KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2017 MURANG'A MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

SEHEMU A:KIDAGAA KIMEMWOZEA – KEN WALIBORA

 1. Lazima
  Kwa kutoa mifano, fafanua maudhui ya utu kama yanavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea. (al. 20)

SEHEMU B:MSTAHIKI MEYA – T AREGE
Jibu swali la 2 au 3

 1. “Mwaka wa kuomba kura utakapofika sitataka mizuka yao kuniandama.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
  2. Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili (al.2)
  3. Ufisadi uliokithiri ndio uliokuwa msingi wa matatizo ya cheneo. Thibitisha kwa mifano mwafaka(al. 14)
 2. “Majuto ni mujukuu huja baadaye.” Thibitisha ukweli wa methali hii ukitoa mifano kutoka kwenye tamthilia ya mstahiki Meya. (al. 20)

SEHEMU C: USHAIRI

 1. SHAIRI

  Hayawihujayakawa, walinena wanenaji
  Nyuma walotakwa kuwa, wakawa ndo wajuaji
  Nao mbele walokuwa, wakazikosa soseji
  Hufika ya wanenaji, hayawi huja yakawa.

  Mwendo usimwone waw, damu yake sileleji
  Kwa watu akikosewa, kwamba hajipi ujaji
  Kimya kikuu angawa, kishindo ukitaraji
  Hufika ya wanenaji, hayawi huja yakawa.

  Hawanacho walokuwa, huja kuwa wasemaji
  Wakawa wanatakiwa, kule wasikotaraji
  Hata walioonewa, kama taka za gereji
  Hufika ya wanenaji, hayawi huja yakawa.

  Hayawi huja yakawa, ulijuwe mjuwaji
  Matope waloumbiwa,huziishi za saruji
  Na saraji walokuwa, tope likang’ang’aniwa
  Hufika ya wanenaji,hayawi huja yakawa.

  Mwovu huyo angakuwa, kampe japo kilaji
  Sijipe kumumbaguwa,hwenda atawale mji
  Kiwa hukumtambuwa, jataka ulimjaji
  Hufika ya wanenaji, hayawi huja yakawa

  1. Andika kichwa mwafaka cha shairi hili (al. 2)
  2. Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mtunzi wa shairi hili (al.4)
  3. Eleza dhamira ya mshairi (al.2)
  4. Eleza umbo la shairi hili (al.4)
  5. Taja methali inayotawala katika shairi (al. 2)
  6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika kwenye shairi
   1. ujaji
   2. walotakwa
  7. Onyesha matumizi mawili ya uhuru wa mshairi (al.2)

SEHEMU D: DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE

 1. Uozo katika jamii ni maudhui yaliyoshughulikiwa pakubwa katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine. Kwa kurejelea hadithi zozote tano fafanua kauli hii (al. 20)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI (AL. 20)

 1.  
  1. Eleza istilahi zifuatazo: (al. 12)
   1. Ayani
   2. Misimu
   3. Nyiso
   4. Mbolezi
   5. Mbazi
   6. Lakabu
  2. Fafanua mbinu nne za kukusanya fasihi simulizi (al. 8)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2017 MURANG'A MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest