Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Samia Joint Mock Examination 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachanguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki, yaani Riwaya, Hadithi Fupi, Tamthilia na Ushairi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya kiswahili.

SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI
(Swali la lazima)

  1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    “Kwa taadhima na ruhusa yenu, wapenzi, ninasema hivi: kwamba thawabu ya mja ni sawasawa na jitihada na suna zake. Siku nyingi tumewinda. Na silalamiki kwa kuwa adinasi kwa kawaida huwinda mengi katika sayari hii kwa kadri ya haja na hekima yake. Hana budi, hata hivyo kutumia ubongo wake kwa namna ambavyo Jaliya alivyomkirimu. Naam! Kwa maana wenye hekima hunaswa kwenye hila zao. Nawaomba kwa hivyo mmakinike, pasiwe kwenu faraka bali mhitimu katika nia moja na ushauri mmoja katika ombi letu. Asenteni!”
    Maswali
    1. Tambua kipera hiki. Fafanua jibu lako. (alama 2)
    2. Fafanua muundo wa kipera ulichosoma. (alama 3)
    3. Eleza njia zozote mbili ambazo mtafiti wa kipera hiki anaweza kutumia kukusanya data kukihusu. (alama 4)
    4. Taja changamoto moja kwa kila mbinu za ukusanyaji data ulizotaja katika swali la (c) (alama 2)
    5. Eleza nafasi ya fanani katika fasihi simulizi. (alama 4)
    6. Eleza sifa nne za mwasilishaji bora wa fasihi simulizi. (alama 5)

SEHEMU YA B: BEEMBEA YA MAISHA
Jibu swali la 2 au la 3

  1. “Lakini nilivyosema, Mungu hamuwachi mja wake…….”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Tambua sifa tatu za msemewa. (alama 4)
    3. Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya katika kukuza tamthilia.(alama 6)
    4. Kwa kurejelea tamthilia nzima, eleza ukweli wa kauli, “Mungu hamwachi mja wake”. (alama 6)
                        AU
  2. “Wenyewe tumewafanya hivyo. Mila na desturi zetu zimewajenga hivyo walivyo na sisi hivi tulivyo.”
    1. Jadili jinsi maneno yaliyopigiwa mstari yanavyojitokeza katika tamthilia hii. (alama 10)
    2. Taja hatua wanazochukua wahusika katika tamthilia ya Bembea ya Maisha kujikomboa kutokana na kauli hii uliyosoma. (alama 6)
    3. Eleza nafasi ya msemaji katika kuendeleza ploti ya tamthilia husika. (alama 4)

SEHEMU YA C: CHOZI LA HERI
Jibu swali la 4 au 5

  1. “Hata hivyo huu wa leo unaskika kama ngonjera kwani baada ya kila ubeti, mwimbaji anasita kwa muda, kana kwamba anampisha mwenzake”
    1. Liweke dondo hili katika muktadha wake. (alama4)
    2. Taja ujumbe wa “ngonjera” inayorejelewa kwa kurejelea ukatili aliotendewa mwasilishaji. (alama 6)
    3. Kwa kurejelea riwaya hii onyesha mchango wa wanawake katika kuzoroteka kwa maisha yao. (alama 3)
                AU
  2. Dhihirisha jinsi ufisadi umejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri

SEHEMU D: MAPAMBAZUKO YA MACHWEO

  1. “Nisikuone tena ofisini mwangu, mwanamke wewe. Kuja kuniaibisha, wapinzani wangu waseme nimeshindwa kumdhibiti mke wangu sembuse kaunti nzima!”
    1. Bainisha muktadha wa dondoo hili (alama 4)
    2. Eleza toni katika muktadha huu. (alama 2)
    3. Asasi ya ndoa imo hatarini. Jadiili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea mandhari ya dondoo hili. (alama 4)
    4. Jadili changamoto zinazowakumba vijana katika hadithi zifuatazo;
      1. Mapambazuko ya Machweo. (alama 5)
      2. Sabina (alama 5)

SEHEMU YA E: USHAIRI

  1. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata
    SHAIRI A
    UCHAFUZI WA MAZINGIRA
    Haya yetu mazingira, tusipochunga taisha,
    Dunia hii duara, yatupa yetu maisha,
    Tutakuwa na vipara, sisi sote tutakwisha,
    Tuyachunge mazingira, la sivyo tuangamie.

    Mto wetu Nairobi, uti wetu maishani,
    Wasaidia mabibi, mabwana huko nyumbani,
    Mto huu ni muhibi, mamboye zingatieni,
    Tuyachunge mazingira, la sivyo tuangamie.

    Elenino ikinyesha, tuonyeshe werevu,
    Majiye nitategeza, tusijekaa kivivu,
    La tutajifedhehesha, tukiwa nao uwivu,
    Tuyachunge mazinira, la sivyo tuangamie.

    Mbuga zetu ni muhimu, Nairobi, Tsavo zote,
    Masai Mara tukima, kuimarisha uchumi wetu,
    Amboseli ilazima, watalii waje kwetu,
    Tuyachunge mazingira, la sivyo tuangamie

    Asojali la mkuu, tavunjika guu lake,
    Maisha yetu makuu, kitafika kikomoche,
    Milima yote mikuu, tusije badilika,
    Tuyachunge mazingira, la sivyo tuangamie.

    Wangari twamkumbuka, alituzwa Nobeli,
    Kenya yetu litukuka, ramani ikawa mali,
    Bunge litahesabika, vijijini ghafimali,
    Tuyachunge mazingira, la sivyo tuangamie.
    MASWALI
    1. Eleza ujumbe wa shairi. (alama 2)
    2. Tambua bahari nne za ushairi. (alama 4)
    3. Eleza uhuru wa kishairi ulivyodhihirika katika shairi. (alama 4)
    4. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
    5. Andika ubeti wa tano katika lugha nathari. (alama 4)
    6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi. (alama 2)
      1. Tutajifedhehesha
      2. kikomoche
  2. SHAIRI B
    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata

    Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki
    Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki
    Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki
    Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka

    Wengine watakuuwa, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo
    Hizi kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakazifuata nyago
    Hadi kwenye wako ua, pasipo hata kupesa, wala kukupa kisogo
    Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka

    Pindi kinunua kitu, hafurahi shaitani, bali tajawa chukizo
    Mtu kiwa mtukutu, tanuna mtimani, kwalo lako tekelezo
    Tamko lake “subutu!”, kuondoa tumaini, na kukuulia wazo
    Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka

    Aliye na taraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kujidai
    Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui
    Hana faida nyumbani, ni mtu akuchimbaye, mradi usitumai
    Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka

    Kwa hakika ni balaa, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo
    Bahati ina hadaa, kukupa alo sadawi, aibatili rohoyo
    Mipangoyo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza kuvunja kaniyo
    Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka

    Ninacho changu kilio, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa
    Ningetoa azimio, lakini uwezo sina, kwa mazito kuambiwa
    Ama nitimue mbio, fuadini ninanena, akilini nazuiwa
    Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
    MASWALI
    1. Lipe shairi anwani mwafaka (alama 1)
    2. Fafanua mambo manne ambayo nafsineni analalamikia (alama 4)
    3. Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
    4. Tambua aina mbili za urudiaji zilizotumika katika shairi (alama 2)
    5. Ukitolea mifano eleza jinsi mtunzi alivyotimiza arudhi katika shairi (alama 4)
    6. Taja kwa kutolea mifano idhini zozote mbili za kishairi zilizotumika katika shairi (alama 2)
    7. Tambua nafsineni katika shairi hili (alama 1)
    8. Andika ubeti wa nne katika lugha nathari. (alama 4)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI 
    1. Kipera hiki ni mawaidha – kuna wosia kwamba kuwepo kwa kumakinika, kuepuka hila, faraka lakini kudumu katika nia moja.
    2.  
      1. Utangulizi – huanza kwa kauli ya kuvuta makini ya hadhira – kwa taadhima kuu na ruhusa yenu.
      2. MWili – mawaidha huwasilishwa kwa kauli sisitizi pamoja na tamathali za usemi
                  –  thawabu ya njia ni sawasawa na jitihada na suna zake.
                  – Adinasi huwinda mengi katika sayari hii kwa kadri ya haja na hekima.
      3. Hitimisho – Anayeusia huonyesha msimamo wake. Mhitimu katika nia moja na ushauri moja katika ombi letu. Asanteni.  3 x 1 = 3
    3.  
      • Kunasa sauti/kurekodi
      • Kunasa picha na sauti
      • Kuandika
      • Kushiriki
      • Kutazama
      • Kutumia hojaji
      • Mahojiano
      • Kusikiliza              2 x 2 =4
    4.  
      • Gharama ya utafiti na kunua vifaa
      • Mtazamo hasi wa wanajami
      • Kudai malipo kutoka wahojiwa
      • Uhaba wa mafanani/wazee/wataalamu.
      • Vikwazo kutoka kwa watawala
      • Ukosefu wa wakati wa kutosha kuwahoji watu.
      • Ugumu wa lugha ya mawasiliano
      • Ukosefu wa umeme
      • Matatizo ya usafiri
      • Usalama.
    5.  
      • Hukusika katika uwasilishaji wa haditthi
      • Hukusika kwa kutoa kitendawili, kupokea majibu na kuomba mji baada ya mteguaji kukosa jawabu.
      • Kutunga tungo na kusisimulia/kuziwasilisha
      • Kutoa elimu kwa hadhira kwa kuonya kuarifu, kuelekeza, kufahamisha na kukosoa hadhira yake.
      • Huendeleza utamaduni wa kupokeza fasihi kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
      • Hudumisha na kuendeleza lugha kwa kubuni miundo mbalimbali ya lugha na kuipokea.
      • Hushirikisha hadhira katika uwasilishaji wake.
    6.  
      • Awe na uwezo wa kupandisha na kushusha mawimbi ya sauti.
      • Matumizi ya miondoko ya mwili za viziada lugha.
      • Kushirikisha hadhira
      • Matumizi ya maleba
      • Aweze kujua hadhira ya na mahitaji yao pamoj na kiwango chao cha elimu.
      • Kumudu na kuielewa mazingira ya hadhira yake.
      • Kuwa jasiri wa kuzungumza hadharani
      • Kujua utamaduni wa hadhira yake.
      • Kuwa mfaraguzi – uwezo wa kugeuza kazi ya fasihi papo hapo na kuwasilisha kwa hadira.
      • Kuwa mcheshi.     (5 x 1 = 5)

SEHEMU YA B: BEMBEA

  1.  
      • Msemaji ni Dina.
      • Msemewa ni Kiwa
      • Mahali ni nyumbani kwa Dina
      • Dina anamwelezea Kiwa kuhusu maisha ya awali ya Sara jinsi walivyosemwa na wanajamii baada ya kukawia kupata motto lakini baadaye Mungu akawajalia watoto.   (4 x 1 = 4)
    1. Msemewa ni Kiwa
      • Mwenye heshima – Anamheshimu mamake na kushirikiana naye licha ya pato dogo.
      • Mdadisi – Anamuuliza mama yake maswali kuhusiana na famillia ya Yona na Sara.
      • Mvumilivu – Anakula chakula kidogo na kusema kuwa maisha yamekuwa magumu kupata chakula kingi ni adimu.
      • Mwajibikaji – Anaenda kumwona/kumtembelea mamake ili kumjulia hali.
      • Mwenye hekima.   (3 x 1 = 3)
    2. Ploti.
      • Anatujuza kuhusu maisha ya awali ya Sara yanayotusaidia kujua hali ya sasa ya Sara.
      • Kupitia kwake tunatambua kuwa Yona hakuwa mlevi awali ila pandashuka za maisha ndizo zilizomsukuma kuingilia ulevi.
      • Pia tunatambua kuwa Yona na Sara walikosa kujaliwa watoto na walisemwa sana a kubandikwa majina na wanajamii.
      • Kupitia kwake tunajua kiwango cha maradhi ya Sara kwani hawezi kufaynya chochote k.v. kupika.
      • Kupitia kwake tunatambua jinsi wanajamii waliwasema kwa kukusa mrithi.
      • Kupitia kwake tunafahamu ukatili wa Yona.
      • Maudhui ya ulevi yana chimuzwa baada ya Yona kukosa mrithi.
      • Ubabedume/taasubi ya kiume yanajitokeza anaopsema wanaume hawawezi kuwasaidia wanawake kazi za nyumbani.
      • Athari za ulevi – anatueleza jinsi Yona alivyoanza ulevi na kumpiga mkewe kwa kutopata mrithi.
      • Utamaduni – anasema Yona alimpiga Sara kwa kukosa motto wa kiume kwa sababu jamii ilithamini sana motto wa kiume.
    3.  
      • Sara na Yona wanakawia sana kupata motto.
      • Mungu kwa wakati wake anawabariki na bititi wa watatu.
      • Yona na Sara wanasemwa kwa kukosa motto wa kiume lakini baadaye tunaona ufanisi wa binti zao.
      • Yona na Sara wanamlea Neema kwa taabu na baadaye anakuja kufanikiwa na kuwasaidia wazazi wake pakubwa.
      • Asna anasema zamani familia ya Dina ilikuwa masikini lakini kwa sasa wana afadhali.
      • Neema anapata ajali mbaya, Bunju analeta Flying Doctors na kugharamia matibabu.
      • Dina anamwambia Kiwa kuwa japo hali ni ngumu hajafikia kukosa chakula.
  2.  
    1.  
      • Kutosaidia katika kazi za nyumbani k.v. kupika
      • Kuketi na kutazama tu bila kufanya chochote
      • Kukosa wepesi wa kufanya kazi/jambo kwa kukosa mazoea.
      • Mwanamme kusemwa ikiwa atasaidia jikoni kuwa anashusah hadhi yake.
      • Kuwapiga wake zao. Yona kumpiga Sara
      • Kuwatusi wake zao.
      • Kuwalaumu wake zao kwa makosa ambayo si yao k.v Sara kuzaa watoto wa kike.
    2.  
      • Wanawake kupata elimu k.v. Neema na Asna.
      • Wanawake kufanya kazi k.v. Neema
      • Wanawake kuendesha magari k.v. Neema gari mjini na kwa kwa mwendo mrefu.
    3. Sara
      • Ametumika kuonyesha wanawake wavumilivu/wastahimilivu.
      • Ametumika kuonyesha mwanamke mwenye hekima anakabiliana na changamoto zote za maisha.
      • Kuonyesha ulezi bora wa watoto.
      • Kutumiwa kutuonyesha mtu ambaye ni mtetezi mzuri k.m. anamtetea mume wake kwa watoto wake.
      • Mpenda amani.
      • Mwenye bidii ya kazi. Anamsaidia mume wakekusomesha watoto kwa kujishughulisha na uuzaji wa maziwa na mazao ya shambani.
      • Mwanamke mwenye ujasiri. Hajuti uamuzi wake wa kuvumilia mateso na kupata ugonjwa wa moyo.
      • Ametumiwa kama mwanamke msema ukweli. Anawaambia watoto wake kwamba familia yake haikuwa na mali.
  3.  
    1. Msemaji ni msimulizi
      • Msemewa – anajisemea mwenyewe
      • Mahali – mtaa wa Afueni akielekea kazikeni.
      • Sababu – Anarejelea mabadiliko yanayojitokeza katika wimbo wa shamsi.
    2.  
      • Wananyang’anywa shamba lao na Bwana Mabavu.
      • Wanafanya vibarua katika shamba lao.
      • Baba shamsi kufanya kazi kwa shamba lake ili alipe karo ya mwanaye.
      • Kukosa kazi baada ya kuhitimu chuo kikuu.
      • Kupata kazi yenye mshahara mdogo – Mkia wa mbuzi.
      • Kuachishwa kazi kwa kuwazia kugoma.
      • Kufurushwa kutoka mabandani mwa kampuni baada ya kufutwa kazi.
      • Kumpteza baba yake mzazi kwa ajili ya njaa.
      • Kumpoteza babake kwa sababu ya ukosefu wa hospitali kijijini.
      • Kukosa kupandishwa nyadhifa kazini nafasi zilipopatikana.   (6 x 1 = 6)
    3.  
      • Tuama anajipeleka kisiri kupashwa tohara inayomfanya kupoteza damu nyingi.
      • Pete anakunywa dawa ya kuulia panya ili afe na kuishia kulazwa hospitalini.
      • Sauna na kangara wanashiriki biashara haramu ya kuiba na kuuza watoto na kuiishia kutiwa mbaroni na kufungwa.
      • Mamake Pete anazorotesha maisha ya Pete kwa kumkatizia masomo na kumwoza kwa Fungo.
      • Makya wa Subira anamzoroteshea maisha kwa kumsingizia kuwa mwizi wa mali aliyotafuta mwenyewe na kumrejelea ‘Muki’
      • Rehema anazorotesha maisha ya Chandachema kwa kumtelekeza na kumwachia bibiye hali iayomfanya kuishia kufanya kazi katika shirika la majani chai.
      • Zohali anawatoroka wazazi wake na kuhamia jijini anakotaabika sana – anapigana na majitu yanayotaka kumnyanyasa kimapenzi
      • Wanawake wanajidharau wenyewe – nyanyake mwangeka anamweleza kuwa unyonge haukuambiwa wanaume bali wanawake.
      • Baada ya Subira kuhamia mjini Kisuka anakunywa kinyanji kikali kinachoishia kumuua.
      • Mwekevu anawania uongozi wa wahafidhina ila wenzake wanastahili kumuunga mkono ili aibuke mshindi wanajitenga naye.
      • Selume anahamia kambini baada ya kutilafiana na kisiasana wakwe zake..
      • Rehema anaanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwalimu wake Fumbu na kuishia kupachikwa mimba.
      • Naomi anakimbia familia yake jambo linalosababisha kifo cha mumewe na kutekwa nyara kwa wanawe.
  4. Dhihirisha jinsi ufisadi umejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.
    • Ufisadi unajitokeza katika sekta ya ajira. Shamsi katika wimbo wake anaeleza nafasi za kazi yalivyotwaliwa na ndugu zao huku wakiambiwa kindanindani, “Viganja huo shana,asomwana aeleke jiwe!” (uk.133)
    • Polisi wanajihusisha na ufisadi. Mwaliko anasema kuwa ana shaka ya kukutana na ndugu zake kutokana na polisi kuacha kuwatafuta.
    • Sauna anauza maji ya mito na madimbwi yaliyotiwa kwenye chupa za vibandiko vya kuvutia vyenye jina ‘Mineral water’ kwa njia ya kuwadanganya wanunuzi.
    • Wanasiasa wanawahonga raia ili wawapigie kura. Kijana aliyevalia shati lililoandikwa ‘Hitaman’ anasema kuwa uhitaji wao unawasukuma kununuliwa kwa vihela vya kushikilia uhai. Vilevile anasema kuwa wakati mwingine wanashiriki katika njama za wanasiasa za kuwahadaa wazee na kuwakanganya ; hivyo kuwafanya wawapigie wanasiasa Fulani kura.
    • Hazina ya jitegemee ambayo inatarajiwa kuwapa vijana mtaji wa kuanzisha biashara inaandamwa na ukabila na unasaba.
    • Viongozi wanawahidi wakazi wa madongoporomoka kuwa watawajengea nyumba za hadhi kwa gharama nafuu. Ajabu ni kwamba wanamadongoporomoka wanashtukia nyumba zenyewe zimechukuliwa na viongozi hao hao. Makiwa ndiye anayemweleza mzee kaizari haya.
    • Tume za kuchunguza visa vya unyakuzi wa ardhi zinaundwa na ripoti kutowekwa wazi kwa umma. Ahadi wanazopewa wananchi ni kuwa waliogawiwa au kununua mali ya umma kwa njia za udanganyifu watakabiliwa kisheria. Haki haitendeki kwa wananchi wa kawaida.
    • Kambini msitu wa mamba, baadhi ya familia zinafanya ujanja wakati wa ugavi wa chakula cha msaada ili kupata mafungu Zaidi. Kwa mfano familia ya aliyekuwa diwani wa kina mzee Kaizari hapo, awali bwana kupe, inajigawa na familia tatu tofauti ili kupata chakula kingi.
    • Kuna kufichwa kwa faili za kesi za jinai ambako kumezifanya kesi zenyewe zikawiye mahakamani kwa muda mrefu bila kusikizwa. Tunaelezwa kuwa Annatila (Tila) alizoea kumwambia babake, ridhaa, kuwa atakapokuwa jaji katika mahakama kuu, kesi za jinai ambazo zimekawia mahakamani bila kusikizwa, faili zake zitapatikana zilikojifungia na kesi hizo kuamuliwa. Baadaye washukiwa watachukuliwa hatua za kisheria.
    • Baadhi ya walinda usalama wanajihusisha na njama za kifisadi. Katika hotuba yake Racheal Apondi anaeleza kuwa kuna baadhi ya walinda usalama ambao wizi unapotokea, wao hushirikiana na wahalifu na kupata mgao wa pesa zinazoibiwa.
    • Magari makuukuu yanaruhusiwa kuwepo barabarani na polisi wa rafiki kwa kuwa wanaoyamilki ni watu wenye vyeo serikalini.
    • Wasimamizi wa hospitali za umma wanajihusisha na ufisadi. Wao huchukuwa shehena za dawa zilizotengewa raia wa kuziuza kwenye maduka yao. Aidha chanjo ya polio inauziwa maskini ambao hata hawamudu kujilisha. Isitoshewanaoweza kujimudu gharama ya dawa ya kukabiliana na makali ya ukimwi na saratani ndiyo wanaoinyakuwa dawa zilizotengewa raa masikini.

SEHEMU YA D: MAPAMBAZUKO YA MACHWEO.

  1. “Nisikuone tena ofisini mwangu, mwanamke wewe kuja kuniaibisha. Wapinzani wangu waseme nimeshindwa kumthibiti mke wangu sembuse kaunti nzima?”
    1.  
      • Maneno haya yalisemwa na Luka
      • Akimwambia mkewe lilia
      • Wako nyumbani
      • Na baada ya Lilia kumtembelea ofisini mwake na kumpata yuko na kimada.   (4 x 1 = 4)
    2. Toni ya hasira. Luka anakasirika baaday ya kufumaniwa na mkewe ofisini.  (2x1 = 2)
    3.  
      • Ndoa imekabwa na dhuluma – Luka anamdhulumu Lilia kwa kumzaba kofi.
      • Imekumbwa na taasubi ya kiume.
      • Imekosa kuheshimiana.
      • Imekumbwa na vitisho. Lilia anatishwa kutomweleza yeyoteanayopitia.
      • Imekabwa na dharau – Luka hamheshimu mkewe.
      • Uasherati/uzinzi – Luka ana kimada.
    4.  

SEHEMU YA E: USHAIRI

  1.  
    1. Ujumbe wa shairi ni kuhusu uchafuzi wa mazingira. Wanajamii wanaonywa didhi ya kuchafua mazingira yao kwani watajutia baadaye.
    2.  
      • Tarbia – Lina mishororo mine katika kila ubeti
      • Ukaraguni - vina vya ndani na vya nje vinabadilika.
      • Mathnawi – Limegawika katika vipande viwili.
    3.  
      • Inkisari – Kufupisha maneno ili kupata urari wa vina mfano asojali – asiyejali
              - Majiye – maji yake
      • Kuboronga sarufi – Haja yetu mazingira badala ya mazingira haya yetu
      • Mazda – Kikooche badala ya kikomo.    (2x2=4)
    4.  
      • Lina mishororo minne katika kila ubeti limegawika katika vipande viwili.
      • Vina vya ndani na vya nje vinabadilikabadilika line beti sita.    (4x1=4)
    5.  
      • Mwandishi anatueleza kuwa asiyesikia la mkuu huvunjika guu na kuwa maisha ya binadamu yataisha tusipotahadhari. Anatueleza pia tuchunge milima yetu na pia tuyachunge mazingira yetu la sivyo tutaangamia.
    6.  
      1. Tutajiaibisha
      2. Mwisho wake
  2.   
    1.  
      • Tama ya binadamu
      • Uovu wa binadamu   (1x1=1)
    2.  
      • Analalamikia unafiki wa binadamu – njama zake zi moyoni.
      • Mauaji ukionekana ukiwa na pesa.
      • Chuki – hufurahi shetani bali tajawa na chukizo.
      • Kusemwa kwa watu faraghani.
      • Kumkirimu mchawi ambaya amejaa uchoyo.
      • Hana wa kumsikiza.      (2x1=2)
    3.  
      1. Tashbihi – Ni hatari kama nyoka
      2. Msemo – kukupa kisogo
      3. Istiara/Istiari – pesa kulinganishwa na maua.
      4. Jazanda – mchawi – mtu mbaya   (2x1=2)
    4.  
      • Urudiaji wa mshororo – shairi lina kibwagizo
      • Urudiaji wa silabi – silabi ya mwisho imerudiwa katika kila kipande cha mshororo kwenye ubeti.
      • Urudiaji wa sauti – ubeti wa pili kipande cha kwanza sauti lal.   (2x1=2)
    5.  
      • Kuna mishororo minne katika kila ubeti
      • Limegawika kwenye vipande vitatu
      • Lina kibwagizo
      • Mizani 24 katika kila mshororo
      • Lina vina.
    6.  
      • Inkisari – Ukweliwe – ukweli wake
              Tanuna – atanuna
      • Kuboronga – hadi kwenye wako ua – hadi kwenye ua wako
      • Mazda – Shaitani – shetani   (2x1=2)
    7.  
      • Mashauri
      • Mtetezi wa haki
      • Mzinduzi
    8. Aliye na targhani ni shida kuishi naye kwani hujidai na kukusema wakati haupo naye ili kuwafurahisha maadai. Hana faida kwani atakuchimba mrudi usijue. Mtu aliye na tama na kutaka kisicho chake huwa ni hatari kama nyoka.   (4x1=4)
      (Mtahini aandike kwa aya)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Samia Joint Mock Examination 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?