KISWAHILI KARATASI YA 2 - 2017 MURANG'A MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp
 1. UFAHAMU (ALAMA 15)

  MAJILIO ya wakoloni barani Afrika ambao walidumisha utawala wao katika’bara jeusi’ kwa takriban kipindi cha miaka sabini kulisababisha mivutano ya kiisimu mpaka leo (Ngugi,1993,uk 42)
  Wakoloni walizipa kipaimbele lugha za kigeni na kuzikandamiza zile za kiasili zisiweze kuelezea uhalisi wa maisha katika viwango vya teknolojia. Kwa hakika, itazichukua lugha hizi muda mrefu kwenda sambamba na maendeleo ya fikra na teknolojia kwa kutoandaliwa vyema kutekeleza wajibu huu.
  Lugha ni kipengele muhimu sana cha utamaduni. Hivyo basi serikali zinawajibika kuzilinda, sio tu kwa sababu lugha zimejaa maarifa mengi ya tangu  jadi, bali pia kwa sababu lugha ni chombo cha maendeleo ya binadamu.
  Maarifa yote na ufanisi wa binadamuu huelezwa kupitia kwa lugha. Mwelekeo ulioonekana kishika sana katika mataifa megi barani afrika, ikiwemo Kenya, ni kuhusudu lugha na tamanduni za kigeni. Lugha za kigeni zimehusishwa na maendeleo na ustaarabu.
  Hatua iliyochukuliwa na serikali ya Tanzania ya kufunza masomo yote kwa lugha ya Kiswahili kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu ilizua kejeli na kicheko kwa baadhi wa wakenya; hususan katika stesheni za fm. Kisa na maana: jambo hili haliwezekani!
  Je, ni lazima tutegemee lugha za kigeni kupiga hatua kimaendeleo? La hasha! Kuna ushahidi wa mataifa kama vile Uchina, Ufini,Sweden, Indonesia,Japan,Malaysia, India,Uyahudi n.k. yalioendeleza  lugha zao kimakusudi ili ziweze kukidhi haja kufundishia masomo yote hadi viwango vya juu sana vya elimu.
  Katika sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa ya ‘lugha mama’ miongoni mwa mataifa wanachama wa umoja wa mataifa (united Nations International Mother Language Day) mnamo februari, 2000, mkurugenzi wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu Elimu,sayansi na utamanduni(UNESCO), jenerali koichiro Matsuura alisema: ‘mojawapo ya vigezo vitumiwayo na wataalmu kukadiria iwapo lugha Fulani inatishiwa kuangamia au kufa ni iwapo watoto wanajifunza lugha hiyo…
  Iwapo takribani asilimia 30 ya watoto, hawajifunzi lugha yao’ya mama’, basi lugha hiyo inatishiwa kuangamia… lugha hiyo bila shaka huenda ikafa pamoja na kizazi kinachoizungumza.’
  Kwa mujibu wa UNESCO, lugha nyingi ambazo zimetishiwa kufa au kutoweka zinapatikana katika mabara ya merakani na Australia. Shirika hililinaongeza  kuwa, nchini Kenya, lugha kama vile suba,El Molo, Lorkoti, Yaaku sogoo,kore,Segeju,Omotik, na KInare’ zimekufa’ au kutoweka huku Bong’om na Terik/Tiriki zimo kwenye hatari ya kutoweka.
  Lugha pia huangamia wakati ambapo lugha hizo zinashindwa kuzihudumia jamii zao ipasavyo kama chombo mahsusi cha mtagusano wa kijamii. Baadhi ya lugha huku na kusambaa huku zingine zikididimia na hatimaye’kumezwa’ na lugha zilizoshaimiri au hata kutoweka kabisa. Kwa mfano, jamii ya Seng’wer ‘imemezwa’ na makabila kama vile Wapokot, Wamarakwet, Wakeiyo, Watugen, Wanandi na Waluhya, ilhali Wakipsigis,Watugen na Wamaasai’wammeza’jamii ya Ogiek.
  Hata hivyo,mkaoni nyanza ya kusini nchini Kenya, wakakti wa uchaguzi mdogo wa useneta katika gatuzi ya Homabay, tulisikia kupitia kwa profesa….(aliyewania kiti), kwamba jamii ya Abasuba ipo-wala’haijamezwa’ na jamii ya waluo.
  Msimamo wa wizara ya elimu nchini Kenya kuhusu ufundishaji wa ‘lugha ya mama’ unaonekana kuyumba. Mara tunaambiwa lugha ya mama itafundishwa katika madarasa ya chini katika shule za mashambani; mara tunaambiwa itafundishwa katika madarsa ya chini katika maeneo Fulani; ilimradi wizara haijitokeza  waziwazi na sera wala mwongozo mwafaka.
  Njogu (2003) anahoji;’mkondo uliopo nchini Kenya hivi sasa ni ule wa jamii nyingi kuwahimiza watoto wao kuzungumza lugha za kigeni kama vile kiingeraza, kifaransa, na hata kijerumani na kupuuza lugha ya kwanza. Hii inatokanan na imani kuwa lugha za kigeni ndizo zitakazofungua njia za kigeni ndizo zitakazofungua njia za maendeleo hapo baadaye.
  Mkondo huu usipozuiliwa, huenda ukasababisha vifo vya lugha za kiasili’ Njogu anaendelea: ‘uwezo wa kuongea lugha nyingine pamoja na yenye asili ya kikoloni huweza kujenga jisia za kujiamini miongoni mwa watu wasiokuwa na uwezo mwingi wa kiuchumi-nako kujiamini ni hatua ya awali ya kuleta maendeleo ya jamii’MAKIWA! Familia, jamaa na marafiki wa Grace Ogot aliyeandika baadhi ya kazi zake kwa lugha ya mama.

  Maswali
  1. Ni nini kisababishi cha mivutano ya kiisimu katika bara la afrika (al. 2)
  2. Serikali zinafaa kuwajibika katika kuzilinda lugha . eleza (al. 2)
  3. Ni hatua gani ambayo ilichukuliwa nan chi ya Tanzania ambayo ilizua kejeli na kicheko kwa baadhi ya wakenya (al. 1)
  4. Lugha ya mama inasemekana kuwa katika tishio la kuangamia kwa kutumia vigezo gani? (al. 2)
  5. Kwa nini jamii nyingi huwahimiza watoto wao kuzungumza lugha za kigeni kigeni (al. 2)
  6. Kuna mabara ambayo yametajwa kuwa na lugha nyingi ambazo zinatishiwa na kufa au kutoweka. Yataje mabara hayo. (al. 2)
  7. “Msimamo wa wizara ya elimu kuhusu ufundishaji wa lugha ya mama unaonekana kuyumba “ Eleza (al. 2)
  8. Eleza maana ya msamiati ufuatayo kwa mujibu wa taarifa au ufahamu
   1. Takriban
   2. Mtagusano
 2. UFUPISHO (alama 15)

  TUMEKWISHA kueleza katika makala ya hapo awli kuwa lugha ni maalum kwa binadamu tu na kwamba hakuna kiumbe yeyote ambaye si mwanadamu mwenye uwezo wa kujua, kujifunza na kutumia lugha zaidi ya binadamu.
  Bila shaka, mawasiliano ya binadamu yanaweza kujumuishwa kama mawasiliano ya wanyama yaliyoendelezwa. Utafiti wa mawasiliano ya wanyama, uitwao’zuosemiotiki’(zoosemiotics) tofauti na ‘athroposemiotiki’( utafiti wa mawasiliano ya binadamu), umechangia pakubwa katika ukuzaji wa uwezo wa mnyama wa kutambua. Jambo hili ni dhahiri kwani binadamu wanaweza kuwasiliana na wanyama kwa kutumia njia za kipekee lakini si’lugha’.
  Makala haya yanalenga kuthmini na kuzamia sifa au tabia za lugha ya mwanadamu. Kimsingi sifa ai Tania hizi ndizo zinazoitofautisha lugha ya mwanadamu na aina nyinginezo za mawasiliano zitumiwazo na ndege au wanyama.
  Unasibu wa lugha ya binadamu unaangaliwa katika ukweli kwamba binadamu hazaliwi na lugha, anakutana nayo kwa unasibu tu. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja au wa aili kati ya kitajwa(kitu au umbo linalomaanishwa au maana).
  Uhusiano wake ni wa unasibu na unatokana na makubaliano ya watu wajua – lugha yao. Hata makubaliano haya ya kwamba kitu kiitwe au dhana Fulani iitwe na kuelezwa kwa namna Fulani ni ya kinasibu tu. Hapa tunamaanisha kwamba mkutano au kikao ambaco binadamu amewahi kukaa akasema mathalani neno “chuki” limaanishe hali ya kutompenda mtu au neno “upendo”  limaanishe hali ya kuonesha huba kwa mtu. Kila jamuiya-lugha ina namna yake ya kuufasili na kuelekezea ulimwengu kwa lugha yake ambayo inatofautiana na jamuiya-lugha nyingine.
  Lugha ya mwanandamu inao uwezo wa kuambukiza utamanduni kutoka katika kizazi kimoja kwenda kizazi kingine au kutoka katika jamuiya-lugha moja kwenda katika nyingine. Leleweke kuwa, uwezo huu wa kuambukiza maarifa ya lugha hufanyika kwa njia ya kusoma au kujifunza na si kurithi. Kwa mfano, mtu anaweza kurithi. Kwa mfano, mtu anaweza kurithi maumbile kutoka kwa wazazi wake, mathaalan aina ya nywele, macho, pua, kucha au masikio lakini mtu hawezi kurithi lugha.
  Lugha inamfikia kwa kuambukiza katika jamuiya-lugha anayokulia na kulelewa. Yatupasa tukumbuke kuwa, ingawa mwanadamu anazaliwa na ule uwezo(kitengo cha lugha) wa kujifunza lugha”language Acquisition Device”kama anavyoeleza mwanaisimu Naom Chomsky, lakini hazaliwi na lugha. Hii ndiyo sababu mwanandamu anaweza kujifunza lugha yeyeote ile na kwa wakati wowote maadamu yupo katika mazingira na hali ya kawaida na saidizi.
  Lugha ya mwanandamu imepangwa katika viwango viwili ambavyo vinashirikiana na kukamilishana. Kiwango cha kwanza I kile kiwango cha utamkaji wa sauti au utoaji wa sauti kwa kutumia ala mbalimbali za matamshi. Sauti hizi zikisimama peke yake hazina maana yoyote, ni kama milio tu kama kupiga chafya, au kelele zinazotokana na kubururwa kwa meza kwenye sakafu au kelele za injini ya pikipiki.
  Sauti hizi zinapounganishwa (kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za lugha husika) tunapata kiwango kingine cha pili cha maana. Sifa ya uwili inadhihirisha sifa ya uwekevu katika lugha ya mwanadamu kwani kwa kutumia sauti hizi chache mzungumza lugha anaweza kutunga na kutamka sentensi nyingi au tungo nyingi na zenye maana tofauti tofauti bila kikomo
  Suala jingine la msingi ni kwamba, tunaposema kuwa lugha imegawika katika viwango viwili, kiwango cha sauti na kiwango cha maana haimaanishi kwamba binadamu anatumia viwango hivi kuipekepeke. Hata siku moja mwanadamu hasemi kwamba sasa naanza kutamka sauti za neno Fulani, halafu ndiyo niweke maana yake. La hasha!
  Binadamu hutamka kwa mara moja sauti pamoja na maana zikiwa zimebebana ndani kwa ndani(hutamka sauti pamwe na maana). Yaani, wakati anatamka sauti na kuziunganisha ndiyo wakati anaambatanisha na maana ndani yake. Hii ndiyo sifa au uwili katika lugha ya mwanadamu.
  Uzalikaji katika lugha ya binadamu unajidhihirisha katika uwezo wa mwanandamu kubuni na kuunganisha maneno na miundo mbalimbali ya tungo bila kikomo. Mjuzi wa lugha anastahili  kutunga na kuzielewa tungo mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile ambazo hajawahi kuzisikia wala kuzitunga yeye mwenyewe.
  Aidha, anapaswa kuelewa tungo zilizotungwa na watu wengine na kufahamu maana ya kisemantiki na ile kipragmatiki zinazodhihirika kadri anaposimbua jumbe zilizomo. Anapaswa kuzielewa tungo sahihi na zile zisizo sahihi. Hivyo uwezo huu unatofautiana na aina nyingine ya mawasiliano inayotumiwa nan a wanyama wengine, kwa mfano,”nyenje ni mnyama mwenye milio au ishara nne za kuchagua ili awasiliane, tumbili ana miito sita tu. Hivyo wanyama wote hawa wana idadi isiyobadilika ya milio na sauti au ishara na hawana uwezo wa kubuni namna nyingine ya kuwasiliana au kubuni milio mingine ya kuwezesha na  kudumisha mawasiliano yao.

  Maswali
  1. kwa maneno kati ya 50- 60 fupisha aya tau za kuanza (al. 8. 1 mtiririko)

   matayarisho

   Jibu
  2. kwa kutumia maneno 60-70 bainisha ujumbe ambao mwandishi anaibua katika ya tatu za mwisho (al. 7, 1 mtirirko)

   matayarisho

   Jibu
 3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Bainisha sifa za sauti ifuatayo /o/ (al. 2)
  2. Kambishi ni nini? (al. 1)
  3. Onyesha matumizi ya kiambishi “ku” katika sentensi ifuatayo
   Nitakupa fedha za mchango ili uende ukaniwakilishe (al. 2)
  4. Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizowekwa katika mabano
   1. pa(kutendeka)
   2. ha(kutendewa) (al. 2)
  5. Tunga sentensi moja katika wakati ujao hali timilifu (al. 1)
  6. Onyesha aina za virai katika sentensi ifuatayo.
   Mteja wangu atawasili kesho saa tatu (al. 2)
  7. Tumia kivumishi kionyeshi kisisitizi cha mbali kidogo pamoja na nomino katika ngeli ya li-ya kutunga sentensi (al. 2)
  8. Tunga sentensi moja yenye kishazi huru na kishazi tegemezi ukitumia’o’ rejeshi tamati (al. 2)
  9. Changanua sente4nsi ifuatayo kwa jedwali/visanduku
   Mkulima alilima kwa bidii lakini hakupata mazao mengi (al. 4)
  10. Onyesha aina za shamirisho katika sentensi uliyopewa
   Babu alisomewa barua na mjukumu wake
  11. Tunga sentensi mbili ili kuonyesha matumizi ya kiambishi ‘po’ cha
   1. Wakati
   2. Mahali
  12. Changanua kitenzi kufuatacho (al. 4)
   Alimlisha.
  13. Kwa kutunga sentensi eleza matumiz mawili tofauti ya kiakifishi (al. 2)
   Parandesi
  14. Eleza maana ya sentensi ya masharti (al. 1)
   Tunga sentensi ya masharti (al. 2)
  15. Andika visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari
   Daktari alipokuwa akimtibu alishikwa na kisulisuli (al. 2)
  16. Bainisha kihisishi na kihusishi katika sentensi
   Naam! Ameingia kabla ya mwalimu kufika (al. 2)
  17. Andika sentensi ifuatayo kwa msemo wa taarifa
   “nitaweza kuondoka kwangu kesho asubuhi.”mwalimu akasema (al. 3)
  18. Bainisha kiima na chagizo katika sentensi
   Mwenyewe alimpenda kwa dhati (al. 2)
 4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
  1. Taja dhana au nadharia zinazohusiana na chimbuko la lugha ya Kiswahili (al. 3)
  2. Eleza maana ya istalahi zifutatazo kama zinavyotumika katika isimujamii
   1. misimu
   2. lafudhi
   3. pijini  (al. 3)
  3. Taja sifa nne za sajili ya maabadini (al. 4)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 2 - 2017 MURANG'A MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest