Kiswahili Questions and Answers - Form 4 Mid-term Exams Term 1 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

MAAGIZO; JIBU MASWALI YOTE KWA NAFASI ULIZOACHIWA
UFAHAMU (Alama15)

Ithibati ya maendeleo ya kiteknolojia nchini Kenya tayari ipo.
Binafsi, nimeshuhudia teknolojia ya juu katika miundo ya simu na kompyuta,mifumo ya malipo ya kidijitali,mawasiliano na matumizi ya roboti yakizidi kurahisisha kazi katika sekta nyingi humu nchini.
Kila mwana uchumi atakubaliana nami kuwa teknolojia ni nguzo muhimu katika kuongeza kiwango cha uzalishaji.
Lakini mbona uzalishaji umepungua katika miongo michache iliyopita,katika kipindi ambapo teknolojia nyingi zilivumbuliwa? Sababu ni nini?
Nikichunguza data katika mataifa mengi ,hasa ya kiafrika,uzalishaji umepungua tangu mwanzo wa karne ishirini na moja(21). Kumekuwa na sababu nyingi zilizochochea kushuka kwa utengenezaji wa bidhaa viwandani.
Sababu si teknolojia zenyewe bali ukosefu wa kueneza teknolojia hizo kufikia kila mwananchi kwa mfano, programu ya “my dawa” ni nzuri lakini ni wakenya wangapi wana uwezo wa kumiliki simuya kisiasa ili kufaidika na huduma zake?
Ili kila mkenya aweze kumudu bei ya simu ya kisasa,basi uchumi wafaa kuimarika kiasi cha kuwa na hela za ziada za kununua vifaa vya kiteknolojia.
Kila mkenya anatambua kuwa ufisadi umelemaza kila sekta ya uchumi wetu,lakini hiki si kikwazo pekee cha teknolojia kukosa kuwafikia wananchi wa matabaka ya chini.
Hali hii pia inasababisha kampuni saba zilizokuwa zimeorodheshwa katika soko la hisa la Nairobi (NSE) kuondolewa kutokana na mapato ya chini licha ya kutumia teknolojia kuimarisha uzalishaji.
Kudorora kwa uzalishaji kunahusiana moja kwa moja na kupanuka kwa pengo la mapato baina ya matabaka mbalimbali ya kiuchumi. Kwa mfano ,kampuni ya Safaricom inapata faida kubwa zaidi kwa sababu teknolojia yake ya M-pesa imeenea kote,huku kampuni pinzani zikiumia.
Hivyo , serikali kupitia mamlaka ya ushindani yafaa kuondoa vikwazo vinavyozua ushindani,na kuweka kanuni zinazozima ukiritimba.
Tukiachia kampuni chache umiliki wa soko husika, tutakuwa tunazuia kufurahia matunda ya teknolojia, hakuna haja ya wagonjwa kukwama mashinani eti kwa sababu hawana simu za kupata huduma za kiafya kidijitali.
Teknolojia haitakuwa na maana iwapo mamilioni ya wakulima hawana uwezo wamiliki simu yenye apu inayowaunganisha na soko la mazao yao pamoja na kuwaelekeza kwa maduka yenye dawa na mbegu za bei nafuu. Tutazidi kuumia iwapo tutaachia Safaricom idhibiti soko la kutuma hela kidijitali.
Sera kuhusu teknolojia nchini zafaa kuboreshwa ili kuvumisha ubunifu na kueneza hadi mashinani.Kuna raha gani kuwa teknolojia nyingi zisizosaidia kukuwa kwa uchumi wetu? Teknolojia isiyoenea itazidi kulemaza uzalishaji tusipochukua hatua.
Maswali

  1. Yape makala uliyoyasoma anwani mwafaka. (al. 2)
  2. Toa sababu za teknolojia kulemaza uzalishaji wa mali. (al. 5)
  3. Kwa mujibu wa makala haya ni nini umuhimu wa teknolojia. (al. 2)
  4. Ni hatua ipi serikali inastahili kuchukua ili kuzuia ukiritimba (al.2)
  5. Ni nini msimamo wa mwandishi kuhusu teknolojia (al. 2)
  6. Fafanua msamiati huu kimuktadha (al.2)
    Idhibati
    Ukiritimba 

MATUMIZI YA LUGHA(Alama25)

  1. Taja nusu irabu ya midomo. (alama1)
  2. Bainisha kirai husishi
    Paka amepanda juu ya mchungwa. (alama1)
  3. Onyesha shamirisho na chagizo
    Mama amelimiwa shamba lake na mwanawe kwa jembe ipasavyo. (alama4)
  4. Bainisha silabi iwekwayo shadda. (alama1)
    Kiswahili
  5. Eleza maana mbili (alama2)
    Tuliitwa na Juma.
  6. Taja aina za mofimu hizi. (alama2)
    1. Mama
    2. Nywa
  7. Changanua kwa mistari
    Walitununulia mapera jana asubuhi. (alama4)
  8. Tofautisha maana ya sentensi hii . (alama2)
    1. Kazi yote ni muhimu
    2. Kazi yoyote ni muhimu
  9. Tunga sentensi ukitumia ni kama . (alama3)
    1. Kitenzi
    2. kiwakilishi
    3. kielezi
  10.                        
    1. Silabi ni nini? (alama2)
    2. Tenga silabi
      alitukimbilia
  11. Unda sentensi moja yenye sehemu zifuatazo (alama3)
    1. kikanushi cha nafsi ya kwanza umoja
    2. wakati ujao
    3. yambwa tendwa
    4. mzizi
    5. kauli ya kutendesha
    6. kiishio

ISIMU JAMII (ALAMA10)
Samahani mteja wa nambari uliopiga, hapatikani kwa sasa..sorry the mobile subscriber cannot be reached.

  1. Taja sajili hii (alama2)
  2. Eleza sifa zinazohusishwa na sajili hii(alama8)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA KARATA YA PILI

Maswali

  1. Yape makala uliyoyasoma anwani mwafaka. (al.1)
    • Teknolojia
  2. Toa sababu za teknolojia kulemaza uzalishaji wa mali. (al. 4)
    1. Malipo ya kidijitali ni ya juu
    2. Teknolojia kutofikia kila mwananchi malipo ya kidijitali ni ya juu
    3. Kutokuwa na uwezo kumiliki simu ya kisasa yenye apu
    4. Ufisadi
    5. Kampuni kuondolewa kutoka soko la hisa
  3. Kwa mujibu wa makala haya ni nini umuhimu wa teknolojia (al2.)
    • Kulinda matumizi
  4. Ni hatua ipi serikali inastahili kuchukua ili kuzuia ukiritimba (al.2)
    • Vikwazo vikali kupitia kwa mamlaka ya ushindani(CAK)
  5. Ni nini msimamo wa mwandishi kuhusu teknolojia(al.1)
    • Sera zafaa kuboreshwa ili kuvumisha ubunifu na kueneza hadhi mashinani
  6. Fafanua msamiati huu kimuktadha (al.2)
    1. Idhibati
      • Mabadiliko
    2. Ukiritimba
      • Kuwa na uwezo mkuu kwa kampuni moja

MATUMIZI YA LUGHA(Alama25)

  1. Taja nusu irabu ya midomo. (alama1)
    • /w/
  2. Bainisha kirai husishi
    • Paka amepanda juu ya mchungwa. (alama1)
      Juu ya mchungwa
  3. Onyesha shamirisho na chagizo
    Mama amelimiwa shamba lake na mwanawe kwa jembe ipasavyo. (alama4)
    • Shamba (SH.kipozi)
    • Mama(SH.kitondo)
    • Jembe(SH.ala)
    • Ipasavyo(chagizo)
  4. Bainisha silabi iwekwayo shadda. (alama1)
    • Kiswahili
      Kiswahili (Tan.mwanafunzi asitie shadda)
  5. Eleza maana mbili (alama2)
    Tuliitwa na Juma
    1. pamoja na Juma.
    2. wao waliitwa na Juma,Juma hakuitwa
  6. Taja aina za mofimu hizi. (alama2)
    1. Mama—mofimu huru
    2. Nywa—mofimu tegemezi
  7. Changanua kwa mistari
    Walitununulia mapera jana asubuhi. (alama4)
    • S--------KN+KT
    • KN-----O
    • KT------T+N+E
    • T---------walitununulia
    • N--------mapera
    • E---------jana asubuhi
  8. Tofautisha maana ya sentensi hii . (alama2)
    1. Kazi yote ni muhimu-bila kubakisha/ujumla
    2. Kazi yoyote ni muhimu-bila kubagua
  9. Tunga sentensi ukitumia ni kama . (alama3)
    1. Kitenzi
      atumie kitenzi kishirikishi kipungufu
    2. kiwakilishi
      atumie nafsi ya kwanza umoja tegemezi
    3. kielezi
      atumie kielezi cha kiambishi mf.alienda kanisani
  10.                  
    1. Silabi ni nini?
      • Pigo/tamko moja la neno (alama2)
    2. Tenga silabi
      • alitukimbilia
      • a-li-tu-ki-mbi-li-a
  11. Unda sentensi moja yenye sehemu zifuatazo (alama3)
    1. kikanushi cha nafsi ya kwanza umoja
    2. wakati ujao
    3. yambwa tendwa
    4. mzizi
    5. kauli ya kutendesha
    6. kiishio
      sitamchezesha

ISIMU JAMII (ALAMA10)
Samahani mteja wa nambari uliopiga, hapatikani kwa sasa..sorry the mobile subscriber cannot be reached.

  1. Taja sajili hii (alama2)
    • mawasiliano-simu   1x2
  2. Eleza sifa zinazohusishwa na sajili hii(alama8)
    1. kitambulisho mf. nani anaongea
    2. msamiati maalum mf.hallo
    3. lugha dadisi mf. maswali kwa majibu
    4. lugha hutegemea tabaka husika mf. vijana ,wazee nk.
    5. kuchanganya ndimi
    6. kuhamisha msimbo    2x4
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 4 Mid-term Exams Term 1 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest