Utangulizi - Kiswahili Fasihi Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

 • Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe unaomhusu binadamu.
 • Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha fikra na hisia za binadamu kama vile maneno, maandishi, uchoraji, uchongaji, ufinyanzi n.k.

Fasihi simulizi ni sanaa kwa vile:

 1. Huwasilisha ujumbe kuhusu binadamu kuhusu utamaduni na uchumi.
 2. Huwa na umbo mahsusi k.m. hadithi huwa na mwanzo, kati na mwisho na mashairi huwa na beti, mishororo, n.k.
 3. Hutumia lugha kwa ufundi k.v. ya kitamathali.
 4. Husawiri mandhari/mazingira mahsusi kwa ufundi mkubwa.
 5. Hujenga wahusika kwa ustadi mkuu ili kusawiri tabia za watu katika jamii.


Tanzu za Fasihi

 • Kuna tanzu mbili kuu za fasihi, na kila utanzu una vipera vyake:
  • Fasihi Simulizi na
  • Fasihi Andishi:

Fasihi Simulizi

 1. Hadithi (Ngano) - hekaya, mighani, visasili n.k
 2. Ushairi Simulizi - ngonjera, nyimbo, maghani
 3. Maigizo - michezo ya kuigiza, ngomezi n.k
 4. Semi- methali, vitendawili n.k
 5. mazungumzo

Fasihi Andishi

 1. Hadithi Fupi - hadithi isiyokuwa ndefu iliyochapishwa katika mkusanyiko wa hadithi nyingine
 2. Riwaya - hadithi ndefu iliyochapishwa katika kitabu chake pekee
 3. Tamthilia - mchezo wa kuigiza uliowekwa kwa maandishi
 4. Ushairi* - mashairi yaliyoandikwa

- Tofauti kuu kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi ni kwamba Fasihi Simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo au matendo ilhali Fasihi Andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.

Tofauti Kati ya Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi

FASIHI SIMULIZI FASIHI ANDISHI
Huwasilishwa kwa njia ya mdomo na/au matendo Huwasilishwa kwa njia ya maandishi
Ni mali ya jamii Kazi andishi ni mali ya mwandishi (na mchapishaji)
Msimulizi anaweza badilisha sehemu fulani Kitabu kilichoandikwa hakiwezi badilishwa
Huhifadhiwa akilini Huhifahiwa vitabuni
Kazi simulizi hubadilika na wakati Kazi andishi haibadiliki na wakati
Huhitaji msimulizi na hadhiwa yake wawe mahali pamoja wakati wa masimulizi Msomaji anaweza kusoma kitabu cha hadithi peke yake, mahali popote, wakati wowote
Mtu yeyote anaweza kutunga na kusimulia Ni lazima mwandishi na msomaji wawe na uwezo wa kusoma
Hutumia wahusika changamano (wanyama, watu, mazimwi n.k) Hutumia wahusika wanadamu 

Jinsi Fasihi Simulizi na Andishi Zinavyofanana

 • Zote mbili hushughulikia masuala yanayohusu maisha maisha ya binadamu.
 • Zote mbili Huhumia lugha kwa ubunifu kuwasilisha maudhui.
 • Zote mbili huwa na vipengele viwili vikuu, maudhui na fani (jumla ya mbinu msanii alizotumia kuwasilisha maudhui).
 • Zote mbili majukumu sawa k.v. kuburudisha, kuadilisha, kuhifadhi na kuendeleza utamaduni, n.k.
 • Zote mbili zina utendaji-pale tamthilia na riwaya zinapoigizwa.
 • Zote mbili huzaliwa, hukua na hufa kutegemea mabadiliko ya wakati.
 • Zote mbili huwa na wawasilishaji-fanani k.m. mtambaji/mganaji au manju/yeli katika fasihi simulizi na mwandishi upande wa fasihi andishi
 • Fasihi simulizi imekopa tanzu za fasihi simulizi k.v. methali, mashairi, n.k.


Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii

 • Kuburudisha jamii. Takribani vipera vyote vya fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira.
 • Kuelimisha. Fasihi hukusudia kuelimisha hadhira kuhusu jamii, mazingira n.k
 • Kudumisha maadili katika jamii kwa kuelekeza, kuonya na kunasihi hadhira jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii.
 • Kuunganisha jamii. Fasihi huleta pamoja watu katika jamii. Kwa mfano, katika nyimbo, miviga, vichekesho.
 • Kukuza lugha. Aghalabu tungo zote za fasihi hutumia lugha. Isitoshe, fasihi hutumia mbinu nyingi za lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na ukwasi wa lugha.
 • Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Aghalabu kazi za fasihi (hasahasa Fasihi Simulizi) huambatanishwa na desturi mbalimbali za jamii husika.
 • Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. k.m vitendawili, ngano za mtanziko n.k


Sababu za Ufaraguzi/Kubadilika kwa Fasihi Simulizi

 • Kuwasilishwa vibaya.
 • Fanani kusahau na kubadilisha yaliyomo na mtiririko.
 • Kubadilisha ili kukidhi mahitaji ya hadhira k.m. umri na uelewa wao- kutumia lugha nyepesi kwa watoto na pevu kwa watu wazima.
 • Mabadiliko ya mandhari/mazingira-vitu vilivyo katika mazingira halisi kukosekana katika mazingira ya usimulizi na msimulizi kutumia vitu katika mazingira yake vinavyokaribiana navyo.
 • Kutoeleweka na hivyo kuhifadhiwa vibaya.
 • Mabadiliko ya wakati k.m kitendawili cha wakati wa mkoloni kutumia mzungu na cha wakati wa mwarabu kutumia mwarabu na maana ni ile ileMzungu/mwarabu amesimama kwa mguu mmoja-mwavuli.
 • Mabadiliko ya falsafa ya vizazi na maingiliano katika jamii kusababisha kurithisha tu yale ambayo ni muhimu na kuacha mengine.
 • Kila fanani huwa na mtindo wake wa kuwasilisha/kisanii.
 • Ubunifu wa fanani ili uwasilishaji uweze kuvutia saidi na uwezo wake wa lugha.
 • Teknolojia kusababisha kuhifadhiwa na hivyo kuiua.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Utangulizi - Kiswahili Fasihi Notes.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Read 4268 times Last modified on Friday, 13 November 2020 12:15
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest