Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

MAAGIZO:

 • Jibu naswali manne katika karatasi hii
 • Swali la kwanza ni la lazima
 •  Maswali mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu zilizobaki
  NB: Usijibu maswali mawili kutoka kitabu kimoja/ sehemu moja

SEHEMU YA A
USHAIRI

 1. Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali

  Mungu naomba subira, subira nayo imani
  Imani iliyo bora, bora hapa duniani
  Duniani mwa kombora, kombora nayo hiani
  Hiani pamwe ukora wenye kuhini.

  Kuhini kwenye kiburi, kiburi na ufidhulu
  Ufidhuli wa kudhuri, kudhuri wangu muwili
  Muwili hata kiclari, kidari kuwa thakili
  Thakili kisinawiri, kisinawiri misuli.

  Misuli kuwa hafith, hafifu kama muwele
  Muwele wa hitilafu, hitilafi ya nduwele
  Nduwele kutakilifu, kutakilifu milele
  Milele kutoniafu, kutoniafu na vishale.

  Vishale vinitomele, vitomele vikwato
  Vikwato pia maole, maole kufanya mito
  Mito ya matozi tele, tele mithili kitoto
  Kitoto kilo vipele, vipele vyenye fiakuto.

  Fukuto lanipa neno, neno hili kutamka
  Kutamka wazi vino, vino subira kutaka
  Kutaka imani mno, mno n’sipate wahaka
  Wahaka wa matukano, matukano na mashaka.

  Mashaka haya ya leo, leo yawe yamepita
  Yaniepita na vilio, vilia vipishe nyota
  Nyota njema ing’arao, ing’arao kunikita
  Kunikita salamani, salamani nikadata.


  1. Kwa nini nafsi neni anaomba subira na amani. (al.2)
  2. Shairi hili ni la Bahari gani kwa kuzingatia;
   1. Mpangilio wa maneno. (Al. 4)
   2. Mpangilio wa vina.
  3. Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4)
  4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (al.4)
  5. Kwa kutolea mifano, elezea jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (Al.6)

SEHEMU YA B RIWAYA (Jibu swali la 2 au 3)
CHOZI LA HERI (Assumpta k. Matei)

 1. “………Unatumia mantiki gani kusema kuwa sisi si watoto wa miaka hamsini?”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al. 4)
  2. Taja mbinu ya lugha inayojiotokeza katika dondoo hili. (al.1)
  3. Kwa kutumia hoja nane, thibitisha wazungumziwa walikuwa watoto wa miaka Hamsini. (al.8)
  4. Eleza wasifu wa msemaji wa maneno haya. (al.4)
  5. Eleza umuhimu wa msemewa wa maneno haya. (al.3)
 2. Fafanua changamoto zinazoikabili jinsia ya kike katika riwaya ya chozi la heri. (al.20)

SEHEMU YA C: TAMTHILIA
KIGOGO (PAULINE KEA) – Jibu swali la 4 au la 5.

 1. Tamthilia ya kigogo ni taswira kamili ya matatizo yanayokumba mataifa mengi barani Afrika. Fafanua ukirejelea tamthilia nzima . (al.20)
 2. “Ukitaka kuwafurusha ndege, kata mti. Hawa wangekuwa sasa wametuliza nafsi zao.
  1. Eleza muktadha wa kauli hii. (al. 4)
  2. Tambua mbinu mbili za uandishi zilizotumika. (al.4)
  3. Onyesha jinsi wahusika kadhaa walivyofurushwa kama ndege. (al. 12)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI.
TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE – Jibu swali la 6 au la 7

 1. Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi;
  1. Mame Bakari (al.10)
  2. Mapenzi ya kifaurongo (al.10)
 2. Thibitisha ufaafu wa jina ‘mashaka’ katika hadithi ya Ndoto ya mashaka. (al.20)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

 1.          
  1. Taja aina mbili kuu za fasihi. (al.2)
  2. Fafanua tofauti baina ya fasihi ulizotaja hapo juu. (al.4)
  3. Tambua istilahi zifuatazo za fasili. (al.8)
   1. Fanani
   2. Jagina
   3. Maleba
   4. Miviga
  4.     
   1. Eleza maana ya vitanza ndimi. (al.2)
   2. Fafanua sifa za vitanza ndimi. (al.4)

Mwongozo wa Kusahihisha

 1. SHAIRI
  1. Kwa nini nafsi neni inaomba subira na amani. (al.2)
   • Ili asiwe na wasiwasi wa kutukanwa na kuhiniwa
   • Ili aepuke kufanyiawa mabaya (2 x2 =4)
  2. Shairi hili ni la Bahari gani kwa kuzingatia;
   1. Mpangilio wa maneno. (Al. 4)
    • Pindu/mkufu/nyoka
   2. Mpangilio wa vina.
    • Ukaraguni
  3. Kwa kutolea mifano eleza mbinu mbili za lugha zilizotumika katika shairi. (al.4)
   • Tashbihi – hafif kama muwele/ tele mithili kitoto
   • Takriri / uradidi – subira- subura, kiburi – kiburi, neno – neno (2 x2 =4)
  4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (al.4)
   • Misulu kuwa dhaifu sana kama ya mgonjwa, hasa mgonjwa mwenye tatozo la uwele ambalo unasumbua daima na usiosikia dawa/ unaofisha/ usio na tiba
  5. Kwa kutolea mifano, elezea jinsi uhuru wa kishairi ulivyotumiwa kutekeleza arudhi. (Al.6)
   • Lahaja/ lugha kale – pamwe – pamoja na, matozi – machozi
   • Mazda – muwili – mwili
   • Inkisari – kitoto kilo vipele – kitoto kilicho na vipele n’sipate – nisipate
    (3 x 2 = 6)

SEHEMU YA B RIWAYA (Jibu swali la 2 au 3)
CHOZI LA HERI (Assumpta k. Matei)

 1.  “………Unatumia mantiki gani kusema kuwa sisi si watoto wa miaka hamsini?”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al. 4)
   • Ni mawazo yanayompitikia Ridhaa anapokumbuka maneno ya marehemu mwanawe Annatila (Tila)
   • Mjadala wenye unahusu mafarikio baada ya uhuru
   • Ridhaa yumo nyumbani kwake akitazama masozo ya aila yake, ambayo ni majivu
   • Hii ni baada ya kuawa kwa familia yake kinyama na mzee kedi alipoliteketeza jumba lake la kifahari.

  2. Taja mbinu ya lugha inayojiotokeza katika dondoo hili. (al.1)
   • Balagha – pana matumizi ya swali lisilohitaji jibu.
   • Jazanda – watoto wa miaka hamsini kumaainisha kuwa bado waafuka wangali wanatawalimu na wakoloni kwa njia isiyo ya moja kwa moja; sifa za ukoloni zingali barani afrika.
   • Kinanya – waafrika wanaendelea kuwategemea wakoloni hata baada ya kupata uhuru.

  3. Kwa kutumia hoja nane, thibitisha wazungumziwa walikuwa watoto wa miaka Hamsini. (al.8)
   • Baada ya miaka hassini ya uhuru, tumebaki kuwa watengemezi wa wakoloni wao hao waliotupa uhuru.
   • Baada ya miaka hamsini ys uhuru, mataifa mengi ya kiafuka hayajakuwa kiuchumi lakini yamebaki kuwa wategemezi wa wakoloni waliowapa uhuru.
   • Wakoloni walioondika Afuka, walowezi (settlers) na waafrika wenye uwezo walimiliki mashamba yaliyokuwa ya wakoloni na kufanya waafrika kuwa maskuota katika vituo usuli wao.
   • Waliokuwa wakoloni ndio wanaoamua waafrika watakuza nini katika ardhi yao
   • Waafrika wanaendelea kuwategemea wakoloni kwa lishe na ajira ambayo ni ya kijungu jiko.
   • Waafrika wanakuza mazao madogo ambayo huenda kumfaidi huyo mkoloni aliyetupa uhuru
   • Hatujaweza kujisagia kahawa yetu ingawa mbegu ni zetu, tunachoka kulikuza lao lenyewe kisha tunawapelekea waliokuwa wakoloni walisage na kutuuzia kwa bei ya juu.
   • Mwafrika aliridhi umilikaji wa ardhi kwa kutumia hatimiliki kutoka kwa mzungu hali ambayo iliwafanya wengi ambao hawakuwa na uwezo wa kununua mashamba kuwategemea wenye uwezo
   • Ubinafsi wa mkoloni ulirithiwa na Mwafrika. Watoto waliosoma na ridhaa walimwita mfuata mvua na kukataa kucheza naye kwa madai aliwashinda mitihani.
   • Kupitia kwa maneno ya Tila kwa babake, tunaelezwa kuwa machumbo ya mawe na hazina za mafuta zimepewa kampuni za ubinafsi ambazo ni za kigeni.
   • Huku nchini uchumbaji, madini unafadhilishwa na wageni ambapo fedha zinazotokana na rasilimali hii huishia kwenye mifuko ya wageni kufaidi nchi zao.
   • Kampuni za kigeni zimewapa wenyeji(Waafrika) ajira ambayo mshahara wake ni mdogo sana (mkia wa mbuzi)
   • Uongozi wa kukatili unaendelezwa, vijana wanauawa kwa mitatu ya bunduki wanapojaribu kujikomboa kutokana na ukoloni.
   • Waafrika wanategemea mahindi yaliyotolewa ili kuwapunguzia makali ya kutotosheleza chakula ambako kunaingata nchi (zozote 8 x 1= 8)

  4.   Wasifu wa msemaji(Tila)
   • Ni mkakamavu - anazungumzia maswala ya sheria na siasa kwa ukakamavu
   • Mwenye busara - Alifahamu kuwa hakuna maendeleo ambayo walikuwa wamepata licha ya kuwa na miaka hamsini ya uhuru/ hakuna aliyempiku kwa maswali ya siasa.(2x2=4)

  5. Umuhimu wa msemewa maneno
   • Anayetumiwa kuonyesha athari za ukabila- mali yake yote inateketezwa kwa ajili ya ukabila
   • Anaendeleza maudhui ya utu -anayoshamini masomo ya wapwa wa mzee kedi.
   • Ni kielezo cha watu wenye bidii- anasoma hadi kuwa daktari, anaanzisha hospitali.
    (zozote 3 x 1=3)
    (mwalimu ahakikishe majibu sahihi)

 2. Changamoto za jinsia ya kike katika Chozi la Heri            
  •  Matusi na vitisho - Bwana Maya alipoulizwa maswali na mkewe alimpiga makonde, kumtisha na matusi.
  • Kubakwa- Sanna anabakwa na babake wa kambo, Bwana Maya. Mamake naya anamsaidia kuavya mimba hiyo
  • Ndoa za mapema. Pete baada ya kupashwa tohara anaozwa kwa mzee Fungo kwa lazima. Nyanyake anajaribu kumtetea lakini hakufaulu.
  • Kukatizwa elimu- Kiu cha Pete cha kuendelea kusoma hukatizwa baada ya ndoa ya lazima kwa Bw Fungo.
  • Waume zao kukosa uaminifu katika ndoa mf Bwana Tenge anashiriki ngono na wanawake wengi wakati Bi Kimai yuko kijijini.
  • Kunyimwa nafasi ya kuongoza- mWekevu anadhalilishwa na mpinzani wake kwa kuandaa maandamano ya kupinga kuchaguliwa kwake.
  • Kutelekezwa - Chandachema anaondoka kwa JIrani yake baada ya kulalamika vitu vidogo vidogo kuonyesha kutoridhika. Pia Zohali anatelekezwa na wazazi wake na kuishia kuwa ombaomba mjini.
  • Kufukuzwa shuleni- Zohah anafukuzwa shuleni baada ya kupata mimba.
  • Utasa- Neema mkewe Mwangemi anakosa mtoto hivyo analazimika kumpanga mtoto(Mwaliko)
  • Ujane- Rachael Apondi ni mjane, lakini anaolewa na Mwongeka baadaye.
  • Umaskini- Umaskini unamfanya Chandachema kufanya kazi duni, Sauna anashiriki biashara ya kulangua watoto.
  • Mabinti kupelekwa madnguroni- Bi Kangara na mumewe waliwaiba watoto wa kike na kuwapeleka madanguroni.
   (zozote 10 x 2=20)
   (mwalimu ahakikishe majibu yoyote mwafaka)

   KIGOGO
 3. Matatizo ya mataifa mengi barani Afrika
  • Mauaji ya kiholela- Jabali, vijana watano
  • Vitisho kwa wananchi- Chopi, Kingi, Tunu
  • Unyanyasaji wa wananchi- kutozwa kodi ya juu sana
  • Unyakuzi wa ardhi ya umma - soko la Chapakazi.
  • Kutiwa Jela bila sababu- Ashua
  • Kugawanya watu kwa matabaka - Matajiri na maskini
  • Kukatiza juhudi za ukombozi- mauaji ya Jabali, shambulizi la Tunu
  • Viongozo wanaendeleza ufisadi
  • Viongozi kutumia propaganda
  • Matumizi ya vyombo vya dola kukandamiza wananchi.
  • Kuendeleza biashara haramu- mamapima kuruhusiwa kuuza pombe.
  • Uongozi wa kiimla
  • Viongozi hawataki kutoka uongozini
  • Kukosa ajira- Ashua amesomea ualimu
  • Viongozi kutumia vyeo vyao kuiendeleza biashara haramu mf dawa za kulevya-Majoka
  • Viongozi kuomba ufadhili kutoka nchi za magharibi kufadhili miradi isiyofaa- uchongaji wa vinyago
  • Uchafuzi wa mazingira - ukataji miti.
  • Viongozi kutumia mamlaka yao kuharibu ndoa za watu mf ndoa ya Sudi na Ashua.
  • Viongozi kuzawadi vikaragosi wanaounga mkono uongozi wao mbaya
  • Viongozi hawachukui hatua kwa wanaoleta vurugu 
  • Viongozi kuwa wabadhirifu.
   ( zozote 20 x 1=20)

 4. Dondoo
  1.          
   • Haya ni maneno ya Kenga
   • Alikuwa anamwambia Majoka
   • Wako ofisini mwa Majoka
   • Ni baada ya Majoka kusoma habari gazetini zinzoonyesha umaarufu wa Tunu wa kupigiwa kura
  2.           
   • Jazanda - ndege -  Wapinzani wa Majoka; kata mti kuwaua
   • Taswira - picha ya mawazoni
  3.            
   • Majoka kumpangia Jabali kifo kwa kupinga utawala wake
   • Wanafunzi kuuziwa sumu ya nyoka (dawa za kulevya) na kubadilishwa kuwa makabeji
   • Vijana wanapofushwa na wengine kufa kwa kunywa pombe haramu kwa Asiya
   • Sudi analazimisha kuchonga kinyago kwa Ashua kufungiwa kwenye Seli na Majoka
   • Ngao Junior anafurushwa kwa matumizi ya sumu ya nyoka- anazirai na kukata roho katika riwaya wa ndege
   • Majoka anafanya familia yake Tunu kuwa na wakati mgumu wa kupata bima ya kifo cha babake kilichotokea kwenye kampuni yake Majoka 'Majoka and Majoka Company.'
   • Ngurumo anafurushwa pale anaponyongwa na chatu akitoka ulevini
   • Baadhi ya waandamanaji wanauawa na wengine kujeruhiwa wanapotetea haki zao.
   • Familia ya Heshima inarushwa karatasi za kuwaamrisha wahame Sagamoyo, eti Sagamoyo si kwao.
   • Majoka anafurushwa pale watetezi wa haki wanapindua uongozi wake.
   • Vijana wanafurushwa pale wanapoteta haki zao kiwandani na kuawa
    (12 x 1= 12)

 5. Maudhui
  1. Mamake Bakari
   • Janadume linamsaliti Sara kwa kumbaka akitoka masomoni 
   • Beluwa anamsaliti Sara kwa kuwafichulia wazazi siri ya mimba yake(Sara)
   • Jamii inasaliti mwanamke kwa kumwona mkosaji tukio la ubakaji linapotokea
   • Babake Sara anamsaliti mkewe kwa kutompa nafasi ya kujitetea
   • Wazazi wa kiume wanawasaliti mabinti zao wanapokuwa wajawazito kwa kuwafukuza kutoka nyumbani.
   • Kupitia kwa mawazo ya Sara wanajamii ni wasaliti kwani wangemtenga iwapo wangejua ujauzito wake.
   • Kupitia kwa mawazo ya Sara mwalimu angemsaliti kwa kumfukuza shuleni na kumwambia kwa hiyo sio shule ya wazazi bali ni ya wanafynzi.
    (zozote 5 x 2 = 10)

  2. Mapenzi ya kifaurongo     
   • Daktari Mabonga anawasaliti wanafunzi kwa kukosa kujibu maswali yao.
   • Penina anamsaliti Dennis anapomfukuza kutoka chumba chake ilhali alikuwa amemwahidi kumpenda bila masharti.
   • Mpenzi awa awali wa Penina anamsaliti kwa kukosa kuaminika katika uhusiano wao.
   • Dennis anaisaliti nafsi yake kwa kushindwa kujibu swali kwenye mahojiano.
   • Wanajamii wanasaliti familia ya kina Dennis kwa kuwakejeli sababu ya umaskini.
   • Mama Shakila anamsaliti Dennis kwa kutompa nafasi ya kujibu swali lingine- alimuuiza swali moja tu (Mwalimu ahakiki majibu mwafaka)
    (zozote 5 x 2=10)

 6. Ufaafu wa jina Mashaka(Ndoo ya Mashaka)
  • Mashaka ni mambo magumu yanayompata mtu, pia ni dhiki, taabu , masaibu etc.
  • Mashaka alikumbwa na matatizo/ dhiki nyingi maishani kv.
   1.  Mamake mzazi anakufa anapomkopoa
   2. Babake anakufa na kufuata mamake kwa kushindwa kustahimili upweke.
   3. Mashaka analelewa na Biti Kidebe mama wa makamo- hivyo anakosa mapenzi ya mama mzazi.
   4. Mama Mlezi (Biti Kidebe) alikuwa na shida ya mguu- hadi kumfanya Mashaka kumlea
   5. Mashaka analazimika kufanya vibarua ili kujikimu kv kukna nazi, kufyeka, ijapokuwa ni mdogo
   6. Mashaka anafiwa na mama mlezi Biti Kidebe baada ya kukamilisha chumba cha nane
   7. Mashaka kuozwa waridi bila mpango
   8. Mashaka kufanya kazi ya sulubu
   9. Mashaka kuishi katika mazingira duni.
   10. Chumba alichoishi kulikuwa kidogo hawakutoshea; wasichana walilala wakibanana na mama yao kwenye chumba, wavulana walilala jikoni mwa jirani alikowaombea baba yao.
   11. Chumbani kulikuwa na vitu vichache, hakukuwa na kitanda , meza.
   12. Paa la nyumba lilivuja kila kuliponyesha 
   13. Mvua iliponyesha ilitapisha vyoo
   14. Chumba cha Mashaka kilikumbatiana na choo cha jirani kusababisha uvundo.
   15. Mfereji wa China kupitisha maji chafu.
   16. Mvua kusababisha mafuriko katika mtaa wa akina mashaka na viongozi kuwaagiza wahamie wasikokujua.
   17. Waridi na Mashaka wanapooana wazazxi wa Waridi wanahamia Yemen, eti kuepuka aibu ya Waridi kuolwa na maskini
   18. Mashaka anatorokwa na mkewe na watoto na kuachwa mpweke
    (zozote 10 x 2- 20) 

 7. Fasihi Simulizi
  1. aina kuu za fasihi
   • Fasihi simulizi
   • Fasihi andishi

  2.  Fafanua tofauti 
   • Fasihi simulizi huwasilishwa kwa mdomo mbele ya hadhira
   • Fasihi andishi huwasilishwa kwa maandishi kv kwenye vitabu na jazanda

  3. Tambua istilahi zifuatazo
   • Fanani - Huyu ni msimulizi wa fasihi simulizi
   • Jagina- Shujaa katika mighani
   • Maleba - Mavazi au vifaa vinavyovaliwa na wasanii
   • Miviga - sherehe za kutamaduni ambazo hufungwa na jamii katika kipindi fulani maalum.
  4.              
   1. Vitanza ndimi
   2. Sifa:
    • Sauti hukaribiana kimatamshi
    • Kuna uradidi/ takriri ya maneno au sauti fulani.  

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Form 4 End Term 1 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest