Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Londiani Joint Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

Kwa matumizi ya mtahini pekee

SWALI

UPEO

ALAMA

1

15

 

2

15

 

3

40

 

4

10

 

JUMLA

80

 

MAAGIZO

  1. Andika jina lako na nambari katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  2. Jibu maswali yote katika sehemu ulizoachiwa
  3. Majibu yatolewe kwa kufuata sheria za mtihani wa kitaifa

MASWALI

UFAHAMU ( alama 15)
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali:
Binadamu kwa wakati huu amemaka kwa sababu amechafua mazingira yake pasipo tahadhari. Mathalani amejaza gesi za sumu zitokazo viwandani na hata kuchafua mito kutokana na maji machafu kutoka viwanda hivyo. Takataka zinazotupwa ovyo ovyo zinarundikana kila mahali. Isitoshe miti inakatwa vivyo hivyo bila simile. Matokeo ya haya yote ni kwa mfano, tunapata mvua ya asidi ambayo huhasiri mimea. Aidha nao ukanda wa ozoni unaotukinga dhidi ya miale hatari kutoka kwa jua umeharibiwa tayari na hivyo kuongeza joto duniani. Sehemu nyingi zimeanza kugeuka na kuwa jangwa huku sehemu zingine zikifurika kwa maji ya mito na mvua. Maji haya yameanza kumeza visiwa vingi vilivyo baharini. Kutokana na madhara haya, binadamu sasa anatapatapa ili kutafuta makao kwingine kwenye usalama. Ndiposa siku hizi nadhari za binadamu zimeelekezwa katika mawanda mengine nje kabisa ya kisayari hiki kidogo kiitwacho dunia.
Kwa miaka mingi sasa binadamu amekuwa akitafakari uwezekano wa kuishi katika sayari nyingine. Hii ndiyo sababu mwaka wa 1969 Waamerika walimkanyagisha binadamu wa kwanza kabisa mwezini. Lengo lilikuwa ni kutalii na kuchunguza uwezekano wa binadamu kuishi huko ili wale watakaoweza wahamie huko, hata mimea. Mwezini ni vumbi tupu lisiloota chochote. Kipatikanacho kwa wingi sana ni madini tu ambayo hayawezi kufaidi binadamu kwa lolote.
Sayari nyingine alizozitalii binadamu ni Zuhura, Mirihi, Mushtara na tuseme karibu zote zinazolizunguka jua. Kilichogunduliwa ni kuwa upo uwezekano wa sayari kama Zuhura na pengine Mirihi kuwa na mvua, lakini nyingi mno isiyoweza kuruhusu mimea kukua. Zuhura inasemekana kuwa joto sana wakati wa mchana ilhali Mirihi ni baridi sana siku zote; baridi kiasi cha kuwa binadamu na wanyama hawawezi kuishi huko. Mushtara yasemekana kuwa joto ajabu, ambapo hizo sayari nyingine zina joto sana au zina baridi sana. Habari hii imemfunga binadamu katika jela ya kijisayari chake kiki hiki kiitwacho dunia anachokichafua uchao.
Je, binadamu amekata tamaa? Hata kidogo! Ndio mwanzo anajaribu sana kuzikata pingu alizofunzwa na maumbile. Vipi? Amejaribu kuchunguza uwezekano wa kuihama ardhi na kuishi baharini, kwa sababu bahari inazidi ardhi mara tatu kwa ukubwa. Na ni vipi binadamu anadhani anaweza kuishi baharini mahali ambapo hakuumbiwa aishi humo kama samaki?Jawabu ni kuwa angefanya hivyo kwa kutumia maarifa yake.
Binadamu anaamini kabisa kuwa ana uwezo wa kujenga miji mikubwa mikubwa humo humo baharini. Mikubwa zaidi ya hii tuliyo nayo ardhini. Anaamini ya kuwa anaweza kuitawala bahari kiasi alichotawala ardhi, na hivyo basi kufanya bahari impe makao na kumlisha bila ya kuyabadilisha maumbile yake. Na iwapo hili halitawezekana basi, ikiwajibika, abadilishe maumbile yake kwa kujiunda mashavu kwa mfano, ili avute pumzi ndani ya maji. Njia ya pili ya kuepukana na pingu za maumbile ni kuishi angani. Hii ina maana ya kujenga miji iliyoelea angani, kama madungu vile. Na kwa vile anga haina kikomo, binadamu atakuwa amejipatia visayari vyake visivyo idadi angani!
Njia ya tatu ni kubadilisha umbo lake ili asihasirike na joto wala baridi. Binadamu wa kisasa anaamini kuwa inawezekana kumuunda upya mtu katika maabara badala ya katika mimba.Mtu huyu wa maabara, aitwaye ‘cyborg’ kwa lugha ya Kiingereza, anaweza kuwa na chuma ndani badala ya mifupa, na mwili wa kawaida wa udongo na maji nje.Kiumbe huyu atakuwa hadhuriki ovyo ovyo kama binadamu wa sasa aliyeumbwa kwa chumvi, maji na protini. Au bora zaidi, binadamu mpya wa maabarani aundwe kwa zebaki. Binadamu huyu wa zebaki hafi wala hakatikikatiki. Na iwapo atakatika vipande vipande, basi kama zebaki hivyo vitaundika tena upya na kumrudishia umbo la awali kamili.
Njia nyingine ya kuepukana na uangamizi ni kutumia viunde vyake vya elektroniki kama vile tarakilishi yaani kompyuta, na mitambo mingine kama hiyo. Binadamu anaamini kwamba uwezo wa vyombo hivi utakapokamilishwa, basi vitamsaidia kwa lolote lile.
Maswali

  1. Inasemekana kwamba binadamu anakichafua hiki kisayari chake kila uchao. Kwa kutumia mifano mitatu, eleza jinsi binadamu amechafua mazingira yake. (alama3)
  2. Kwa nini ongezeko la joto limeleta jangwa duniani na wakati huo huo likaleta mafuriko? (alama 2)
  3. Eleza sababu mbili zinazomfanya binadamu kuhangaika na kutafuta makao kwingine (alama 2)
  4. Ni mambo gani yanayomfunga binadamu katika ardhi. Taja mawili. ( alama 2)
  5. Unadhani ni kwa nini madini mengi yaliyoko mwezini hayaletwi duniani. Taja na ufafanue sababu mbili. ( alama 2)
  6. Kulingana na aya mbili za mwisho, eleza jambo ambalo binadamu anajaribu kukwepa (alama 2)
  7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. ( alama 2)
    1. Mashavu………………………………………………………………………………………....
    2. Madungu………………………………………………………………………………………

2.UFUPISHO: (ALAMA 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali :
Maendeleo ya taifa hutegemea jinsi wananchi wanavyojitolea katika kulibingirisha gurudumu la uchumi wao. Kila mwanajamii anahitajika kujibidiisha katika kazi au taaluma yake. Mzalendo yeyote yule hupata motisha ya kufanya kazi iwapo anaweza kupata ile kazi aliyokuwa akiitamani.
Kumakinika katika taaluma fulani si jambo jepesi na huchukua muda kutengeneza. Kwa mfano, ili mhazili apate staha ya uhazili sharti apitie ngazi mbalimbali. Mwanzo kabisa, lazima ahitimu vyema katika masomo rasmi darasani. Masomo hayo pamoja na cheti huweza kumpa fursa ya kujiunga na vyuo mbali mbali vya uhazili. Anapojiunga na vyuo hivyo ndipo safari inapoandaliwa. Kukamilisha safari hii kunahitaji muda wa miaka minne. Anapohitimu huwa tayari ameimudu shughuli hiyo. Hata hivyo, anatakiwa afanye mazoezi kila mara ili asisahau yanayohitajika katika taaluma hiyo.
Wengi waliokwishapata ujuzi huo wa uhazili huona kuwa hawatapata kazi nzuri yenye mshahara mkubwa. Baadhi yao hujilinganisha na wale wenzao ambao katika masomo hawana utaalumu kama wao. Ijapokuwa wote ni wahazili, viwango vyao ni tofauti na mishahara pia hutofautiana. Tofauti hapa ni daraja zao za vyeo. Baada ya kuhitimu na kupata vyeti vya uhazili ni rahisi kupata au kutopata kazi zenye ujira wa kuvutia. Anayefanikiwa ana safari ya kujikakamua hasa kwa upande wa uzingativu wa kazi kikamilifu na kutunza hadhi ya ofisi yake.
Kuna mashirika makubwa yanayojiweza kiuchumi, ambayo raslimali yake ni imara. Mashirika madogo huwa yana raslimali chache. Mashirika haya yana wahazili na wafanyikazi ambao hupata mishahara duni. Wafanyakazi hawa hufanya kazi kwa kutokuwa na uhakika wa kulipwa mshahara mwisho wa mwezi. Watu kama hao hawawezi kutilia maanani kazi zao. Mashirika mengine hayana utaratibu maalum wa kulipa mishahara kwa vile hutegemea utu wa mkurugenzi.
Baadhi ya wakuu hawa huwa wabanizi na huwapunja wafanyikazi wao. Hili ni suala nyeti ambalo linahitaji litatuliwe kwa kuwa na chama cha kupigania haki za wafanyakazi. Wakati wanapotafuta kazi, wahazili wengi huwa ni wahitaji na hukubali chochote wanachopewa.
Wale waliobahatika kupata nafasi ya ajira katika kampuni kubwa za kimataifa, mishahara huwa ni ya kutia moyo. Katika dunia hii wahazili wana vibarua vigumu kwa sababu lazima wapate tajriba na uzoefu wa taaluma inayoendelea na shirika fulani. Wakurugenzi mara nyingi huwa hawana subira. Mhazili anapotumia msamiati usioenda sambamba na shughuli za kiofisi hawasiti kufoka. Wavumilivu miongoni mwao hula mbivu. Hawa hawafi moyo bali hujitahidi zaidi ili wasikumbwe na kimbunga cha kufokewa. Kuna wengine ambao humwaga unga.

  1. Fupisha aya ya tatu za kwanza. (maneno 60-70) (alama 6, 1 ya utiririko)
    MATAYARISHO

    JIBU

  2. Huku ukizingatia aya mbili za mwisho, eleza masuala muhimu ambayo mwandishi anaibua. (maneno 65-70) (alama 7, 1 ya utiririko)
    MATAYARISHO

    NAKALA SAFI 

 

  1. MATUMIZI YA LUGHA- (ALAMA 40)
    1. Eleza sifa nne za sauti /a/ (alama 2)
    2. Bainisha muundo wa silabi katika maneno yafuatayo. (alama 2)
      1. Nywesha ………………………………………………….
      2. Gongwa………………………………………………………
    3. Akifisha sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti ili kuleta maana mbili
      kidhamira/kimajukumu (alama 2)
      Mtihani utafanywa leo
    4. Bainisha mofimu katika neno lifuatalo:
      1. Hajamjia (alama 3)
    5. Eleza dhima ya viambishi tamati mbali na kauli ya kutenda/kiishio: (alama 2)
    6. Ziweke nomino zifuatazo katika ngeli zao (alama 2)
      1. Wembe ………………………………………………………………………
      2. Parachichi ……………………………………………………………………….
    7. Andika kwa wingi. (alama 1)
      Ua wake una ua zuri na kubwa
    8. Huku ukitoa mifano, bainisha miundo miwili ya nomino za ngeli ya U-I (alama 2)
    9. Tunga sentensi kuonyesha nomino zifuatazo (alama 2)
      1. Nomino ya pekee
      2. . Nomino ya wingi
    10. Changanua kwa kielelezo cha sanduku. (alama 3)
      Maimuna hupenda kufanya kazi nyingi kupindukia
    11. Tunga sentensi kuonyesha tofauti kati ya:
      1. Kiwakilishi cha nafsi huru na kiwakilishi cha nafsi tegemezi (alama 2)
      2. Kiwakilishi cha ‘a’ unganifu na kivumishi cha ‘a’ unganifu (alama 2)
    12. Tambua chagizo, kijalizo na kiarifa katika sentensi hii. (alama3)
      Kijakazi Yule mzuri yu hospitalini alimokimbilia matibabu ya kuugua
    13. Tambua vielezi vinne katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Mwalimu mkali sana alitufunza jana mara tatu uwanjani
    14. Tunga sentensi ukitumia viunganishi vifuatavyo. (alama 2)
      1. kiunganishi cha kinyume…………………………………………………
      2. kiunganishi cha uteuzi………………………………………....................
    15. Tumia vihisishi vifauatavyo kwenye sentensi kuleta dhana iliyokusudiwa (alama 2)
      1. Naam!
      2. Kefule!
    16. Tunga sentensi kubainisha matumizi yafuatayo ya kiambishi ‘na’ (alama 2)
      1. Wakati uliopo …………………………………………………..
      2. Kihusishi cha mtendi/mtendaji
    17. Tambua vihusishi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Rais mteule alipiga dua kabla ya kusimama kwa haraka juu ya jukwaa
    18. Tunasema kifurushi cha kalamu………………cha mboga………….......ya udongo. (alama 2)

ISIMU JAMII (alama 10)

  1. Wewe ni mtaalamu wa kutoa ushauri nasaha kwa vijana. Umealikwa na shule ya upili ya Bidii kuwazungumzia wanafunzi. Taja mambo matano uatakayozingatia kufanikisha mazungumzo yako. (alama5)
  2. Fafanua jinsi yafuatayo yanavyoathiri matumizi ya lugha. (alama2)
    1. Madhumuni
    2. Uana
  3. Taja mambo matatu yaliyofanyika kukabiliana na changamoto zinazokabili ukuaji wa kiswahili nchini kenya. (alama3)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

UFAHAMU ( alama 15)
Maswali

  1. Inasemekana kwamba binadamu anakichafua hiki kisayari chake kila uchao. Kwa kutumia mifano mitatu, eleza vile binadamu amechafua mazingira yake. (alama 3)
    Gesi hatari kutoka viwandani
    Moshi kutoka viwandani
    Utupaji ovyo ovyo wa taka
  2. Kwa nini ongezeko la joto limeleta jangwa duniani na wakati huo huo likaleta mafuriko? (alama 2)
    Miti ikishakatwa mizizi iliyoshikilia udongo haiko tena hivyo kukinyesha maji yanateremka ovyoovyo.
    Maji ya bahari yakipata joto yanapanuka na kufukika yenyewe.
    Maji yakipata joto mvuke unakuwa mwingi na mawingu mazito yanaleta mvua nyingi ghafla.
    Miti ikikatwa joto linaleta majangwa.
  3. Eleza sababu mbili zinazomfanya binadamu kuhangaika na kutafuta makao kwingine (alama 2)
    Ongezeko la watu duniani
    Amechafua mazingira yake
  4. Ni mambo gani yanayomfunga binadamu katika ardhi. Taja mawili. ( alama 2)
    Kugundua kuwa mwezini hakuna mvua wala hewa.
    Kugundua kuwa sayari nyingine zina mvua lakini ni nyingi zaidi mf. Mirihi.
    Kuwa sayari nyingine zina joto zaidi na nyingine baridi zaidi.
  5. Unadhani ni kwa nini madini mengi yaliyoko mwezini hayaletwi duniani. Taja na ufafanue sababu mbili. ( alama 2) Hakuna hewa huko ambayo wachimbaji wangetumia wakichimba.
    Ni ghali sana kupeleka watu na mitambo kuchimba madini hayo.
  6. Kulingana na aya mbili za mwisho, eleza jambo ambalo binadamu anajaribu kukwepa (alama 2)
    Mauti, anajaribu kuunda kiunde cha zebaki na pia kutumia viunde vya kielektroniki au kompyuta.
  7. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. ( alama 2) (i)Mashavu viungo vya samaki vya kuvutia hewa (ii)Madungu makao yanayoelea angani/viota vya ndege

2.UFUPISHO: (ALAMA 15)

  1. (alama 6, 1 ya utiririko)
    Maendeleo ya taifa hutegemea bidii/kujitolea kwa wananchi kazini (ii) mzalendo hupata motisha apatapo aliyotamani (iii) Taaluma yoyote huchukua
    muda kutegemea kumakinika katika taaluma fulani. Huchukua muda kujitegemea (iv) Mhazili lazima ahitimu darasani/mhazili ahitimu katika
    masomo rasmi ya darasa (v) anatakiwa afanye mazoezi kila mara ili asisahau (vii) wengi huona kuwa hawatapata kazi nzuri/ ya msharara mzuri. Wengi
    hulinganisha wenzao wenye viwango tofauti au mishahara tofauti/ ni rahisi kupata au kutopata kazi zenye ujira wa kuvutia (viii) anayefanikiwa ni lazima/ni sharti ajikakamue kazini.
    Hoja 8x1= (alama 8) Makosa ya sarufi jumla 10 x ½ =05 Hijai: 06 x ½ =03 Ziada: maneno 10 zaidi alama tano zaidi ½
  2. Mashirika makubwa yanajiweza kiuchumi kuliko madogo. (2) Mashirika madogo hulipa mishahara duni isiotegemewa (3) wafanyikazi hawawezi kutilia maanani kazi yao (4) Baadhi ya wakurugenzi huwa wabanizi na huwapunja wafanyakazi wao au/ ulipaji wa mishahara hutegemea utu wa mkurugenzi
    au/Mashirika mengine hayana utaratibu maalum wa kulipa mishahara (5) kuna haja ya kuwa na chama cha kupigania haki za wafanyakazi. (6) Wahazili
    wengine ni wahitaji na hukubali chochote wanachopewa (7) wanaoajiriwa katika kampuni za kimaataifa na mashirika makubwa hulipwa mishahara
    mikubwa (8) Wahazili lazima wapate tajriba/ uzoefu na wawe wavumilivu (9) wakurugenzi wasio na subira huwafokea na /au kuwafuta kazi/wahazili wasio makinika hufokewa na au hufutwa kazi
    Hoja 9x1=9

 

  1. MATUMIZI YA LUGHA- (ALAMA 50) 2
    1. Eleza sifa nne za sauti /a/ (alama 2)
      • Ni irabu
      • Hutamkwa sehemu ya kati ya ulimi
      • Mwinuko wa ulimi-chini
      • Ni tandazwa
    2. Bainisha silabi katika maneno yafuatayo. (alama 2)
      1. Nywesha -KKIKI ii. Gongwa-KIKKKI
    3. Akifisha sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti ili kuleta maana mbili kidhamira/kimajukumu (alama 2)
      Mtihani utafanywa leo
      • Mtihani utafanywa leo. (taarifa)
      • Mtihani utafanywa leo? (swali)
      • Mtihani utafanywa leo! (hisishi/mshangao)
    4. Bainisha mofimu katika neno lifuatalo:
      1. Hajamjia (alama 3)
        • Ha-kikanushi cha nafsi, ja- kikanushi cha hali, m-kitendwa, j-mzizi, -i- kauli -a- kiishio ½ x 6=3 ii. (alama 3)
    5. Eleza dhima ya viambishi tamati mbali na kauli ya kutenda/kiishio: (alama 2)
      1. Kauli ya kutendea/kutendesha – walimsomesha
      2. Kirejeshi – aliaye
      3. Kiulizi – wasomaje/walani
      4. Rai/ombi- nisaidie
    6. Ziweke nomino zifuatazo katika ngeli zao (alama 2)
      1. Wembe –U-ZI
      2. parachichi –LI-YA
    7. Andika kwa wingi. (alama 1)
      Ua wake una ua zuri na kubwa
      • Nyua zao zina maua mazuri makubwa.
    8. Huku ukitoa mifano, bainisha miundo miwili ya nomino za ngeli ya U-I (alama 2)
      1. M-MI- mto-mito
      2. MW-MI- mwezi-miezi
      3. MU-MI- muhula-mihula/muhogo-mihogo
    9. Tunga sentensi kuonyesha nomino zifuatazo (alama 2)
      Kadiaria jibu la mwanafunzi.
    10. Changanua kwa kielelezo cha sanduku (alama 3)

      S

      KN

      KT

      N

      Ts

      T

      N

      V

      E

      Maimuna

      Hupenda

      kufanya

      kazi

      nyingi

      kupindukia

    11. Tunga sentensi kuonyesha tofauti kati ya:
      1. Kiwakilishi cha nafsi huru na kiwakilishi cha nafsi tegemezi (alama 2)
        Mimi/sisi/wewe/nyinyi/yeye/ wao- nafsi huru (atunge sentensi)
        Nitakuja/tutakuja/utakuja/mtakuja/atakuja/watakuja –nafsi tegemezi
      2. Kiwakilishi cha ‘a’ unganifu na kivumishi cha ‘a’ unganifu (alama 2)
        • Cha mtoto kimevunjika (kiwakilishi cha ‘a’ unganifu)
        • Kiti cha mtoto kimevunjika (kivumishi cha ‘a’ unganifu
          Tanbihi: Sharti apigie kistari a pamoja na nomino na si ‘a’ pekee itakuwa kihusishi cha ‘a’ unganifu
    12. Chagizo-hospitalini,alimokimbilia alama 1
      Kijalizo-hospitalini alimokimbilia matibabu ya kuugua alama 1
      Kiarifa-yu hospitalini alimokimbilia matibabu ya kuugua alama 1
    13. Tambua vielezi vinne katika sentensi ifuatayo (alama 2)
      Mwalimu mkali sana alitufunza jana mara tatu uwanjani.
      1. Sana- namna
      2. Jana- wakati
      3. Mara tatu –idadi/kiasi
      4. Uwanjani-mahali ½ x 4=2
    14. Tunga sentensi kubainisha viunganishi vifuatavyo. (alama 2)
      1. Kiunganishi cha kinyume
        • Lakini,ilhali,bali,ingawa,ijapo : Mwalimu alitufunza lakini hakutupa zoezi ii. Kiunganishi cha uteuzi
        • au,ama , : Mgeni anaweza kula wali au kitoweo 1 x 2=2
    15. Tumia vihisishi vifauatavyo kwenye sentensi kuleta dhana iliyokusudiwa (alama 2)
      1. Naam!
        • Kihisishi cha kuitika au kuafikiana . Naam! Amepata kuelewa vizuri. 
      2. Kefule!
        • Kihisishi cha kubeza au kudharau: Kefule! Utapata wapi hela za kusafiri ughaibuni?
    16. Tunga sentensi kubainisha matumizi yafuatayo ya kiambishi ‘na’ (alama 2)
      1. Wakati uliopo
        • Mwalimu anaandik ubaoni
      2. Kihusishi mtendi/mtendaji
        • Maswali haya tulipewa na mwalimu. Chakula hiki kilipikwa na mpishi
    17. Tambua vihusishi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      1. Rais mteule alipiga dua kabla ya kusimama kwa haraka juu ya jukwaa
        • Kabla ya- kihusishi cha wakati
        • Kwa- kihusishi cha namna
        • Juu ya –kihusishi cha mahali 1 x 2=2
    18. Tunasema kifurushi cha kalamu kicha cha mboga shumbi ya udongo. (al. 2)

4. ISIMU JAMII (alama 5)

  1.  
    1. Kutumia lugha rahisi ya kueleweka na wanafunzi.
    2. Kuchanganya ndimi ili kutaka dhana/ maelezo Fulani yaeleweke zaidi.
    3. Kutumia ucheshi ili kusisimua.
    4. Kurudia baadhi ya mambo nitayotaka kusisitiza.
    5. Kuhusisha nyimbo za mafunzo ili kufanya mazungumzo yavutie.
    6. Kuwahusisha kwa vipindi vya maswali na majibu.
    7. Kuwapa mada za kujadili katika makundi ili kila mmoja ahusike kufanya jambo.
    8. Kutoa mifano ya mambo wanayoyafahamu vizuri.
  2.  
    1. madhumuni- Watu Huteua msamiati kulingana na sababu ya mazungumzo yao. Kwa mfano ikiwa ni mazungumzo ya kumshawishi mtu, mzungumzaji huteua maneno ya kushawishi.
      Mtu hutumia toni tofauti kulingana na madhumuni.
      Madhumuni huamua lugha ambayo mtu atatumia. Kuchanganya ndimi/usanifu wa lugha n.k
    2. Uana- Kuna tofauti baina ya lugha ya wanaume na wanawake. Kwa mfano lugha ya wanawake usheheni matumizi mengi ya vihisishi kinyume na ili ya wanaume.
  3.  (alama 3)
    1. Ongezeko la walimu wa Kiswahili
    2. Vitabu na machapisho zaidi ya Kiswahili Kukifanya Kiswahili lugha ya taifa na rasmi
    3. Kiswahili ni somo la lazima shule za msingi na za upili Kiswahili kufunzwa vyuoni
    4. Kuwa na vyama vya Kiswahili katika shule Utafiti zaidi wa Kiswahili
    5. Makongamano ya kuimarisha Kiswahili kwa walimu na wanafunzi Vipindi vya maigizo kwa Kiswahili/
    6. Taarifa za habari na magazeti ya Kiswahili Kuna vituo vya redio na runinga vinavyopitisha ujumbe kwa Kiswahili tu
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Londiani Joint Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?