawe katika hali ya kuvunjika moyo, hakumhurumia, badala yake anaamrisha watu wamuache ajitose majini afe. Pia anampa kamba atumie kujitia kitanzi.

Ucheshi

Samueli ni mcheshi. Anachekesha anaposema udongo uliowaumba babake na mamake ni tofauti na ndio sababu mama angeweza kuelewa kidogo atakapojua amefeli mtihani lakini baba hawezi.

Anapomwangalia Mwalimu Mkuu, anamwona ni kama aliyezidiwa na maumivu au anayepaswa kufanyiwa oparesheni ya ubongo na anayehitaji maombi.

Anapoamka kuchukua hatua ya kujiangamiza, anatazama juu kumpasha Muumba wake ujumbe kuwa alikuwa njiani akielekea mbinguni. “Naja huko juu mbinguni mapena kidogo Baba. Nitengee nafasi. Nimeruka foleni…”

Nafasi ya Mwanamke

Mwanamke anapuuzwa katika jamii hii. Inathibitishwa na mtazamo wa baba kupitia elimu. Ingawa baba aliyaonea fahari mafanikio ya binti zake, aliwaona kama wanawake tu.

Fahari yake ya dhati ilikuwa katika kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu. Samueli haamini vipi angeweza kushindwa katika mtihani na dada zake ilhali ni wanawake.

Mwanamke kupitia kwa mhusika mama amechorwa kama aliye na utu na matumaini. Anamshika Samueli mkono na kumwambia waende nyumbani na kumweleza maneno ya kumpa tumaini. Pia anapenda amani na ni mshauri mwema. Anamshauri mumewe aende shuleni wasuluhishe sintofahamu kuhusu karo.

Kufa moyo/kuvunjika moyo

Samueli alipoanguka mtihani hakuona haja ya kuendelea kuishi na anaamua kujitosa majini afe. Anasema, “Acha nijiondokee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe.” Katika ujumbe wake na Muumba anasema itabidi aende mbinguni kwa sababu stahamala zimekwisha.

Elimu

Elimu ni muhimu maishani. Wasichana katika jamii hii wanafanya vizuri kuliko wavulana. Wavulana wanamchezo shuleni (Mahoka) unaochangia kuanguka kwao.

Hakuna anayepewa matokeo yake ya mtihani kabla ya kumaliza kulipa karo. Athari za kuanguka mtihani ni kama vile aibu na hata kujiangamiza.Wahusika

Samueli

Ndiye mhusika mkuu

Mcheshi

Anaposema, “labda Mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu. Labda anapaswa kufanyiwa operesheni ya ubongo ama anahitaji maombi hasa atakuwa na akili razini tena.”

Samueli anasema kuwa mamake na babake wameumbwa kwa aina tofauti kabisa ya udongo.

Anamuarifu Muumba kuwa yumo njiani akienda mbinguni basi atengewe nafasi kwani ameamua kuruka foleni.

Mwenye Matapo

Anaposema yeye hana moyo wa bua. Kile asomacho ndicho kijacho kwenye mtihani.

Anaelewa kuwa yeye si mwerevu sana lakini anajua kupanga mikakati na pia anaamini ana bahati ya mtende anaamini kuwa amepita mtihani wake vyema na kuwa motokeo yake yangemshtua Mwalimu mkuu ambaye hakuwa na imani naye.

Mwongo

(uk 137) Samueli anamdanganya babake kuwa hakupata matokeo yake kwa sababu hakuwa amemaliza kulipa karo.

Mwoga

Uk 133: Anaogopa anapoingia katika osi ya Mwalimu mkuu. Woga unajitokeza kutokana na anavyozungumza/anasitasita. “Mwa…limu nimekuja kuchu…chukua matokeo…” “samaha…ni. Waa…zazi wangu.”

Samuel anatetemeka anapomwona babake pale kwenye bwawa(uk 132)

Mwenye machoka

(uk 134)ni kutokana na tabia hiyo pale shuleni ndipo akapewa jina 'Rasta'

Kufa moyo/kuvunjika moyo

Kuanguka mtihani kwa Samwueli si jambo alilokuwa akitarajia. Alikuwa ana uhakika kuwa amepita mtihani wake. Jambo hili ameliona kama la kumletea aibu mbele ya wazazi wake, alivyopendekeza Samueli.

Anakata kauli kujitosa majini afe. Hakuna maana ya kuuendelea kuishi. Anasema “Acha nijiondokee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe anamwambia Mungu kuwa amekosa stahamala.”

Mamake Samueli

Mwenye utu

Mamake Samuel anafika kwenye bwawa la maji alipokuwa amejitosa Samuel, anamshika Samuel mkono na kumwomba waende nyumbani. Anamwambia Samuel maneno ya kumpa moyo, “huwezi kushindwa na mtihani wa shule na vilevile kushindwa na mtihani mwisho.

Mwenye Matumaini

Hata kana kwamba Samuel ameanguka mtihani wa shule, mamake Samuel anaamini kuwa kuna matumaini hata baada ya kuanguka mtihani huo. Anaamini Samuel hajaanguka mtihani wa mwisho.

Anaamini pia kuwa Mungu hamkoseshi mja wake yote. (UK 139)

Mwenye Kuelewa Mambo

Samuel anasema kuwa kweli amemusaliti mamake kwa kuanguka mtihani lakini mamake tofauti na babake, ataelewa.

Mpenda Amani

Samuel anapomdanganya babake kuwa hakupata matokeo ya mtihani wake ati kwasababu hajamaliza kulipa karo, anakereka.

Mamake Samuel anaingilia kwa upole na kumshauri mume wake amuone Mwalimu mkuu ili wasuluishe suitofahamu hiyo.

Baba Samueli

Katili

Samueli anamlinganisha babake na hayawani ambaye anaweza kumrarua mtu na kumla mzimamzima.

Baada ya Samueli kuanguka mtihani alikuwa na kipindi kigumu na anaamua kujiangamiza. Babake hakuwa na huruma naye hajali kama atajitosa maji afe. Anasema “mnamzuia kwa nini? Mwachie ajitose majini kama anataka. Ana faida gani huyo? Sikuzaa mwana nilitoa tu maradhi tumboni.” Uk 139

Anampa Samueli kamba aitumie kujiangamiza.

Mwenye moyo mgumu

Babake Samueli ana moyo usiojua kusamehe. Anaamrisha watu wamuache ajitose majini afe. Anampa Samueli kamba ajitie kitanzi ikiwa anaogopa kujitosa majini. Samueli anasema kuwa mamake ataelewa atakapojua kuwa Samueli amefeli mtihani, lakini babake aliyeumbwa na udongo tofauti hawezi.

Amewajibika

Aliweza kulipa karo yote ya shule.

Mwalimu mkuu

Mwenye madharau

Samueli alipoingia katika ofisi yake, anachukuwa muda mrefu sana kuinua uso wake kumuangalia Samueli. Baada ya kuzichambua zile stakabadhi za matokeo, anatoa moja na kumtupia Samueli. Anamtupia kwa mtu anavyomtupia mbwa mfupa.

Amemakinika kazini

Hakuamini Samueli alipomwelezea kuwa amekamilisha kulipa karo, alitumia “daftari la karo” kuhakikisha. Anasema mali bila ya daftari hupotea bila ya habari. Ndio maana ameweka daftari la kuweka kumbukumbu ya wanaodaiwa karo na waliolipa karo.Mbinu za Uandishi

Tashbihi

Uk 131:waliokuwepo waliotoka wamenywea kama kuku walionoa maji ya mvua.
Uk 132:akitoka ndani atakuwa akitembea kama fahali.
Uk 131:amamtupia kama mbwa anavyomtupia mbwa mfupa.
Uk 137:anamuona baba akilini kama hayawani.
Uk 135:imekwenda kama chendacho kwa mganga kisichokuwa na marejeo.

Tashhisi/uhaishaji/uhuishi(personification)

Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai(sifa za kibinadamu).
Uk 134:Nzi wa kijani ya samawati waliokula wakashiba.
Linampokea kwa vilio nao mnuko kwa kughasi unampokea kwa vigemo.
Uk 135: Safu safi ya D na E ilimkodolea macho bila kupesapesa.
Uk 137:Ilimuradi mawazo yana mwadhibu sasa.
Uk 138:Alitupia jicho safu ya maji akaona yanasumbuka na kuhangaika.

Msemo

Uk 132:Uso wake wenye makunyanzi ulipiga mapeto.
Uk 133:Anakitazama kidole cha Mwalimu mkuu kupiga masafa.
Uk 135:Juhudi zake zimegonga ukuta.
Uk 137:Nina kuambulia patupu.
Uk 139:…huhu kila mtu akipigwa na kibuhuti.

Kichanganya ndimi

Kutumia zaidi ya lugha moja tofauti.
Uk 132:come on :yes

Utohozi

Kuswahilisha maneno/kutamka maneno yasiyo ya Kiswahili kama ya Kiswahili.
Uk 133: Bodi,operesheni.

Maswali balagha

Maswali yaliyoulizwa bila ya kutarajia majibu.
Uk 131: Mtu angesemaje ati? Wanafunzi na wakati huo huo wanasononeka?
Uk 133: Nazo fedha ulitoa wapi mtoto pale ulipo.
Uk 135: Karo yote niliolipa iwe bure? Pesa aliyolipa baba tusome imekwenda bure?
Uk 136: Ali umefeli mtihani ? sasa nitafanya nini?

Methali

uk 132:Mdharau biu hubiuka.
uk 132:Usione wembamba wa reli kwani gari moshi hupita juu yake.
uk 135:Imekwenda kama kiendacho kwa mganga kisichokua na marejeo.
uk 139: Mambo ni kuganga huenda yakaja.

Uzungumzi nafsia

Mhusika hujizungumzia ama kwa kuongea au kuwaza bila kukusudia kusikika na yeyote.
Uk 132:mimi tangu hapo najijua bwana. Sina moyo wa bua. Mtihani haunibabaishi sana.
Uk 132:hajawai kuniamini huyo hambe. Lakini mimi mwenyewe najiamini. Lazima mtu ajiamini… au sio?
Uk 135: Hivyo ndivyo kusema lolote wala chochote . kwamba mimi si lolote wala chochote. Kwamba mimi si chochote wala lolote katika medani ya masomo?

Mdokezo/usemi usiokamilika

Uk 132:tena angaa sikukutana na paka mweusi njiani siku zote za mtihani...
Uk 133:…chukua matokeo…
Uk 135:si mjinga mimi. Najua vitu vingi tu…
Uk 136: Mama ataelewa lakini baba…

Sadfa

Matukio mawili au zaidi yanayotokea kwa pamoja bila ya kupangwa.
Uk 135:Ilisadifu kuwa siku na wakati ambapo Samueli alitaka kujitosa majini ili afe, siku hiyo ilikua tofauti kwani wachunga wapitia hapo wakiwapeleka mifugo malishoni hawakuwepo. Ikawa rahisi kuweko kujitosa majini.
Uk 138: Inasadifu pia kuwa baada ya Samueli kujitosa majini na kupiga mikupuo kadhaa ya maji, mwanamume mmoja akawa ameachwa na basin na akaamua kutumia njia karibu ya kamwokoa Samueli.

Taharuki

 1. Kuna wanafunzi waliotoka ofisini mwa Mwalimu mkuu wakiwa na furaha na huku machozi yanawatoka. Msomaji anabaki hata hamu ya kujua ikiwa walikuwa wamepita mtihani au la.
 2. Msomaji pia angetaka kujua ikiwa Nina alimuacha Samueli kutokana na vituko vyake au la.
 3. Msomaji anabaki na hamu ya kutaka kujua maisha ya Samueli yaliendelea vipi. Je alifaulu maishani. Baba alibadilika na kumsamehe .
 4. Kuanguka mtihani wa elimu na kuanguka mtihani wa maisha?


Maswali

 1. Andika sifa za wahusika hawa kama zinavyojitokeza katika hadithi ya mtihani wa maisha.
  1. Samueli
  2. Babake Samueli
  3. Mamake Samueli
  4. Mwalimu Mkuu
 2. Jadili nafasi ya mwanamke katika hadithi ya Mtihani wa Maisha.
Join our whatsapp group for latest updates

Download MTIHANI WA MAISHA - Mwongozo wa TUMBO LISILOSHIBA.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest