Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Mathioya Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

MAAGIZO

 • Jibu maswali yote.
 • Andika majibu yako katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
 • Majibu yako yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili

UFAHAMU
               Katiba ni utaratibu wa sharia unaoweka mpango wa jamii kuendesha mambo.Ni muhimu kila raia ajue katiba ya nchi yake.
            Katibu yaweza kuwa imeandikwa au haikuandikwa .Katika jamii za jadi,katiba ilihifadhiwa na kupokezwa kwa mdomo. Mtindo wa kuandika katiba ulianza nchini Marekani mwaka 1787.Ingawa katiba hii imefanyiwa mabadiliko hapa na pale,bado ni ili ile .Kenya ilipowekwa chini ya himaya ya Uingereza mwaka 1895,ilianza kutumia katiba ya Uingereza. Baada ya masetla wa kikoloni kujikita,walitangaza Kenya kuwa koloni.Hii ililazimu pawe na katiba nyingine mwaka 1920.Waafrika waliupinga mfumo huu kwa sababu haukuwahusisha kikamilifu kwenye masuala ya uongozi.Utetezi wa wanasiasa uliilazimisha serikali ya Uingeza kuitisha makongamano mbalimbali kama vile lile la Devonshire na mengine ili kurekabisha katiba.Waafrika hawakuridhika .Wakaendelea kudai katiba mwafaka.Harakati hizi zilileta kuitishwa kwa kongomano la katiba la Lanchester.Lengo lilikuwa kuandika katiba itakayotumiwa nchini hadi leo.Kati ya wajumbe walioenda Uingereza kuandika katiba mwaka 1962 ni pamoja na Tom Mboya ,,Jean Marie Seronney,Julius Kiano,Jomo Kenyatta,Masinde Mulio,Oginga Odinga,Ronald Ngala,Daniel Arap Moi na James Gichuru.Wengine ni Martin Shikuku,Dennis Akumu,Taita Towett,Abdilahi Nasssi,Jeremiah Nyaga na John Keen.
            Katiba ni kitovu cha taifa.Baina ya mambo inayotokeleza ni kuweka utaratibu na kanuni za utawala,kwa mfano,utawala wa kimikoa na serikali za wilaya.Pamoja na haya ,katiba hufafanua vyombo vikuu vya serikali,mamlaka yavyo na mipaka yavyo ya kutenda.vyombo hivi ni bunge,mahakama,urais,jeshi n.k.Halikadhalika,katiba hupambanua haki za raia.
            Hii hudumisha demokrasia na huwawezesha wananchio kupata uhuru na haki za kimsingi.Katiba hukinga haki za kila raia,hasa kutokana na udhalimu na wengi au wenye uwezo mkubwa .Zaidi ya yote,katiba huimarisha asasi za umma ili kudumisha uwajibikaji.
Katiba huhalalishwa na watawaliwa.Hii hutokea wanaposhirikishwa katika uandishi wake.Kuanzia miaka ya themanini ,RAIA WALIANZA KUDAI KATIBA IGEUZWE.mwamko wa kutaka mageuzi ulianza kwa harakati za kibadilisha mfumo wa kisiasa kutoka ulee wa chama kimoja hadi ule wa demokrasia ya vyama vingi.Haja ya mfumo mpya wa kisiasa kutoka ule wa chama kimoja hadi ule wa demokrasia ya vyama vingi.Haja ya mfumo mpya wa kisiasa ulilenga kuwashirikisha wananchi katika utawala na kuondoa uimla.
            Harakati zilitia fora miaka ya tisini.Mambo yaliyochochea hali hii ni mengi.Kwanza katiba iliyokuwa imeandikwa na watu wachache ilikuwa imefanyiwa marekebisho mengi.Marekebisho haya yalimpa rais mamlaka mengi juu ya serikali kuu na vyombo tofauti vya serikali.Pili,viongozi na watu wenye uwezo na utajiri walipuuza katiba.Raia walihisi wanadhulumiwa .Walipinga hali ya wachache waliomzunguka rais kunufaika huku umma ukitengwa.Tatu,kutokana na uongozi uliokuweko wakati huo,wanawake,Watoto na walemavu walidhulumiwa na kukosa uwakilishi ufaao.Hatimaye,pakawa na ongezeko la uharibifu wa mazingira,ufisadi na unyakuzi wa mali ya umma kama vile ardhi.
            Waliopigania katibu mpya walikuwa na haja ya katiba ambayo uanddikaji wake ungewahusisha Wakenya wote.Mwanzoni,serikali ilipinga mwito wa madiliko.Lakini mnamo mwaka 2001 iliunda Tume ya marekebisho ya katiba ili kutekeleza mahitaji ya wananchi.Tume hii iliwahamasisha na kuwashawishi raia kutoa maoni.Tume iliandaa vikao katika maeneo ya ubunge 210 ambapo wananchi walitoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya katiba.
Katika mapenekezo hayo raia walisisitiza mambo kadha.Jambo la kwanza ni utawala mwema na uwajibikaji wa viongozi na maafisa wa wa umma .Jambo linguine ni kulinda haki za binadamu zikiwemo za wanawake,Watoto na walemavu .Raia walidai kanuni za usawa na ulinganifu.Aidha walitia mkazo mahitaji ya msingi kama chakula,afya nzuri,makao,elimu,usalama,uchumi na kadhalika.
            Msingi wa mapendekezo haya yote ni kuwepo na amani ya kitaifa,umoja na uadilifdu ili kulinda maslahi ya wananchi wote na taifa.

Maswali

 1. Eleza kilichosababisha kongamano la Lancaster. (alama 3)
 2. Taja mambo matatu yaliyotiliwa mkazo na raia katika maonoi yao kuhusu katika. (alama 3)
 3. Eleza umuhimu wa katiba kwa mujibu nwa taarifa. (alama 3)
 4. Taja sababu zilizochangia ubadilishaji wa katiba. (alama 3)
 5. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa. (alama 3)
  1. Kitovu
  2. Harakati
  3. Hamasisha

UFUPISHO

              Miongoni mwa maadui wanaotupa dhiki na wanaohitaji kudhibitiwa hima na serikali ni magonjwa, ujinga na umaskini. Kati ya maadui hawa, maradhi yanayotokana na mitindo ya maisha kama kisukari, shinikisho la damu, ukimwi na msongo wa akili ndiyo hatari sana. Yamekuwa chanzo cha kuvurugika kwa maisha ya Wakenya wengi na kuwasababishia umaskini.
              Ndipo tunachukua fursa ya mapema ya kuiomba serikali kujitahidi kwa hali na mali kuelimisha umma kuhusu maradhi haya ili tuwe na Wakenya wenye afya na uwezo wa kushiriki katika miradi ya maendeleo. Hadi leo kuna Wakenya wasioamini maradhi haya yanasababishwa na mitindo ya Maisha. Jinsi tunavyoishi; tunavyokula, kunywa,kutangamana na wenzetu ndicho cha maradhi.
              Lakini utawakuta wakikimbilia kwa waganga kuganguliwa na kutibiwa kwa mitishamba . wengi wao wanafanya hivyo kwa kukosa kujua chanzo cha shida. Tungeomba maafisa wa Wizara ya Afya, Elimu na Habari na Utangazaji kubuni mikakati dhabiti ya kuelimisha Wakenya chanzo cha magonjwa na jinsi ya kujikinga. Waelezwe kwa njia chepesi ili waweze kushawishika na kuokoa maisha yao.
              Kwa mfano, wengi wa watu hula nyama kwa wingi na kunywa pombe. Nyama inaelezwa kuwa hatari kwa afya. Nyama ya ngómbe mbuzi na kondoo ndio inayoongoza na wale wanaotumia wamejikuta wakiugua maradhi kadhaa. Badala yake watu wahimizwa kula samaki na kuku ambao hupatikana kwa urahisi ingawa siku hizi ni ghali kidogo.
              Kulingana na wataalamu, mwili wa m tu huhitaji gramu 70 za nyama kila siku. Lakini wengi kutokana na tamaa na ujinga tunakula nus una hata kilo! Ndivyo tunavyojimaliza. Nina hakika tukiendelea kutegemea matibabu pekee bila kupata elimu inayohusu maradhi haya, huenda shoda ikadumu nasi. Upo umuhimu wa kudhibiti tatizo hili ili kiafya iimarike.
              Najua kuwa tumezungumzia swala la maradhi tangu tupate uhuru miaka 50 iliyopita, na hadi leo hakuna kilichobadilika sana. Ukweli ni kwamba sasa magonjwa yaliyodhaniwa kuwa ya matajiri yamewavamia maskini. Tunaendelea kupoteza Wakenya ambao wangelisukuma gurudumu la maendeleo ya taifa kutokana na magonjwa yanayozuilika pia kutibika.
              Wengine wanaingia na kutoka hospitalini, jambo ambalo huzorotesha uchumi na hatimaye wao huwa na mizigo kwa familia. Watakaokabiliwa na jukumu la kuwatunza wagonjwa watashindwa kufanya kazi na akiba ya pesa itaisha. Serikali inapoahidi kutupa matibabu ya bure, ingefaa pia kuelimisha umma jinsi ya kujikinga na maradhi.


Maswali

 1. Fupisha aya nne za kwanza kwa maneno yasiyozidi 80. (alama 8)
  matayarisho
  Jibu
 2. Kwa maneno yasiyozidi 60 fupisha aya tatu za mwisho. (alama 6)
  matayarisho
  Jibu

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA

 1. Bainisha sifa mbilimbili za sauti zifuatazo (alama 2)
  1. /o/
  2. /n/
 2. Weka maneno yafuatayo katika ngeli mbilimbili tofauti. (alama 2)
  1. Chumvi
  2. Kiboko
 3.       
  1. Eleza maana ya sauti mwambatano. (alama 1)
  2. Toa mfano wa neno moja lenye sauti mwambatano ya ufizi (alama 1)
 4. Eleza dhima ya sentensi ifuatayo. (alama 1)
  Wote wameadhirika!
 5. Bainisha mofimu katika neno ;, jipya. (alama 1)
 6. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. (alama 2)
  Nomino dhahania+ kirai kivumishi+ kitenzi kishirikishi kipungufu+kivumishi
 7. Bainisha aina za vielezi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
  Mfanyibiashara maarufu sana alimaliza biashara yake kikondoo.
 8. Eleza matumizi mawili ya parandesi. (alama2)
 9. Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
  Ijapokuwa alifika mapema, hakumpata kwake
 10. Tunga sentensi moja kudhihirisha maana mbili za neno ; chungu. (alama 2)
 11. Pambanua kwa kutumia mstari. (alama 2)
  Somo lenyewe litafunzwa mwakani.
 12. Bainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama2)
  Baba alijengewa nyumba na mjenzi kwa mawe.
 13. Tunga sentensi kubainisha matumizi ya kielezi ku- kama:
  1. Kiambishi ngeli cha nomino
  2. Kuonyesha mahali kusikodhihirika
 14. Eleza matumizi ya kwa katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
  Alipata tatu kwa kumi kwa kuwa hakuhudhuria somo lake vizuri.
 15. Tumia viuynganishi vifuatavyo katika sentensi kwa usahihi. (alama 2)
  1. Fauka ya
  2. Ilhali
 16. Jibu kulingana na maagizo yaliyo kwenye mabano. (alama 3)
  1. Ukikesha utasinzia darasani. (tumia wingi na ngali ya masharti
  2. Hawajui ambako walitorokea. (tumia ‘o’rejeshi)
  3. Ngome ya wanajeshi ilfanyiwa ukarabati. ( andika katika hali ya mazoea)
 17. Andika sentensi ifuatayo upya katika wingi ukubwa. (alama 2)
  Ngómbe huyo alimuumiza msichana huyo.
 18. Akifisha (alama 3)
  juma aliamrisha mwanawe toka nje na uache kupiga kelele
 19. Yakinisha (alama 2)
  Asipokomelea mwenyeji na mgeni asikome hapo.
 20. Toa maana mbili za sentensi hii. (alama 2)
  Mama alimletea taa.

ISIMU JAMII

 1. Umechaguliwa na mgombea wa ubunge katika eneobunge lenukatika kufanya kampeni za uchaguzi. Fafanua sifa tano za lugha utakayotumia katika kuendeleza kampeni hizo.
 2. “Maulana akuzidishie baraka.”
  “Amina! Nawe akukinge na dhiki za ulimwengu na baraka ziongezeke kama mchanga baharini.”
  “Atatupa sote tukimwamini kama ilivyo katika maandiko takatifu.”
  1. Taja sajili inyahusishwa na mazungumzo haya. (alama 1)
  2. Fafanua sifa nne za lugha ziliyotumiwa katika mazungumzo haya. (alama 4)

Mwongozo Wa Kusahihisha

 1. UFAHAMU

  Maswali
  1. Eleza kilichosababisha kongamano la Lancaster. (alama 3)
   • Waafrika walipinga katiba ya 1920 kwa kutohusishwa kikamilifu.
    Utetezi wa wanasiasa ulilazimisha serikali ya Uingereza kuitisha makongamano
    Waafrika hawakuridhika na katiba zingine.
  2. Taja mambo matatu yaliyotiliwa mkazo na raia katika maonoi yao kuhusu katiba. (alama 3)
   • Utawala mwema na uwajibikaji wa viongozi
    Kulinda haki za binadamu
    Usawa na ulinganifu
    Mahitaji ya msingi
  3. Eleza umuhimu wa katiba kwa mujibu nwa taarifa. (alama 3)
   • Huweka utaratibu na kanuni za utawala
    Hufafanua vyombo vikuu vya serikali
    Hudumisha demokrasia
    Hukinga haki za kila raia
    Huimarisha asasi za umma ili kudumisha uwajibikaji
  4. Taja sababu zilizochangia ubadilishaji wa katiba. (alama 3)
   • Katiba iliyokuwa imeandikwa na watu wachache ilikuwa imefanywa marekebisho mengi
    Viongozi na watu wenye uwezo walipuuza katiba
    Wanawake, Watoto na walemavu walikosa uwakilishi ufaao
  5. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa. (alama 3)
   • Kitovu -Kitu chenye mambo muhimu
   • Harakat i-shughuli
   • Hamasisha -Shawishi kufanya jambo Fulani
 2. UFUPISHO
  Maswali
  1. Fupisha aya nne za kwanza kwa maneno yasiyozidi 80. (alama 8)
   • Jibu
   • Miongoni mwa maadui wanatupa dhiki ni magonjwa , ujinga na umaskini.
   • Kuna maradhi yanayotokana na mitindo ya kisasa
   • Maradhi hayo ndiyo chanzo cha kuvurugika kwa Wakenya wengi
   • Tunaomba serikali kueliumisha umma kuhusu maradhi haya.
   • Kuna Wakenya wasioamini maradhi haya yanasababishwa na mitindo ya kisasa
   • Wanakimbilia waganga kutibiwa kwa mitishamba.
   • Wizara za Afya, Elimu na Hahari zielimishe chanzo cha magonjwa na jinsi ya kujikinga.
   • Waelezwe njia nyepeshi ili waweze kuokoa Maisha yao.
   • Nyama ya ng,ombe, mbuzi na kondoo ni hatari kwa afya.
   • Watu wahimizwe kula samaki na kuku.
  2. Kwa maneno yasiyozidi 60 fupisha aya tatu za mwisho. (alama 6)
   • Jibu
   • Binadamu huhitaji gramu 70 za nyama kila siku.
   • Tukitegemea matibabu pekee bilka elimu shida itadumu nasi.
   • Magonjwa yaliyodhaniwa kuwa ya matajiri yamevamia maskini.
   • Tiunapoteza Wakenya kutokana na magonjwa yanayozuilika na kutibika.
   • Wanaoingia na kutoka hospitalini wanazorotesha uchumi.
   • Wanaowatunza wagonjwa wanashindwa kufanya kazi
   • Serikali ielimishe umma jinsi ya kujikinga na maradhi.
    • a-8 hoja 8
    • b-6 hoja 6
    • u-1 mtahiniwa atumie aya moja katika kila jibu
 3. SARUFI
 4. NA MATUMIZI YA LUGHA
  1. Bainisha sifa mbilimbili za sauti zifuatazo (alama 2)
   • /o/ irabu ya nyuma, kati na viringwa
   • /n/ nazali, ufizi, sauti ghuna
  2. Weka maneno yafuatayo katika ngeli mbilimbili tofauti. (alama 2)
   • Chumvi
    • I-I, I-ZI
   • Kiboko
    • KI-VI, A-WA
  3.        
   1. Eleza maana ya sauti mwambatano. (alama 1)
    • Sauti iliyoundwa kwa sauti mbili au zaidi kabla ya irabu.
   2. Toa mfano wa neno moja lenye sauti mwambatano ya ufizi (alama 1)
    • Ndizi, ndugu,
  4. Eleza dhima ya sentensi ifuatayo. (alama 1)
   • Wote wameadhirika!
   • Mshangao, hisia
  5. Bainisha mofimu katika neno ;, jipya. (alama 1)
   • Ji-umoja
   • -pya- mzizi
  6. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. (alama 2)
   • Nomino dhahania+ kirai kivumishi+ kitenzi kishirikishi kipungufu+kivumishi
   • Bidii hiyo yake ni nzuri
  7. Bainisha aina za vielezi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
   • Mfanyibiashara maarufu sana alimaliza biashara yake kikondoo.
   • Sana- nanma halisi
   • Kikondoo- namna mfanano
  8. Eleza matumizi mawili ya parandesi. (alama2)
   • Kutoa maelezo Zaidi kuhusu neno/maneno
   • Kufungia nambari/ herufi za kuorodhesha
   • Kufungia ufafanuzi katika mazungumzo
  9. Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
   • Ijapokuwa alifika mapema, hakumpata kwake
   • Ijapokuwa alifika mapema – tegemezi
   • Hakumpata kwake- huru
  10. Tunga sentensi moja kudhihirisha maana mbili za neno ; chungu. (alama 2)
   • Chombo cha kupikia
   • Mdudu
   • Isiyokuwa tamu
  11. Pambanua kwa kutumia mstari. (alama 2)
   • Somo lenyewe litafunzwa mwakani.
   • S-KN(N+V) +KT(T+E)
  12. Bainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama2)
   • Baba alijengewa nyumba na mjenzi kwa mawe.
   • Baba – kitondo
   • Nyumba- kipozi
   • Mawe-ala
  13. Tunga sentensi kubainisha matumizi ya kielezi ku- kama:
   1. Kiambishi ngeli cha nomino
    • Kusoma kwake kulimfaidi.
   2. Kuonyesha mahali kusikodhihirika
    • Kule ni kwake.
  14. Eleza matumizi ya kwa katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
   • Alipata tatu kwa kumi kwa kuwa hakuhudhuria somo lake vizuri.
   • Tatu kwa kumi- sehemu ya kitu kizima
   • Kwa kuwa -sababu
  15. Tumia viuynganishi vifuatavyo katika sentensi kwa usahihi. (alama 2)
   1. Fauka ya
    • Dhana ya kujumuisha
   2. Ilhali
    • Dhana ya kukataa kwa nia ya kupambanua
  16. Jibu kulingana na maagizo yaliyo kwenye mabano. (alama 3)
   • Ukikesha utasinzia darasani. (tumia wingi na ngali ya masharti)
    • Wangalikesha wangalisinzia darasani.
   • Hawajui ambako walitorokea. (tumia ‘o’rejeshi)
    • Hawajui watarokeako
   • Ngome ya wanajeshi ilfanyiwa ukarabati. ( andika katika hali ya mazoea)
    • Ngome ya wanajeshi hufanyiwa ukarabati.
    • Andika sentensi ifuatayo upya katika wingi ukubwa. (alama 2)
    • Ngómbe huyo alimuumiza msichana huyo.
    • Magombe yale yaliwaumiza masichana hayo.
    • Akifisha (alama 3)
    • juma aliamrisha mwanawe toka nje na uache kupiga kelele
    • Juma aliamrisha mwanawe, “ Toka nje na uache kupiga kelele!”
    • Yakinisha (alama 2)
    • Asipokomelea mwenyeji na mgeni asikome hapo.
    • Akikomelea mwenyeji na mgeni akome hapo.
    • Toa maana mbili za sentensi hii. (alama 2)
    • Mama alimletea taa.
    • Kifaa cha kutoamwangaza
    • Aina ya samaki

ISIMU JAMII

 1. Umechaguliwa na mgombea wa ubunge katika eneobunge lenukatika kufanya kampeni za uchaguzi. Fafanua sifa tano za lugha utakayotumia katika kuendeleza kampeni hizo.
  • Matumizi ya msamiati maalum
  • Tamathali za usemi k.v methali
  • Chuku
  • Kuchanganya ndimi
  • Matumizi ya michoro na ishara
  • Matumizi ya nyimbo
  • Lugha legevu/ isiyo zingatia sarufi
 2. “Maulana akuzidishie baraka.”
  “Amina! Nawe akukinge na dhiki za ulimwengu na baraka ziongezeke kama mchanga baharini.”
  “Atatupa sote tukimwamini kama ilivyo katika maandiko takatifu.”
  1. Taja sajili inyahusishwa na mazungumzo haya. (alama 1)
   • Sajili ya dini/ maabadini
  2. Fafanua sifa nne za lugha ziliyotumiwa katika mazungumzo haya. (alama 4)
   • Msamiati maalum- Maulana
   • Lugha yenye matumaini
   • Tashibihi- kama mchanga baharini
   • Kurejelea vitabu takatifu

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Mathioya Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?