SEHEMU YA A: USHAIRI
Soma shairi na kisha uyajibu maswali yafuatayo:-
- Ni sumu, sumu hatari
Unahatarisha watoto
Kwa ndoto zako zako leweshi
Za kupanda ngazi
Ndoto motomoto ambazo
Zimejenga ukuta
Baina ya watoto
Na maneno laini
Ya ulimi wa wazazi - Ni sumu, sumu hasiri
Unahasiri watoto
Kwa pupa yako hangaishi
Ya kuwa tajiri mtajika
Pupa pumbazi ambayo
Imezaa jangwa bahili
Badala ya chemichemi
Ya mazungumzo na maadili
Baina ya watoto na mzazi - Ni sumu, sumu legezi
Unalegeza watoto
Kwa mazoea yako tenganishi
Ya daima kunywa ‘moja baridi’
Mazoea mabaya ambayo yanafunga katika klabu
Hadi saa nane usiku
Huku yakijenga kutofahamiana
Baina ya watoto na mzazi - Ni sumu, sumu jeruhi
Unajeruhi watoto kwa pesa,
Kwa mapenzi yako hatari
Ya kuwaliwaza watoto kwa pesa
Zinawafikisha kwenye sigara na ulevi
Na kisha kwenye madawa ya giza baridi
Barabara inayofikisha kwenye giza baridi la kaburi la asubuhi
Maswali
- Pendekeza kichwa kwa shairi hili. (alama 1)
- Fafanua maudhui ya shairi hili. (alama 2)
- Ni kwa njia gani kinachozungumziwa kinajenga ukuta? . (alama 2)
- Dondoa tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi na uzitolee mfano (alama 4)
- Eleza umbo la shairi hili. (alama 3)
- Uandike ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
- Eleza maana ya vifungu hivi vilivyotumika katika shairi . (alama 4)
- Giza baridi
- Yanakufunga katika klabu
SEHEMU B:FASIHI SIMULIZI
-
- Taja na ueleze sifa za mtambaji bora katika fasihi simulizi. (alama 10)
- Nyimbo zina wajibu gani katika jamii. (alama 4)
-
- Eleza maana ya vitendawili. (alama 2)
- Onyesha sifa za kitendawili. (alama 4)
-
- Taja na ueleze aina nne kuu za hadithi (alama 8)
- Eleza mbinu tatu ambazo mtambaji anaweza kutumia kuishirikisha hadhira yake.(alama 6)
- Fafanua vipera vifuatavyo vya fasihi simulizi. (alama 6)
- Majigambo
- Mivigha
- Lakabu
MARKING SCHEME
USHAIRI
- Kichwa
- Kielelezo kibaya
- Tabia mbovu kwa watoto
- Wazazi wabaya/ walegevu
- Maudhui ya shairi
- Mshairi anasema kuwa wazazi wanahasiri watoto kwa pupa yao ya kulewa kila wakati na kuwa kielelzo kibaya
- Wazazi kukaa vilabuni mpaka usiku wa manane bila kufahamiana na watoto wao ni vibaya
- Wazazi kuwapa watoto pesa nyingi ni tabia potovu kwani wanazitumia dawa za kulevya
- Wazazi wanatafuta utajiri na kukosa wakati wa kuwashauri/ kuwafunza maadili mema
- Kinachojenga ukuta
- Hapana mazungumzo ya kishauri baina ya watoto na wazazi nah ii hujenga ukuta baina ya watoto na wazazi
- Kulewa kila wakati na kukaa kilabuni kwa mpaka usiku wa manane hujenga ukuta kwa kuwa mzazi huwa hapati wakati wa kuzungumza na mtoto 2x1=2
- Tamatahli za usemi
- Takriri – ni sumu, sumu
- Tashihisi – ndoto zinajenga ukuta/ yanakufunga katika klabu
- Istiara – ni sumu Kutaja – 1, Mfano – 1
- Umbo la shairi
- Lina beti nne
- Kila mshororo una mishororo tisa isipokuwa ubeti wa mwisho
- Ni shairi huru kwa kuwa halizingatii arudhi
- Lugha nathari- ubeti wa nne
- Mshairi anasema kuwa wazazi wanaumiza watoto kwa kuwapa pesa
- Ni vibaya kuliwaza watoto kwa kuwapa pesa
- Kwani huwaingiza katika maovu ya kuvuta sigara na ulevi na mihadarati
- Hali hii inaishia upotofu wa watoto/ huwaingiza katika hali mbaya/ kifo
- Maana ya vifungu
- Giza baridi – hali mbaya/ kifo
- Yanakufunga katika klabu – kuwa na mazoea mabaya ya kukaa kilabuni kulewa mpaka usiku wa manane
FASIHI SIMULIZI
-
- Sifa za mtambaji bora
- Awe na uwezo wa kuwasilisha hadithi.
- Anafaa kutumia njia inayochangamsha hadhira.
- Awe na ujuzi wa kuifahamu hadhira yake.
- Awe na ufahamu mpana wa lugha pamoja na utamaduni unaohusika.
- Awe na uwezo wa ufaraguzi.
- Aweze kufahamu tabia za binadamu na mikondo mbalimbali ya jamii. 5 x 2 = 10
- Wajibu wa nyimbo
- Hutumbuiza
- Kuwasifu watu maarufu
- Kusahihisha maovu ya jamii
- Huhifahi utamaduni
- Huelimisha watu
- Hukuza lugha
- Huhamasisha watu
- Kufariji waliofiwa
- Kuendeleza uhai wa jamii n.k (1 x 4)
-
- Kitendawili ni fumbo/msemo wa kinafumbo amabao hufumbua jambo Fulani na hutolewa hadhira au wasikilizaji ili waufumbue. 1 x 2= 2
- Hutangulizwa kwa njia maalumu
- Ujumbe wake ni wa kimafumbo
- Ufananisho wa kihazanda
- Ni fupi kwa maelezo
- Hutegemea mazingira/sehemu Fulani 4 x 1 = 4
- Sifa za mtambaji bora
-
-
- Visasili - Hadithi zinazosimulia asili ya watu, vitu ama tabia Fulani.
- Ngano za mazimwi - Husimulia kuhusu mazimwi
- Hurafa - Hadithi ambazo zina wahusika wanyama lakini waliopewa tabia za binadamu.
- Hekaya - Ngano fupi zinazosimulia matukio ya kushangaza yanayoonyesha hila au ujanja wa mwanadamu
- Mighani huwa na lengo la kueleza visa na mikasa ya watu ama mashujaa wa jamii fulani.
-
- Kutumia viungo vyake vya mwili kuikuza na kuifanya hadithi kusisimua.
- Msimuliaji kuchukua nafasi ya wahusika katika hadithi ili kuishirikisha hadhira.
- Uwezo wa kuiga matendo na wahusika kwa kuimba na kupiga makofi ili kuvutia hadhira.
- Ucheshi na mvuto wa lugha ili kuifanya hadhira kushikika.
-
- Majigambo – Mazungumzo yanayotolewa na mtu fulani ili kutapa
- Mivigha – sherehe maalum za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi maalum.
- Lakabu – Majina ya utani au kupanga ambayo watu hujipa au kupewa
-
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili paper 3 Questions and Answers - Form 3 End Term 1 Exams 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students