Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Catholic Diocese of Kakamega Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Jibu maswali Manne pekee
  2. Swali la kwanza ni la lazima
  3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu zingine zilizobaki yaani, Riwaya, Tamthilia, Hadithi fupi na Fasihi simulizi.

SEHEMU A: USHAIRI

  1. LAZIMA
    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Daima alfajiri na mapema
    Hunipita na jembe na kotama
    Katika njia iendayo Kondeni
    Kama walivyofanya babuze zamani;
    Nimuonapo huwa anatabasamu
    Kama mtu aliye na kubwa hamu
    Kushika mpini na kutokwa jasho
    Ili kujikimu kupata malisho

    Anapotembea anasikiliza
    Videge vya anga vinavyotuimbiza
    Utadhani huwa vimengojea
    Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
    Pia pepo baridi kumpepea
    Rihi ya maua zikimletea
    Nao umande kumbusu miguu;
    Na miti yote hujipinda migongo;
    Na yeye kuendelea kwa furaha
    Kuliko yeyote ninayemjua
    Akichekelea ha ha ha ha ha...

    Na mimi kubaki kujiuliza
    Kuna siri gani inayomliza?
    Au ni kujua au kutojua?
    Furaha ya mtu ni furaha gani
    Katika dunia inayomhini?
    Ukali wa jua wamnyima zao
    Soko la dunia lamkaba koo;
    Dini za kudhani zamsonya roho
    Ayalimia matumbo ya waroho;
    Kuna jambo gani linamridhisha?
    Kama si kujua ni kutokujua
    Laiti angalijua, laiti angalijua!

    MASWALI
    1. Eleza hali ya mzungumzaji katika shairi hili.     (alama 3)
    2. Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili.    (alama 2)
    3. Fafanua aina mbili za taswira ukirejelea ubeti wa pili.     (alama 2)
    4. Bainisha vipengele viwili vya kimtindo katika shairi hili.     (alama 2)
    5. Bainisha aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili.     (alama 2)
    6. Eleza toni ya shairi hili.     (alama 2)
    7. Tambua nafsineni katika shairi hili.    (alama 1)
    8. Eleza muundo wa shairi hili.    (alama 2)
    9. Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari.      (alama 4)

SEHEMU B: RIWAYA

A. Matei-Chozi La Heri
Jibu swali la 2 au la 3

  1. "Dickson wewe jikaze. Mzee wako hayupo hapa....."
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
    2. Bainisha hali inayorejelewa ambayo ilimhitaji mhusika huyu kujikaza.(alama 2)
    3. Jadili mikakati ambayo mrejelewa alitumia kukabiliana na hali yake.(alama 6)
    4. Eleza umuhimu wa mandhari yanayorejelewa katika dondoo hili.(alama 8)
  2. Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo.(alama 6)

    1. Lakini kumbuka mtu huenda msalani baada ya shibe! Tumbo shinda hata haja ndogo haliendi! Ugenini humu hamkuwa na mashamba. Waliokuwa wamebahatika kwa kubeba nafaka haba walizotoa zikatumiwa kwa ujima. Sasa matumbo yalianza kudai haki hata baada ya kujua kuwa haki yenyewe haikuwa mikononi mwetu. Haki ilikuwa mikononi mwa walio na nguvu ambao ndio waliotufanya kuwa wageni wa pori. Vilio vya watoto wenye njaa vilianza kusikika. Polepole vilio hivi vilianza kupungua, njaa na ugonjwa vimefanya kazi. Nilianza kufikiria kuwa hali ikiendelea hivi tutaipungia dunia mkono.

    2. "Wakati mwingine tunashiriki katika njama zao chafu za kifisadi, tunawasaidia vikongwe
      wasiojua kusoma na kuandika.....afaaye! mama unataka KIBOKO, au PAPA?
      1. Tambua swala linalodokezwa katika kauli hii.(alama 2)
      2. Wanaorejelewa katika kauli hii, wamechangia kurudisha nyuma maendeleo ya jamii kwa njia mbalimbali. Fafanua
        (alama 12).

SEHEMU C: TAMTHILIA
Timothy M. Arege: Bembea ya Maisha
Jibu swali la 4 au la 5.

  1. "Ndivyo...ndivyo...hayakuishia hapo. Baada ya ile mvua ya baraka iliyowanyea, watu walianza tena
    kuwasema kuwa hawana mtoto wa kiume."
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
      (alama 4)
    2. Tambua mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili.
      (alama 2)
    3. Fafanua umuhimu wa msemaji katika kuijenga tamthilia hii.
      (alama 4)
    4. Eleza sifa mbili za msemaji wa kauli hii.
      (alama 2)
    5. Kwa kutolea mifano, onyesha jinsi mwandishi alivyoshughulikia maudhi ya utamaduni wa kale katika tamthilia hii.
      (alama 8)
    1. Jadili changamoto zinazokumba asasi ya ndoa kwa mujibu wa tamthilia ya Bembea ya Maisha.
      (alama 8)
    2. Asna na Sara ni wahusika wawili wenye mitazamo tofauti kuhusu maisha. Thibitisha.
      (alama 6)
    3. Changanua mtindo katika dondoo hili.
      Ukilazwa tayari unakuwa umeonja seli. Hata wenyewe hawana mlahaka mwema. Amri na vitisho kama askari. Unashindwa kama uuguze moyo ama ugonjwa. Katika wodi hewa iliyojaa harufu ya dawa imezagaa, vitanda vimesalimu amri mpaka shiti zikagura. Yaani hali nzima haikupi matumaini ya kutoka ukiwa bora.
      (alama 6)

SEHEMU D: HADITHI FUPI
D.W Lutomia na P. Muthama
Mapambazuko ya Machweo na Hadithi Nyingine.
Jibu swali la 6 au 7

  1. Wanawake wanafaa kujilaumu kwa kudhalilishwa na jamii. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo:
    1. Fadhili za Punda.
      (alama 10)
    2. Kifo cha Suluhu.
      (alama 10)
  2. Rayya Timammy: Ahadi ni Deni.
    (alama 6)
    1. Changanua mtindo katika dondoo hili. Maneno hayo yalikua kama hirizi aliyoamua kuivaa ili yamwongoze na aliamua hilo akijiambia kimoyomoyo kuwa ingawa babake hayupo tena; hata huo mwaka haukufika nusu alipata tena habari mbaya... mwalimu mkuu alimwita afisini siku hiyo kutoka darasani...Alipofika afisini mwa mwalimu mkuu, mwalimu mkuu aliweza kusoma wahaka usoni mwake. Akanena naye kwa upole...Aliona kuwa shule yake ingefanya vyema sana kama wasichana wote wangekuwa...kwa vitendo!
    2. Bainisha mbinu mbili zinazoweza kutumiwa kutambua sifa za mrejelewa wa maneno haya.
      (alama 2)
    3. "Likizo ilipoisha alirudi kwanza kidato cha pili lakini moyo ulikuwa mzito. Jambo lilompa ari ya kufanya hivyo ni yale mazungumzo ya mwisho na babake."
      1. Tambua suala linalodokezwa katika kauli hii.
        (alama 2) 
      2. Fafanua sifa mbili za mrejelewa katika kauli hii.
        (alama 2)
      3. Suala ulilotaja hapo juu (i) limekumbwa na changamoto mbalimbali katika hadithi hii. Fafanua.
        (alama 8)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

  1. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
    Hapo zamani za kale paliishi mtoto katika kisima kimoja. Siku moja mtoto huyu aliokota kijiwe karibu na soko kuu. Kijiwe kilikuwa kikimeremeta kwa rangi mbalimbali na kilizingirwa na pete ya dhahabu.

    Mtoto huyu na wenzake walianza kurushiana kijiwe hicho. Baada ya muda kilianza kuongezeka umbo na kuonekana kama kiwiliwili cha binadamu. Kikaanza kuwakimbiza wale watoto. Kutokana na ukelele wao watu walikuja kutazama nini kilikuwa cha mno. Walipofika walikutana ana kwa ana na dubwana hilo. Lilizidi kuongezeka umbo na likawameza wote pamoja na mifugo wao. Wachache waliojaribu kukimbia liliwashika kwa mikono yake mipana na mirefu. Kwa bahati njema alikuwepo mama mmoja aliyeona haya yote. Alikuwa mbali na hapo. Aliteremka kutoka kilele cha mlima na kuwapata wakulima makondeni na sawia akawajuza kuhusu kitendo kilichomwogofya sana. Wote wakaacha shughuli zao na wakatwaa silaha zao wakaelekea soko kuu.

    Dude sasa lilikuwa limejilaza baada ya shibe, wakulima wale walichagua watu sita ambao walijulikana kwa ushujaa wao. Pamoja walilinyemelea lile nyangarika na kulikata mara moja. Lilitoa mkoromo mkuu kabla halijakata kamba. Punde, wanakijiji kwa uangalifu mkubwa walitoboa tumbo lake wakitarajia kupata maiti za wapenzi wao pamoja na mifugo wao. Wote walijawa na furaha kuu walipoona wapenzi wao wakijichomoza kutoka tumboni, mmoja baada ya mwingine hadi akatoka yule wa mwisho. Mbuzi, kondoo na ng'ombe wote walitoka mmoja mmoja.

    Siku hiyo kuliandaliwa sherehe ya kumshukuru Muumba kwa wema wake. Watoto walishauriwa wasithubutu kuchezea vitu wasivyovijua.

MASWALI.

  1. Bainisha kipera cha utungo huu.
    (alama 1)
  2. Eleza mambo matatu yanayoonyesha kwamba kipera hiki ni sanaa.
    (alama 3)
  3. Tambua mifano miwili ya fantasia katika hadithi hii.
    (alama 2)
  4. Unakusudia kutumia mbinu ya kushiriki kufanya utafiti kuhusu tungo za aina hii. Eleza manufaa manne ya mbinu hii.
    (alama 4)
  5. Fafanua mikakati sita ambayo jamii inaweza kutumia ili kuudumisha utanzu huu.
    (alama 6)
  6. Bainisha shughuli mbili za kiuchumi na mbili za kijamii zinazoendelezwa na jamii inayojawiriwa katika utungo huu.
    (alama 4)

MWONGOZO WA KARATASI YA TATU

  1. SEHEMU YA A: MWONGOZO WA USHAIRI
      1. Mwenye tumaini/tamaa-kubwa hamu
      2. Mwenye bidii-alfajiri na, mapema, kutokwa na jasho
      3. Anayefurahia mandhari-anapotembea anasikiliza videge
      4. Mtulivu-kuna siri gani inayomliwaza
      5. Aliyedhulumiwa-soko la dunia lamkaba koo
      6. Aliyeridhika-kuna jambo gani?
        (3x1=3)
      1. Inkisari-babuze-babu zake
      2. Kufinyanga sarufi/miundo ngeu ya kisintaksia-kubwa hamu-hamu kubwa
        (2x1=2)
      1. Taswira mnuso/harufu-rihi ya maua
      2. Taswira mguso-kumpapasa, kumbusu miguu
      3. Taswira usikivu-anasikiliza videge
      4. Taswira ya mwendo-yeye kuendelea kwa furaha
        (2×1=2)
      1. Tashhisi-umande kumbusu, miti kumpapasa, upepo kumpepea
      2. Kinaya-nafsineni inafurahi ilhali dunia inamhini
      3. Tashbihi-kama mtu aliye na kubwa hamu
        (2×1=2)
      1. Urudiaji wa maneno-kama-ubeti 1
                                      -furaha-ubeti 3
      2. Urudiaji wa sauti-a, a-ubeti 2,3
                                     -0, 0-ubeti 3
      3. Urudiaji wa silabi-ma, ma, za, za, ha, ha
        (2×1=2)
      1. Toni ya uchungu-furaha ya mtu ni furaha gani katika dunia inayomhini?
      2. Toni ya kuajabia/kushangazwa na jambo-kuna jambo gani linamridhisha?
      3. Kuhuzunisha/masikitiko/kuhurumia-laiti angalijua
        1x2=2
        Kutaja-1
        Kueleza-1
      1. Mtetezi wa haki/aliyezinduka anayelalamikia dhuluma ya wanyonge
      2. Mtu anayemtazama mkulima kipita
        (1×1=1)
      1. Lina beti tatu
      2. Kila ubeti una idadi tofauti ya mishororo na beti nyingine
      3. Kila mshororo una kipande kimoja
      4. Shairi halina mpangilio maalum wa vina
      5. Idadi ya mizani katika mishororo inatofautiana
        (2×1)
    1. Kila alfajiri na mapema ananipita na jembe na kotama katika njia inayoenda shambani kama
      waliyofanya mababu zake zamani; ninapomuona huwa anatabasamu kama mtu aliye na hamu kubwa. Anashika mpini na kutokwa jasho ili ajikimu
      (4×1=4)

SEHEMU YA B: RIWAYA CHOZI LA HERI

  1. "Dickson wewe jikaze. Mzee wako hayupo hapa..."
    1. Mawazo ya Dick
      Akiwa katika uwanja wa ndege akisubiri kukaguliwa Anakumbuka hapo awali alipokuwa akitumiwa kuuza dawa za kulevya. Mara nyingine aliponea chupuchupu kunaswa ndipo angejiambia maneno haya
      (4×1=4)
    2. Sauna alimpeleka kwa Buda ambaye alimlazimisha Dick kulangua dawa za kulevya na
      kuhatarisha maisha yake
      (alama 2)
    3. Alikubali kulangua dawa za kulevya ili kuepuka adhabu ya mwajiri wake
      Ili kukimu mahitaji yake, alilazimika kulangua dawa za kulevya
      Kuuchukulia uamuzi wake wa kuingilia maovu kwamba ni hali aliyoandikiwa na mwenyezi mungu
      Aliwazia matendo yake na kuamua kuacha ulanguzi wa dawa
      Kujiendeleza kitaaluma-alisomea teknolojia ya mawasiliano Alianzisha biashara ya vifaa vya mawasiliano
      (6x1=6)
      1. Kubainisha migogoro katika riwaya-dickson kuibwa na sauna aliyemtosa katika ulaghai wa dawa za kulevya
      2. Kubainisha changamoto zinazowakumba watoto baada ya ndoa kuvunjika
      3. Kuwatambulisha wahusika k.m Dickson, Sauna, Buda
      4. Kuonyesha sifa za wahusika - Dickson, Sauna
      5. Kuchimuza maudhui k.m ulanguzi wa dawa za kulevya, wizi wa watoto, elimu, mabadiliko
      6. Kuibua dhamira ya mwandishi k.m umuhimu wa elimu katika kujiendeleza
      7. Kuendeleza ploti-kuturudisha nyuma kwenye kisa cha Sauna kuwaiba Dick na mwaliko
      8. Hapa ndipo Umu na Dick walikutana baada ya kutenganishwa na Sauna
        (Zozote 4×2)
  2.  
    1.  
      1. Tashhisi-Tumbo shinda hata haja ndogo haliendi!
                      Sasa matumbo yalianza kudai haki...
      2. Takriri-vilio, vilio
      3. Taswira-(Sikivu) vilio vya watoto wenye njaa vilianza kusikika
      4. Nahau-pungia dunia mkono
      5. Mbinu rejeshi/kisengere nyuma-waliokuwa wamebahatika kubeba nafaka...
      6. Tasfida-haja ndogo haliendi             (6×1=6)
    2.  
      1. Siasa/uchaguzi     (1×2=2)
      2. Wanaorejelewa ni "Vijana"
        • Wanapalilia ufisadi kwa kutumiwa na wagombeaji uongozi kuwaibia kura
        • Wanasababisha uharibifu wa mali kwa kuchoma magari
        • Wanasababisha mauaji kwa kuwachomea watu kwenye magari. (uk 24)
        • Wanaendeleza wizi wa mali ya umma kwa kuiba kwenye maduka
        • Wanaendeleza matumizi mabaya ya vileo. Shamsi anadai kugeukia pombe kwa kuvunjikiwa
        • Wanapalilia utegemezi. Shamsi na yule kijana aliyevaa shati lililoandikwa Hitman wanaulaumu uongozi kwa misiba inayowapata
        • Wanaendeleza desturi kandamizi zinazowaletea madhara. Tuama anapashwa tohara
        • Wanashindwa kujidhibiti hisia na kuishia kujisababishia uzazi nje ya ndoa. Mfano Rehema
        • Wanaingilia burudani bila tahadhari na kusababisha maafa. Mfano Tindi, Lemi
        • Wanaendeleza unyanyasaji wa kimapenzi mabarobaro wanabaka Mwanaheri na Lime
        • Wanaendeleza ulanguzi wa dawa za kulevya. Awali Dick alitumiwa na Buda kusafirisha dawa
        • Wanachangai kuzorota kwa maadili. Sauna anawauzia watu maji ya mito yakiwa kwenye chupa za 'mineral water'.    (12×1=12)
  3. MWONGOZO WA TAMTHILIA
    1. Msemaji-Dina
      Msemewa-Kiwa
      Mahali-nyumbani mwa Dina
      Ni baada ya Kiwa kumtembelea mamake. Mamake anasimulia hali ya ndoa ya Sara mwanzoni
      (4×1=4)
    2. Takriri-Ndivyo...ndivyo
      Mdokezo-ndivyo...
      Kisengere nyuma-baada ya ile mvua ya baraka iliyowanyea, watu walianza tena kuwasema
      (2×1=2)
    3. Dina
      1. Anajenga maudhui mbalimbali. Malezi, ushirikiano
      2. Anachimuza sifa za wahusika wengine kama vile Dina kuwa mlezi mwema
      3. Kielelezo cha watu wenye utu katika jamii. Anamsaidia dina kuandaa chakula wakati alikuwa mgonjwa
      4. Anaendeleza ploti. Anaturudisha kwa matukio ya awali kuhusu maisha ya Sara
        (4×1=4)
    4.  
      1. Mwenye huruma-Sara anapougua, Dina anamsaidia kupika chakula
      2. Mwenye uhusiano mwema-anapoitwa na Sara amsaidie kupika bwana yake anaitikia wito
      3. Mwenye mapenzi ya dhati-anamsaidia rafiki yake kazi ya nyumbani        (Zozote 2×1=al 2)
    5.  
      1. Wanajamii wanasisitiza kuwa familia sharti iwe na mtoto wa kiume. Familia ya Yona inadharauliwa kwa kukosa mtoto wa kiume. (uk 10)
      2. Luka anawaalika wazee wenzake; Yona na Beni ili kuonja mavuno ya kwanza na kuibariki (uk 58)
      3. Bunju anashikilia utamaduni wa kutowakubali wazazi wake au wa Neema kulala nyumbani kwake (uk 24, 29)
      4. Sara anamweleza Asna kuwa siku zao msichana akisha baleghe ilikuwa hana amani. Lazima aozwe. (uk.52)
      5. Mila na desturi za zamani zimewaumba wanaume kama watu wasioweza kusaidia katika kazi za jikoni. (uk. 66)
      6. Sara anaambia Yona kuwa fimbo wanarithi watoto wa kiume, si wa kike. (uk.2)
      7. Yona anaambia Sara kuwa fimbo ya mzee hurithiwa na mtoto wa kwanza (uk.20) Luka anaambia Yona na Beni kuwa zamani mila zao hazikuruhusu watoto wa kike kwenda skuli kurithi kitu (uk.60)       (8×1=alama 8)
  4.  
    1.  
      • Kuchelewa kupata Watoto-Sara na Yona waliitwa wagumba walipokaa muda mrefu bila kuzaa
      • Jamii kuthamini mtoto wa kiume-watu waliwasema Yona na Sara kwa kukosa mtoto wa kiume
      • Wanaume kuwapiga wake zao-Yona alivyompiga Sara kwa kukosa mtoto wa kiume
      • Ulevi-Yona kuingilia ulevi
      • Wanaume kutowajibikia majukumu yao-uk 14 Sara analalamika namna wanawake wanaachiwa kazi zote za nyumbani
      • Kufutwa kazi-Yona alifutwa kazi ya ualimu kwa kuingilia ulevi
      • Wazazi kukosa muda wa kubarizi na watoto wao-Neema alikuwa akifika nyumbani wakati Lemi ashalala, Bela aliishi akifanya kazi hadi wanawe wakapevuka wakawa watu wazima
      • Watoto kulazimika kubeba majukumu ya kwao wakishaolewa-Neema alihitajika kusaidia mamake apate matibabu mjini, kumtumia babake pesa za dawa, kulipia elimu ya wanuna wake. kujengea wazazi wake nyumba
      • Ukosefu wa fedha za kutosha-Bunju kuchukua mkopo wa benki
      • Wazazi kutoelewana katika maswala ya ulezi wa watoto wao-Bunju anamtarajia Lemi kuamka mapema sana, kupata alama bora zaidi shuleni ilhali Neema ana maoni tofauti
        (Zozote 8×1)
    2.  
      • Asna anapenda maisha ya mjini ambapo anaweza kutafuta kazi akafanya ilhali Sara anaona kuwa ni maisha ya shida
      • Asna anafurahia kuishi kwa servant quarter katika mtaa mzuri, Sara anaona chumba hicho kuwa kama kichuguu ama kizimba cha kuku
      • Asna anaona afadhali umaskini na matatizo ya mjini kuliko kijijini ambako umaskini umekithiri zaidi, Sara anaona ni afadhali mtu awe maskini akiwa kwao kuliko ugenini
      • Asna anathamini wembamba wa umbo lake ilhali Sara anamkejeli kwa kukonda sana
      • Sara anamtarajia Asna kutafuta mume aolewe, Asna anadai hayuko tayari kuzungushwa kichwa na maisha ya ndoa
      • Asna hakuridhika na usaidizi wa Bunju kwa familia yao, alimwona mkono birika ilhali Sara alishukuru kwa usaidizi wote ambao Bunju aliwapa
      • Sara alitaka kurudi kijijini haraka baada ya matibabu ili akatazame mtama wake ilhali Asna alimtaka asubiri mjini hadi apate nafuu zaidi kisha babake ashughulikie majukumu ya nyumbani
      • Asna aliamini kuwa angekataa kunyanyaswa na utamaduni na kuolewa alipobaleghe
      • Sara aliamini ndoa ina raha kuwa wawili, Asna anaogopa ndoa ina mateso hasa kupigwa na mume     (6×1=6)
    3.  
      • Utohozi-seli, wodi, shiti
      • Tashbihi-amri na vitisho kama askari
      • Taswira (mnuso) - hewa iliyojaa harufu ya dawa
      • Nahau-vitanda vimesalimu amri
      • Tashhisi-vitanda kusalimu amri,shiti zikagura
      • Takriri-amri,amri.       (6×1)
  5.  
    1. Fadhili za punda
      • Lilia ndiye alimshinikiza babake amruhusu kuolewa na Luka baadaye Luka akamgeuka
      • Pastor Lee Imani alipomtenga Lilia na Luka, Lilia alishindwa kujizuia, waliandikiana barua na jumbe za simu
      • Lilia alikubali kuacha kazi ya meneja wa benki ili kwenda kudhibiti fedha za kanisa
      • Luka alipoanza kumtesa Lilia hakuchukua hatua mwafaka za kumkomesha
      • Lilia alipoambiwa na Luka kuwa ahamie kijijini ili kuwa karibu na raia, alijinyamazia tu kama mke mtiifu
      • Alipata fununu kuwa Luka ana wanawake wengine, hakumkabili, alidhani ni uvumi tu
      • Lilia alipomkabili mumewe ofisini akiwa na mwanamke mwingine, Luka alimwamuru kurudi nyumbani naya akajiendea zake kwa vile hakupenda ugomvi
      • Lilia alipoamua kumripoti Luka kwa kituo cha polisi alibadili nia akarudi nyumbani kusubiri hatima yake
      • Mwanamke kiruka njia alifahamu kuwa Luka ana mke lakini alikubali kutumiwa kimapenzi na Luka
      • Lilia alikubali masharti ya mumewe ya kutotoka nje ya lango
      • Lilia anapigwa na mumewe hadi kuumizwa lakini hachukui hatua    (10×1)
    2. Kifo cha Suluhu
      • Abigael mwenyewe alijitolea kuwa kupe kwa wanaume ili apate pesa ya kusaidia wanuna wake
      • Abigael alifahamu kuwa Bwana Suluhu ana mke lakini aliamua kujihusisha naye kimapenzi
      • Natasha alimchochea Abigael kumwekea Bwana Suluhu dawa ili ampore pesa watumie pamoja
      • Abigael na Natasha walijirembesha ili kuwavutia wanaume zaidi
      • Abigael alichoshwa na majivuno ya Suluhu lakini aliendelea kukubali kwenda chumbani kulala
        naye
      • Bi Suluhu alifahamu kuwa Bwana Suluhu alimpachika mimba binti wa chuo kikuu. Pia alikuwa
        na hawara aliyempangia chumba mjini lakini hakumchukulia hatua yoyote
      • Bi Suluhu aliyavumilia mateso ya mumewe kwa ajili ya watoto wao
      • Bi Suluhu alijua siri za ufisadi wa mumewe, vile alifuja pesa za wananchi kwa kuwalipa wasichana wa vyuo vikuu baada ya kula uroda, lakini alinyamaza tu
      • Bi Suluhu aliona kuwa ni heri yeye afe ili mumewe arejee nyumbani kuwatunza watoto wao
      • Bi Suluhu aliachiwa mzigo wa kulea watoto lakini hakuchukua hatua
        (10×1=10)
  6.  
    1.  
      • Tashbihi-Maneno hayo yalikuwa kama hirizi
      •  Utohozi-afisini
      • Takriri-tena, mwalimu, afisini
      • Kisengere nyuma-hata huo mwaka haukufikia nusu alipata tena habari mbaya
      • Nidaa-kwa vitendo!
      • Tashhisi-maneno...kuivaa ili yamwongoze
      • Taswira (oni)-mwalimu mkuu...kusoma-wahaka usoni mwake
    2.  Mrejelewa-"Fadhumo"        (6×1=6)
      1. Ayasemayo mhusika-anasema kuwa hawezi kuwa kimada wa mzee aliyetaka aishi naye kama kimada-msimamo dhabiti
      2. Matendo ya mhusika-anaamua kuolewa kwa mume wa pili ili nduguye amalize shule na yeye pia atasoma-mwenye matumaini, bidi
      3. Wayasemayo wahusika wengine-mwalimu mkuu anasema wasichana wote wangalikuwa kama Fadhumo kwa bidii na utiifu, shule ingefanya vyema-mwenye bidii, mtiifu.
      4. Maelezo ya mwandishi-mwandishi anaeleza kuwa Fadhumo alikuwa amepata barua iliyokuwa imemwita katika shule moja kati ya zile nzuri katika kaunti yao-Ni mwerevu masomoni       (2×1=2)
    3.  
      1.  Elimu/Masomo
      2.  
        • Mwenye bidi-Anatia bidii shuleni mpaka kufikia kusifiwa na mwalimu mkuu
        • Mtiifu-bali na kuwa na bidi, Fadhumo alikuwa mwanafunzi mtiifu.
        • Mwenye msimamo dhabiti-alikuwa na kiu ya elimu hata baada ya kuolewa aliendelea na masomo ili kutimiza ndoto yake   2×1=2
      3.  
        • Ukosefu wa karo unachangia Fadhumo kukatiza elimu yake         
        • Ndoa za mapema. Fadhumo anasitisha masomo yake na kuolewa ili aweze kuwaunza ndugu zake
        • Vifo vya wazazi. Vifo vya wazazi wake Fadhumo vimechangia yeye kuhangaika hasa katika kupata elimu
        • Utamaduni/taasubi ya kiume. Mjombake Fadhumo anapendelea kumsomesha kaka yake kwa sababu anaamini mvulana ndiye anastahili kusoma
        • Umaskini-wazazi wake Fadhumo hawana pesa za kutosha lakini wanajikaza kulipa karo na mahitaji mengine
        • Utovu wa nidhamu/ezembe miongoni mwa wanafunzi shuleni uk. 65 si watiifu
        • Baadhi ya wanafunzi kushindwa kukamilisha masomo yao shuleni/wengine kukamilisha japo kuwa kuchelewa. Fadhumo.
        • Baadhi ya wanafunzi kukosa kutangamana/ kukaa karibu na wazazi wao au jamaa zao na kusababisha msongo wa mawazo. Mfano Fadhumo              (8×1=8)
  7. MWONGOZO WA FASIHI SIMULIZI
    1. Ngano ya mazimwi-kuna matumizi mengi ya fantasia. Kijiwe kuongezeka umbo. (1x1=1)
    2.  
      1. Kina umbo maalum, kwa mfano kina mwanzo. Hapo zamani za kale...
      2. Mandhari/mazingira yamesawiriwa kwa ufundi mkubwa
      3. Wahusika wamejengwa kwa ufundi mkubwa ili kusawiri tabia za wahusika katika jamii
      4. Lugha imetumika kwa ufundi. Kwa mfano lugha ya kitamathali. Kuna tashhisi, Uhuishi, takriri n.k (3×1=3)
    3.  
      1. Zimwi kuweza kumeza umati wa watu pamoja na mifugo
      2. Watu na mifugo kutoka tumboni mwa zimwi wakiwa hai
      3. Kijiwe kuongezeka umbo na kuonekana kama kiwiliwili cha binadamu (2×1=2)
    4.  
      1. Mtafiti atakuwa karibu zaidi na jamii na hupata habari za kuaminika
      2. Ni njia bora ya kukusanya habari kutoka kwa watu ambao hawajui kusoma na kuandika
      3. Mtafiti anaweza kuuliza maswali kuhusu kipera kinachowasilishwa
      4. Mtafiti anawezakunakili anayotazama au sikiliza na kuhifadhi sifa za kiimbo, toni..
      5. Mtafiti hupata hisia halisi ya yanayowasilishwa kwa vile anakabiliana ana kwa ana na watendaji
      6. Hukuza utangamano kati ya mtafiti na wanajamii        (4×1=4)
    5.  
      • Kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa ngano za mazimwi
      • Kufunza shuleni
      • Kutambua na kutuza wale wanaoendeleza utanzu huu
      • Kuandaa tamasha na mashindano ya ngano za mazimwi
      • Kufanya utafiti zaidi kuhusu ngano
      • Kuchapisha vitabu zaidi vya ngano
      • Kuwahimiza wazee kuwa na vikao na wajukuu ili kuwasimulia ngano
      • Kupeperusha ngano kwenye vyombo vya habari      (6×1=6)
    6.  
      • Shughuli za kiuchumi
      • Biashara-soko kuu
      • Uchimbaji madini-pete ya dhahabu
      • Ufugaji-mifugo (mbuzi,kondoo, ng'ombe)
      • Ukulima/kilimo-wakulima makondeni
      • Kupigana vita-wakatwaa silaha
      • Dini-sherehe za kumshukuru muumba
      • Malezi ya watoto-wanajamii kuwashauri watoto            (2×1=2)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Catholic Diocese of Kakamega Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?