Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Catholic Diocese of Kakamega Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu
  2. Jibu maswali yote
  1. UFAHAMU                                             (alama 15)
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yanayobadilika mno. Mtazamo wake maishani ni tofauti kabisa na ule wa wanawake walioishi karne za ishirini na kumi na tisa. Yeye hatarajii kuzaliwa, kukua, kuolewa, kuwa mke wa bwana, kumzalia mumewe watoto na daima dawamu kuwa mwendani wa vijungu jikoni akiwapikia watoto wa bwanake chakula na akitoka jikoni aelekee shambani kulima, kichakani kuchanja kuni, mtoni kufua nguo na kuteka maji ya kutumia nyumbani. Mwanamke wa kisasa huandamana na mwanamume. Akanyagapo mume papo naye huutia wayo wake.

    Mwanamke wa kisasa huenda shule na kujifunza yote yafunzwayo huko. Hushindana na wanawake kwa wanaume na kuibuka mshindi si mara haba. Huibuka mshindi katika masomo ya lugha, historia, jiografia, hesabu, sayansi na mengineyo sawa na mwanamume.

    Mwanamke wa kisasa huzifanya kazi zote. Kuna walimu, madaktari, wahandisi n ahata mabalozi. Mwanamke wa kileo si tena mama jikoni. Anataka apae angani, apigane vitani bila kusaza kushiriki katika uongozi wa mataifa yao. Wametokea wanawake waliotamalaki ulimwenguni mzima. Marehemu waziri mkuu wa Uingereza Margaret Thatcher ni miongoni mwa wanawake mashuhuri waliosifika katika ulimwengu huu.

    Siku hizi mwanamke huolewa tu wakati amepata kazi ya kumwezesha kujikimu maishani au pale anapokuwa na hakika kwamba biashara yake, iwapo ni mfanyi biashara, imepiga hatua ya kutomrudisha ukatani.

    Mwanamke wa kisasa haamuliwi jambo lolote, bali hufanya maamuzi yake mwenyewe. Kuna upande mwingine, mwanamume wa kisasa, ambaye bado amefungwa pingu na taasubi za kiume, hapendezwi na mwanamke huyu. Huuma kidole akitamanai ya kale lakini wapi! Analazimika kumkubali mwanamke huyu kama mshirika sawa maishani, na kuishi naye, apende asipende. Shingo upande analazimika kukubali kwamba mabadiliko haya sio mithili ya kiwingu kipitacho, bali ni aushi.
    1. Msemo 'mwendani wa vijungu jiko' unadhihirisha hali gani ya mwanamke katika jamii? (alama 2)
    2. Jamii inafanya mwanamke kuwa hayawani wa mzigo. Fafanua  (alama 2)
    3. Eleza maana ya akanyagapo mume. Naye papo huutia wayo wake. (alama 1)
    4. Tofauti zipi za kimsingi zilizopo baina ya mwanamke wa kisasa na wa zamani?  (alama 3)
    5. Mwanamume wa kisasa anamwonaje mwanamke wa kisasa?  (alama 1)
    6. Taja mifano mitatu ya mawazo ya kihafidhina kama yanavyojitokeza makalani. (alama 3)
    7. Eleza maana ya:
      1. Tamalaki
      2. Ukatani
      3. Taasubi za kiume      (alama 3)
  2. UFUPISHO
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Ukame ni tukio hatari la kimaumbile. Athari zake hutofautiana kutoka eneo moja hadi lingine. Kwa sababu hiyo, si rahisi kuelewa dhana ya ukame; kwa hakika si rahisi kuifafanua dhana hii. Katika eneo la Bali, kwa mfano, isiponyesha kwa muda wa siku sita wenyeji huchukulia hali hiyo kuwa ukame japo kiasi hicho cha mvua ni kikubwa mno ikilinganishwa na Libya ambayo hupata kiasi kidogo cha chini ya milimita 180 ya mvua kwa mwaka.
    Katika hali ya kawaida ukame hutokana na kipindi kirefu cha uhaba wa mvua hasa katika mwaka mzima au zaidi. Uhaba huu wa mvua huweza kusababisha uhaba wa maji kwa shughuli, kundi au sekta Fulani. Shughuli za binadamu huweza kufanya hali ya ukame kuwa mbaya zaidi. Shughuli hizo ni pamoja na kilimo, unyunyiziaji maji na ukataji wa miti.
    Ni vigumu kubaini wakati mahususi ambao ukame huanza kwani kipindi hicho cha ukosefu wa mvua huwa cha mfululizo, nae neo huendelea kupata mvua iliyopungua kwa miezi au hata miaka. Mimea hukauka na wanyama hufa kutokana na ukosefu wa maji. Ukame basi huwa tayari kwa maisha ya binadamu na viumbe wengine kwa kuwa huweza kusababisha njaa na kuyafanya maeneo kuwa majangwa.
    Mbali na ukosefu wa mvua, ukame pia husababishwa na kiangazi. Kiangazi huongeza kiwango cha joto. Joto hilo hufanya maji yaliyohifadhiwa kuwa mvuke haraka, hivyo kiwango chake kupungua. Hali ya el ninyo pia husababisha ukame katika baadhi ya maeneo ambayo huwa hayana mvua. Upepo huivutia mvua mahali panaponyesha na kuliacha kame eneo ambalo halina mvua ya aina hii. Hata katika maeneo yenye mvua ya el ninyo, kiangazi kikali huifuata na hivyo kusababisha ukame. Hali hii huitwa la nina. Mambo yanayotokana na mabadiliko ya hali ya anga ulimwenguni pia yanaweza kuchangia kuwepo ukame. Ongezeko la joto duniani linafanya hali ya ukame kuwa mbaya Zaidi.
    Ukame una madhara chungu nzima kwa binadamu. Madhara hayo huweza kuwa ya kiuchumi, kimazingira au hata kijamii. Ukame husababisha kupungua kwa mimea na mavuno. Huweza pia kutokea dhoruba za mchanga. Dhoruba hizi hutokea palipo na jangwa. Ukosefu wa maji ya kunyunyizia mimea husababisha njaa na magonjwa kama vile utapiamlo yanayotokana na ukosefu wa lishe bora. Makazi ya wanyama wa nchi kavu na wale wa majini pia huathiriwa vibaya. Hali kadhalika, ukame husababisha uhamaji. Hii inamaanisha kuwa jamii huweza kutoka katika makazi asilia na wakati mwingine huweza hata kuwa wakimbizi.
    Ukame husababisha ukosefu mkubwa wa maji. Ukosefu huu huwa na athari hasi kwa maendeleo ya viwanda kwa kuwa vingi huhitaji kiasi kikubwa cha maji. Juu ya hayo, maji huhitajika katika kuzalisha umeme. Umeme una matumizi mengi katika viwanda, nyumbani, afisini na hata hospitalini. Ukosefu wa umeme basi huwa ni tatizo kuu.
    Aidha, ukame husababisha madhara mengi, binadamu wanaweza kujikinga kutokana na uhaba wa rasilimali za asili kama vile chakula na maji. Pia mioto mikubwa huweza kuenea haraka wakati wa ukame na hivyo kusababisha vifo vya binadamu na wanyama na uharibifu wa rasilimali nyingine.
    Ingawa ukame husababisha madhara mengi, binadamu wanaweza kujikinga kutokana nao kwa kupunguza makali ya ukame. Jambo la kwanza wanaloweza kufanya binadamu ni kuhifadhi maji. Maji ya mvua yanafaa kuhifadhiwa katika mabwawa na mapipa. Haya yanaweza kutumiwa wakati wa ukame hasa katika kukuza mimea. Mkakati mwingine ni kutumia mbinu za kupunguza chumvi na kemikali nyingine zilizomo kwenye maji ya bahari ili yaweze kutumika katika unyunyiziaji wa mimea. Hili litapunguza tatizo la ukosefu wa chakula. Pia ni muhimu kufanya utafiti kuhusu hali ya anga ili kupanga na kuweka mikakati ifaayo kukabiliana na hali hiyo.
    Ni muhimu kuwa na mipangilio mizuri ya matumizi ya ardhi. Mathalani upanzi wa mimea itakayozuia mmomonyoko wa udongo, kubadili aina ya mimea inayokuzwa sehemu fulani Pamoja na upanzi wa mimea isiyohitaji mvua nyingi ni hatua mwafaka. Aidha, ni vizuri kupunguza matumizi ya maji hasa katika mazingira ya nyumbani kwa mfano tunapofua na kuosha. Njia nyingine ya kukabiliana na tatizo hili ni kusafisha maji yaliyotumiwa ili kuyatumia tena.
    1. Kwa maneno 50, eleza visababishi vya ukame kwa mujibu wa taarifa          (alama 4; 1 mtiririko).
      • Matayarisho      
      • Nakala safi
    2. Fupisha ujumbe wa aya ya tano hadi saba kwa maneno 70.                         (alama 6; 1 mtiririko)
      • Matayarisho
      • Nakala safi
    3. Eleza masuala ambayo mwandishi ameibua katika aya mbili za mwisho kwa maneno 60.        (alama 5; 1 mtiririko)
      • Matayarisho
      • Nakala safi
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Andika neno lenye muundo ufuatao.                        (alama 40)  (alama 2)
      Kipasuo ghuna cha midomo, irabu ya kati mbele, kipasuo hafifu cha ufizi, irabu ya juu mbele.
    2. Weka shadda kwenye neno ALA ili kutoa maana mbili tofauti.  (alama 2)
    3. Tasfidi sentensi kwa wakati ujao hali timilifu.               (alama 2)
      Mama alizaa msichana.
    4. Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizoko mabanoni.
      1. Chota (tendesha)                         (alama 2)
      2. Fa (tendea)                                  (alama 2)
    5. Ainisha mofimu katika neno lifuatalo: KATIKA (Kitenzi)        (alama 3)
    6. Unda nomino mojamoja kwa kila kitenzi.                                  (alama 2)
      1. Shuku
      2. Kwea
    7. Eleza matumizi ya kiambishi 'O' katika sentensi ifuatayo.        (alama 2)
      Waliopita mtihani walifanya marudio vizuri.
    8. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia matawi                 (alama 4)
      Wanafunzi wengi walipita mtihani ulioandaliwa.
    9. Toa mfano mmoja wa neno lenye muundo wa silabi ufuatao KIK          (alama 1)
    10. Andika katika ukubwa wingi.                                                       (alama 2)
      Meza ilikarabatiwa kwa nyundo ile
    11. Mwadime alinunua simutamba mpya kwa shilingi elfu kumi na kumtuza mwanafunzi bora.   (alama 3)
      (Anza sentensi kwa shamirisho kitondo)
    12. Onyesha miundo yoyote miwili ya majina ya ngeli ya LI-YA.                       (alama 2)
    13. Tambua aina za virai katika sentensi ifuatayo.                                    (alama 3)
      Aisee! Yale mawimbi ya tsunami yaliangamiza biashara nyingi.
    14. Tunga sentensi moja kudhihirisha maana mbili ya neno BUNDA.                   (alama 2)
    15. Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi.                                         (alama 3)
      Kibibi alisema kuwa kile kiguu cha kijibwa cheusi siku hiyo kingekuwa marufuku kwake.
    16. Tambua maana mbili ya sentensi ifuatayo: Waite wale                          (alama 2)
    17. Eleza matumizi matatu ya kibainishi.                                                         (alama 3)
  4. ISIMUJAMII
    1. Eleza sifa nne za lugha ambayo wewe kama nyapara wa kiwanda cha kuoka mikate cha matopeni utatumia ukiwahutubia walio chini yako.               (alama 4)
    2. Taja lahaja zozote tatu za Kiswahili zinazozungumzwa Pwani mwa Kenya.                  (alama 3)
    3. Thibitisha kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu.                                               (alama 3)

MARKING SCHEME

  1. MAJIBU YA UFAHAMU
    1. Hali duni AU
      Nafasi yake ni jikoni          (Yoyote 1×2=2)
    2. Jamii imemfanya mwanamke kuwa mjakazi/imemtwika majukumu mengi ya sulubu kama
      vile kulima, kuchanja kuni, kufua, kuteka maji n.k.        (alama 2) 
    3. Kila afanyalo mwanamme, mwanamke vilevile aweza kufanya.              (alama 1)
    4. Mwanamke wa kisasa huenda shule
      Yeye huzifanya kazi zote afanyazo mwanamume kama ualimu, udaktari, uhandisi n.k si ma- ma jikoni kama wa hapo awali
      Ana sauti yaani anatetea haki yake
      Anajikimu si kama awali aliyetegemea mume
      Hufanya maamuzi mwenyewe si kama wa awali aliyeamuliwa na mume                 (Zozote 3×1=3)
    5. Amehiari kumkubali japo shingo upande.                 (alama 1)
      1. Kuwa mwanamke anapaswa kumzalia mumewe watoto na daima kuwa mwandani wa vijungu jikoni
      2. Mwanamke kuamuliwa mambo na mwanamume
      3. Anapaswa kufyata ulimi                                              (zozote 3×1=3)
    6. Maana ya
      1. Tamalaki-kuwa na uwezo
      2. Ukatani-umaskini
      3. Taasubi za kiume-ubabedume
        -mwanamume kujiona bora                        (alama 3)
  2. UFUPISHO/MUKHTASARI (alama 15)
    1.                                       (3 zozote, 1 mtiririko)
      • Uhaba wa mvua
      • Shughuli za binadamu kama vile kilimo, unyunyiziaji maji na ukataji miti
      • Kiangazi
      • Hali ya el ninyo
      • Mabadiliko ya hali ya anga
    2.                                      (5 zozote, 1 mtiririko)
      • Madhara ya ukame ni mengi
      • Madhara ya kiuchumi, kimazingira na hata kijamii
      • Kupungua kwa mimea na mavuno
      • Dhoruba yam changa
      • Njaa na magonjwa
      • Kuathiriwa vibaya kwa makaazi ya wanyama wa nchi kavu na majini
      • Uhamaji
      • Ukosefu wa maji
      • Ukosefu wa umeme
      • Uhasama kwa jamii
      • Mioto
    3.                                        (4 zozote, 1 mtiririko)
      • Kuhifadhi maji
      • Kutumia mbinu za kupunguza chumvi na kemikali zingine zilizomo kwenye maji ya bahari
      • Kufanya utafiti kuhusu hali ya anga ili kupanga mikakati ifaayo kukabiliana na hali hiyo ✓ Kuwa na mpangilio mzuri wa matumizi ya ardhi
      • Upanzi wa mimea inayozuia mmomonyoko wa udongo
      • Kubadili aina ya mimea inayokuzwa sehemu fulani
            Wale-kiashiria cha mbali
    4.  
      1. kudhihirisha sauti ya king'ongo. i.f. ng'ombe
      2. Kuonyesha sauti/silabi Fulani imedondoshwa kwenye neno k.m
        n'sasa-ni sasa
      3. Kuonyesha kuwa tarakimu Fulani imedondoshwa m.f Alizaliwa mwaka' 99
  3. ISIMU JAMII (alama 10)
    1. Sifa za sajili ya viwandani
      • Matumizi ya msamiati teule-unda
      • Kuchanganya ndimi-nani yuko duty
      • Sentensi ndefu ndefu ili kutoa taratibu na masharti Lugha ya udadisi ili kujua ukweli wa suala Fulani
      • Maswali balagha-ukichelewa kazini, unataka nini Lugha ya ukali-hakuna kubembelezana tena!
      • Lugha ya maagizo/amrishi-mtu yeyote asipige simu wakati wa kazi 
      • Utohozi-mashine,meneja
      • Lugha ya kauli kamilifu ili kueleweka bila utata
      • Lugha ya misimu-sitaki uniletee!
      • Lugha legevu-baadhi ya wafanyikazi huenda hawana kisomo kingi
        Lahaja za Kiswahili mnchini Kenya
    2. Kiamu, kipate, kitikuu, kibajuni, kisiu, kimvita, kijomvu, kingare, kivumbi, kimvita, kingozi   Zozote 3 x 1 = Alama 3
    3. Ushahidi kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu
      • Msamiati wake unalingana na ule wa lugha za kibantu k.m mtu mguu
      • Mpangilio mwa sauti kuunda silabi. Una muundo wa Kl + Kl
      • Mfumo wa m ngeli - Kiswahili mkama lugha nyingi za kibantu huainisha nomino zake katika ngeli
      • Mnyambuliko wa vitenzi
      • Viishio mvya kitenzi katika lugha za kibantu ni 'a'   Zozote 3 x 1 = Alama 3
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Catholic Diocese of Kakamega Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?