MAAGIZO
- Andika insha mbili.Insha ya kwanza ni ya lazima.
- Chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia
- Kila insha isipungue maneno 400
- Kila insha ina alama 20

MASWALI
- Wewe ni katibu wa kamati iliyoteuliwa na rais kuchunguza madhara ya pombe haramu na mbinu za kuangamiza pombe hiyo. Andika ripoti rasmi.
- Vijana wanakumbwa na changamoto si haba.
Thibitisha - Andika insha itakayothibitisha ukweli wa methali
‘’Mwiba wa kujichoma hauambiwi pole. - Andika kisa kitakachokamilika kwa maneno yafuatayo…………… waliwasili saa tatu baadaye.Uharibifu wa mali na maisha ulikuwa umeshatendeka

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
- Ni insha vya ripoti.Muundo uzingatie mambo yafuatayo :
- Kichwa
- Kitaje mada ya ripoti na tarehe
- kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe mstari
- utangulizi-uhusishe usuli mfupi au maelezo ya jumla kuhusu mada ya ripoti
- Orodha ya majina ya wanakamati
- hadidu za rejea-mambo yaliyohitajika kufanywa wakati wa utafiti
- utaratibu-mbinu zilizotumiwa kutekeleza utafiti
- mwili-ueleza maudhui(matokeo)-inaweza kuwa na visehemu vyenye vichwa vidodo vidogo
- mapendekezo-inapendekeza namna ya kutatua tatizo lililotafitiwa.
- Hitimisho-ushauri kuhusu mada iliyoshughulikiwa.
- Kitambulisho-jina la mtayarishi
- sahihi
- tarehe
Baadhi ya madhara ya pombe haramu - magonjwa
- ukosefu wa maadili
- kusambaratika kwa familia
- watoto kukosa elimu (mahitaji ya kimsingi)
- vifo
- upofu
- ubadhirifu
- huendeleza ufisadi
Njia za kuangamiza pombe haramu (mapendekezo) - kuelimisha wananchi kuhusu madhara ya pombe haramu
- kufutwa kazi kwa viongozi wanaokubali uuzaji wa pombe haramu kwenye sehemu wanazosimamia
- kushtakiwa,kuhukumiwa,kutozwa faini kwa wauzaji wa pombe haramu
- mikakati ya kupunguza umaskini
- mafunzo ya dini
Mwalimu akadirie hoja za mwanafunzi
- Changamoto zinazowakumba vijana
- shinikizo la rika
- athari za utandawazi
- uigaji wa tamaduni za kigeni
- ukosefu wa ajira
- umaskini
- dawa za kulevya
- ushababi (ujana)
- lugha
Mwalimu akadirie hoja nyingine
- Ni insha ya methali
- insha ishughulikie pande mbili za methali
- mwanafunzi atunge kisa cha kuthibitisha ukweli wa methali
- Kisa kihusu mhusika ambaye amefanya jambo/mambo mabaya kwa maksudi kisha likaishia kumletea madhara
- Hii ni insha ya mdokezo
- mtahiniwa lazima amalizie insha yake kwa mdokezo.
- Insha inaweza kuhusisha uvamizi,mkasa au tukio lingine lenye hatari,ambapo wanaofaa kutoa msaada hawakufika kwa wakati unaofaa
Download Kiswahili P1 Questions and Answers - Form 3 Term 3 Opener Exams 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates