Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 End Term 1 Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI YA INSHA
KIDATO CHA TATU

 • Jibu maswali mawili pekee.
 • Idadi ya maneno isipungue 400
 • Swali la kwanza ni la lazima
 • Chagua lingine kutoka kwa matatu yaliyobaki
 1. Swali la lazima
  Wewe ni mwanahabari kutoka Gazeti la ‘KENYA STAR’
  Andika mahojiano yako na Mbunge kuhusu mpango wa miradi ya hazina ya eneo – bunge analowakilisha.
 2. Swali la pili
  Wewe ni wakili uliyefuzu kutoka chuo kikuu cha Nairobi. Andika barua ya kuomba nafasi ya kazi ikiandamana na wasifu kazi wako katika ‘Mugoh Kangi Law firm’.
 3. Swali la tatu
  Mti ukifa shinale na tanzuze hukauka.
 4. Swali la nne
  Andika insha itakayoishia kwa maneno haya.
  ……………………………. niliinua kichwa juu nikapiga magoti na kumshukuru Mungu kwa kuyanusuru maisha yangu.


MUONGOZO WA KUSAHIHISHA 

SWALI LA KWANZA

 1. Swali la Mahojiano
  1. Mwanafunzi aendeleza mahojiano baina ya watu wawili au zaidi.
  2. Yahusishwe maswali na majibu
  3. Maswali yalenge mambo muhimu katika mada
  4. Lugha iwe ya mnato, komavu na ya kuvutia
  5. Pawe na msamiati unaolenga mada
  6. Mhoji awe na utaratibu mwafaka wa kuuliza maswali.
  7. Insha ichukue sura ya kitamthilia

SURA

 • Mtahiniwa ataje, majina/cheo/vyeo vya mhoji na mhojiwa
 • Herufi kubwa au ndogo itumiwe
 • Matumizi ya hisia au masolugha yawekwe kwenye mabano (husuni, furaha, n.k.)

MIFANO YA HOJA
Chanzo cha utovu wa usalama

 1. Uzembe
 2. Njaa
 3. Ufisadi
 4. Umaskini
 5. Ukosefu wa elimu katika jamii
 6. Kuvunjika kwa taasisi za kijamii (ndoa, elimu)
 7. Insha ichukue sura ya kitamthilia
 8. kuwepo kwa silaha hatari miongoni mwa raia.
 9. Ulanguzi wa madawa ya kulevya
 10. Ukosefu wa kazi
 11. Uzembe na mapuuza ya walinda usalama
  Mwalimu akisie hoja zingine zozote
  *Mtahiniwa asipofuata sura ya tamthilia aondolewe maki nne.
 1. Swali la pili
  1. Barua ya kuomba nafasi ya kazi itangulie
  2. Hii ni barua rasmi, kwa hivyo ifuate mtindo huo
  3. Muundo wa wasifukazi ufuate.

*SURA ZOTE MBILI ZIWEPO. AKIKOSEA AONDOLEWE Maki 4.
Wasifu kazi
Pawepo na vichwa vidogo vidogo

 1. Anwani (Sio lazima aiandike tena kwa vile iko katika barua )
 2. Jina
 3. Tarehe na mahali pa kuzaliwa
 4. Ndoa
 5. Watoto
 6. Anwani
 7. Simu
 8. Masomo yote
 9. Tajiriba
 10. Mambo ya ziada
 11. Machapisho (publications)
 12. Uraibu
 13. Huduma kwa jamii
 14. Warejelewa
  Sahihi iwe katika barua
 1. Swali la 3
  Insha izingatie maana ya methali hii
  Pia ina maana sawa na mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.
  Maana: Ikiwa shina la mti limekauka au kukatwa hata matawi yake yatakauka .
  Kwa mfano: Kiongozi akifariki, wafuasi wake hutawanyika na muungano wa kusambaratika.
  Mzazi akifa wanawe huweza kutatizika ikiwa tegemeo lao lilikuwa kwake tu.
  Mifano mingine yoyote
  Mtahiniwa ashughulikie pande zote mbili za methali. Akiegemea upande mmoja aadhibiwe.
 2. Swali la 4
  Hii ni insha ya mndokezo mwanafunzi amalizie kwa maneno aliyopewa. Akikosa kufanya hivyo aadhibiwe.

Makosa ya Sarufi

 1. Sahihisha kwa makini sana ukionyesha makosa yote yanayotokea. Makosa ya sarufi huwa katika: -
 2. Kuakifisha vibaya: Mifano. vikomo, vituo alama ya kuuliza n.k.
 3. Kutumia herufi ndogo au kubwa mahali si pake.
 4. Matumizi mabaya ya ngeli na viambishi, nyakati, vihusiano, muundo mbaya wa sentensi na mnyambuliko wa vitennzi na majina.
 5. Kuacha au kuongeza maneno katika sentensi kwa mfano, ‘kwa kwa’
 6. Matumizi ya herufi kubwa.

TAZAMA: MATUMIZI YA HERUFI KUBWA

 1. Mwanzo wa sentensi
 2. Majina ya pekee
 3. Majina ya mahali, miji, nchi n.k.
 4. Siku za juma, miezi n.k.
 5. Mashirika, masomo, vilabu n.k.
 6. Makabila, lugha n.k.
 7. Jina la Mungu.

Makosa ya hijai/tahajia
Haya ni makosa ya maendelezo. Sahihisha huku ukionyesha yanapotokea mara ya kwanza tu. Makosa ya tahajia huwa katika

 1. Kutenganisha maneno kama vile ‘aliye-kuwa’
 2. Kuunganisha maneno kama vile ‘kwa sababu
 3. Kukata silabi vibaya kama vile ‘ngan-o’
 4. Kuandika herufi isiyofaa katika neno kama ‘mahari’ badala ya ‘mahali’
 5. Kuacha herufi katika neno kama alikuja badala ya aliyekuja
 6. Kuongeza herufi isiyofaa katika neno kama pia badala ya pia
 7. Kuacha alama inayotarajiwa kuwepo katika herufi
 8. Kutoandika kistari cha kuunganisha neno ufikiapo pambizo au mwisho, au kuandika mahali si pake.
 9. Kuandika kistari pahali pasipofaa.
 10. Kuacha ritifaa au kuiweka mahali pasipofaa
 11. Kuandika maneno kwa ufupi mfano k.m.nk.v.v.

Mtindo
Mambo yatakayochunguzwa

 1. Mpangilio wa kazi kiaya
 2. Mtiririko wa mawazo
 3. Hati nzuri inayosomeka kwa urahisi
 4. Namna anavyotumia methali,misemo,tamathali za usemi na mengineyo.
 5. Unadhifu wa kazi
 6. Kuandika herufi vizuri k.m. Jj,Pp,Uu,n.k.
 7. Sura ya insha
  Msamiati
  Jumla ya maneno yaliyotumiwa kuafikiana na mada au kichwa kilichopendekezwa.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 3 End Term 1 Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest