Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 Mid Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp

SEHEMU A: TAMTHILIA
P. Kea: Kigogo

 1. LAZIMA
  “...binadamu ni mavumbi na mavumbi atarejea kwa maana, kwa tamaa mtu anapenda kula kuku huku nduguze wakila kama kuku. Na katika uchu huo huo amependa kufikia kilele cha ufanisi kwa kukanyaga migongo ya wenziwe...
  1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
  2. Kwa kutoa mifano mitatu katika dondoo hili, ainisha taswira zinazojitokeza. (alama 6)
  3. Huku ukitoa mifano kumi, jadili namna Wanasagamoyo walilemaza juhudi
   zao za kujikomboa. (alama 10)

SEHEMU B: RIWAYA
Matei: Chozi la Heri

Jibu swali la 2 au 3

 1. “Barafu iliyokuwa imegandia moyoni ilianza kuyeyuka na moyo kutwaa uvuguvugu. Hatimaye uyabisi wa moyo wake ulitoweka.”
  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Taja na ueleze sifa sita za mrejelewa. (alama 6)
  3. Jadili maudhui yanayobainika katika dondoo hili. (alama 10)

AU

 1. “Mama mtu alikuwa ameamua kwamba hapa hapamweki. Alikuwa amehudumu katika afisi za umma kama mhazili mwandamizi kwa miaka mingi mpaka kazi hii akaiona inamfanya kusinyaa, hana hamu tena.”
  1. Eleza umuhimu wa mrejelewa katika kukuza riwaya ya Chozi la Heri. (alama 6)
  2. Huku ukitoa mifano jadili changamoto zinazokumba asasi ya ndoa kwa
   mujibu wa riwaya hii. (alama 14)

SEHEMU C: USHAIRI

Jibu swali la 4 au 5

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

  Ningeuzwa kuchaguwa, mambo nisiyo yapenda
  Pasipo na kuchelewa, ningeanza na kukonda
  Kujapo kwa kuuguwa, kunilaza kwa kitanda

  Ningeishutumu njaa, kama adui mkuu
  Aso na fao kufaa, mwana wala mjukuu
  Mtu hapati kukaa, hatui ya juujuu.

  Kisha ningetaja vita, nduli ya tangu zamani
  Fundi wa vyembe na nyuta, si mwema simtamani
  Ni mtu wa vutavuta, kamwa hapendi amani

  Na katika mlolongo, kwenye huu msururu
  Ningetaja na kifungo, kutokuwa na uhuru
  Heri kwangu kuwa chongo, itakuwa haidhuru.

  Kadhalika na ukata, ningasahau siwezi
  Hauna pato kupata, kuyakidhi matumizi
  Hana haramu mkata, dawamu ya muombezi

  Ninguelani ukuwa, pamwe na athari zake
  Nijapo kuvunjikiwa, ukanikuta upweke
  Ni kama madhila huwa, una dhiki ndani yake

  Na mishale kama hiyo, ifumayo moyo wangu
  Inganipa jakamoyo, siyo matilaba yangu
  Ngawa siridhiki kwayo, ni kudura zake Mungu

  Maswali

  1. Eleza mambo ambayo nafsi neni hayapendi na kwa nini? (alama 5)
  2. Kwa kurejelea shairi hili, eleza umuhimu wa: (alama 6)
   1. inkisari
   2. tabdila
   3. kufinyanga sarufi
  3. Ainisha bahari tatu za mashairi ukirejelea shairi hili. (alama 3)
  4. Andika ubeti wa tano kwa lugha ya nathari. (alama 3)
  5. Eleza mbinu tatu ambazo zimetumiwa kusanifu ubeti wa tatu. (alama 3)

AU

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

  Bustani za jadi
  Maua ya kuchezea vipepeo
  Na pua kufurahisha
  Sasa ni mabaki ya kumbukumbu
  Za yaliyojiri hapa
  Na kukiacha kijiji kinywa wazi.

  Hapa walimpiga mwereka
  Dada yangu; mdogo wangu
  Shuleni akitoka
  Na mkoba wa kilo nzito za vitabu
  Chini akakandamiziwa
  Wakachana mbuga na wake ubikira!

  Pale kando ya mto
  Walimvizia na kumburura shangazi
  Binamu zangu wadogo wakiona
  Marinda wakamchania
  Kabla ya kumtia kidonda shangazi
  Naye ami kumchania kovu moyoni!

  Ni hapa kando ya barabara kuu
  Ambapo nyanyangu walimshika mkono
  Uchochoroni wakamburuta
  Na kumfanya kujutia
  Bahati mbaya ya kuishi kwingi
  Akaganda uchochoroni
  Hadi alipoletwa nyumbani kesho yake
  Na wachungaji wa machungani.

  Si hapa walipomshurutisha mama
  Chini wakamkanyagia
  Kama kuku wa kuchinja
  Baada ya yake sidiria kuikata?
  Si hapa sebuleni mwetu?

  Si hapa sokoni
  Nilipopata vazi la stara
  La wangu mke mpendwa
  Lililokatwa yake mihimili?
  Yule kichaa wa mwetu sokoni.
  Akawa kichwani amelivaa
  Na kuimba wimbo wa maombolezi
  Huku wanakijiji wakimpuuza
  Na watoto kumcheka?

  Ni hapa ambapo usiku ulipoingia
  Hawakusita kuhakikisha kuwa
  Yule kichaa amawazalia mtoto
  Na kujitia kundini kushangaa
  Kilichomtuma atake kujifungua!

  (Timothy Arege)

  Maswali

   

  1. Tambulisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2)
  2. Eleza dhamina ya mshairi. (alama 2)
  3. Fafanua mbinu za kimtindo zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 5)
  4. Bainisha aina za taswira katika shairi hili. (alama 4)
  5. Onyesha toni ya mshairi. (alama 2)
  6. Onyesha matumizi ya mishata katika shairi hili. (alama 1)
  7. Fafanua muundo wa shairi hili. (alama 4)

SEHEMU D: HADITHI FUPI
Jibu swali la 6 au 7

A.Chokocho na D. Kayanda (Wah): Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

 1. D. Kayanda: “Mwalimu Mstaafu”

  “Watu wa kwetu husema, ‘Usilipe jema kwa baya’, kwa hiyo mimi ninacho changu ambacho nitakupa kwa hiari yangu mwenyewe...”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. 'Usilipe jema kwa baya’. Fafanua kinaya katika kauli hii kwa kurejelea hadithi ya ‘Mwalimu Mstaafu”. (alama 16)

AU

 1. Mtihani Wa Maisha (Eunice Kimaliro)
  1. “Labda hata tayari ameona maajabu niliyoyafanya kwenye mtihani. Atanipa hongera kabla ya kunipa matokeo”.
   1. Eleza mbinu kuu ya kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
   2. Fananua umuhimu wa msemaji wa dondoo hili ukirejelea hadithi ya ”Mtihani wa Maisha”. (alama 6)
  2. S. O. Hamad: “Shibe Inatumaliza”
   “Ndugu yangu kula kunatumaliza.
   “Kunatumaliza au tunakumaliza?”

   Jadili ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kutoa mifano kwenye hadithi. (alama 12)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

 1. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.

  Kila kukicha mashaka
  Ni kero hili si huba
     Mimi pendo la viraka, heri demu la mkoba
     Ingawa mno nataka, kuishi nawe muhiba
     Pendo viraka viraka
     Litanishinda kuziba

  Kamwe sitoshughulika
  Nawaje wenye kuziba
     Viumbe wanosifika, kwa fedha, chuma na shaba
     Walostarabika, si mimi wa tobatoba
     Pendo viraka viraka
     Litanishinda kuziba

  Naapa sitojitweka
  Limenichosha si haba
     Nasomba vyangu viraka, nitie kwenye mkoba
     Sikuye ya kuzinduka, mjinga hawi ni juba
     Pendo viraka viraka
     Litanishinda kuziba

  1. Huu ni wimbo wa mapenzi. Thibitisha. (alama 2)
  2. Eleza sifa tatu za nafsinenewa katika wimbo huu. (alama 3)
  3. Fafanua mbinu nne ambazo nafsineni ametumia kufanikisha uwasilishaji wake. (alama 4)
  4. Eleza faida tano za kurithisha wimbo huu kwa vizazi vijavyo. (alama 5)
  5. Unanuia kufanya utafiti kuhusu utungo wa maigizo:-
   1. Eleza hatua tatu utakazofuata katika utafiti wa utungo huu. (alama 3)
   2. Fafanua udhaifu wa kuhifadhi utungo huu kwa njia ya maandishi. (alama 3)


Marking Scheme

 1.  
  1.  
   1. maneno ya Babu(Daktari) UK84
   2. anamwambia Majoka
   3. Majoka yuko Hospitali
   4. Majoka alizimia baada ya kupata habari ya kifo cha mwanaye/aliwehuka akaanza kuzungumza na Daktari kana kwamba ni Babu yake- Ngao 1X4
  2.  
   1. taswira maono - binadamu anaonekana kuwa mavumbi/kukanyaga
    migongo
   2. taswira muonjo -kwa tamaa mtu anapenda kula kuku
   3. taswira mnuso -kula kama kuku/kuku kula hata vilivyonuka
   4. taswira mwendo -kufikia kilele cha ufanisi
    Zozote 3X2
  3.  
   1. baadhi walikubali kuhongwa/kuhonga –Asiya anapata kandarasi ya kuoka keki/Nguruma anapendelewa
   2. Wanasagamoyo hawakuwa na umoja - baadhi waliwasaliti wenzao, Kombe na Boza wanajipendekeza kwa Kenga
   3. Baadhi walishiriki katika matumizi ya vileo na kutokujua leo la kujikomboa
   4. Baadhi ya Wanasagamoyo hawakuweza kutambua uongozi wa kike, walimchukia Tunu kwa vile alikuwa mwanamke-taasubi ya kiume
   5. Baadhi ya Wanasagamoyo hawakuwa na elimu iliyostahili, Ngurumo anamkumbusha Tunu kuwa walisoma pamoja na alipendelea Historia. Tunu alimpiku kimasomo
   6. Kulikuwa na vitisho – Baadhi ya Wanasagamoyo waliandikiwa vijikaratasi vya kuwatishia kuhamishwa
   7. Kulikuwa na mauaji ya wapinzani, Baadhi ya wanasagamoyo waliwaua wenzao ambao walipinga utawala dhalimu – Jabali
   8. Utamaduni au desturi za kurithi mamlaka, Majoka alirithi uongozi kutoka kwa babake naye anataka kumrithisha mwanaye Ngao Junior/ Kenga anaudhika na hali hii.
   9. Ukosefu wa ajira, walio na elimu bora wananyimwa nafasi za kuajira na uongozi wa Sagamoyo kwa vile ni tishio kwa nafasi zao. Wanakosa uwezo wa kifedha na kuishia kutegemea
   10. Wanasagamoyo kama Ngurumo wanashiriki kuwapiga wenzao na kuwaumiza, Tunu aliumizwa.
   11. Vituo vya habari vya Wanasagamoyo vilivyowahamazisha vilifungwa na uongozi wa Sagamoyo – Runinga ya Mzalendo
   12. Askari wa Sagamoyo walivunja mikutano ya Wanaharakati kwa amri ya Majoka
   13. Wanasagamoyo kama Kenga walimhimiza Majoka kuwatia mbaroni wapinzani wake, Ashua anatiwa ndani kwa kusudi la kumshurutisha Sudi.
    Zozote 10X1
 2.  
  1.  
   1. Maneno ya mwandishi/msimulizi UK114
   2. anamrejelea Mwangeka
   3. Ni katika ukumbi wa mikutano/warsha
   4. Apondi alipomaliza hotuba yake, Mwangeka alikuwa hajiwezi tena kihisia alimpenda Apondi.
  2.  
   1. Mwenye bidii – masomoni
   2. Amewajibika –
   3. ana msimamo thabiti
   4. Mzalendo
   5. Mvumilivu/mstahimlivu
   6. mkarimu
   7. Mnyenyekevu/mpole
   8. mcheshi
  3.  
   1. mapenzi/ ndoa/usuhuba – Mwangeka alianza kuhusiana na Apondi kimapenzi
   2. ustahimilivu- Mwangeka hakutaka tena kuoa baada ya kifo cha mkewe
   3. maombolezi/upweke- hali ya upweke na chuki kwa Mwangeka na Apondi kwa kufiwa na wapendwa wao
   4. maridhiano/haja ya kuwa na amani- suala kusameheana na kuishi kwa amani
   5. wajibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali – Msalaba Mwekundu- kusaidia serikali katika kudumisha hali ya ushwari
   6. Usawa wa kijinsia/ wanawake kupewa nafasi sawa/ Apondi anadhibiti wasilisho vilivyo - anashangiliwa
   7. athari za vita – mke na watoto wa Mwangeka kuangamizwa/mme wa Apondi kufia vitani ughaibuni
   8. utayarivu katika kupambana na mikasa/ raia au serikali wasitegemee
    mashirika au wageni kuwaauni
   9. walinda usalama kutagusana na raia kwa njia ya urafiki/salama/polisi wanastahili kushirikiana na raia bali si kuwadhalilisha
    Zozote 5X2
 3.  
  1. UK 64

   Umuhimu wa Annette

   1. Anaonyesha watu waliokengeuka, wanathamini tamaduni za kigeni na kutukuzwa ugeni kuliko vya kwao
   2. Athari anazopata mwanandoa mmoja anapoamua kugura ndoa – upweke/kifo
   3. Udhaifu wa Kiriri kama bwana wa nyumba – anadhibitiwa na mkewe/anashindwa kumshawishi mkewe
   4. Umuhimu wa kuwa na mashauriano katika ndoa ili iwafae wote kifamilia
   5. Imani kuwa ng’ambo kuna maisha mazuri – Green Card kuwa tikiti ya maisha mazuri
   6. Mishahara iliyo midogo inawafanya wenyeji kuacha kazi na kwenda kuliko na mishahara mizuri.
   7. Ukosefu wa uzalendo – Annette anaongozwa na ubinafsi- hajali nchi yake wala mmewe
   8. Namna mzazi anavyoweza kuwaathiri watoto wake visivyo. Songoa anakashifu hali ya nchi yake/mawazo yake ni sawa nay a mamake
   9. Elimu inayotolewa ni duni, elimu ya ughaibuni inathaminiwa na matajiri
   10. Anaonyesha umaskini uliopo nchini mwake ilhali hawa matajiri ndio wanaostahili kuimarisha nchi kiuchumi
    Zozote 6X1
  2.  
   1. Ukabila- Selume/Subira wanabaguliwa na jamii zao kutokana na tofauti za kikabila. Kangata alikashifiwa na ndugu zake kwa kumwoza binti yake kwa watu wa ukoo ‘mbaya’
   2. mauaji- ndoa ya Ridhaa/Mwangeka/Apondi inaathirika kutokana na wenzao wa ndoa kuuawa
   3. Uhalifu-ndoa ya Kaizari inatatizika kutokana na kutendewa unyama mkewe na mabinti zake mbele ya macho yake
   4. Ndoa za lazima – Pete anaozwa kwa Fungo ambaye ni wa umri wa babu yake kwa lazima. Ndoa hii hatimaye inavunjika
   5. Ubakaji wa mabinti – Sauna anabakwa na baba mlezi. Mamake Sauna anamshauri asiliseme hadharani kwa vile ndoa yake itavunjika
   6. Ndoa haramu – Nyangumi anaishi na Pete kwa majaribio akimwahidi kuwa atamwoa ilhali ana mke tayari. Anampachika mimba ambayo Pete anang’ang’ana kuitoa
   7. Uasherati – Tenge anawaleta vimada kwa nyumba mbele ya wanawe pindi mkewe anapoenda shamba
   8. Kuwakana wana – Babake Kipanga anamkana na kumfukuza kwake kuwa sura yake haifanani nay a wanawe wengine
   9. Ukengeushi – Annette anamwacha mumewe Kiriri na kuhamia ughaibuni bila kujali hisia za mumewe/anamdhibiti mumewe.
 4.  
  1.  
   1. Kukonda -kwa kuugua na kulazwa
   2. Njaa -kwa kushindwa kukaa
   3. Vita -kwa kusababisha mvutano/ukosefu wa amani
   4. Kifungo -kwa kutokuwa huru
   5. Ukata/Umaskini -kwa kumkosesha pato la kujikimu
   6. Ukiwa/Upweke -kwa kusababisha dhiki za ndani/kisaikolojia
  2.  
   1. Ningeulaani -ningeulaani
    Ngawa -ingawa
    Umuhimu- kupata urari wa mizani
   2. Kuuguwa -kuugua
    Kuchaguwa-kuchagua
    Umuhimu- kupata urari wa vina
   3. Kufinyanga sarufi
    Hana haramu mkata- mkata hana haramu
    Ukanikuta upweke-upweke ukanikuta
    Umuhimu-kupata urari wa vina
    Mfano-1
    Umuhimu-1
    3 ×2 =6
  3.  
   1. Mathnawi-vipande viwili kwa mishororo
   2. Ukaraguni-vina vya kati na vya nje vinabadilika kwa kila ubeti
   3. Sabilia-kila ubeti una kiishio/halina kibwagizo
    3x1
  4. Siwezi kusahau umaskini vilevile.Unasababisha mtu kukosa kipato cha kujikimu kimaisha.Maskani hana cha haramu daima huwa anaomba.
   3 × 1
  5.  
   1. Mishororo mitatu kwa ubeti
   2. Vipande viwili kwa kila mshororo
   3. Mizani 8×8 kwa kila mshororo
   4. Vina vya ndani ni-ta na vya nje ni-ni
    Za kwanza 3×1=3
 5.  
  1. Mwanaume ambaye jamaa zake ni wahasiriwa wa ubakaji (alama 2x1)
  2. Kuonyesha namna watu mbalimbali wanavyoathiriwa na matendo ya ubakaji (alama 2x1)
  3.  
   1. Maswali balagha – na watoto kumewaka?
   2. Nidaa – Kilichomtuma atake kujifungua! Siyahi
   3. Taswira – Ya ubakaji
   4. Kinaya – wabakaji kujitia kundini na kushangaa kilichomtuma atake kujifungua!
   5. Tasfida – wakachana mbuga na wake ubikira
   6. Tabaini – si hapa walipomsurutisha mama. Si hapa sebuleni mwetu. Si hapa sokoni mwetu
   7. Takriri – si hapa
   8. Tashbihi – kama kuku wa kuchinja
   9. Kuboronga sarufi – Shuleni alitoka na wangu mke mpendwa
   10. Chuku – mkoba wa kilo nzito za vitabu
    (Zozote 5x1)
  4.  
   1. Taswira mnuso – maua ya kufurahisha pua
   2. Taswira mguso – Walipiga miereka, kumburura shangazi, walimshika mkono
   3. Taswira oni/mwono – binamu zangu wakiona
   4. Taswira mwendo – wakachana mbuga na wake ubikira
   5. Taswira hisi – Baada ya yake sidiria kuikata?
    – si hapa sebuleni mwetu?
    (Zozote 4x1)
  5.  
   1. Toni ya uchungu – kwa jamaa ya nafsi heri kubakwa
   2. Toni ya masikitiko – kubakwa kwa kichaa
    (2x1)
  6.  
   1. Za yaliyojiri hapa
   2. Na pua kufurahisha
   3. Na kumfanya kufutia
   4. Si hapa sokoni
    (1x1)
  7.  
   1. Beti saba
   2. Mishororo inatofautiana kwa kila ubeti
   3. Vina vinatofautiana kwa kila ubeti
   4. Mizani inatofautiana kwa kila mshororo
   5. Lina kipande kimoja kwa mshororo
    (Zozote 4x1)
    =alama 4
 6.  
  1.  
   1. Maneno ya Jairo
   2. Anamwambia Mwalimu Mosi
   3. Nyumbani kwa Mwalimu Mosi
   4. Mosi alimzawidi Jairo zawadi alizopewa; sasa Jairo naye ameona heri naye amletee zawadi mwalimu wake
  2.  
   1. Mwalimu Mosi aliwafunza wanafunzi wake kutobagua wenzao. Jairo alibaguliwa kwa kunyimwa fursa ya kutoa dukuduku lake
   2. Jairo anamdhalilisha mwalimu wake kwa kumtolea cheche za maneno hadharani
   3. Jairo hakuzingatia nasaha za Mwalimu Mosi. Aliishia kuwa miongoni mwa waliokosa kufaulu maishani
   4. Jairo anawakashifu wenzake aliosoma nao. Anawaita majizi ilhali yeye mwenyewe hakutaka kufanya bidii shuleni
   5. Jairo anafurahia kustaafu kwa Mwalimu Mosi kwa vile anaona hakuna mtoto mwingine akayeathiriwa vibaya na Mosi huku Mosi anasifiwa kwa kuwakuza wanafunzi wengi
   6. Jairo anamwona Mosi kama mwongo aliyewapa matumaini yasiyokuwepo
   7. Jairo anaona kuwepo shuleni kulimpotezra wakati angekuwa mwizi hivyo kuishioa kuwa mtu wa maana zaidi katika jamii
   8. Jairo alikatazwa pombe lakini yeye anaona kuwa ukisha lewa unaona raha ya maisha; eti hata ukiimia ukiwa mlevi huhisi uchungu.
   9. ushauri wa kuwa muadilifu maishani, Jairo anaona usiyo na maana, anaona haramu kuwa tamu/ anaona maisha ni mafupi
   10. Jairo hakumshukuru Mwalimu kwa kumpelekea zawadi
   11. Jairo aliwatukana waliotumwa kumpelekea zawadi
   12. Jairo alichukulia kupelekewa zawadi kama jambo la kumdunisha/kumwaibisha ihali ni mhitaji
   13. Jairo anampa Mwalimu Mosi mke na watoto kama zawadi kutoka kwake
   14. Amamkosea heshima mke wake kwa kumtoa kama zawadi/bidhaa kwa mtu mwingine
   15. Anamwingilia mwalimu kwa utundu mapema kwa kuipeleka aila yake kwa mwalimu pasipo kujali hisia za mwalimu na mke wake/alimdhalilisha mwalimu mbele ya mke wake
   16. Anafuata uvumi na kumvamia mwalimu kwa nia ya kumdhuru kwa upanga
   17. Hajui kuomba msamaha badala yake alipogundua makosa yake anataka kujitoa uhai
 7.  
  1.  
   1. Kinaya-Samueli anapuuzwa na mwalimu mkuu badala ya kupongezwa.
   2. Umuhimu wa Samueli
    • Anabainisha uwajibikaji wa mwalimu mkuu –anapothibitisha kuwa amemaliza karo ndipo anampa matokeo yake
    • Anabainisha maudhui ya taasubi za kiume /ubabedume -babake kumwonea fahari mwanawe wa kiume akifua dafu.
    • Ni kielelezo cha ukosefu wa maadili -kuchanganya mapenzi na masomo.
    • Ni kielelzo cha watu wanaokabiliana na changamoto za maisha kwa kujiua- anapoanguka mtihani anajitosa majini ili afe.
    • Anajenga maudhui ya elimu –kufeli mtihani ni fedheha
    • Ni kielelezo cha watu wasiowajibika –kuficha matokeo yake baada ya kufeli mtihani
  2.  
   1. kula kunawafanya Sasa na Mbura kuwa wategemezi; wakishiba hawafanyi lolote
   2. Mzee Mambo ni waziri asiye na wizara maalum, analipwa mshara wa walipa kodi pasi kufanya kazi
   3. Licha ya Mzee Mambo kutokuwa na wizara maalum yeye na wenziwe wanajiamulia kima cha mshahara watakaopokea
   4. Mzee Mambo alipewa wadhifa huu kwa nia ya kuongeza walaji
   5. Dini inatumiwa kuhalalisha haramu/ulafi. ‘Hadhaa min fadhil rabbi’
   6. Wafanyakazi hufika kazini ila hawatendi kazi zenyewe lengo ni kuwepo
   7. Wanabadhiri fedha za umma kwa sherehe chapwa; mtoto kuota meno/kuanza darasa la chekechea
   8. wanajinadi kwa mitandao ili wajulikane ndio wafadhili wakuu na kupata sifa
   9. Magari ya umma/ rasilmali inatumiwa yanatumiwa kwa shughuli za kibinafsi- kusomba maji/kuleta mapambo/kubeba jamaa
   10. Vyakula anuai vinaandaliwa ilhali raia wana njaa
   11. Watu wanafika kula tu/ Sasa na Mbura wanakula duru kadhaa ilhali hawachangii chochote
   12. Walaji hawajali asili ya chakula chenyewe/ wanafanyiwa hisani
   13. Wanaposhiba wanalala
   14. Kula kunawafanya kudharau vyakula vya kiasili kama mchele wa Mbeya; wanafisha kilimo chao kwa kuagiza basmati
   15. Viongozi ni mafisadi, wanachota fedha za umma na hawajali kulaumiwa
   16. Dawa zinaibwa kutoka mabohari za serikali na kuuzwa katika maduka ya watu binafsi
   17. Kula huku kunasababisha maradhi kama sukari, presha, saratani
   18. Kula kunawafanya wauane kifikira na kimawazo/wananyang’ana vinavyoonekana na visivyoonekana
    Zozote 12X1
 8.  
  1.  
   1. Ni kero hili si huba
   2. Mgani nataka kuishi nawe muluba oendo viraka viraka, linanishinda kuziba
  2.  
   1. Mwenye tamaa – kupenda fedha/ pesa
   2. Mwenye ubinafsi – kujali pesa kuliko
   3. Msaliti – kupenda pesa badala ja fuata penzi
   4. Mwenye mapuuza – anapuuza penzi
   5. Mgomvi – lala kulinena washako
    Za mwanzo 3
  3.  
   1. Jazanda/ sitiari – mimi pendo la mvika
   2. Takriri – Pendo viraka viraka, titani, shindo kuziba
   3. Inkisari – Wanasifika, walostarabika silaiye n.k
   4. Kuboronga sarufi – Nasomba vyangu viraka ingawa mno nataka
   5. Mishata – Pendo viraka viraka
    Za kutuza nne
  4.  
   • Hutumiwa kuburudisha jamii.
   • Hutumiwa kutakasa hisia za anayeamba kama vile huzuni.
   • Hutumiwa kusifu/kukashifu tabia za mpenzi katika jamii.
   • Hutumiwa kukuza ubunifu wa jamii ili kuibua hisia k.v huzuni, huruma n.k
   • Ni nyenzo ya kupitisha maarifa au elimu ya jamii.
    Zozote 5X1
  5.  
   1.  
    • Kufanya maandalizi – ili kujua walengwa, muda wa utafiti, gharama na mbinu za utafiti
    • Kukusanya data kwa kupitia kwa hojaji, mahojiano, kushiriki ama kutazama.
    • Kurekodi data kupitia kwa maandishi, kunasa sauti ya mhojiwa,
    • Kuchunguza data upya/maelezo yaliyotolewa na kuyanakili jinsi yalivyo ili kuchanganua baadaye.
    • Kuchanganua data na kufasi kwa matokeo ya uchunguzi kuhusu maigizo.
     ZOZOTE 3X1
   2.  
    • Kupotea kwa sifa muhimu kama vile ishara, hisia, toni, kiimbo n.k
    • Kupotea kwa uhai asilia wa kutenda na kusema
    • Kukosa kwa ile taathira asilia kunanyima hadhira fursa ya kuuliza maswali na kushiriki
    • Kupunguza kwa hadhira na usambazaji wake.
     Zozote 3x1

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 3 Mid Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest