Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 End Term 2 Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Andika Insha mbili
  2. Swali la kwanza ni la lazima
  3. Chagua insha nyingine kutoka hizo tatu  zilizobaki
  4. Kila insha isipungue maneno 400
  5. Kila insha ina alama 20

 Watahiniwa wanastahili kuona kuwa maswali yote yako na hakuna yaliyoachwa.



MASWALI

  1. Halmashauri ya utunzi wa mitihani nchini imewatahadharisha watahiniwa dhidi ya udanganyifu katika mitihani ya kitaifa. Andika tahadhari hiyo na hatua zitakazochukuliwa dhidi ya watakaozikiuka.
  2. Katiba mpya imewapa vijana uhuru wa kujitegemea na kujiendeleza kimaisha. Thibitisha
  3. Pilipili usiyoila yakuashiani?
  4. Andika hadithi itakayomalizikia kwa:
    …………………kisa hiki kilinifundisha kwamba kuzaliwa masikini si hoja.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SWALI LA KWANZA

Ni swali  la onyo au ilani. Sura lazima izingatiwe

HOJA.

  1. Mtahiniwa haruhusiwi kuiingia katika chumba cha mtihani akiwa na simu/rununu
  2. Wasimamizi hawafai kuingia  na rununu katika chumba cha mtihani
  3. Wasimamizi wakuu wa mitihani na walimu wakuu wa shule pekee yao wanaruhusiwa kuwa na simu lakini ni kwa minajili ya mawasiliano kwa waziri wa elimu, mkuu wa elimu wilayani, mkurugenzi wa elimu mkoani ama halmashauri ya mitihani nchini Kenya(KNEC)
  4. Msimamizi mkuu wa mitihani na mwalimu mkuu hawatakikani katika chumba/vyumba vya mitihani wakiwa na rununu zao
  5. Mawasiliano ya karatasi za maswali hayafai kukaguliwa na mwalimu mkuu wala mwalimu yeyote kabla ya muda wa mtihani huo kukamilika
  6. Msimamizi mkuu haruhusiwi kutoa masalio ya karatasi za maswali katika chumba cha mtihani
  7. Wasimamizi wanafaa kuifunga bahasha ya maswali na kkuweka mbele ya chumba cha mtihani
  8. Ni hatia kwa mtahiniwa kuingia katika chumba cha mtihani na kifaa chochote kisichohitajika kama vile nakala za kusoma, vitabu vya maandalizi, na majibu  yoyote ya mtihani
  9. Ni hatia kwa mtahiniwa kubeba karatasi bila maandiko katika chumba cha mtihani au maelekezo ya kikokotozi au kifaa chochote kitakachomwelekeza mtahiniwa.
  10. Ni  hatia kwa mtahiniwa kujihami katika chumba chaa mtihani  na/au kikokotoo kilicho na maelekezo au kifaa chochote kitakachomsaidia kudnaganya
  11. Ni hatia kwa watahiniwa kusaidiana kujibu maswali ya mtihani
  12. Ni hatia kwa mtu yeyote kufanya mtihani kwa niaba ya mtahiniwa mwenyewe
  13. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuzingatia kanuni hizi atakuwa amekiuka kanuni za halmashauri ya mitihani  ya kitaifa  nchini na atachukuliwa hatua kali.
    1. Kuvunja sheria au kanuni 1,8, 10 na 11 ; matokeo ya mtahiniwa katika somo husika yatatupiliwa mbali na atatuzwa alama ‘Y’ hivyo alama yake ya matokeo itakuwa ‘Y’ na kisha hataruhusiwa kufanya mitihani minane ya KNEC kwa miaka miwili.
    2. Kuvunja kanuni ya 2, 3, 4, 5, 6 na 7 ; watashtakiwa na wakipatikana na hatia wataachishwa kazi.
    3. Kuvunja kanuni ya 12 ;(Kufanya mtiihani kwa niaba) mtahiniwa atatiwa mbaroni au kushtakiwa na kulipa faini.

KUTUZA

  • Tahadhari zake ziwe zaidi ya 7 kisha atoe hatua 3 muhimu zitachukuliwa
  • Akitaja tahadhari pekee akadiriwe kwa kiwango cha C+(Alama 10)
  • Akitaja hatua pekee bila kuzongatia tahadhari atakuwa amejitungia swali(Kiwango cha D-)

SWALI LA PILI

Thibitisha : Ni kutoa maelezo yenye  kudhihirisha kuwa linalosemwa ni la ukweli au si la ukweli.

Uhuru wa vijana

Hoja za kuunga mkono

  1. Vijana wametengewa nyadhifa za uongozi katika ngazi za ugatuzi
  2. Vijana  huchagua viongozi wao wa kisiasa
  3. Vijana wameruhusiwa kutoa maoni yao katika maswala ya kijamii
  4. Vijana huruhusiwa kujiunga na kundi  lolote la kidini kukuza imani yao
  5. Vijana wana uhuru wa kujiunga na makundi au mashirika ya kuwawezesha kutwaa mikopo ya fedha  kutoka katika hazina ya vijana
  6. Vijana wana uhuru wa kutangamana na wale wawapendao
  7. Vijana wana uhuru wa  kuchagua wa kuoa au kuolewa ili kuanzisha familia
  8. Vijana wana uhuru wa kujichagulia taaluma za kusomea
  9. Vijana wana uhuru wa kukuza vipawa vyao kwa kushiriki mashindano  yanayoandaliwa katika  ngazi zote kuanzia mashinani hadi kitaifa kama vile mashindano ya riadha, kandanda, muziki ili kushindania tuzo tofauti.

Hoja za kupinga

Vijana hawana uhuru wa kushiriki mambo yafuatayo.

  1. Kutumia vileo au dawa za kulevya
  2. Kuvalia mavazi yasio na adabu/heshima
  3. Kuiga kikasuku desturi  za kigeni
  4. Kutazama au kusoma filamu au fasihi ghushi
  5. Kushiriki ukahaba au ushoga
  6. Kushiriki burudani au tafrija katika majumba ya starehe
  7. Kushiriki mapenzi nje ya ndoa
  8. Kushiriki katika ujambazi, wizi na ugaidi

KUTUZA

Akidhihirisha ni ukweli au si ukweli atoe hoja zote 

SWALI LA TATU

Ni swali la methali

  • Abainishe maana ya ,ethali kisha atungie kisa kimoja kinachothibitisha methalli hio
  • Maana: Jambo lisilokuhusu linakukera kivipi au kwa njia gani?
  • Ni vyema kutoingilia mambo yasiyotuhusu na yanayoweza kutuleta matatizo. Kwa mfano ugomvi au vita kati ya watu wawili.

KUTUZA.

Methali huwa na pande  mbili. Asipojihusisha na pande zote mbili amejitungia swali lake mwenyewe na kulijibu.

Akitoa kisa kisichooana na methali yenyewe atakuwa amejitungia swali

SWALI LA NNE

Swali la mdokezo

  1. Lazima mtahiniwa amalizie kwa mdokezo huu. Asipofanya hivyo amejitungia swali.
  2. Akipunguza idadi ya maneno katika mdokezo amejitungia swali
  3. Akiongezea maneno matano au zaidi baada ya mdokezo, atakuwa amejitungia swali
    Kisa kilenge kufunza mtu anaweza kuwa amezaliwa katika jamii maskini lakini ajibidishe kimaisha na awe tajiri
    Au
    Mtu asisitikie hali yake ila afanye biddii kuirekebisha

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 End Term 2 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest