Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Asumbi Girls Highschool Pre-Mock Exams May-June 2022

Share via Whatsapp

Maagizo.

 1. Jibu maswali matatu pekee.
 2. Swali la kwanza ni la lazima.
 3. Maswali mengine matatu yachanguliwe kutoka sahemu nne zilizobaki; yaani:Riwaya, tamthilia, ushairi na fasihi simulizi.
 4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
 5. Kila swali lina alama 20.
 6. Karatasi hii ina kurasa nne zilizopigwa chapa
 7. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.


MASWALI

SEHEMU YA A: HADITHI FUPI
Alifa Chokocho na Dumu Kayanda; Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.
1. Lazima
“Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. Rudi, rudi kwa Mola wako.”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
 2. Eleza tamathali mbili za usemi zinavyojitokeza katika dondoo hili (ala 2)
 3. Eleza madhara yanayotokana na vitendo vya mnenewa vya kuteketeza umma. (ala 8)
 4. Eleza umuhimu wa mnenaji wa maneno haya. (ala 6)

SEHEMU YA B: TAMTHLIA
PAULINE KEA: KIGOGO

Jibu swali la 2 au 3
2. “Hata nami naona pengine amenusa sumu.”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
 2. Eleza ni kwa nini mrejelewa anasemekana kuwa amenusa sumu. (ala 2)
 3.  Tambua mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo hili. (ala 1)
 4. Mwandishi wa Tamthlia hii amefaulu sana katika matumizi ya mbinu hii uliyotaja hapo juu. Kwa kutoa hoja saba thibitisha haya. (ala 7)
 5. Eleza umuhimu wa mzungumziwa (ala 6)

3. “Fungua macho uone. Keki imeliwa kwingine, mwaletewa masazo.

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
 2. Tambua mbinu ya kisanaa iliyotumika katika dondoo hili (ala 4)
 3. Thibitisha kuwa keki imeliwa kwingine (ala 6)
 4. Eleza sifa za msemaji wa maneno haya (ala 6)

SEHEMU YA C: RIWAYA YA CHOZI LA HERI
ASSUMPTA K. MATEI.

Jibu swali na 4 au 5
4. “Vipi binadamu anavyoweza kuyazoa maji yaliyomwagika?

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili (ala 4)
 2. Tambua mbinu ya lugha iliyotumika (ala 2)
 3. Jadili sifa tatu za msemaji (ala 3)
 4. Hakiki jinsi binadamu alivyomwagikiwa na maji katika Riwaya (ala 11)

5. “ Kiu ilipobisha hodi, tulijaribu kujikuna tulipojipata.”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili (ala 4 )
 2. Tambua tamathali mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili. (ala 4)
 3. Kando na tatizo lililodokezwa katika dondoo hili, eleza matatizo mengine sita waliyokumbana nayo msemaji na wenzake. (ala 6)
 4. Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya (ala 6)

SEHEMU YA: USHAIRI
Jibu swali la 6 au 7
6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
SIPENDI KUCHEKA

Pana jambo natukiya, kwangu hilo muhali,
Kitenda naona haya, kujishusha yangu hali
Sipendi unipe hidaya, sipendi kutenda hili
Sipendi mimi kucheka

Sipendi mimi kucheka, kuchekea mawi
Sipendi na ya dhihaka, kwangu nyemi hiwi
Sipendi kwa hakika, mwovu kistawika
Halafuye nikacheka!

Maskini akiteswa
Yatima akinyanyaswa
Mnyonge naye akinyonywa
Sipendi hata ikiwa
Uwezo nguvu najuwa
Ni hili sitatekezwa

Mbona lakini nicheke, kwayo furaha?
Na wewe ukajiweke, uli na siha?
Na yatima ali pweke, ye anahaha?
Amenyimwa haki yake, hanayo raha!
Na moyo wangu ucheke, kwa ha ha, ha!
Kumbuka kwa kucheka Mimi katu sitacheka.

Maswali

 1. Shairi hili ni la aina gani? Thibitisha (ala3)
 2. Taja sababu zinazomfanya mshairi asitake kucheka. (ala3)
 3. Chambua umbo la shairi hili kwa kuzingatia ubeti wa mwisho. (ala4)
 4. Tambua nafsineni na nafsinenewa katika shairi hili. (al2)
 5. Tambua toni ya shairi hili. (ala1)
 6. Fafanua uhuru wa mshairi katika shairi hili. (ala2)
 7. Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi. (ala3)
 8. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumka katika shairi (ala2)
  1. Mawi
  2. Nyemi

7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yatakayofuata.
Kimya changu kimezidi, navunja yangu subira,
Narejeya miradi, kuhitimisha dhamira,
Kukejeli sina budi, niwafunze utu bora,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

Serikali bila hadi, ndo kiini cha madhara,
Yanopiga kama radi, isokuwa na ishara,
Yamini kuwa gaidi, watupora mishahara,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

Wamejifanya hasidi, wasopatana fikira,
Wana yao makusudi, kujisombea ujira,
Wakilenga kufaidi, tumbo zao za kichura,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

Nchi yetu kufisidi, ni jambo linonikera,
Tangia siku za jadi, ufukara ndo king’ora,
Kutujazeni ahadi, nyie mkitia fora,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

Fakiri watozwa kodi, wa pwani na walo bara,
Kwa uvumba hata udi, mwawalipa kwa hasara,
Hamudhamini miradi, mejihisi masogora,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

Mesema kazi ni chudi, basi sirikali gura,
Nafsi zenu mzirudi, mkubali kuchakura,
Makondeni mkirudi, muondoe ufukara,
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

Ujanjenu umezidi, demokrasia bakora,
Debeni takaporudi, michirizi kwenye sura,
Kuwachuja ndo! muradi, kwa za mkizi hasira
Nani aali zaidi, Wakenya au vinara?

Maswali.

 1. Toa anwani mwafaka kwa shairi hili. (ala1)
 2. Ainisha shairi hili kwa jinsi tatu huku ukitoa sababu. (ala3)
 3. Onyesha mbinu mbili za lugha katika shairi hili. (ala2)
 4. Bainisha matumizi matatu ya uhuru wa mshairi katika shairi hili. (ala3)
 5. Andika ubeti wa nne katika mtindo tutumbi. (ala4)
 6. Fafanua maudhui matatu yanayojitkeza katika shairi hili. (ala3)
 7. Taja mpango mmoja unaotajwa kama njia ya kutatua matatizo ya nchi. (ala1)
 8. Eleza muundo wa shairi hili. (ala3)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
8.

 1. Eleza sifa tatu za nyimbo. (ala6)
 2. Tofautisha dhana zifuatazo: (ala4)
  1. Misimu na misemo
  2. Ulumbi na malumbano ya utani.
 3.                            
  1. Eleza maana ya mawaidha. (ala2)
  2. Fafanua majukumu manne ya mawaidha katika jamii. (ala8)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

Alifa Chokocho na Dumu Kayanda; Tumbo lisiloshiba na hadithi nyingine.

 1. Lazima
  “Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. Rudi, rudi kwa Mola wako.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
   1. Haya ni maneno ya mkumbukwa
   2. Alikuwa akimwambia Mkubwa
   3. Walikuwa nyumbani kwa Mkubwa
   4. Alimwambia maneno haya bada ya kutoka kororkoroni na akawa ameamua kuwachana na biasahara haramu ya kusambaza dawa za kulevya biashara aliyoajiriwa na Mkubwa
  2. Eleza tamathali mbili za usemi zinavyojitokeza katika dondoo hili (ala 2)
   1. Takriri- Rudi, rudi
   2. Tashibihi- Usiteketeze umati kama kuni
   3. Jazanda- kuteketeza umati
  3. Eleza madhara yanayotokana na vitendo vya mnenewa vya kuteketeza umati. (ala 8)
   1. Dawa za kulevya zinawadhoofisha kiafya vijana wanaozitumia. Tunaelezwa kuwa vijana wamekonda na kukondeana.
   2. Vijana wanaishia kuwa wezi ili wapate pesa za kununulia dawa za kulevya
   3. Vijana wengi wanakamatwa na kusalia korokoroni kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya
   4. Vijana wanaotumia dawa hizi za kulevya wanafanya vitendo vichafu vya kaumu luti kama wanyama
   5. Dawa za kulevya zinmawafanya watu wengi kupoteza maisha yao. Mkumbukwa anamweleza Mkubwa wazi kuwa watu wengi wanaangamia kutokana na matumizi ya dawa hizi za kulevya
   6. Dawa za kulevya zinawafanya vijana kuwa wapyaro. Kijana mmoja anamwuuliza mkubwa ikiwa walikula kwa babake na kumwita makande.
   7. Dawa za kulevya zinawafanya vijana kuwa mazuzu.
   8. Dawa za kulevya zinawafanya watu kukosa raha kwa ujumla
   9. Vijana wanatokwa na denda midomoni kutokana na matumizi ya dawa hizi za kulevya
   10. Watumizi wa dawa hizi wanasinzia mchana kweupe na hata kupatwa na ndoto za mchana.mfano kijana mmoja anaota akielekea kwa Obama na kudai kuwa Mkubwa amemkatizia safari yake. (Hoja zozote 8x 1 =ala 8)
  4. Eleza umuhimu wa mnenaji wa maneno haya. (ala 6)
   1. Ametumiwa kuonyesha watu wenye bidii maishani. Mkumbukwa anafanya kazi yake ya kumfanyia mkubwa kampeni hadi anapigiwa kura.
   2. Anawakilisha watu fisadi katika jamii. Anawahonga wapiga kura wakishirikiana na Bi. Kibwebwe.
   3. Anaendeleza maudhui ya usaliti. Mkumbukwa ana msaliti M,kubwa anapodinda kwendelea na biashara haramu ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
   4. Ni kielelezo cha watu wanaoongozwa na tamaa na baadaye kujipata matatani. Tamaa yake ya kutajirika inamfanya kushiriki katika biashara ya uuzaji wa dawa za kulevya na baadaye anatiwa mbaroni.
   5. Ametumiwa kufichua uozo uliopo katika jela zetu. Pale watuhumiwa wanakaa katikas mazingira mabovu na hatass kupokwa chakula na walinzi.
   6. Anaonyesha watu wanaojutia matendo yao na kuuamua kubadilika maishani. Mkumbukwa anajutia kushiriki katika biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya na baadaye anaiasi biashara hiyo.
   7. Anawakilisha watu wapyaro kwenye jamii. Anamtusi mkubwa anapokuwa akiikataa kazi ya uuzaji wa dawa za kulevya. (hoja zozote 6x 1 = ala 6)

SEHEMU YA B: TAMTHLIA
PAULINE KEA: KIGOGO

2. “Hata nami naona pengine amenusa sumu.”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
  1. Haya ni maneno ya Kenga
  2. Anamwambia Majoka
  3. Wako ofisini mwa Majoka
  4. Alikuwa akimzungumzia Chopi baada yake kutomwangamiza Tunu kama alivyoagizwa basi Kenga akawaanaamwona kama ambaye tayari alikuwa anshiriki katika matumizi ya dawa za kulevya.
 2. Eleza ni kwa nini mrejelewa anasemekana kuwa amenusa sumu. (ala 2)
  Chopi hakumwangamiza Tunu kama alivyokuwa ameagizwa na badala yake alimvunja tu mguu wa muundi. Kutokana na hili Kenga alimwona kama ambaye alikuwa ameanza kushiriki katika matumizi ya dawa za kulevya( kunusa sumu).
 3. Tambua mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo hili. (ala 1
  Jazanda – kunusa sumu
 4. Mwandishi wa Tamthlia hii amefaulu sana katika matumizi ya mbinu hii uliyotaja hapo juu. Kwa kutoa hoja saba thibitisha haya. (ala 7)
  1. Wanafunzi wanageuka kuwa makabeji shuleni- Ashua anasema hivi kumaanisha kuwa wanafunzi hafaulu shuleni kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
  2. Siafu ni wengi na ni vigumu kuwamaliza- Bi. Hasshima anasemamaneno haya kumaanisha kuwa wananchi ni wengi na wana nguvu kuliko viongozi wakishirikiana.
  3. Kisima kimeingia mchanga na maji hayanyweki tena- hii jazanda amabyo inamamnisha kuwa masmbo yameharibika Sagamoyo.
  4. Huwezi kunitoa tonge kinywani- Husda anamrejelea Majoka kama tonge. Anamwambia Ashua kuwa hawezi kumyaganya Majoka.
  5. Huwezi kujipeleka kwenya pango la joka- Hashima anamwambia mwanawe Tunu hivi kumaanisha hawezi kujipeleka hatarini.
  6. Majoka anasema hattacha kula mkate kwa kuchelea kiungulia. Hii ni jazanda inayomaanisha hawezi kukosa kumpenda ASshua hta kama ana bwana.
  7. Kenga anasenma Chopo lazima aende safari. Hii ni jazanda inayoomanisha kuwa Chopi auawe.
  8. Keki ya taifa- jazanda ya raslimali za umma
  9. Chopi anamwaambia Sudi kuwa akishindwa kulima shamba aseme. Hii ni jazanda inayomaanisha kuwa Suddi akishindwa kumtunza Ashua aseme. (hoja zozote 7x 1= ala 7)
 5. Eleza umuhimu wa mzungumziwa (ala 6)
  1. Majoka anatumiwa kuonyesha viongozi ambao hutumia mamlaka yao kuwaangamiza wengine. Alishirikiana na Kenga kumuua Jabali.
  2. Anawakilisha viongozi wabinafsi. Analifunga soko la Chapakazi ili apate pa kujenga mkahawa wake.
  3. Anawakilisha viongozi wenye vitisho- Anamtisha Kingi kuwa angemfuta kazi kwa kutowaagiza askari kuwwatawanya watu wa Tunu.
  4. Anatumiwa kuendeleza maudhui ya ufisadi. Majoka anampa Mamapima kibal cha kuuza pombe haramu
  5. Anawakilisha viongozi saliti katika jamii.
  6. Anawasaliti wanasagamoyo kwa kufunga soko na hata kukubasli uuzaji wa pombe haramu.
  7. Anawakilisha viongozi wenye mapendeleo. Alikuwa anataka kumwajiri Ashua kenye Shule ya Majoka and Majoka Academy bila kumfanyia mahojiano tyoyote ili akubali kuwa mpenzi wake. (hoja zozote 6x1= ala 6)

3.“Fungua macho uone. Keki imeliwa kwingine, mwaletewa masazo.

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
  1. Haya ni maneno ya Sudi
  2. Anamweleza Kombe
  3. Walikuwa kwenye karakana katika Soko la Chapakazi
  4. .Sudi anajaribu kumwambia kombe kuwa atazame kuwa walioletewa ni masazo tu ya keki ila keki imeliwa kwingine.
 2. Tambua mbinu ya kisanaa iliyotumika katika dondoo hili (ala 4)
  Jazanda- keki imeliwa kwingine
 3. Thibitisha kuwa keki imeliwa kwingine (ala 6)
  1. Kuna watu ambao wana usalama wa kutosha wakati wengine wanahangaika. Kenga na Majoka wana walinzi wakati akina Hashima wanalalamikia usalama wao.
  2. Kuna wale ambao wanapata chakula na mapochopocho wakati wengine hawana.
  3. Viongozi kama Majoka wanapata maji safi, hatas wamejichimbia visima kwao ilhali wananchi wengine kama Bi. Hashima wanahangaika.
  4. Viongozi wanakunywa chai ya maziwa wakati wananchi kama Sudi wanakunywa chai ya mkandaa.
  5. Viongozi wanajinyakulia ardhi kubwa kubwa wakati wananchi hawana hata pahali pa kuuzia bidhaa zao.
  6. Watoto wa viongozi kama vile Ngao Junior wanaenda kusomea ng’ambo wakati watoto wa wananchi wanapata elimu duni ncini mwao.
  7. Kuna wale walio na usafiri mwema kama vile Majoka ilhali wananchi hawana
  8. Kuna walio na nmadaktari wa kibnafsi kama Majoka ilhali wananchi wanasumbuliwa na ndwele za kawaida. (hoja zozote zinazo angazia ubaguzi/ ubinafsi 6x1 =ala 6)
 4. Eleza sifa za msemaji wa maneno haya (ala 6)
  1. Ni mtetezi wa haki- anatetea haki zxa wanasagamoyo
  2. Ni jasiri- anashirikiana na Tunu kumkabili Majoka na kutetea haki za Wanasagamoyo
  3. Mwenye msimamo dhabiti- anakataa kutotengeneza kinyago cha Ngao hata baada ya kusawishiwa.
  4. Mwenye maadili- hashiriki ufisadi Sagamoyo hata kuila keki
  5. Mtambuzi- anatambua kuwa keki imeliwa kwingine na wao kuletewa masalio
  6. Mwenye mapenzi ya dhati- anawapenda wanawe naq mkewe kwa dhati (hoja zozote 6 x1= ala. 6 )

SEHEMU YA C: RIWAYA YA CHOZI LA HERI
ASSUMPTA K. MATEI.

4. Vipi binadamu anavyoweza kuyazoa maji yaliyomwagika?

 1. Liweke dondoo hili katika muktadha wake (ala 4)
  1. Haya ni manenoYA Mwanaheri
  2.  Akiwaambia Kairu na Umu
  3.  Walikuwa katika shule ya Tangamano
  4.  Ni baada ya kukutana na kuanza kusimuliana kuhusu yaliyowafika hadi wakakutana pale.
 2. Tambua mbinu ya lugha iliyotumika (ala 2)
  Swali balagha- vipi, binadamu anavyoweza kuyazoa maji yaliyomwagika?
 3. Jadili sifa tatu za msemaji (ala 3)
  1. Mwenye mawazo mapevu. Kulingana nay eye nmama yake angetafuta sduluhu kwa mgogoro kati yake na wakwe zake badala ya kujiua.
  2. Mwenye busara- anaamini kuwa hakuna haja ya kujishughulisha na mambo ambayo hawezi kuyabadilisha
  3. Mwenye bidii- anatia bidii shuleni. Anafuata uhauri wa mwalimu Bahati kuwa elimu itamletea mabadiliko maishani.
   Sifa zozote 3x 1 =ala 3)
 4. Hakiki jinsi binadamu walivyomwagikiwa na maji katika riwaya (ala 11)
  1. Lunga kumwagikiwa na maji asnapowachwa na mkewe Naomi
  2. Umu nas nduguze wanamwagikiwa na maji kwa kuwachwa mayatima wakati Lunga anaaga
  3. Ridhaa anamwagikiwa na maji wakati anapoipoteza aila yake yote isipokuwa Mwangeka.
  4. Mwangeka anamwagikiwa na maji kufuatia kifo cha mkewe na mwanawe.
  5. Zohari anamwagikiwa na maji anapotungwa mimba katika umri wa ujana nas kupelekea afukuzwe shuleni na kuteswa na wazazi
  6. Waafrika wanamwagikiwa na maji pale wanapokatazwa na wakoloni kulima mazao yaletao fedha huku ikiwalazimu kufanya vibarua kwao
  7. Baadhi ya vijana wa rika la Tuama wanakufa baada ya kupashwa tohara
  8. Hjospitali inamwagikiwa ansa maji pale Selume analamikia ukosefu wa mwangaza, glavu na deni na usimamizi duni.
  9. Wakaazi wa msitu wea Mamba wanaharibikiwa pale wanapofurushwa huku vyakula walivyolima vikkibwa na viongozi
  10. Vijana barobaro wanaotumiwa na wanasiasa kuandamana wanamwagikiwa na maji pale wanapomiminiwa risasi vifuani na walinzi huku wakiuawa
  11. Kitoto kinachookotwa na Neema kilimwagikiwa na maji pale kilitupwa na mamam mzzazi badalas ya kukilea
  12. Ridhaa anasimulia mwasnawe Mwangeka vile walivyobomolewa nyumba zao kwenye mtaac wa Zari na hawakupewa fidia yoyote na wale waliowauzia viwanja hivi wakatoweka
  13. Lunga kufutwa kazi na mkurugenzi kwa kupinga mradi wa ununuzi wa mahindi. (zozote 11x 1 = ala 11)

5.“ Kiu ilipobisha hodi, tulijaribu kujikuna tulipojipata.”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili (ala 4 )
  1. Haya ni maneno ya Kaizari
  2. Kaizari alikuwa anamsimulia Ridhaa
  3. Walikuwa kwenye msitu wa Mamba
  4. Kaizari anamsimulia Ridhaa matatizo waliokuwa wamekumbana nayo kule katika msitu wa Mamba.
 2. Tambua tamathali mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili . (ala 4)
  • Tashhisi- kiu ilipobisha hodi
  • Msemo- tulijikuna tulipojipata
 3. Kando na tatizo lililodokezwa katika dondoo hili, eleza matatizo mengine sita waliyokumbana nayo msemaji na wenzake . (ala 6)
  1. Baridi kali- Kaizari anaeleza jinsi kulikuwa na baridi kali hadi kuwafanya akate miti na kujenga vibanda.
  2. Njaa- anaeleza jinsi siku ya kwanza walikula mate kwani hawakujua hata kwa kupata matunda mwitu.
  3. Makazi mabovu- wanajenga vibanda vilivyoezekwa kwa nyasi
  4. Mauti- Kaizari anaeleza jinsi alivyoshuhudia watoto wadogo wakiaga dunia. Anaogopa kuwa hata wao huenda wakaipungia dunia mkono.
  5. Ukosefu wa vyoo/ mazingira mabovu- inabidi watumie vyoo vya kupeperushwa kabla yao kuchimba vyoo.
  6. Magonjwa- wanaugua magonjwa kama homa ya matumbo kutokana na uchafu.
  7. Ukosefu wa mavazi- watoto wengi walikuwa wakicheza uchi kutokana na mavazi ya kuwasetiri. (hoja zozote 6 x 1 =ala 6)
 4. Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya alama 6)
  1. Mtamaushi- Kaizari anakata tama ya kuishi. Anatamani kufia walikokuwa kuliko kufia ugenini
  2. Mcheshi- anaserma kuwa siku ya kwanza walikula mate
  3. Mvumilivu- anavumilia kushuhudia mkewwe akikatwa kwa sime na wanawe kutendewa unyama
  4. Mdubira- gari lao linaisha petrol wanapoelekea mwituni
  5. Mwenye busara- aliyajenga maisha ya familia yake upya baada ya kutoka msituni na kurudi nyumbani
  6. Mwenye mapenzi- anaijengea familia yake makazi. Baada ya mkewe kutoweka anmtafuta kwao na pia mjini kutokana na mapenzi
   (sifa zozote 6 x 1 =ala 6)

Jibu swali la 6 au 7
6. shairi
Maswali

 1. Shairi hili ni la aina gani? Thibitisha (ala3)
  • Shairi huru
   • Thibitisho
    • Hakuna urari wa vina
    • Vipande vinatofautiana
    • Idadi ya mishororo inatofautiana
    • Mizani haijitoshelezi
 2. Taja sababu zinazomfanya mshairi asitake kucheka. (ala3)
  • Atakuwa anajishusha hali
  • Hapendi kuchekea mawi/mabaya
  • Hapendi dhihaka
  • Hapendi kustawisha mwovu
  • Hapendi kucheka mnyonge amenyimwa haki
  • Anaona haya kucheka.
 3. Chambua umbo la shairi hili kwa kuzingatia ubeti wa mwisho. (ala4)
  • Una mishororo saba
  • Mishororo mitano ya kwanza imegawika katika vipande viwili huku miwili ya mwisho ina kipande kimoja
  • Vina vya kati ni – ke – na nje ni –ha- isipokuwa miwili ya mwisho ambayo ni –ka-
  • Haina urari wa mizani.
 4. Tambua nafsineni na nafsinenewa katika shairi hili. (al2)
  • Neni – mtetezi wa mizani
  • Nenewa – wanyonge! Wadhulumiwa/ walionyimwa haki zao
 5. Tambua toni ya shairi hili. (ala1)
  • Malalamishi/masikitiko/huzuni
 6. Fafanua uhuru wa mshairi katika shairi hili. (ala2)
  • Tabdila – najuwa- najua
  • Inkisari – kitenda – nikitenda
  • Ali – aliye
  • Kwayo – kwa hiyo
  • Kuboronga sarufi – sipendi mimi kucheka
   Mimi sipendi kucheka
 7. Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi. (ala3)
  • Mshairi anasema kwmaba hapendezwi maskini akiteswa na mayatima kunyayaswa naye mnyonge akinyonywa. Hata iliwa anayewanyanyasa aan nguvu anajua kuwa hili halitamtikisa.
 8. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumka katika shairi (ala2)
  1. Mawi-maovu/mabaya
  2. Nyemi-furaha

7. shairi
Maswali.

 1. Toa anwani mwafaka kwa shairi hili. (ala1)
  • Nani aali zaidi
 2. Ainisha shairi hili kwa jinsi tatu huku ukitoa sababu. (ala3)
  • Tarbia – mishororo mine kila ubeti
  • Mathnawi – vipande viwili katika kila mshororo
  • Mtiririko- vina vya kati na vya mwisho vinafanana
 3.  Onyesha mbinu mbili za lugha katika shairi hili. (ala2)
  • Jazanda – bakora, debeni
  • Methali – kwa mkizi hasira
  •  Misemo – sina budi
  •  Mkitia fora
  • Kwa uvumba na udi
  • Tashbihi – yanopiga kama radi
  •  Tumbo zao za kichura
  •  Inkisari – isokuwa, ujanjenu, ndo
  •  Koboroga sarufi – navunja, nyangu subira
  •  Kukejeli sina budi.
  •  Tabdila – sirikali, marejeya
 4. Bainisha matumizi matatu ya uhuru wa mshairi katika shairi hili. (ala3)
 5. Andika ubeti wa nne katika mtindo tutumbi. (ala4)
  • ufisadi unaoendeleshwa nchini mwetu unanihudhi. Kutoka zamani umaskini ndilo swala letu. Mantupatia ahadi mkijipa mali. Kati ya wakneya na viongozi ni nani bora zaidi?
 6. Fafanua maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (ala3)
  • Uongozi mbaya
  • Ufisadi
  • Unafiki
  • Umaskini
  • Upunjiwaji
  • Demokrasia
 7. Taja mpango mmoja unaotajwa kama njia ya kutatua matatizo ya nchi. (ala1)
  • Kufanya kazi kwa bidii (kulima mashambani)
 8. Eleza muundo wa shairi hili. (ala3)
  • Vipande viwili kila mshororo
  • Mishororo mine kila ubeti
  • Lina kibwagizo
  • Urari wa vin – di, ra
  • Beti saba
  • Mizani nane kila upande isipokuwa ubeti wa pili mshororo wa tatu kipande cha pili – mizani 9

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
8. 

 1. Eleza sifa tatu za nyimbo. (ala6)
  • Huwa na mahadhi/kupanda na kushuka kwa sauti.
  • Lugha ya mtato
  • Huandamana na ala za muziki
  • Vifungu hurudiwarudiwa
  • Huandamana na uchezaji wa viungo
  • Lugha yenye taswira ha hisia nzito
 2. Tofautisha dhana zifuatazo: (ala4)
  1. Misimu na misemo
   • Misimu - Semi za muda katika mazingira maalumu na katika kipindi maaluu.
   • Misemo - Kauli fupi za kisanaa zenye maana na mafunzo yaliyofichika.
  2. Ulumbi na malumbano ya utani.
   • Ulumbi – uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee (mvuto na ufasaha)
   • Malumbano ya utani – majibizano kati ya watu wawili yanayotaniana.
 3.                              
  1. Eleza maana ya mawaidha. (ala2)
   • Mazungumzo ambayo hutolewa ili kumpa mtu ushauri au nasaha kuhusu jambo Fulani.
  2. Fafanua majukumu manne ya mawaidha katika jamii. (ala8)
   • Kuelekeza
   • Kuelimisha
   • Huadilisha
   • Hutambulisha jamii
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Asumbi Girls Highschool Pre-Mock Exams May-June 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest