Kiswahili Trial Exams Paper 3 Questions - Alliance Boys High School Mock December 2020

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Jibu maswali manne pekee.
  2. Swali la kwanza ni la lazima.
  3. Maswali hayo mengine yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobakia. (Yaani, Chozi la Heri, Tumbo Lisiloshiba, Fasihi Simulizi na Kigogo)
  4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  5. Karatasi hii ina kurasa 5 zilizopigwa chapa.
  6. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
SWALI  SEHEMU  ALAMA  ALAMA ZA MWANAFUNZI 
 1  A. USHAIRI  20  
 2/3  B. CHOZI LA HERI  20  
 4/5  C. TUMBO LISILOSHIBA  20  
 6/7  D. FASIHI SIMULIZI  20  
 8/9  E. KIGOGO  20  
   JUMLA  80  


MASWALI

SEHEMU A: USHAIRI
SWALI LA 1: LAZIMA

Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali yanayofuata:
Jukwani naingia, huku hapa pasokota,
Kwa uchungu ninalia, hii tumbo nitaikata,
Msiba mejiletea, nimekila kisotakata,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Wazee hata vijana, wote umewasubua,
Huruma nao hauna, heshima kawakosea,
Ukambani na Sagana, hata mbwa wararua,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Wahasibu ofisini, kibwebwe mejifunga,
Miaka mingi vitabuni, iliwasikose unga,
Nadhariwa nadhamini, hesabu wanazirenga,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Wapenzi wa kiholela, pia wanakuogopa,
Baada yao kulala, wana wao wanatupa,
Wakihitaji chakula, wanachokora mapipa,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Wafugaji hata nao, kama dawa wakwamini,
Hawajalijiranio, wamesusia Amani,
Wanaiba ng'ombe wao, nakuzua kisirani,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Nayo mizozo ya maji, kaonekana kwa mara,
Hiyo nayonidibaji, sababu sio harara,
Njaa wahepe wenyeji, huo ndio mkarara,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Ningeweza kukuuza, ingekuwa siku njema,
Tena kwa bei ya meza, sokoni nimesimama,
Wala tena singewaza, kuhusu walinasima,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Hatima umefikika, naenda zangu nikale,
Mate yalidondoka, kwa mnukiowa wale,
Naomba kwenda kukaa, wala sioni kalale,
We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

Maswali: 

  1. Lipe shairi hili anwani mwafaka. (Alama 1)
  2. Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (Alama 1)
  3. Huku ukitolea mifano mwafaka, thibitisha matumizi ya arudhi inavyojitokeza katika ubeti wa tatu. (Alama 4)
  4. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (Alama 4)
  5. Jadili vile mbinu alizotumia mwandishi ili kutosheleza mahitaji ya kiarudhi (Alama)
  6. Taja madhila anayoelezea mtunzi wa shairi hili yaletwayo na tumbo. (Alama 4)
  7. Taja na ueleze tamathali ya usemi iliyotumika katika kibwagizo cha shairi hili. (Alama 2)

SEHEMU B: RIWAYA: CHOZI LA HERI - ASSUMPTA K. MATEI
Jibu swali 2 au 3.

2. Haya ni matokeo ya ubahimu wa binadamu

  1. Tia maneno haya kwenye muktadha wake (Alama 4)
  2. Eleza umuhimu wa msemaji wa kauli hii (Alama6)
  3. Kwa hoja kumi, Jadili ubahimu mwingine unaotendwa na binadamu riwayani (Alama 10)

3."Alijihisi kama samaki aliyetiwa kwenye dema. Haya ni mazingira mageni kwake na
hakuja hapa kwa hiari." Thibitisha jinsi wahusika wafuatao walivyotiwa kwenye dema kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri. 

  1. Pete (Alama 6)
  2. Dick (Alama 6)
  3. Subira (Alama 4)
  4. Selume (Alama 4)

SEHEMU YAC: TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
Jibu swali 4 au 5.

4."Penzi lenu na nani? ............. Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali wee!"

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
  2. Taja na ufafanue mbinu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.  (Alama 4)
  3. Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyojitokeza katika hadithi nzima. (Alama 6)
  4. Eleza sifa za mzungumzaji. (Alama 6)

5. Sekta ya elimu imekubwa na changamoto nyingi. Thibitisha ukirejelea hadithi zifuatazo: (Alama 20) 

  1. Mapenzi ya Kifaurongo.
  2. Shogake Dada ana Ndevu.
  3. Mwalimu Mstaafu.
  4. Mtihani wa Maisha.

SEHEMU YAD: FASIHI SIMULIZI
Jibu swali 6 au 7. 6. a).
6.               

  1. Maudhui na Fani ya maigizo hutegemea mwigizaji. Thibitisha kwa hoja tano. (Alama 5)
  2. Taja mifano minne za miviga (Alama 2)
  3. Eleza hasara tatu za miviga (Alama 3)
  4. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

    Ikiwa wewe kweli ni mkazamwanangu
    Name ndiye nilompa uhai mwana unoringia
    Anokufanya upite ukinitemea mate
    Chakula kuninyima, wajukuu kunikataza ushirika,
    Miungu nawaone chozi langu, wasikie kilio changu,
    Mizimu nawaone uchungu wangu
    Radhi zao wasiwahi kukupa,
    Laana wakumiminie,
    Uje kulizwa mara mia na wanao,
    Usiwahi kufurahia hata siku moja pato lao,
    Watalokupa likuletee simanzi badala ya furaha
    Wakazawanao wasikuuguze katika utu uzima wako!

    Maswali
    1. Tambua aina ya mazungumzo katika tungo na utoe sabau (Alama 2) 
    2. Msemaji ni nani katika tungo hili (Alama 1)
    3. Tambua sifa mbili za anayeelekezewa mazungumzo haya (Alama 2)
    4. Taja na ueleze sifa tano za kipera hiki cha mazungumzo (Alama 5)

7.

  1. Ngano ni nini? (Alama 1)
  2. Eleza tofauti iliyoko kati ya visasili na visakale. (Alama 2)
  3. Fafanua umuhimu wa ulumbi katika jamii. (Alama 5) 
  4. Eleza umuhimu wa vitendawili katika jamii. (Alama 5)
  5. Tega na utegue vitendawili vyovyote viwili vilivyo na lugha ya takriri na lugha ya mlio.(A14)
  6. Taja sifa zozote tatu za methali. (Alama 3)

SEHEMU YA D: KIGOGO
Jibu swali 8 au 9.

8."Kila mwamba ngoma huvutia kwake" Thibitisha kauli hii ukirejelea wahusika mbalimbali tamthiliani. (Alama 20)
9. "...lazima chatu mmoja atolewe kafara ili watu wajue kuwa usalama upo," 

  1. Eleza mutktadha wa maneno haya. (Alama 4)
  2. Taja na ueleze mbinu moja ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili. (Alama 2)
  3. Eleza sifa nne za anayeambiwa maneno haya (Alama 4)
  4. Fafanua mbinu kumi hasi zilizotumiwa na utawala wa Sagamoyo. (Alama 10
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Trial Exams Paper 3 Questions - Alliance Boys High School Mock December 2020.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest