Kiswahili Form 2 Questions and Answers - Term 3 Opener Exams 2021

Share via Whatsapp

Maswali

  1. Insha ya kiuamilifu. (alama 20)
    Hali ya usalama imekuwa ikizorota katika lokesheni yako.Andika barua kwa chifu wa eneo lenu ukionyesha visa vya ukosefu wa usalama na upendekeze njia za kukabiliana na hali hiyo.

  2. UFAHAMU( AL.15)
    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

    Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendelea. Wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya matumizi ya vidhibiti mwendo na kanda za usalama. Ajali za barabarani zinaangamiza idadi kubwa ya watu kila mwaka, wakiwemo viongozi na watu mashuhuri.

    Miongoni mwa sababu ambazo zinaleta maafa barabarani ni pamoja na uendeshaji kasi kupita inavyotakikana, yaani kukiuka masharti yaliyowekwa na wizara ya uchukuzi na mawasiliano. Madereva wengi hung’oa vithibiti mwendo vilivyowekwa hawarekebishi mikanda ya usalama, wala hawa peleki magari yao kwa ukaguzi mara kwa mara kama inavyopaswa kutekeleza kanuni zilizowekwa kwa hivyo hutegemea hongo kuwa barabarani. Fauka ya hao, madereva wa malori na matrela mara nyingi huendesha magari hayo wakiwa walevi. Dawa za kulevya kama vile miraa na bangi, hutumiwa sana na watu hawa, na matokeo yake huwa ajali mbaya.

    Hata hivyo, lawama haiwezi kuelekezewa madereva pekee. Ukiangazia barabara nchini utapata kuwa barabara nchini Kenya haziko katika hali nzuri . Zile za lami zimekuwa na mashimo makubwa ambapo mvua ikinyesha hufanya vidimbi mithili ya machimbo ya madini yaliyojaa maji baada ya kuachwa wazi. Na zile barabara zisizokuwa za lami zimeharibika kiasi kwamba ni vigumu kuzitofautisha na njia za ng’ombe kwenye maeneo kame.Kinachohitajika ni serikali kuzifanyia ukarabati ili kuzirudisha katika kiwango ambacho zitaweza kufaa tena.

    Wananchi pia inafaa waelimishwe ili wasikubali kuingia kwenye magari ambayo tayari yamejaaa kupita kiasi. Hili litawasaidia wananchi wenyewe kudumisha usalama wao barabarani. Pia inafaa watambue ya kwamba wana jukumu la kuwaarifu walinda usalama endapo dereva anaendesha kwa kasi sana kuliko ile ya kilomita 80 kwa saa iliyokubaliwa.

    Inafahamika kuwa maafisa wa uslama ndio wafisadi zaidi, hivyo basi huchangia katika kuongeza idadi ya vifo barabarani. Katika vita dhidi ya ufisadi na ajali za barabarani, ni mwananchi mwenyewe ambaye anawezesha kukomesha hali hii. Kwa mfano, afisa wa usalama akipatikana akichukua hongo, yeye pamoja na yule aliyetoa hongo wapelekwe kwenye vituo vya kukabiliana na ufisadi na wachukuliwe hatua kali, matatizo haya yataisha.

    Lakini kabla kufika hapo, ni muhimu kumhamasisha mwananchi kuhusu haki zake na namna ya kukabiliana na suala hili la ufisadi. Hali hii inatuonyesha kwamba mipango maalum inapaswa kufanywa na serikali ili kuwaelimisha wananchi kama hatua ya kwanza ya kukabiliana na ufisadi hatimaye izilainishe sekta zote wala si ya uchukuzi na mawasiliano pekee.

    Maswali

    1. Mbali na ajali za barabarani, taja, tatizo lingine sugu ambalo linakumba nchi ya Kenya (al.1)
    2. Ajali za barabarani zinasababishwa na nini? (al.4)
    3. Mwandishi anapendekeza hatua zipi zichukuliwe na serikali ili suluhisho la kudumu lipatikane? (al.2)
    4. Taja hatua ambazo serikali imechukua ili kuimarisha uchukuzi (al.3)
    5. Ni kitu gani ambacho kinaonyesha kuwa serikali imeshindwa kukabiliana na ajali barabarani? (al.2)
    6. Eleza maana ya maneno haya:-                                                                     (al.3)
      1. Tatizo sugu.
      2. Vithibiti mwendo.
      3. Machimbo.
      4. Ukarabati.
      5. Hongo.
      6. Kuhamasisha..
  3. Matumizi ya lugha (alama 40)

    1. Jaza mapengo:- 
              Kutenda                     Kutendesha
      1. Chota                       .........................  (ala 1)
      2. Lewa                       ........................... (ala 1)
    2. Taja sauti moja ya; 
      1.   King’ong’o  (ala 1)
      2. Kiyeyusho    (al.1)
    3. Tumia neno “shujaa” katika sentensi kama:-
      1. Kivumishi     (al. 1)
      2. Kielezi          (al. 1)
    4. Tambua vitenzi katika sentensi hii kwa kuvipigia mistari:-  (al. 2)
      Sisi tulikwisha kutambua alikuwa na nia mbaya. Yeye ndiye mwizi 
    5. Andika wingi wa sentensi hii katika hali ya ukubwa:-   (al. 2)
      Kichinjio hiki kilikarabatiwa kwa pesa nyingi 
    6. Eleza maana mbili ya sentensi ifuatayo  (al.2)
      Wanafunzi waliwaaandikia barua
    7. Jaza neno ambalo ni kinyume cha lile lililopigwa mstari katika sentensi:-  (al.2)
      1. Vile vitu ulivyovichanganya itakubidi
      2. Bomba hili limeziba mwite fundi aweze 
    8. Unganisha sentensi hii kwa kutumia ‘O’ rejeshi :- (al. 1)
      Wavu umekatika. Wavu ni wao   
    9. Eleza maana ya :-  (al. 2)
      1. Kiimbo
      2. Shadda
    10. Yakinisha sentensi hii:  (al. 2)
      Sijafahamu kwa nini hawamkaribishi mpwa wao.
    11. Andika katika usemi halisi:- (al. 2)
      Mama aliwahimiza warudi siku hiyo la sivyo wangekosa tuzo 
    12. Akifisha sentensi ifuatayo:-   (al.3)
      Sijaona kitabu kizuri kama mayai waziri wa maradhi, utaniazima siku ngapi bashiri alimwuliza rita
    13. Changanua kwa njia ya mishale.  (al. 4)
      Mama anapika na baba akisoma gazeti
    14. Panga nomino hizi katika ngeli mwafaka  (al. 2)
      1. Kipofu
      2. Uyoga
    15. Tambulisha kundi nomino na kundi tenzi ktika sentensi (al.2)
      Wanafunzi watundu wanacheza darasani
    16. Pambanua viambishi mbalimbali katika sentensi ifuatayo (al. 3)
      Waliwapendezea
    17. Eleza maana ya misemo:-  (ala. 2)
      1. Fuga mtu
      2. Kuwa na faragha 
    18. Chai hiyo iliwavutia watalii (Anza : Watalii…………..)   (al. 2)
  4. Isimu Jamii ( al.10)

    1. Lugha ya kiswahili inakabiliwa na matatizo mengi sana. Yataje na kuyaeleza.

     

  5. USHAIRI( ALAMA 15)
    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata              

    1. Yawile matononofu majani, hali yoyote iwavyo
      Yefura ukamilifu majani, yalikiota vilivyo
      Pamoja yalimakifu majani, kwa jinsi mambo yendayo
      Fahali kayatilifu majani, ndivyo igeuke sivyo
      Wanapowana fahali ziumiazo n’ nyasi

    2. Ingawa yali dhaifu majani, pamoja yalishikana
      Ama katika wakifu majani, au kwa kusaidiana
      Ndugu yali bainifu majani, tokea zamani sana
      Yakapondwa bila hofu majani, fahali walipowana
      Wanapowana fahali ziumiazo n’nyasi

    3. Pondaponda mepondeka majani, fahali wakivutana
      Tena yakatawanyika majani, kwa jambo lisilo kina
      Yakabaki kudhiika majani, ndugu wanaofanana
      Fahali wanayacheka majani, wala habri hawana
      Wanapowana fahali ziumiazo n’nyasi

    4. Fahali wanapotaka yakini, hata hutembeleana
      Na makoo kadhalika yakini, wanapotoka kuonana
      Ndama pia watavuka yakini, ng’ombe ile kulishana
      Tena nyasi hazochoka yakini, karibu kazikutana
      Wanapowana fahali ziumiazo n’ nyasi

    5. Si ndaama si ukoka majani, si mbuga si wanda tena
      Yamebaki mabaka majani, vipande kuoteana
      Kwa machaka hazoshika majani, hayawezi kupachana
      Na fahali watimka majani’,ngali wakisuguana
      Wanapowana fahali ziumiazo n’nyasi

      Maswali
      1. Mwandishi ana ujumbe gani katika shairi hili? (al.1)
      2. Eleza muundo wa shairi hili.  (al. 5)
      3. Mwandishi amefauluje katika kutumia uhuru wa kishairi?  (al.3)
      4. Andika ubeti wa pili katika lugha ya nathari (al. 4)
      5. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi (al. 2)
        1. Mabaka
        2. Kupachana

Majibu

  1. Hii ni barua rasmi
    Iwe na sura ifuatayo:
    1. Anwani mbili; ya mwandishi na mwandikiwa
    2. Sehemu ya maamkuzi; kwa Bw/ Bi
    3. Mtajo: KUH: YAH: (Kiini cha barua)
    4. Mwili wa barua Sehemu ya maudhui (Hoja)
    5. Hitimisho au mwisho wa barua
      Mimi wako
      Sahihi
      Jina
      Baadhi ya hoja za insha
      Visa
      • Wizi
      • Mauaji
      • Matumizi ya dawa ya kulevya
      • Unajisi/ubakaji
      • Magenge ya majambazi

        Mapendekezo
      • Kujenga vituo vingi vya polisi
      • Mabaraza kufanywa ili kuwashauri wananchi kuepuka maovu/ uhalifu
      • Wageni vijijini kuchunguzwa
      • Hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahalifu
      • Serikali ijishughulishe kumaliza umaskini – kazi kwa vijana/ mikopo ya biashara
      • Kuimarisha doria wakati wa usiku n.k
        Anayekosa kuzingatia sura ya barua rasmi aondolewe maki 4 baada ya kutuzwa   
  2.  
    1. Ufisadi     (al.1 x 1=al. 1)   
    2.  
      1. Ajali za barabarani zinasababishwa na kuendesha gari kwa kasi sana
      2. Kung’olewa kwa vidhibiti mwendo kinyume na masharti ya uchukuzu na mawasiliano.
      3. Kuwepo kwa magari mabovu barabarani ambayo hayakutimiza masharti ya ukaguzi.
      4. Ufisadi wa maafisa wa usalama
      5. Barabara mbovu zenye mashimo
      6. Matumizi ya madawa ya kulevya miongoni mwa madereva wa malori na matrela
    3.  
      1. Wananchi wafahamishwe ya kwamba wana jukumu la kuwaeleza walinda usalalam endapo gari linapelekwa kwa kasi kupita kiasi.
      2. Wananchi waelimishwe ili wasikubali kuingia kwenye magari ambayo yamejaa kupita kiasi
    4.  
      1. Kuwekwa kwa vidhibiti mwendo kwenye magari ya abiria
      2. Kuwachukulia hatua wale wanaotoa na kuchukua hongo 
      3. Kurekebisha baadhi ya barabara mbovu
      4. Kuwekwa kwa mikanda ya usalama kwenye magari   
    5.  
      1. Kung’olewa kwa vidhibiti mwendo
      2. Kutokuweko kwa mikanda ya usalama
      3. Gari kwenda kwa kasi zaidi kutokana na kurekebishwa kwa vidhibiti mwendo ( 2 x 1)
    6.  
      1. Shida ambayo imedumu muda mrefu bila suluhisho kuliko kiwango kilichokubaliwa   
      2. Mashimo yaliyoachwa baada ya madini kutolewa 
      3. Vifaa vya gari kwenda kwa kasi kuliko kiwango kilichokubaliwa
      4. Urekebishaji
      5. Kuchukua au kutoa mlungula/rushwa 
      6. Tia hamu ya kufanya jambo  (6 x ½ =al. 3 )     
  3. SEHEMU YA LUGHA

      1. Chota - chotesha (al.1)
      2. Lewa – lewesha  (al. 1)   
    1.  
      1. King’ong’o – m, n, ny, ng’     (yoyore 1x1 =al.1) 
      2. Kiyeyusho – y,w       (yoyote 1x1=al.1)     
    2. Kwa mfano:-
      Kivumishi : Askari shujaa ametuzwa       (1x1= al. 1)
      Kielezi: Askari yule alipigana kishujaa     (1x1=al. 1)
      (Hakiki jibu la mwanafunzi) 
    3. Vitenzi – tulikwisha, kutambua, alikuwa ndiye   (hoja 4 x ½ = al. 2)
    4. Ma(ji) chinjio haya ualikarabatiwa kwa ma(ji) pesa mengi (al. 2)
    5.  
      1. Kila mmoja aliandika kwa niaba ya mwenzake
      2. Kila mwanafunzi aliandika kwa sababu ya (al.2)
    6.  
      1. Uvichanganue  (al. 1) 
      2. Kulizibua         (al. 1) 
    7. Wavu uliookatika ni wao   (al. 1) 
    8. Kiimbo – Ni upandaji na ushukaji wa sauti unaofanyika wakati mtu anapozungumza (al. 2)
      Shadda – Ni mkazo wa silabi katika neno     
    9.  Nimefahamu kwa nini hawamkaribishi mpwa wao.
    10.  “Harakisheni mrudi leo, la sivyo mtakosa tuzo” mama alisema     (al.2) 
                                            au
        Mama alisema “Harakisheni mrudi leo, la sivyo mtakosa tuzo”. 
    11.  “Sijaona kitabu kizuri kama “Mayai waziri wa Maradhi,” Utaniazima siku ngapi?” Bashiri alimwuliza Rita.  (al.2)
    12.  Mama anapika na baba akisoma gazeti.  (al. 4)

      S            S1 + U + S2

      S1           KN + KT

      KN           N

      N             Mama

      KT            T

      T              anapika

      U              na

      S2           KN + KT

      KN           N

      N             baba

      KT           T+KN

      T            akisoma

      KN          N  

      N            gazeti

       

    13.  
      1. A – WA
      2. U – ZI   (al. 2)  
    14.  
      • wanafunzi watundu- KN
      • wanacheza darasani-KT   (al. 2)
    15.  wa – nafsi 
       li   – wakati
       wa – nafsi (mtendewa)
       pend – mzizi .shina
      eze- kauli/kinyambuzi
      a – kiishio        6x ½ = 3)
    16.  
      1. Nyima mtu uhuru unaohitajika  (al.2) 
      2. Kuwa na siri
    17. Watalii walivutiwa na chai hiyo (al.2
  4. Isimu Jamii ( al.10)
    1. Ushindani kutoka lugha nyingine kama kiingereza
      • Hadhi – Kiswahili kimedumisha
      • Athari za lugha ya mama
      • Mitazamo hasi kuhusu Kiswahili
      • Kutokuwepo kwa sera mwafaka kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa muda mrefu
      • Kuhusishwa kwa lugha ya Kiswahili na dini ya kiislamu/ eneo la pwani
      • Wamishenari walieneza dini zao kwa lugha ya kiingereza
      • Kutokouwa na vitabu vya kutosha vilivyoandikwa kwa Kiswahili
      • Uchache wa wataalamu wa lugha ya Kiswahili
      • Mkazo wa ufundishaji wa lugha za kikabila katika shule za msingi
      • Kuwepo kwa sheria katika shule kuwa Kiswahili kizungumzwe siku moja kwa juma
      • Lugha imetengwa katika matumizi ofisini za kiserikali 
                                                                                   (zozote 5x2=10 ambazo zimeelezwa)
  5. SEHEMU YA USHAIRI
  1. Viongozi wanapovurutana umoja miongoni mwa raia husambaratika
    • ingawa raia wanaishi katika hali ya uchochole bado wanashirikiana na kusaidiana kama ndugu
    • viongozi huchekelea raia baada ya kuwakosanisha
    • viongozi na familia zao hushirikiana pamoja baada ya kugoganisha wananchi
    • viongozi wanaendelea na shughuli zao na kuwaacha raia wakizozana wenyewe kwa wenyewe baada ya kuchochea uhasama kati yao
    • raia /watawaliwa hukosana kwa mambo madogo yasiyo na msingi wowote ` (yoyote 1x1=alama 1)
  2.  
    • shairi lina beti tano
    • mishororo mitano katika kila ubeti
    • shairi lina pande tatu yaani ukwapi,utao na mwandamizi
    • vina vya ushairi vinahitilafiana katika beti zote isipokuwa vina vya utao vinavyotiririka
    • kuna mizani 19 katika kila mshororo mgao wa 8,3,8 isipokuwa kibwagizo chenye mizani kumi na 16
    • shairi lina kibwagizo wanapowana fahali ziumiazo ni nyasi (zozote 5x1=alama 5)
  3.  
    • mazida(kurefusha maneno)kwa mfano yawile-yawe, yalikiota-yaliota
    • inkisari(kufupisha maneno)yali badala ya yalikuwa yendayo-yaendavyo,mepondoka-yamepondeka,hazoshika-hayashika-hayashiki,hazochoka-yasiyochoka, ngali-wangali.
    • Tabdila (kubadilisha matamshi) ng’ambu-ng’ambo, Hayeshika-hayashiki, mabaku-mabaki
    • Kuboronga sarufi-ingawa yali dhaifu majani ,badala ya ingawa majani yalikuwa dhaifu    (zozote 3x1=alama 3)
  4. lugha ya nathari
    japo raia ni maskini walionekana kuwa na umoja,walijitosheleza kwa kusaidiana undugu ulidhihirika miongoni mwao tangu zamani,viongozi walitenganisha raia hawa bila kujali,walipoanza kuvurugana wenyewe viongozi wanapozozana raia ndio wanaoumia. (hoja 4x1=alama 4)
  5.  
    • mabaka-masalio
    • kupachana-kufanana  (hoja 2x1=alama 2)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Form 2 Questions and Answers - Term 3 Opener Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest