Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Bunamfan Cluster Pre Mock Exam 2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali yote. Andika majibu yako katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.
  • Majibu yote yaandikwe kwa Kiswahili.


Maswali

UFAHAMU: (ALAMA 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali:

              Takwimu zilizothibitishwa zaonyesha kuwa kila sekunde nane mtu mmoja hufa duniani kutokana na utumiaji wa tumbako. Kwa siku basi, watu 10,800 hufa. Wengi wa wavuta sigara huanza katika umri kati ya miaka kumi na mitatu hadi kumi na tisa. Takwimu zaonyesha kuwa mtu akivuta sigara kwa zaidi ya miaka ishirini huupunguza umri wake kwa kati ya miaka 20 hadi 25 zaidi ya ambaye hajawahi kuvuta. Hii ni kwa kuwa tumbako ina zaidi ya kemikali 4,000 zinazodhuru afya.
              Mojawapo ya madhara makuu zaidi yanayosababishwa na sigara ni saratani. Kunayo saratani ya ngozi – vidonda visivyopona huchubuka ngozini na baada ya muda hugeuka na kuwa kansa. Iri ya mapafu hutokea vifuko vya hewa vinapopasuka na hivyo kutatiza uvutaji wa oksijeni na utoaji wa kabondayoksaidi. Moshi pia husababisha madhara kwa njia ya kupitisha hewa, yaani umio, ambapo njia hii yaweza hata kuzibika hivyo kulazimu tundu kutobolewa kooni ili mgonjwa aweze kupumua. Kabla ya kufika kooni na mapafuni, moshi hupitia mdomoni. Saratani ya mdomo na ulimi basi hupatikana zaidi miongoni mwa wavuta sigara. Pia kidonda chochote, kwa mfano baada ya kung’olewa jino, huwa vigumu kupona kwa mvutaji sigara.
              Kwa wanawake, kuna hatari ya kupatwa na iri ya fuko la uzazi. Madhara kwenye njia nzima ya uzazi huifanya iwe vigumu kwa wanawake wavuta sigara kuhimili. Ni rahisi pia kuzaa njiti. Mtoto wa mvutaji huzaliwa akiwa mwepesi zaidi ya kawaida. Hii husababishwa na kabonimonoksaidi kutoka kwa sigara inayomdhuru mtoto tumboni. Saratani hii husababisha hata kifo cha mtoto aliye tumboni. Wengine wazaliwapo huwa na hatari ya kupatwa na saratani zaidi ya waliozaliwa na akina mama wasiovuta sigara.
Aina zaidi za saratani zinazowakumba wavuta sigara ni kama vile saratani ya pua, ya tumbo, ya figo, ya kibofu cha mkojo, ya kongosho, ya njia ya kinyesi na hata saratani ya matiti inayowaathiri zaidi wanawake.
              Shida za sigara sio saratani pekee; sigara husababisha shida za macho na masikio kwa kiasi kikubwa. Mboni ya jicho yaweza kufunikwa na utando, hali inayoweza kusababisha hata upofu. Macho yaweza kuwashwa na moshi mkali wa sigara au mishipa ya macho iathirike na kemikali zinazofika kwayo kupitia kwa mishipa mapafu yanapoathirika. Masikio nayo huathiriwa na uchafu wa tumbako unaoganda kwenye mishipa hadi sehemu za ndani za masikio. Damu hupunguza mwendo ufaao masikioni hivyo yanaugua. Moshi na kemikali za tumbako pia hujeruhi sehemu za ndani na athari hii yaweza kuenea hadi ubongoni na kusababisha utando unaofunika ubongo. Hali hizi zaweza kusababisha uziwi.
              Mifupa na meno huathirika pia. Mifupa huwa myepesi, hukosa nguvu na kuwa rahisi kuvunjika. Mvuta sigara akivunjika mfupa huchukua muda wa asilimia themanini (80%) kupona zaidi ya mtu asiyevuta. Meno nayo hutatizika katika ukuaji wake kutokana na kugandwa na moshi wenye kemikali. Hali hii husababisha harufu mbaya, uchafu pamoja na kuoza kwa meno.
Ngozi ya mvuta sigara hukaushwa na kemikali kwa sababu uwezo wake wa kujirekebisha na kujilainisha hupunguzwa pakubwa. Hali hii husababisha ukavu unaoonekana pamoja na makunyanzi yanayomfanya mvuta sigara aonekane mzee zaidi ya umri wake. Vidole navyo vilevile hugandwa na kutu ya sigara, nazo kucha na vidole hugeuka rangi vikawa vya manjano, hudhurungi au maji ya kunde. Vidole pia hukaushwa na moto na kemikali ya sigara. Nywele za mvuta sigara pia huathirika kwa kuwa kemikali huipunguza kinga ya mwili hivyo mizizi ya nywele kukosa nguvu. Nywele za mvuta sigara zaweza kung’oka mapema.
              Sigara husababisha magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo. Kwa moyo, sigara husababisha shinikizo la damu na hatimaye mshtuko wa moyo waweza kutokea na kusababisha hata kifo. Kwa tumbo, sigara hupunguza uwezo wa kinga zake wa kuikinga dhidi ya asidi zinazosaga chakula. Pia hupunguza uwezo wa mwili wa kujikinga dhidi ya vidonda vya tumboni. Vidonda vya tumbo vya mvuta sigara huwa vigumu kupona na, ni rahisi kutokea tena baada ya kupona.
              Kwa mwanamume, mpigo wa damu kwenye sehemu za uzazi huathiriwa. Hali hii ikizidi husababisha hata upungufu wa nguvu ya mbegu kwenye shahawa. Hata ugumba waweza kutokea. Pia watoto wa mwanamke mvuta sigara waweza kuzaliwa wakiwa na kasoro. Mimba zingine zilizotungwa na wanawake wavuta sigara pia hutunguka. Na si hayo tu; madhara ya sigara ni mengi zaidi.

Maswali

  1. Yape makala haya kichwa. (alama 2)
  2. Mbali na athari kwa uzazi kwa wanawake na wanaume na sura/umbo la binadamu, taja madhara mengine ya uvutaji sigara kwa binadamu. (alama3)
  3. Kwa kurejelea kifungu onyesha kwamba sigara kwa wanawake hasa ni hatari mno. (alama 4)
  4. Je, ni kweli kuwa vifo vingi hutokea kwa sababu ya uvutaji sigara? Toa sababu. (alama 2)
  5. Eleza namna ambavyo uvutaji sigara huathiri sura ya mhusika. (alama 3)
  6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa kwenye taarifa. (alama 1)
    Gandwa

UFUPISHO: (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali

            Runinga kama kifaa kingine chochote cha mawasiliano kina manufaa yake. Kwanza kabisa, ni nyenzo mwafaka ya kufundishia. Vipindi vinavyopeperushwa katika runinga huwa na mafunzo kemkemu kwa mtu wa kila rika. Halikadhalika, runinga huweza kuleta vipindi ambavyo huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingira yao na duniani. Aidha, runinga ikitumika pamoja na michezo ya video huauni katika ukuzaji na ustawishaji wa stadi ya kujifundisha au kujielimisha. Michezo ya video, hasa ya kielimu, huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuchua misuli ya ubongo na kuwafanya watu kuwa macho wanapofanya kazi.
            Fauka ya hayo, televisheni ni chemchemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha. Hakuna mtu asiyependa kuchangamshwa. Televisheni ni mojawapo ya vyombo mwafaka vya kutekeleza hayo kutokana na vipindi vyake. Uburudishaji huu huwa ni liwazo kutokana na shinikizo na migogoro tunayokabiliana nayo kila siku. Uburudishaji huu hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu. Vivyo hivyo, runinga hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii. Vingi vya vipindi vya runinga huwa ni kioo ambacho huakisi mikakati na amali za jamii.
            Kwa upande mwingine, hakuna kizuri kisichokuwa na dosari. Licha ya manufaa yake, televisheni imedhihirika kuwa na udhaifu wake. Kwanza, baadhi ya vipindi vya runinga na video hujumuisha ujumbe usio na maadili, kama vile matumizi ya nguvu za mabavu, ngono za kiholela, lugha isiyo ya adabu, ubaya wa kimavazi na maonevu ya rangi, dini, jinsia, kabila na utamaduni. Si ajabu kuwa baadhi ya vijana wetu wanaiga baadhi ya mambo haya. Vijana wetu siku hizi wameingilia ulevi wa pombe na afyuni, ngono za mapema kabla ya ndoa na mavazi yanaowaacha takribani uchi wa mnyama. Wengi wamekopa na kuyaiga haya kutoka katika runinga. Ukiwauliza wafanyacho, watakujibu kuwa ni ustaarabu kwani wameupata katika runinga.
            Matumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa familia. Matumizi kama haya huwapa wanafamilia fursa ya kujitenga. Imedhihirika kuwa runinga haichangii kujenga uhusiano bora wa kijamii. Ukilinganisha na vyombo vingine vya burudani ambavyo hutoa nafasi ya watu kutangamana na kujenga uhusiano bora, televisheni haichangii haya. Badala yake, tajriba ya televisheni huwa ya kibinafsi. Hali hii inapotokea katika kiwango cha familia, televisheni inaweza kutenganisha wazazi na watoto wao.
            Halikadhalika, runinga na video aghalabu hueneza maadili yasiyofaa. Mathalani, baadhi ya vipindi vya televisheni huendeleza hulka ya kuhadaa, ngono za kiholela, kuvunjika kwa ndoa, na kadhalika. Hulka hizi zisizoendeleza maadili ya kijamii huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na waliostaarabika. Huu ni upotovu.
            Isitoshe, baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya dawa za kulevya kama tembo na sigara. Vitu hivi vinapotangazwa, hupambwa kwa hila na udanganyifu mwingi ambao huwavutia vijana na watoto wengi. Si ajabu mtu anapouliza wanaotumia vileo hivi walivyoanza, watajibu kutokana na athari za matangazo katika runinga na vyombo vingine.
            Utafiti umeonyesha kuwa vipindi vya runinga na video ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi. Wazazi wengi huchukulia vibonzo katika televisheni kuwa vinalenga kuburudisha tu na havina ubaya wowote. Lakini ukweli ni kuwa vipindi vingi vya vibonzo hushirikisha matumizi ya hila na nguvu za mabavu. Haya huibusha hamu ya vijana na watoto huyaiga.
Kwa hivyo, ni muhimu wazazi na jamii kutambua madhara ya televisheni. Utambuzi huu utawafanya wawaelekeze vijana na watoto jinsi ya kutumia televisheni na video ili kuepukana na madhara yake.

  1. Fupisha aya tatu za kwanza kwa maneno 70 – 75 (alama 8, 1 ya utiririko)
    Matayarisho
    Jibu
  2. Eleza udhaifu wa runinga na video. (maneno 50 – 51) (alama 5, 1 ya utiririko)
    Matayarisho
    Jibu

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1. Eleza maana ya kipashio kidogo cha lugha. (alama 1)
  2. Andika maneno yenye sifa zifuatazo: (alama 2)
    1.  kikwaruzo ghuna cha ufizi, vokali ya chini-wastani, kizuiwa ghuna cha midomo, kiyeyusho cha midomo, irabu ya chini-kati
    2. Kipua ghuna cha ufizi, kipasuo cha ufizi, irabua ya mbele-juu, nazali ghuna ya midomo, irabu ya nyuma-juu.
  3. Ainisha uamilifu wa kisarufi wa mofimu kwenye neno hili. (alama 3)
    Lilimjisha
  4. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili ya “tu”. (alama 2)
  5. Unda kitenzi kutokana na nomino toba kisha ukitungie sentensi. (alama 2)
  6. Yakinisha kwa kutumia kiambishi cha masharti ya uwezekano kwa wingi. (alama 2)
    Usiposoma kwa bidii hutofaidika.
  7. Tumia nomino ya ngeli ya mahali dhahiri pamoja na kivumishi kirejeshi cha kati kwa sentensi. (alama 2)
  8. Andika kinyume cha sentensi hii. (alama 2)
    Mjomba alimtwika mwanawe mzigo akabana mlango.
  9. Bainisha kijalizo katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
    Tajiri huyo shupavu ana magari makubwa mno.
  10. Tunga sentensi kwa kutumia chagizo cha ulinganisho. (alama 2)
  11. Andika upya sentensi kwa wakati uliopita hali endelevu, kauli ya tendesheka. (alama 2)
    Wenyeji wamewapokea wageni kwa taadhima.
  12. Tunga sentensi moja kuonyesha maana mbili za neno tema. (alama 2)
  13.  Ainisha aina ifuatayo ya sentensi kiutendakazi. (alama 1)
    Safari imekuwa ikitusumbua sana.
  14. Onyesha kiima na utambue muundo wake katika utungo huu. (alama 2)
    Pesa zote zilihifadhiwa na mwekahazina shujaa.
  15. Tumia kishazi tegemezi kwenye sentensi kuonyesha vigezo vifuatavyo. (alama 2)
    1. Wakati
    2. Jinsi
  16. Changanua kwa kielelezo cha mistari. (alama 4)
    Aliponijia kwa mkopo, nilikuwa nasali sebuleni.
  17. Andika upya kwa kuanza na yambwa tendwa. (alama 2)
    Mvua iliwanyea wanunuzi sokoni hivi majuzi.
  18.  Tunga sentensi kwa hali ya kudunisha ukitumia kihusishi cha uhusiano. (alama 2)
  19. Eleza matumizi ya kiambishi po katika sentensi. (alama 2)
    Achezapo anapofika sisi hushangilia.
  20. Twasema oyee tunapofurahia jambo……………..tunapotahadharisha na ……………….
    Tunapotoa himizo. (alama 2)

ISIMU JAMII (ALAMA 10)

  1. Eleza maana ya usanifishaji wa lugha. (alama 2)
  2. Taja lahaja zozote mbili za kati. (alama 2)
  3. Kulingana na habari zinazotufikia hivi punde, maafisa watatu wa polisi jana walikana mashtaka ya mshukiwa wa mauaji ya watoto 13 kutoroka kutoka kituo cha polisi.
    1. Tambua sajili inayorejelewa. (alama 1)
    2. Eleza sifa tano za sajili hii. (alama 5)


Mwongozo Wa Kusahihisha

UFAHAMU (ALAMA 15)

  1. Uvutaji sigara/tumbaku.
    Madhara ya uvutaji sigara/tumbaku (alama 1x2=2)
  2.        
    1. Husababisha saratani
    2. Husababisha shida za macho na masikio.
    3. Huathiri mifupa na meno.
    4. Husababisha magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo (ala 3 x1=3)
  3.   
    • Madhara kwa njia ya uzazi huifanya iwe vigumu kuhimili.
    • Ni rahisi kwao kuzaa njiti.
    • Huzaa watoto wepesi
    • Huweza kusababisha kifo cha mtoto aliye tumboni.
    • Mtoto huweza kuzaliwa akiwa na kasoro.
    • Mimba huweza kutunguka. (alama 4 x 1=4)
  4. Ndio: Kwa kila sekunde nane mtu mmoja hufa duniani kwa sababu ya kutumia tumbaku/kwa siku watu 10,800 hufa. (alama 1 x 2=2)
  5.       
    • Ngozi ya mvutaji hukauka/fanya mtu kuonekana mzee.
    • Vidole hugandwa na kutu ya sigara.
    • Kucha za vidole hugeuka rangi vikawa vya manjano/hudhurungi.
    • Nywele hukosa nguvu
    • Nywele hung’oka mapema. (Zozote 3 x 1=3)
  6. Kwamiliwa/kataliwa. (1 x 1=1)

UFUPISHO (ALAMA 15)

  1.          
    1. Runinga ina manufaa yake
    2. Ni nyenzo mwafaka ya kufundishia
    3. Vipindi vinavyopeperushwa huwa na mafunzo kwa kila mtu
    4. Huleta vipindi ambayo huwafahamisha watu mambo ambayo yanaendelea katika mazingira yao
    5. Ikitumika pamoja na michezo ya video husaidia katika ukuzaji na ustawishaji wa stadi ya kujifundisha/kujielimisha
    6. Michoro ya video huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuwafanya watu kuwa makini wanapofanya kazi
    7. Ni chemchemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha
    8. Uburudishaji huu huwa ni liwazo kutokana na shinikizo na migogoro
    9. Hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu
    10. Hutumika kama nyenzo ya kuendeleza utamaduni, kaida na amali za jami
      ( zozote 8x1=7, ut=1)
  2.    
    1. Baadhi ya vipindi hujumuisha ujumbe usio na maadili
    2. Vijana mengi wamekopa na kuyaiga wanayoyaona katika runinga
    3. Matumizi yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa familia/ Huleta utengano wa kifamilia.
    4. Baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya dawa za kulevya
    5. Ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi
      (Zozote 5x1=5, ut=1)

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1. Eleza maana ya kipashio kidogo cha lugha. (alama 1)
    • Sauti ni kipashio kidogo cha lugha kinachoweza kutamkika. (alama 1/0)
  2. Andika maneno yenye sifa zifuatazo: (alama 2)
    1. kikwaruzo ghuna cha ufizi, vokali ya chini-wastani, kizuiwa ghuna cha midomo, kiyeyusho cha midomo, irabu ya chini-kati
      • zabwa (alama 1/0)
    2. Kipua ghuna cha ufizi, kipasuo cha ufizi, irabu ya mbele-juu, nazali ghuna ya midomo, irabu ya nyuma-juu. ndimu (alama 1/0)
  3. Ainisha uamilifu wa kisarufi wa mofimu kwenye neno hili. (alama 3)
    • Lilimjisha
    • li-mofimu ya ngeli
    • li-mofimu ya wakatim-mofimu ya mtendwa
    • j-mzizi
    • ish-mofimu ya kauli ya kutendesha
    • a-mofimu ya tamati/kiishio (alama 1/26=3)
  4. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi tu. (alama 2)
    • Kuonyesha nafsi ya kwanza wingi k.m Tulisoma
    • Kuleta dhana ya kudhibitisha k.m Alinipa kalamu moja tu
    • Kama kitenzi kishirikishi kipungufu k.m Sisi tu wazima
    • Kama yambwa k.m Alitubariki
    • Mfano: Tulikuwa tu wazima kabla ya ugonjwa wa Korona.
      nafsi t
    • Tanbihi: Mtahiniwa atunge sentensi moja (alama 21=2)
  5. Unda kitenzi kutokana na nomino toba kisha ukitungie sentensi. (alama 2)
    • Toba-Tubu
    • Waumini wote walitubu dhambi zao. (alama 21=2)
  6. Yakinisha kwa kutumia kiambishi cha masharti ya uwezekano kwa wingi. (alama 2)
    Usiposoma kwa bidii hutofaidika.
    • Mngesoma kwa bidii mngefaidika. (alama 2/0)
  7. Tumia nomino ya ngeli ya mahali dhahiri pamoja na kivumishi kirejeshi cha kati kwa sentensi. (alama 2)
    • Pahali panapopendeza panatufaa
    • Kirejeshi cha kati kijitokeze kwa kitenzi
    • Tathmini majibu ya watahiniwa (alama 2/0)
  8.  Andika kinyume cha sentensi hii. (alama 2)
    Mjomba alimtwika mwanawe mzigo akabana mlango.
    • Mjomba alimtua mwanawe mzigo akabanua mlango. (alama 21=2)
  9. Bainisha kijalizo katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
    Tajiri huyo shupavu ana magari makubwa mno.
    • Tajiri huyo shupavu ana magari makubwa mno.
      Kijalizo (alama 1/0)
      Kijalizo husaidia kukamilisha maana ya sentensi na huja baada ya vitenzi vishirikishi
  10. Tunga sentensi kwa kutumia chagizo cha ulinganisho. (alama 2)
    • Msichana mrembo alitembea kitausi.
    • Chagizo cha ulinganisho ni sawa na kielezi cha ki ya mfanano
    • Tathmini majibu ya watahiniwa (alama 2/0)
  11. Andika upya sentensi kwa wakati uliopita hali endelevu, kauli tendesheka. (alama 2)
    Wenyeji wamewapokea wageni kwa taadhima.
    • Wageni walikuwa wakipokezeka kwa taadhima na wenyeji.
      au
      Wageni walikuwa wanapokezeka kwa taadhima na wenyeji. (alama 2/0)
  12. Tunga sentensi moja kuonyesha maana mbili ya neno tema. (alama 2)
    • Tema ni kutoa kitu kinywani mfano chakula, mate
    • Tema ni hali ya kukata kitu kama vile mti, mkono kwa mfano;
    • Alitema mate alipokuwa akitema mti kwa shoka.
    • Maana iwe dhahiri na iwe kwa sentensi moja. (alama 21=2)
  13. Ainisha aina ifuatayo ya sentensi kiutendakazi. (alama 1)
    Safari imekuwa ikitusumbua sana.
    • Sentensi ya taarifa/kauli (alama 1/0)
  14. Onyesha kiima na utambue muundo wake katika utungo huu. (alama 2)
    Pesa zote zilihifadhiwa na mwekahazina shujaa.
    • Mwekahazina shujaa- N+V
      Kiima
      Kiima huonyesha mtendaji (alama 21=2)
  15. Tumia kishazi tegemezi kwenye sentensi kuonyesha vigezo vifuatavyo. (alama 2)
    1. Wakati
      • Nyumba ilipojengwa, tuliishi ndani. (PO ya wakati itumike) (alama 1/0)
    2. Jinsi
      • Mwalimu alitutembelea tulivyotarajia jana.
      • Watoto wote walituzwa tulivyoona shereheni. (alama 1/0)
      • Tathmini majibu ya watahiniwa
  16. Changanua kwa kielelezo cha mistari. (alama 4)
    Aliponijia kwa mkopo, nilikuwa nasali sebuleni
    • S-KN+KT
      KN-N/W+S
      N/W- Ø
      S-aliponijia kwa mkopo
      KT-Ts+T+E
      Ts-nilikuwa
      T-nasali
      E-sebuleni (alama 1/28=4)
  17. Andika upya kwa kuanza na yambwa tendwa. (alama 2)
    Mvua iliwanyea wanunuzi sokoni hivi majuzi.
    • Wanunuzi walinyewa na mvua sokoni hivi majuzi. (alama 2/0)
  18. Tunga sentensi kwa hali ya kudunisha ukitumia kihusishi cha uhusiano. (alama 2)
    • Kijikalamu cha kijitoto kimepotea.
    • Kijumba cha kijimama kitabomolewa.
    • Hali ya kudunisha ni sawia na hali ya udogo.
    • Kihusishi cha uhusiano ni sawa na kihusishi cha a-unganifu (alama 2/0)
  19. Eleza matumizi ya kiambishi po katika sentensi. (alama 2)
    Achezapo anapofika sisi hushangilia.
    • achezapo-hali ya mazoea
    • anapofika-wakati maalum (alama 21=2)
  20. Twasema oyee tunapofurahia jambo simile/hario tunapotahadharisha na harambee tunapotoa himizo. (alama 21=2)

ISIMU JAMII (ALAMA 10)

  1. Eleza maana ya usanifishaji wa lugha. (alama 2)
    • Ni uamuzi wa kuchagua lugha moja au mojawapo ya lahaja za lugha na kuifanyia marekebisho ya kimatamshi, kisarufi, kimaana na kimaandishi ili iweze kutumika katika shughuli rasmi. (alama 2/0)
  2. Taja lahaja zozote mbili za kati. (alama 2)
    • Kimvita-Husemwa Mombasa kisiwani
    • Kijomvu-Husemwa maeneo ya jomvu, nje ya Kisiwa cha Mombasa
    • Kingare-Husemwa Mombasa (alama 21=2)
  3. Maafisa watatu wa polisi jana walikana mashtaka ya mshukiwa wa mauaji ya watoto 13 kutoroka kutoka kituo cha polisi.
    1. Tambua sajili inayorejelewa. (alama 1)
      • Sajili ya matangazo/matangazo ya redio/matangazo ya runinga/ Sajili ya magazetini (alama 1/0)
    2. Eleza sifa tano za sajili hii. (alama 5)
      • Mada/anwani huwa fupi na yenye mvuto
      • Matumizi ya tarakimu mfano 13
      • Matumizi ya lugha ya kuvutia
      • Ujumbe huandikwa au husomwa kwa aya fupi fupi ili kuokoa muda.
      • Sentensi aghalabu huwa ndefu kwa lengo la kufafanua.
      • Mara nyingi hutumia wakati uliopita
      • Matumizi ya lugha sanifu
      • Matumizi ya lugha nyepesi/rahisi ili kueleweka
        (Hoja za kwanza 5 alama 51=5, Asipofafanua atuzwe 1/2)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Bunamfan Cluster Pre Mock Exam 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest