Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Mid Term 1 Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

  1.          
    1. Tofautisha sauti irabu na konsonanti. (alama 2)
    2. Andika neno la silabi moja lenye sauti mwambatano. (alama 1)
    3. Kanusha sentensi ifuatayo:
      Wewe unapenda kuongea na kutenda. (alama 2)
    4. Ainisha mofimu katika sentensi Alimapo. (alama 2)
    5. Tunga sentensi moja kubainisha matumizi ya vivumishi vya majina. (alama 1)
    6. Eleza matumizi ya viakifishi vifuatavyo. (alama 4)
      1. Dukuduku
      2. Nukta pacha
    7. Nyambua vitenzi katika kauli ya kutendesha. (alama 2)
      1. Oa
      2. Ona
    8. Eleza maana ya kirai. Toa mfano. (alama 3)
    9. Tunga sentensi kuonyesha upatanisho wa kisarufi ukitumia nomino ‘Tambi’. (alama 2)
    10. Tumia ‘gani’ kama kivumishi na vilevile kama kiwakilishi. (alama 3)
    11. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya urejeshi; (alama 1)
      Amani yetu inatusaidia.
    12. Badilisha sentensi iwe kinyume: (alama 2)
      Mtanashati amesifiwa kwa kukitakasa kiti chake.
    13. Sisitiza katika umoja na wingi, ‘ukuta’ ukiwa karibu’. (alama 2)
    14. Eleza matumiza mawili ya ‘Ku’ (alama 2)
    15. Tunga sentensi moja yenye kitenzi kishirikishi kikamilifu. (alama 2)
    16. Ziweke nomino hizi katika ngeli zake. (alama 2)
      1. Waya
      2. Kilembwe
  2. Isimu jamii.
    1. ‘… unaweza kukata rufaa iwapo unaonelea kuwa umehiniwa ,,,’
      1. Bainisha sajili ya mazungumzo haya. (alama 1)
      2. Fafanua sifa za matumizi ya lugha katika muktadha huu. (alama 4)
    2. Jadili changamoto zinakumba kuimarika kwa Kiswahili katika jamii ya sasa. (alama 4)
  3. TAMTHILIA YA KIGOGO
    1. Fafanua mbinu nane alizotumia Majoka ili kudumisha uongozi wake. (alama 8)

Mwongozo wa Kusahihisha

  1.         
    1. Irabu ni sauti ambazo hutamkwa kwa ulaini bila hewa kuzuiliwa ilhali konsonanti ni sauti ambazo hewa huzuiliwa na ala za kutamkia.

    2. pwa

    3. Wewe hupendi kuongea wala kutenda.

    4. A- Nafsi
      lim- mzizi
      a-kiishio
      po- kirejeshi

    5. Mwalimu mkulima ametuzwa zawadi kemkem

    6.      
      1.  Duku duku      
        • kuonyesha maendeleo yalioandikwa yanaendelea mfano: Mariam kwa nini....
        • Kuonyesha maneno yanatanguliwa na mengine ambayo hayajaandikwa mf.....kesho
      2. Nukta pacha
        • Kuonyesha kukatizwa usemi katika mazungumzo
    7.           
      • Uza
      •   onyesha/ onya
    8. Ni fungu la maneno lililo maana yasiokalimika 
      mfano: mtoto huyu ni wetu

    9. Tambi hizi zitawashwa kesho

    10. Kiatu gani kilichoniniliwa? - Gani - V
      Gani kilichonunuliwa - Gani - W

    11. Amani yetu iliyotusaidia
      amani yetu inayotutusaidia

    12. Mtanashati amekashifiwa kwa kukilaani kitu chake.

    13. Ukuta uu huu umebomoka
      Kuta zizi hizi zimebomoka
    14.     
      1. Kama nafsi ya pili umoka mfano: alikuja
      2. Kuonyesha mahali mf kule
      3. Kama nomino ya kitenzi jina kusoma kwake kuna kunanitia

    15. Mama alikuwa shambani

    16. Waya - U-ZI
      Kilembwe - A- WA
  2.                
    1.      
      1. Sajili ya mahakamani
      2.           
        • Msamiati maalum mfano rufaa
        • Matumizi ya mdokezo
        • Kunukuu na kurejelee vifungu vya sheria za nchi
        • Kidadisi / kuuliza maswali
        • Lugha ya unyenyekevu/ heshima
        • Matumizi ya sentensi ndefu
        • Sarufi hutangazwa
    2.           
      • Matumizi kiholela ya lugha bila kuzingatia kanuni za kisarufi miongoni mwa wananchi
      • Athari za lugha nyingine za kiafrika
      • Athari za sheng' miongoni mwa vijana
      • Uhaba wa machapisho kwa lugha ya Kiswahili
      • Somo la Kiswahili kutengewa vipindi vichache shuleni ikilinganishwa na somo la Kiingereza.
      • Masomo mengi shuleni hufunzwa kwa lugha ya Kiingereza kuanzia shule za malezi isipokuwa somo la Kiswahili.
      • Matumizi mabaya ya Kiswahili kwenye vyombo vya habari ambavyo vinahitajika kukuza Kiswahili.
      • Kasumba ya kikoloni miongoni mwa wananchi kuwa Kiswahili ni lugha ya hadhi ya chini inayotumika na wasiosoma.
      • Kutokuwa na sera madhubuti inayoelekeza kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili.
  3.                 
    • Propaganda -  vyombo vya habari kama vile redio ilitumika kueneza propaganda wimbo katika redio ni wa kumsifu majoka shupabu anayehusindiwa daima.
    • Kuua washindani km Jabali, jaribio la mwanganmiza Tunu, Kuamrisha kingi apige watu risasi.
    • Vitisho vya kufutwa kazi kama Kingi
    • Kutawanya mikutano mf ya Tunu
    • Kuhangaisha raia na kuwaogofya mf Akina Situ. Kurushiwa vijikaratasi vya kuwaamuru wahame.
    • Kuvunja sheria akipendelea wafuasi kama Ngurumo lupata kibali cha kuuza pombe ili apate watu wa kumuunga mkono .
    • Kuwa na washauri kama Kenga
    • Mbinu ya tenga tawale, alisema alitaka kuongea na Tunu na Sudi kila mmoja pekee yake.
    • Kuwaua mashahidi wa uovu wake mf Ngurumo kisha alipanga kumuua Chopi.
    • Kufukuza wafadhili wanaunga mkono wapinzani wake 
    • Kuharamisha maandamano ya kudai haki.
    • Kutumia hila na kudanganya umma anashughulikia malalamishi yao kwa mfano kuongeza mishahara kisha kupandisha kodi.
    • Kunyima watu habari za ukweli za jimbo kwa mfano kufunga kituo cha runinga ya matendo ili watu wasimpinge.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 3 Mid Term 1 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest