Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kangundo Subcounty Pre Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

 1. Andika insha mbili.
 2. Insha ya kwanza ni ya lazima.
 3. Chagua insha nyingine moja kati ya tatu zilizobakia.
 4. Kila insha isipungue maneno 400.
 5. Kila insha ina alama 20.
 6. Kila insha sharti iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

 

 1. Andika wasifu wa ndugu yako ambaye anakaribia kuustaafu hivi karibuni.
 2. Andika insha kuhusu umuhimu wa vijana katika kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
 3. Tunga kisa kinachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
  Chombo cha kuzama hakina usukani.
 4. Andika insha itakayomalizika kwa maneno yafuatayo:
  Tulijifunga kibwebwe kuwaopoa wahasiriwa waliokuwa wamefunikiwa na vifusi vya
  maporomoko ya jengo hilo lakini juhudi zetu ziliambulia patupu.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. WASIFU
  Mtahiniwa azingatie muundo wa wasifu.
  Mambo chanya yatakayowasilishwa mfano.
  • Mwaka wa kuzaliwa mhusika.
  • Alikozaliwa mhusika.
  • Wazazi wake ni akina nani na pia aila yake.
  • Alikosomea/elimu yake.
  • Vikwazo alivyoweza kukabiliana navyo katika elimu yake.
  • Ufanisi wake katika elimu.
  • Kazi na vyeo alivyopata.
 2. Hii ni insha ambayo inamhitaji mtahiniwa kufafanua/kujadili mawazo yake au mwelekeleo wake kuhusu nafasi ya vijana katika utangamano wa kijamii.
  Baadhi ya hoja.
  • Vijana ndio wengi.
  • Vijana wanathaminiana na kuaminiana hivyo ni rahisi kuwasihi wenzao kutangamana.
  • Ikiwa vijana wataweza kufunzwa maarifa au pengine mbinu ishi za kukabiliana na matatizo wataweza kuwasilisha mbinu hizi kwa wenzao.
  • Ni muhimu vijana kuepukana kutumiwa na viongozi.
  • Kundi la vijana laweza kutumia nishati kuleta shughuli zinazoleta utangamano kama vile michezo.
  • Vijana wanaweza kujisajili katika vyuo mbalimbali nchini na kuleta utangamano.
  • Vijana wanaweza kutumia lugha yao kama Sheng’ na kuleta utangamano.
  • Vijana wanaweza kutumia himizo kukomesha ukabila na kuleta utangamano.
  • Kushiriki katika shughuli za kiusomi kama vile kongamano za vijana huwezesha vijana kuja pamoja.
  • Mshikamano unaweza kudumishwa kupitia ndoa za mseto.
   Na mengineyo yakadiriwe pia
   Tanbihi.
  • Mtahiniwa anaweza kuchukua mwelekeo wa kuonyesha mambo ambayo vijana wanaweza kufanya ili kuleta mshikamano wa kitaifa.
  • Mtahiniwa anaweza kuonyesha hatua ambazo vijana wamechukua kuleta mshikamano wa kitaifa.
  • Mtahiniwa anaweza kuandika na kuchanganya mielekeo yote miwili akataja hoja na kuitolea ufafanuzi kwa kuonyesha hatua ambazo vijana tayari wamechukua kuhusiana na swala hili.
 3. Ni insha ya methali
  Chombo ambacho kimepangiwa kuzama/ama ambacho kina kasoro na kinaweza kuzama hata kikiendeshwa na nahodha wa aina gani, kitazama tu.
  Jambo la kuharibika hata ukajaribu kulirekebisha haitawezekana.
  Ruwaza zifuatazo za mawazo zaweza kujitokeza
  • Mtahiniwa amsawiri msimulizi/mhusika ambaye anapuuza jambo hadi pale linapoharibika kisha akaanza kulirekebisha.
  • Mtahiniwa abainishe hali ambapo licha ya juhudi za mhusika kurekebisha jambo hafanikiwi.
  • Mtahiniwa anaweza kuandika kisa kinacholenga kuonyesha umuhimu wa kuyarekebisha mambo kabla kuharibika.
   Tanbihi
  • Masharti ya usahihishaji wa insha za methali yazingatiwe – mtahiniwa lazima aelezee pande zote mbili za methali ili zijitoze wazi wala si kutaja upande wa pili akimalizia.
 4. Kisa kioane na kimalizio
  • pengine mtahiniwa aweze kuandika kuhusu maporomoko ya jengo kubwa lililokuwa linaendelea kujengwa kisha likaporomoka, au mashambulio ya ugaidi.
  • Aeleze chanzo cha mapomoroka hayo na kama baada ya juhudi zao na wahusika wengine zilipoambulia patupu walipata msaada.
  • Shughuli za baadaye zilikuwaje, kulikuwa na maafa au ni majeruhi.
   Tanbihi
  • Kazi ya mtahiniwa isahihishwe/na kukadiriwa kulingana na viwango vya usahihishaji
   wa insha.
  • Insha yoyote ni alama 20.
  • Alama za makosa ya sarufi na hijai ziondolewe.
  • Mwanafunzi yeyote yule apewe haki yake kulingana na kazi aliyoiwakilisha.

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kangundo Subcounty Pre Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest